Jerry Muro azungumzia alivyokamatwa 01/02/2010
Shukrani kwa TheUwazi kwa kupakua video # I + II kwenye tovuti ya YouTube. Hapa wavuti.com tumeziunga pamoa na kuzifanya kuwa moja kwa urahisi wa kutizama. Sababu ya kuwa na mbili kule YouTube ni kutokana na tovuti hiyo kutokuruhusu kupakua video ya muda wa zaidi ya dakika 10 au faili la ukubwa wa zaidi ya saizi ya 2gb, lolote litakalotangulia (ni mabadiliko mapya ya YouTube). CommentsBwana Jerry, pole kwa yaliyokupata. Sasa nimeelewa, kumbe kufichua rushwa polisi wamekuchukia. Maoni yangu ni kumuomba Raisi wa nchi akulinde maana, mpaka hapo wnakutafuta kwa kila mbinu. Ila pia kwa kuwa unaonewa kwa kutenda haki, ulinzi wa Mungu uko pamoja na wewe, atakayejaribu kukutenda baya litamrudia yeye nanchi nzima itajua ameadhibiwa na MUNGU. Tuko nyuma yako wananchi wote. Usiogope...
Reply
01/02/2010 8:55pm
Mtanzania, naomba kwanza nitoke nje ya mada kidogo, nataka kusifu ubora na uzuri wa tovuti yako. Naam, vijana wa leo wanasema, 'imetulia'!
Reply
Mtanzania 01/02/2010 9:25pm
Nakushukuru kwa pongezi hizo hapo juu. Ila nakiri wala si mimi mmiliki wa hiyo tovuti, na hata wkt naandika sikujua ipo, ila kilikuwa kichaka. Ulipotoa hizo pongezi ndo namimi nikafuatilia. Namimi namrudishia sifa mwenye hiyo tovuti.
Reply
01/02/2010 9:32pm
Mtanzania, asante kwa kuwa mkweli kuhusu tanzania.com, natumai mmiliki atapokea pongezi hizi.
Reply
Lumza 01/02/2010 9:50pm
Hamna lolote, nchi haina shukrani iyo kula kona kaka Jerry kabla hawajakufanya kama yule Mwandishi wa Loliondo gate. We bishana nao tu,tutakuimbia mapambio(Tumpeleke baba huyu.....)
Reply
wk 02/02/2010 12:05am
tanzania ya leo ina uongozi mbaya sana. viongozi wa kesho tafadhali leo hii jitoeni wazi na msiwaogope viongozi wachache ambao are rotten like kidonda ndugu.
Reply
Tuma 02/02/2010 12:22am
This guy got guts meeeeeeeen, especially that sentence "huyu kova ni mtu minor sana....aulize nimevitoa wapi", I like your courage dude!!!1
Reply
02/02/2010 12:40am
its true ,usifanye ubishi nao hao watu,watakuua au kukufunga kama yule
Reply
HII INATHIBITISHA KUWA RUSHWA INAMTANDAO MKUBWA, HAO POLICE WADOGO HUWA WANATUMWA NA WAKUBWA ZAO KUKUSANYA PESA TOKA KWETU SI WALALAHOI HII NI DHAMBI KUBWA SANA. NAHISI HATA MAWAZIRI HUWA WANAPATA MGAO NA MKUU WA POLISI PIA ANA MGAO WAKE YA NINI WAMFANYIE HIVYO NA KAMA SI KWELI BASI MPANGO KAMA HUU HAUWEZI KUWA WA NGAZI ZA CHINI NI MPANGO TOKA NGAZI ZA JUU UMEHALALISHWA NA NGAZI ZA JUU ZA POLISI, KWA MAANA HIYO HATA IGP ANAHUSIKA, SHAME ON YOU POLICE
Reply
makono 02/02/2010 2:31am
inatubidi tuwe watulivu wakati tunasubiria uchunguzi ufanyike tusiwe mashabiki wa upande wowote kwa kujibu wa sheria za TZ nothing is predictable
Reply
uk 02/02/2010 2:33am
Pole sana sana Jery.
Reply
mfurukutwa 02/02/2010 2:51am
nimesoma habari hii kwa masikitiko makubwa sana serikali iikiliee kati khs suala hili na kikwete aone jinsi wafanyakazi wenzeke wasivyotaka maendeleo ya nchi jeri kazi buti kama kubenea
Reply
mbongo 02/02/2010 3:56am
kwanza pole sana ndugu Jerry. Wakati umefika sasa, mambo ya zamani ya watu kutumia vyeo vyao sasa umekwisha. Ndugu Jerry, wewe ni kama wale watu ambao waligombania haki za binadamu huko U.S.A katika miaka hiliyopita. Lakini tunataka kukueleza kwamba Dunia inaona vitu unavyotendewe sio haki. Watu wengi tumechoka na tabia ya watu mbali mbali ktk serikari yetu, tunaju kwamba wako watu wazuri lakini na wabaya wafichuliwe.
