Josiah Kibira University College - Tanzania 01/10/2010
Mchakato majimboni - Kigoma Kusini 30/09/2010
credit: Kennedy Kimaro 1 Comment Yule golikipa aliyetoa kituko cha kushangilia baada ya kuokoa penati badala ya kuukamata mpira akajitapa kwa kujipiga kifua kujizolea ujiko, ameendelea na vituko vyake, safari hii katimuka kiwanjani kabisaaa! Robo Saa - Amin 28/09/2010
wimbo huu nimeshausikiliza "repeatedly" sijui mara ishirini na ngapi... na hata sichoki! Shukrani za kipekee mno zimfikie kaka Kennedy Kimaro wa kennedytz.blogspot.com kwa kutumia muda na rasmilimali yake kurekodi na kupakia video ya vijana wanasiasa wanaowania nyadhifa za uongozi Tanzania. Dk. Slaa Usitutanie... 27/09/2010
Baada ya kupata video hizi toka YouTube na kuziweka hapa, sikuwa na matarajio kuwa zitawafurahisha watu. La hasha. Na tovuti hii haiweki habari za kufurahisha tu, bali kufikirisha. Lengo langu kuu ndilo hilo. Kuweka kinachonikamata akili na kunisababisha mtu awze au kufikiri "ni sababu gani hasa iliyomsababisha mtu kusema hivi? au kutenda vile nk nk," si kuchekesha tu au kukejeli wengine kwa starehe zetu. Mtu usiingie katika mapambano halafu, kama mbuni ujitahidi kuficha kichwa pekee ndani ya shimo, kisha mwenyewe ujione upo salama il hali kiwiliwili chote kipo nje. Vile vile, tusisahau kuwa mtu uingiapo vitani, adui yako humchagulii silaha atakayokupiga nayo. Hivyo video hizi nimeziweka makusudi kwa wasiofahamu wazione, na kwa wale wanaozifahamu, basi "warudishe mapigo" kuielimisha jamii ikiwa kinachotamkwa ni upotofu. Yawezekana ukawa mwenye akili na mwepesi kung'amua "mpunga" na "chuya", lakini usisahau wengine huhitaji "kupeta" au "kuchekecha" ama "kutafuna" kwanza kabla ya kujua ipi kweli "pumba" na ipi ndiyo "chuya", ndivyo tunavyotofautiana kiakili. Tusijisahaulishe kuwa tunawalalamikia wananchi ati wanawachagua viongozi wasiofaa na papo hapo hatuwaelimishi. Ikiwa mawazo yao ndiyo kama yaliyomo kwenye video hizi au ni wepesi kuamini ujumbe uliopo kwenye video hizi, bila kutizama video na kuyafahamu, tutaanza vipi kumwelimisha huyu mwananchi? Tutamhubiria? Mbona wanahubiriwa sana tu Makanisanina Misikitini lakini maovu yanaenelea? Mi nadhani ili kutoa elimu maridhawa, inampasa mwelimishaji ajue awazacho mtu ndiposa ajue namna ya kuchukuliana na kumwelimisha yule wanayetofautiana mtizamo. Hapo ndipo malumbano ya hoja yanapokuwa sawia. Haya mnayoyaona kwenye video ni muhtasari na uwakilishi wa mawazo yaliyotanda katika jamii. Tusiwe waoga wa kufahamu habari tusizozipenda. Tusipende kukaa kwenye "comfort zote" na kutaka habari za kutufurahisha tu. Kufanya hivyo ni kupoteza fursa ya kumsoma mpinzani wako anavyokuharibia. Changamoto Ikiwa kweli wapo wanaokerwa na video hizi, ni hatua gani wanachukua nao "kuwafukunyua" wapinzani wao? Nachelea kusema, mbinu ya "zuia isionekane" na "jidai hatufahamu", hiyo ni mbinu iliyofeli. Hizi ni siasa za tit-for-tat. Stepping into the ring, means you are ready for a fight. If you have the potential to attack and destroy me, so do I. Dare to show me what you've got and I'll show you what I've got. credit: hanskara credit: hanskara | LIVEsports links
Myp2p.eu Iraqgoals.net Rajangan.net LiveScoreHunter.com Scorepage.com LiveTv.ru xScores.com NowGoal.com Vieo CategoriesAll Video Archive
April 2011 |