Reply
Bro 02/02/2010 4:48am
Nadhani Tanzania ina mwanasheria mkuu wa serikali,masuala ya watendaji wa serikali ambao, kisheria,hawawatendei haki wananchi ususani katika hii kesi, anapaswa kulifuatilia jambo hili kwa karibu zaidi,kutokana na ukweli kwamba huyu bwana(Jerry)alihusika katika kuwaanika maofisa wa polisi wala rushwa,tunamuomba mwanasheria mkuu wa serikali na wale wote wanaohusika na maswala ya rushwa walifuatilie jambo hili kwani hawa wote ni watendaji wa jamii.Lakini jamii haitokaa kimya,kisheria lazima Jerry afikishwe mahakamani, na kufunguliwa mashtaka,na aidha kukubali au kukataa mashtaka yake aliyosomewa,na wahusika wote watajwe kama upande wa mashtaka na mshtakiwa unavyowataja,Tunaomba wanahabari kuendelea kutuletea taarifa hizi wazi wazi ili kila mwenye uchungu na nchi hii na jamii hii kuona na kusikia ni nini hasa kinaendelea.MUNGU USIIBARIKI TANZANIA KWANI NI WEZI TU NDIO WENYE KUFAIDI.
Reply
Makadara 02/02/2010 5:38am
Ni jambo lakusikitisha sana kuona hadi leo kuna kesi nyingi zinazohusu rushwa zinashindwa kumalizika, aidha wahusika wanashindwa kuchukuliwa hatua au serikali haioni haja ya msingi kuzimaliza kesi hizo,sisi wananchi tumechoka na alifu ulela ulela,viongozi wetu karibu wote wameshindwa kudhibiti rushwa,sababu wao wenyewe ni walaji rushwa,jela zetu zimejaa wezi wa kuku, wakati wale wezi wa mamilioni na mabilioni, wanaonekana sio wezi badala yake wanaitwa wala rushwa,Tanzania ni nchi yenye viongozi wengi wabovu,na wasiojali nchi na wananchi wake kwa,watanzania wamepita kwenye misukosuko mingi,bila matarajio,tumejionea ni jinsi gani uhuru unavyotumiwa vibaya ni afadhali mkoloni,kuliko huku kujitawala tunashidwa hata kuendesha mabenki ipasavyo mpaka tusaidiwe tunachoweza ni wizi(rushwa) mfano :wakati Julius tulijionea wenyewe jinsi gani ilivyokuwa njaa,watanzania hawakuwa na haki ila mkimbizi ndio mwenye haki,tulidhubutu kuvaa matairi ya gari wakati wakimbizi wanavaa kandambili safi, tuliwajazia chakula makambini mwao na sisi kupanga mistari ya kilo moja moja ya mchele kwa kaya,wakati wa Mwinyi angalau kidogo,lakini majambazi serikalini waliota mizizi kila mtu alikuwa anautafuta utajili hata ikiwa kumzika mtu mzima,wakati wa Mkapa,ndio kila kiongozi alikuwa mfalme anafanya atakavyo walijiuzia majumba, machimbo nk,na sasa tunajionea wenyewe viongozi wanadhubutu kumpiga mtu risasi,Bado Historia inaendelea,Vyama vya upinzani hatuna wapinzani wapo kwa kusubiri ruzuku za serikali hawana sera za msingi,hawana utaifa,watawala wa nchi ni wazee, hawana fikra zozote mpya badala ya kila kitu kiitwe Julius hawana zaidi,wanasheria wetu wasomi wetu wamegeuka mabubu hawajui walifanyalo wanasubiri labda na wao hipo siku watakuwa viongozi ,wabunge au makada, koila mtu ana tamaa,siasa imekuwa ndio mchezo wa kila mzazi kumuombea mwanae apate.Watanzania wengi sio wakaazi wa Daresalaam,bado nchi yetu ni maskini sana tembeeni muone. NAMUOMBA MUNGU ASHUSHE MARADHI KWA WATANZANIA ILI KILA MWENYE MAFUTA MENGI MWILINI AFARIKI.
Reply
02/02/2010 6:56am
AIBU KWA SULEIMAN KOVA na Saidi Mwema.
Reply
Raia mwema 02/02/2010 7:21am
Jerry, kwanza pole sana kwa yaliyokukuta. Mungu aliyekuwezesha kufanya kazi ya kuwafichua wahalifu ndio yeye atakayekulinda na kukupigania hata kwa haya.Jerry Mungu wetu si muongo hata alivyosema, Atatupigania na sisi tutanyamaza kimya. Katika hili kwa nguvu zako na kwa akili zako hauwezi. Jerry tuna imani na wewe, na tunaamini huwezi kuwa kama walivyosema. Wale wote walioshiriki kukusingizia uhalifu huo, kama Mungu aishivyo, ukawarudie mara saba zaidi ya walioyakusudia juu yako. Naungana ya yule aliyesema sasa hivi utulie kimya, Bwana Yesu akuchagulie Mwanasheria mzuri ambaye atafanya kazi yake kwa uangalifu na Mungu wa amani amlinde. Jipe moyo mkuu.
Reply
Mummie 02/02/2010 7:48am
Jerry be strong mdogo wangu.... dont panic this is really Bongo hatutoendelea kamweeeee!!! kila lisemwapo la ukweli chombo cha dola kinanyamazisha inauma sanaaa... JK hebu saidia hawa vijana nchi yako iendelee maana ya Kubenea yameisha hivihivi na kumnyamazisha kimyaaaaa!!!Kwa kweli acheni vijana wakimbilie nje tu wakasake maisha.
Reply
Joyce 02/02/2010 7:55am
Jery umewahi kuona mwenye haki ameachwa?tunakuombea Mungu yupo kama kweli hukufanya yote yaliyoko Sirini Mungu atayafichua,Jipe Moyo ni Majaribu
Reply
Joyce 02/02/2010 8:02am
Mungu kama upo naomba umnusuru Jery mwana wa Muro kwenye majaribu haya yaani mimi imeniuma sana Jery kaka yangu ona hayo ni majaribu na ni Challenge kwako kuon akun awatu wanakuzunguka Watanzania tumuombee kijana mwenzetu katik ahali hii kwani ni mdogo na anahitaji msaada wetu wa hali ya juu.Mungu baba wa mbinguni asubuhi ya leo namleta Jery Muro mikononi mwako naomba Ujidhirishe kwake kwa kufichua ukweli ili watu wakutukuze,E mungu muepushe kijana huyo katika mapito haya magumu nakouomba kwa kuwa najua Utatenda na wote tusme Amen
Reply
shame be on you the so called f***k**n police, we are sick and tired of your damn things,
Reply
Jovinth 02/02/2010 8:34am
Inatubidi tuwe watulivu wakati tunasubiria uchunguzi ufanyike tusiwe mashabiki wa upande wowote kwa kujibu sheria za TZ nothing is predictable. Uchunguzi ukishafanyika tuendeleze libeneke kama kawa.
Reply
mwanaharakati 02/02/2010 8:37am
hii ndo aza ya kupeana uongozi kwa kujuana ooh mara shemejii mara nini,kaka jerry be strong na endelea kuwaanika wala rushwa,wewe polisi unakuwa na kitambi cha nini?.hiyo dhana yao ya polisi jamii ndo iko wapo sasa
Reply
EE MUNGU, NAKUOMBA USIMAME KAMA MUNGU, MTETEE JERRY MURO, DAMU YA YESU KRISTO MFUFUKA MPIGANIE JERRY MURO.EE MUNGU WETU UNAYEIJUA KESHO DAMU YA JERRY MURO IKO MIKONONI MWAKO, MAISHA YA KIJANA HUYU YAKO MIKONONI MWAKO. TENDA HAKI MUNGU, TENDA HAKI BWANA JINA LAKO LIINULIWE KATIKA KUMTETEA JERRY.EE MUNGU UNAYEPENDA HAKI, USIMWACHE KIJANA HUYU KATIKA MIKONO YA ADUI ZAKE.
Reply
02/02/2010 8:54am
Mi nashangaa Tanzania watu wanakata vichwa albino badala ya wala rushwa, matokeao yake nchi inakuna rushwa. Ni heri nchi kunuka damu ila sio rushwa. Pole Jerry Mungu atakusaidia.
Reply
flora 02/02/2010 9:18am
Pole sana Muro, but you need to be verry strong,as a human being you need to talk,jaribu kuongea na watu wako wa karibu sana, upo bado katika mitego mingi sana,MUNGU NI MWEma ATAKUSAIDIA
Reply
mama dollar 02/02/2010 9:24am
Mwanangu Jerry Murro pole kwa yaliyokukuta na usihofu Mungu yuko pamoja nawe, najua sikweli ukutwe na pingu hiyo ni mikakati ya kukudhoofisha katika kupambana na wala rushwa , kwa kweli hawana hata aibu wangetafuta njia nyingine siyo hiyo ya kukubambikia pingu. mwanangu nakushauri soma mara kwa mara Zab. 35;1-10 Mungu atakusikia na atakusimamia kwa kila jambo
Reply
Mwanja 02/02/2010 9:34am
JELLY GOD IS ON YOUR SIDE.DONT WORRY!!!!!!
Reply
REUBEN 02/02/2010 9:43am
KAKA JELLY!!!!!!
Reply
Ferry 02/02/2010 9:44am
jamani huyo Jerry amekuwa gumzo hata mie mwanzo kabisa nilishtuma police kuwa wamembambika kesi lakini acha tuendelee kuona uchambuzi, kwa swala la rushwa ni uongo mtupu kwa jerry lakini tatizo litakaro mbana ni yeye kuwa na pingu!!!!!!!!! kitu ambacho ulimwengu mzima hakuna raia anaruhusiwa kumiriki pingu, na imesemekana amehojiwa akajibu kuwa alizinunua somewhere in TZ pamoja na bastora, uozo uko serikalini.
Reply
Ferry 02/02/2010 9:51am
Nawashauri watanzania msitumie kauri chafu kwa police, kabla hatujamtukana police tujiangalie na sisi wenyewe tumekamilika????????? hakuna mtanzania asiyekula rushwa hilo tulikubali, si police pekee anayekula rushwa sana sana wanakula vijisenti tu. Hata wewe unayetoa kauli chafu jiangalia ndani ya roho yako kama kweli hujawahi kula rushwa toa matusi kwa police, ila roho yako itakusuta. tuangalie haki tusitumie jasiba za chuki binafsi
Reply
mtanzania 02/02/2010 10:03am
pole sana jerry naamini binadam watakuacha lakini mungu hatakuacha.
Reply
02/02/2010 10:04am
Huku China Mtu akila rushwa anakatwa kichwa. Sheria zinafuatwa. Na mara nyingi adhabu hizo zinaenda kwa wakubwa, wakuu wa miji na watu wenye vyeo vya juu. Hakuna jela za bure huku. Bongo inabidi ibadilike, sheria zifatwe. Itaweza kuchukua muda lakini ikitiliwa mkazo basi siku moja nchi itakuwa sehemu nzuri ya kurudi. Pole sana Jerry, tuko nawe. Tunaamini haki itatendeka.
Reply
tatu bora. 02/02/2010 10:05am
yaani mimi polisi wananikera siwapendi
Reply
elly 02/02/2010 10:34am
Wewe unaysema tujihoji et hakuna mtu asiye kula rushwa, acha ujinga hatuko hivo ndugu yangu, nahisi wewe ni police na umezoea kula lushwa kwa hiyo unaona ni jambo la kawaida sanandyo style yako ya maisha shame up on u
Reply
Saaduni songoro, ole Muhogoni 02/02/2010 10:44am
Ndugu yangu Jerry,
Reply
Adam 02/02/2010 10:45am
YAWEZA KUWA NI AGENDA PANA YA MAFISADI KUTAKA KUKATISHA TAMAA WATANZANIA ILI WAENDELEE KUAMINI KUWA,.. tazama wote wametenda dhambi.. ni mafisadi watupu...
Reply
ferry 02/02/2010 10:47am
ndugu yangu ujiitaye elly acha ufala hatuko kwenye marumbano hapa, mambo ya ujinga yamekujaje?? hakuna mjinga hapo inaonekana limikuuma, kuwa tu mstaarabu kama huwezi kuwa mstaarabu tovuti hii huiwezi ni watu wenye akili timamu inionesha wewe zimeruka kidongo sijaona anayetoa matusi kama wewe.
Reply
02/02/2010 10:50am
Jerry dia nakujua toka tulivyokuwa shule kolila moshi najua umtu mwenye msimamo ila sehemu ulipoingia si pazuri hawa jamaa mitandao yao ni hatari wameifanya hii nchi kama yao wakitaka lolote wafanye wasizuiwe ujue rushwa wanazochukua police wadogo huwa wanatumwa na wakubwa hii issue usiifatilie juu juu imesukwa na wanamtandao hii watu wametumia pesa zao kukuangamiza wako wapi kina Kolimba,Sokoine wale wote waliojifanya shupavu wako wapi wote leo imebaki story u kijana jasiri unayefanya kazi yako kwa kujituma huogopi ushupavu llakini si katika nchi hii wengi wanajitokeza lakini wanaundiwa mtandao mfano rais Jakaya kikwete umeona alivyowabadilikia wanamtandao leo hii wanatakaa kuanzisha vyama vyao kisa wameonewa wkt wameambiwa ukweli be strong hapa ukitoka kwenye hii issue tokomea mdogo wng watakutanguliza mbekle ya haki ht kwa kukusababishia ajali au kuwekewa sumu itakayokula taratibu bd unafight maisha unaweza ukawa na watu watakaokutetea ila watanunuliwa tu neno NJAA ndio linalofanya tusalitiane kituo ulichopo ni cha serikali km kn issue ya mkubwa hapo utaumia TANZANIA kwa kuteteana kwenye habari bado tupo nyuma hapa watu wanalindana mtu yuko radhi kuinunua habari na hivi neno NJAA ndio LINALOTUUMIZA mdogo wng utaangamia na hii issue iko mikononi mwa haohao unaowafukuzisha kazi watakuonea hapa omba JAKAYA aingilie kati utoke sisi tuko pamoja na ww ht maandamano tutafanya ili haki itendeke wadau tulivalie njuga hili janga bila ya hivyo mwanaharakati mwenxzetu anaangamia
Reply
Judith 02/02/2010 10:52am
Reply
Borafia Kisonge Zanzibar 02/02/2010 10:53am
Watakugeuza Kabendera Shinani mwili wake uliokotwa ndani ya Mto Kagera unaelea. Jeshi hili linahitaji restructuring ya mwaka. Kwani hawajifunzi wenzao polisi wa Uk walivyo polisi jamii. Jee huku ndio kuwa polisi jamii tunayoambiwa kubambikizana makesi
Reply
Ana and Janeth 02/02/2010 11:03am
Pole sana kak yetu Jery kwa yalokukuta,
Reply
kaka Jerry,
Reply
mudiko 02/02/2010 11:08am
hi kaka muro usijari mungu takupa nguvu na swala litamaliza vizuri wakakutwa wao na hati
Reply
Mkereketwa 02/02/2010 11:11am
Kwanza ningependa kumpa pole Jerry na kumwambia asife moyo na aendelee na mapambano kama kawaida. Na pia aangalie sana wakati huu kwa kuwa wote waliomzunguka si wema kama yeye anavyofikiri.
Reply
Jovinth 02/02/2010 11:11am
mwanaharakata nilikuwa sijafatilia story kwa kina. Tumuombee Jerry
Reply
Evelyne 02/02/2010 11:30am
Kaka Jerry wewe ni shujaa, ila vita hii ni kali kama vile Osama na Bushi, basi vaa silaha za Mungu na wala usiogope kutenda haki mwamini na kumtegemea sana Mungu naye atakushindia. Vijana wote wa kitanzania tupo nyuma yako kukupa support kimawazo na kimaombi pia tutafunga na kuomba kwa ajili yako na hakika Mungu huyu anayetenda miujiza atakutendea na wewe. Mabaya yote waliyokuombea yakawarudie wenyewe, kila anayenyosha kidole juu yako kwa ubaya ukamrudie, kila anayenena juu yako kwa ubaya ukamrudie, kila anayewaza na kutenda mabaya juu yako ukamrudie mara elfu na zaidi. (Shimo wamekuchimbia wewe watatumbukia wenyewe. EE, MUNGU MBARIKI JERRY MURO, MBARIKI KILA ANAYETENDA HAKI NA KUONEWA KAMA JERRY WOTE HAWA UKAWAKUMBUKE KATIKA UFALME WAKO NA KUWASHINDIA KATIKA MAJARIBU YOTE WANAYOKUMBANA NAYO. AMEN!!!!!!
Reply
halooos,fikra zangu zinanijia kuwa askari hawajui kazi yao,ndugu zangu tunapaswa kujua na kuinuka kujua askari hatuna,Jerry muro alicho fanyiwa ni njama tu,amewahaibisha ndiyo mana wanamchukia,ni ujinga kutumwa mambo mabovu,ipo siku tutafikia walipo wenzetu kutokubali kuonewa sasa mda umefika,waandishi endeleheni kueneza habari bila kuogopa,jasho la mtu aliliwi,ONE DAY YES,God bress you J.morro.
Reply
jamijem 02/02/2010 11:50am
yaani nchi hii ukiwagusa tu watu flan flan unakua wanted pole jerry kakwakua victim...bt watz tunataka waandishi km ww na co wababaishaji...chukua ushauri unao ona utakufaa....
Reply
Mtanzania 02/02/2010 12:04pm
Kwa mara nyingine tena nimerudi, nilikuwa wakwanza kutoa maoni katika suala hili. Nawashukuru sn waTanzania wote mliotoa maoni yenu ila ndg mmoja amenishangaza hapa katika maoni yake.
Reply
mdau nje 02/02/2010 12:11pm
Wee jamaa unayejiita ferry wee ndo shetani kabsaa na ni polisi walewale na inaelekea ndo mla rushwa mkubwa.mie naungana na watz wenzangu kuwa nipo nyuma ya huyu kaka Jerry!serikali yetu imeonza ukitaka kujua njoo nje uone ndo utaona real stn ya tz.yaani bro ikiwezekana baada ya kesi tulia kwanza na cha muhimu sasa ni kudai haki yako ikiwa ni pamoja na maombi yetu najua utafanikiwa na haya yatakuwa historia.Mie kwa kweli sina hata hamu ya tanzania nipo nje lakini ninaumia sana na hiyo nchi.mmh!natamani hata kulia jinsi viongozi wanavyotunyonya.
Reply
Evelyne 02/02/2010 12:22pm
Kwa kuwa sasa matukio ya uonevu kwa raia yamekuwa mengi tumona ya Zombe na hatimaye kuisha kienyeji, tumeona ya kubenea na kuishia pasipo julikana, tumeona ya yule kijana aliyechomwa na bisibisi na askari hadi kufa na sasa ni Jerry katika taswira nyingine, Je? haki za raia ziko wapi kama ikiwa hawa waliopewa dhamana ya kulinda na kutetea haki za raia ndio wanakuwa msitari wa mbele kuzivunja tena kwa makusudi. Je? Rais haoni kuwa umefika wakati sasa wa yeye kutoa tamko kwa Jeshi la polisi kwa kulichambua na kulipanga upya kama alivyofanya benki kuu kwa kumuondoa gavana ndg balali na kupanga watendaji wengine wote upya, na kidogo wanachi tukaanza kupata imani. Sasa tunaomba Mh. Rais atuongezee imani kwa hili la kusingiziwa uhalifu la Muro na lile la kijana aliyechomwa na bisibisi hadi kufa na askari ambao wako mbaroni sasa,
Reply
Kaju-France 02/02/2010 12:51pm
SHAME ON YOU, (Kova mambo mengine yanahitaji busara tu kuyaweka sawa taarifa yako mimi haijaniingia akilini KABISAA) INAONEKANA JINSI GANI HAMKO SERIOUS...MARA MILIONI KUMI...NA SASA PINGU? TUMESHAWATSITUKIA....TUMECHOSHWA NA KAZI ZENU ZA KINAFIKI...LAZIMA MJUE WATANZANIA WOTE TUNAUMIA SAAANA NA MAMBO MNAYOFANYA (NYIE MNAOJIONA MKO KWENYE SYSTEM)....TUMEWACHOOOKA? PIGA MOYO KONDE JERRY MURO, TUPO PAMOJA KWA SALA NA MAOMBI
Reply
stella 02/02/2010 1:31pm
jerry tupo pamoja nawe mungu atakulinda
Reply
Martha 02/02/2010 1:46pm
Jerry Muro Kufa Kiume tunakuombea tupo pamaja fichua zaidi ni wivu tu
Reply
Kai Rooney 02/02/2010 1:59pm
Hizi ndio zao police kubambikia watu mashitaka, ni watu wengi wameshakuwa victim kwa hii style wanayomfanyia Jery, Thank god Jery anasauti kaweza kuongea na watu wamejua ukweli. jeshi la police linanuka kwa rushwa kuanzia ngazi ya juuu mpaka kwa police wa doria wanataka kumnyamazisha Jery,ili waendeleze mchezo wao, shame
Reply
ZeSinia 02/02/2010 2:12pm
Ingekuwa ni kamari ningesema siwezi kuweka mtaji hapo kwa MURO. Hawa waandishi sometimes hujisahau na kuvuka mipaka ya utendaji! Mimi nasubiri mahakama iamue na nipate maelekezo ya raia kumfunga mwenzake pingu!
Reply
Mwana 02/02/2010 2:37pm
Kaka Jerry Mungu yuko pamoja na wewe.
Reply
maeda 02/02/2010 2:46pm
i realy hate this 4th govenment. no human rights, no peace, what they have done to our journalist jerry muro is bad its a trup.big up jerry may God be with u for this had time. dont hesitate to tel the truth to the public. God bless Tanzania, God bless Africa
Reply
mkereketwa 02/02/2010 2:55pm
pole saana kaka Jery!Mungu yupo nawe daima na atakushindia,hii nchi nosense kwel,watu wanaofichua maovu ndo wanawindwa lakin wale mafisadi wanakula raha ya nchi,kaka Jerry be strong na Mungu akuongoze jaman
Reply
Mtanzania nje ya nchi 02/02/2010 3:13pm
Reply
hans 02/02/2010 3:30pm
yaani tusubiri tuone maana hata Bwana Yesu aniuzwa kwa pesa kidogo kulinda watawala jerrrrrrrry, big up ila usirudishe majeshi nyuma
Reply
Grace 02/02/2010 3:36pm
Reply
Kaju 02/02/2010 3:38pm
Zesinia...mambo mengine yanakera sana, hii issue siyo cheusi chekundu na kuchagua rangi...dunia ya sasa we have to stick on facts...sasa hao polisi si waweke facts hadharani, hakuna swala la mipaka kwenye haki ya kila mtanzania...waandishi ni kazi yao kutujulisha kila kitu kizuri na kibaya...hawawezi kusimamia sheria kwa style hii, ...kwa issue hii kusubili mahakama ni kupoteza muda...unless hao wote walishiriki kuplan huu upuuzi waanikwe hadharani....boofu boofu
Reply
Mtanzania nje ya nchi 02/02/2010 3:44pm
Enzi za TANU jeshi la polisi lilikuwa jeshi la kulinda Jamii.Enzi hizi za CCM, limekuwa jeshi la kuwalinda MAFISADI wa CCM. Wengi waliojitoa kwa ujasiri kuwatoa Watanzania kwenye GIZA walilowekewa na CCM wote wameuwawa. Mnamkumbuka Sokoine?, Col. Kombe?
Reply
Mullah 02/02/2010 3:52pm
Reply
Mwananchi 02/02/2010 4:13pm
Nimeamini kwamba kweli kama wanavyotolewa kwenye katuni hawa mapolisi ni kweli ni viazi kweli kweli.
Reply
Allan 02/02/2010 4:18pm
Mtetezi wko Yesu anaishi, so my fr dont worry utaishi na hauta kufa bila kuleta ukombozi ktk hili. U are the Herro.
Reply
IRENE 02/02/2010 4:38pm
ee mungu baba tunahitaji muujiza wako utedeke kwa jerry muro,
Reply
tina 02/02/2010 4:44pm
pigana m2 wangu naamini wewe ni simba wa yuda. hiyo ni ishu tu usijali mungu atakupingania.
Reply
sipher 02/02/2010 4:50pm
jerry kaka usijali huyu wage sichochote asikutishe yeye mwenyewe ana ishu ya ufisadi ndio maana anataka nawe akuharibie jina usijali haya nimajaribu tu hata yesu aliyapata na akashinda tupo pamoja nawe.
Reply
mdada 02/02/2010 4:59pm
jerry love, woooooooooote wataongea lakini hata mtoto mdogo huwezi mwambia hii story akaona kosa liko wapi,kwanza kova is jst f...k d up kwa sababu hajui kazi yake anatakiwa ajiuzuru maana inaonyesha hata taarifa huwa hanaga sahihi ye anachoambiwa ndo anachoropoka.mi namuonaga sana pale best bite anavyochongaga mingo na watu ila ni bwege tu.if only the president of the united republic angejua how important ur in this country, angekulinda. coz ukitaka kujua mambo yanaendeshwa bila sheria ona ditopile alivyoshtakiwa kwa kosa la manslaughter wakati duniani hamna kosa kama ilo.kosa ni murder alaf ushaidi ukikamilika ikaonekana hakukusudia ndio kwenye hukumu wanapunguza kosa kuwa maslaughter, je kama kosa la murder halina dhamana,dito morogoro guest alifikaje watu tunajua yuko segerea mpaka hukumu itoke.ilikua ni aibu sana kwa tanzania alafu watu bado tukae kimya????????????????????helllllllllll NOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO.JERRY C UNAONA DITO ALIVYOMTEMBELEA JUDGE WA MAJUDGE? NAOMBA NA HUYO KOVA ANGEFATA.ILA malipo ni hapa hapa wangu.watanzania wote tuko nyuma yako.
Reply
Ray 02/02/2010 5:01pm
Big up Jery. usijal komaa nao wazee wa vijicent hao
Reply
mwarain 02/02/2010 5:04pm
yap man chunga sana isije ikawa kama dada AMINA CHIFUPA maana hawacheleweshi hawa jamaa ni noma sana ila amini ya kuwa mtetezi wako anaishi leo.
Reply
Lizo 02/02/2010 5:09pm
Iviiiii, wajameni eti walingoja mpaka afuchue ufisadi kwa trafic ndo wamchunguze? unajua hata mtoto mdogo wa leo atajua kua hili ni tego tuu kaundiwa mwanatuu Jery? Kova be careful jiji litakushinda mjomba oohh!anyway kwasabu washatugeuza sie wa enzi za midle skul eh? watanzania nawadeiz are very creative! MUNGU MSIMAMIE JERY. Amin.
Reply
mfwangavo ugweno 02/02/2010 5:10pm
Reply
frizo 02/02/2010 5:16pm
Edenali umwana vavene uyo JERY, agitile uli? mwinasambi kwa nguruvi nye vahidzi unye!
Reply
sandra 02/02/2010 6:46pm
Pole sana Jerry kwa kuonewa sababu ya kazi yako nzuri,Askari police wote wamekuchukia sababu umewafichuwa wanapenda sana rushwa!na ndiyo maana wanakutafutia kila sababu ili uonekane ni mhalifu,lakini watanzania tunajua kuwa ni uongo wamekusingizia tu!Mungu yupo nawe na sisi tunakuombea Mungu akulinde,tunaiomba serikali ya Tanzania na viongozi wake waingilie kati suala hili ili haki itendeke!Na askari wala rushwa na waonevu wafukuzwe kazi!
Reply
mama salma 02/02/2010 7:03pm
Kwanza nakupa hongera kwa kazi nzuri unayoifanya ya kuwafichua askari wala rushwa!askari na trafik polisi wamezowea sana kuwaonea wanyonge,wao wanadhania wenzao pesa wanaokota?Na nakupa pole sana kwa kusingizia kesi mbili tofauti zisizokuwa na maana,sasa wameumbuliwa kwa kula rushwa na ndiyo maana wameona ni bora wakusingizie kesi zisizokuwa na ushahidi wowote!sote tunajua ni umuongo tu,Na wote wanaokusingizia Inshallah kwa uwezo wa Mola atawahukumu,fimbo ya mnyonge hulipwa na Mungu,Duniani ni malipo na akhera ni hesabu.
Reply
Che guevara 03/02/2010 8:32am
Kamanda kova,naomba unifafanulie jambo moja, katika scenario kama ya muro huko nyuma tumeona wahusika wakiwa wanatumia mitego ili kuwanasa watuhumiwa,kwa nini wewe na vijana wako hamkuweka mtego wakumkamata shujaa muro na hiyo rushwa??????.....mbona ilikua rahisi sana kwasababu alishafika eneo la tukio kuchukua mzigo wake!!!!!
Reply
Kama mungu aishivyo, Jerry hakuna atakayekuweza, watanzania tuko nyuma yako na mbele yako yuko mwanamume wa wanaume Simba wa Vita, vita vyetu si vya mwili na damu. soma zaburi ya 35: 1 - kuendelea, upate silaha ya rohoni. Uwe na amani. Rushwa ni adui wa haki biblia inasema na ni aibu kwa Taifa. ulipaswa kupokea tuzo uliyopewa, bado tanzania inahitaji wakina jerry wengi katika nyanja mbali mbali ili tufike tunakotarajia kufika, lakini kila anayeibuka anazimishwa, kwa hili la Jerry Mungu tunakuomba uingilie kati, maana hii ni sehemu ya ukuu wako udhihirishe umma wa watanzania na mafisadi wote wanaoitafuna nchi hii waangushwe chini wote wanaoifuatilia nafsi yako. Hongera sana na mungu akuwezeshe kuwasamehe maana hawajui walitendalo, hawana dhamana ya roho zao, kumbuka Anania na Safira, walipigwa papo kwa papo. Mungu anatenda jipe moyo, kama kweli una kesi ya kujibu basi sheria ichukue mkondo wake, lakini kwa jinsi ya kibinadamu hatuamini hivyo na ndio maana tunakuombea kikombe hiki kikuepuke katika jina la YESU. Amen.
Reply
Esther F 03/02/2010 2:22pm
Kaka Jerry, pole mwaya,
Reply
sy 03/02/2010 2:51pm
Siamini kama Jerry Muro anaweza kutenda kama Polisi wanavyosema.Hii ni fitina tu.Kazi yake ni nzuri daima.Naamini Mungu atamsimamia na haki itatendeka.Keep it up Jerry.Bravo!!!
Reply
Kaka Jerry Muro pole sana, nakuombea kwa Mungu zishindwe kwani hizo zote hizo ni nguvu za giza dunia imejaa dhambi sana hata kama una haki lakini yaweza kupotezwa na mabaradhuri wachache siunaikumbuka issue ya police mwingine anayeitwa zombi alivyowafanya wale jamaa?
Reply
anna 04/02/2010 9:41am
Pole sana Jerry.Kama kweli umebambikizia,ninasema ama kweli serikali sasa haiaminiki labda tufe wote na wazaliwe wengine wapya.Inaniuma sana kweni msema kweli yeyote wa nchi hii huwa haishi jamani.Eeh mungu tusaidie
Reply
Singawakona Amiry 04/02/2010 11:12am
Yaani mpaka sasa siamini kama Jery anaweza kufanya kitu kama hicho, huwezi kunishawishi katika staili yoyote ile nikakubaliana nawee kuhusu mkubwa Jery.
Reply
Sion Lema 04/02/2010 11:45am
Mi naamini Mungu atamsaidia Kaka Jery mana amesingiziwa baada ya kufichua ukweli.watu wamekaa na kutunga kesi.na kwa nini hawakumpeleka kwa Taasis ta kuzuia Rushwa kwanza?mbinu za mapolisi.na bado waache waendelee wataachishwa kazi tubaki na waaminifu.
Reply
Kaka Jery pole.kumbuka kuwa kila muumini wa haki ni Adui wa shetani.hao wamepandwa na hasira baada ya kuumbuka.kwa hiyo hivyo ni visasi.wameshindwa kuwajibika,hawawezi kufichua wahalifu hadi raia wawatonye.hawana mbinu za kipelelezi ona walivyojiumbua.mara ngapi wamebambikia raia kesi?muone zombe leo,yuko wapi juma banatoz?je kubenea
Reply
na wengi wengineo wapo magerwzani kwa kubambikiwa kesi. hwaoni majambazi ambao wanaiba mbele ya vituo vyao? Katika mabenki mfano ujambazi wa NBC TMK? najinsi mapolisi wengi wanavyojihusisha na majambazi kiasi cha kuwakodisha silaha?NA WAKIJUA KUWA WANATAMBUANA UTASKIA OO TUMEUWA MAJAMBBAZI.Kwa nini wasikamatwe watoe ushahidi kwanza? kwakuwa watawachoma.
Reply
FLo 05/02/2010 10:57am
Bro Jerry, nakuombea Mungu akasimame akutetee, wabaya wote wakashindwe na kuabishwa! Mungu akutie nguvu na akakushindie!
Reply
Comments are closed. | LIVEsports links
Myp2p.eu Iraqgoals.net Rajangan.net LiveScoreHunter.com Scorepage.com LiveTv.ru xScores.com NowGoal.com Vieo CategoriesAll Video Archive
April 2011 |



