Raisi Kikwete alipoanguka Jukwaani Jangwani 21/08/2010
UPDATE 2: video imechomekwa upya. Asante ya dokezo "lapppt" (katika maoni yake @ Sun, 22 Aug 2010 6:43:27 pm) yaliyosababisha kupata video. video credit: mYnAMeiSnoNeOfUirbIZ UPDATE Nimepokea anwani pepe toka kwa mtu ambaye hajajitambulisha, yenye linki ambayo ina video iliyokuwa hapa awali. Kwa yeyote mwenye kuitaka, tafadhali tumia www.wetransfer.com kupakua video hiyo. Kwa sheria za wetransfer.com, video huhifadhiwa kwa siku 14 tu tangu siku ilipopakiwa na kisha hufutwa, video hii imepakiwa leo, hivyo ukichelewa kupakua, usirejee tena hapa na kuanza kulaumu. credit: Issa Michuzi CommentsMtanzania mkweli 21/08/2010 8:26pm
Nampa pole mgombea urais kwa kuanguka jukwaani nadhani dhamira pia imemsuta kwa ahadi za chama chake ambazo hakuzitekeleza na sasa anaogopa kudanganya tena.nadhani wajipange upya waje na sera ambazo wanajua wataziztekeleza ili ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania itimie.Utampaje Mtanzania ahadi mpya wakati bado hujatekeleza uloahaidi mwanzo? Viongozi wake alowapa mamlaka ndo wanampaka matope rais na kwa kuwa yeye ndo kiongozi dhamira yake imemsuta, Nampa pole achague sasa viongozi waadilifu na wachapakazi kkt baraza lake la mawaziri endapo atashinda urais.
Reply
msimbmo 21/08/2010 9:49pm
kwa nchi nyingine, Kikwete angekuwa hafai tena. Rais anayeanguka bila maelezo ya maana ni kwamba hafai.
Reply
Mgongofimbo 21/08/2010 9:59pm
Huyo ni Kanali wa jeshi aliyepitia chuo kikuu cha kijeshi Monduli anaangukaanguka ovyo! There must be something very wrong....wadanganyika amkeni!!
Reply
pcman 22/08/2010 12:54am
Reply
Mzawa 22/08/2010 1:09am
kwa nini mmetoa video ya kikwete alipoanguka? hata nyie kina michuzi na wenzio wote ni wanafiki tu. sioni sababu ya kuondoa video hiyo hata km kuna watu wamekwambieni mtoe. kwani kikwete yeye nani si binadamu km wanadamu wengine. kina Bushi walirushiwa viatu video zipo all ver mpaka leo, Federo cstro aliteleza akaanguka video mpaka leo tunaziangalia sasa nyie watanzania mnafanya big deal. mtaendelea kutaliwa mpaka yesu atakaporudi na kamwe maendeleo hamtoyapata kwa kuzidi kuwa na mentallity zenu za 19 kweusi.
Reply
Mdau, Bloomsbury 22/08/2010 2:27am
Wametoa kwa sababu mkono wa CCM mrefu. Wameshatishiwa. Shida ya waTanzania ndio hiyo sasa...wanatakiwa waone kuwa kama CCM wanaweza kuficha jambo kama hilo je yale yanayotokea bila watu kuona?
Reply
Juma 22/08/2010 5:52am
TURUDISHIE CLIP..YAANI NA WEWE SUBI USHAKUWA MWOGA..TATIZO NINI KWANI..SUbi ishi kama mtu ulioko na uishie marekani..pleaseeeeeeeeeee..Dont be a wolf in a sheep's clothing...
Reply
mpekenyuzi 22/08/2010 5:54am
sikupend tena dada yangu
Reply
Tafadhali, mnaonilaumu mimi kwa video kuondoka mnafanya kosa sana. Video imepakiwa YouTube na issamichuzi, mimi nime-copy code na kuibandika hapa, baadaye video imeondolewa huko YouTube, kwa maana hivyo code haitafanya kazi kwa kuwa hakuna video, sasa mimi niipate wapi na haipo YouTube? Ningekuwa nimeiondoa hata hii posti isingebaki hapa. Jaribu kuuliza na kujua kitu kinavyofanyika na si kulaumu na kuanza kushutumu kwa maneno ya kudhani na kutunga uongo mtupu.
Reply
Mkeleketwa 22/08/2010 8:43am
Wapakulie Subi maana hizo ndo zao.Wao ni kulaumu, kutunga, fitina, majungu na kudhaniana vibaya. Kwa mtindo huo ndugu zangu Watz hata tukifurukuta hatufiki popote.
Reply
mpekenyuzi 22/08/2010 8:55am
Dada shubi lakin haya ni makosa yako tena sana, watu wanaponakil kutoka sehemu huwa wanaandika "imenakiliwa toka ..." ama vyovyote utakavyopenda kuonyesha kwamba hiyo si kazi yako. hatukuiona hiyo ndio maana tukakulaumu wewe na kama tungekuwa tunasifia tungekubariki sifa za mwingine na ungelifurahia hilo.. nawatetea wenzangu kwamba hilo la kukulaumu si kosa letu
Reply
Mpekenyuzi upende kusema ukweli na kamwe uongo usiufanye hima yako. Hiyo video ilipowekwa hapo tangu mwanzo na hadi sasa, chini yake kuna maneno 'credit: Issa Michuzi' siku zote unaona ninaweka credit ya kazi kwa kila ninakoitoa, iwe picha, habari au video za taarifa toka kwa Kennedy Kimaro, leo unajifanya hujaiona? Acha uongo, nathubutu kusema huo ni uongo kwa kuwa credit ipo hapo na credit hupewa mhusika wa posti. Usinitafute visa visivyo na upekenyuzi wako huo.
Reply
mpekenyuzi 22/08/2010 9:13am
nimeliona, nimekubali hilo lilikuwa ni kosa langu la kutokupekenyua habar zako vizur sababu nilikuamin sana.. naomba mnisamehe kwa hilo wewe pamoja na ndugu wasomaji
Reply
Bongo Pix 22/08/2010 9:16am
Video yenyewe haipo tena, why? hilo ni tukio kama mengine, mmeogopa nini hata kuitoa?
Reply
@mpekenyuzi, adhabu yako nakucharaza viboko hapa hapa mbele ya kadamnasi ili nawe wakucheke, haya, geuka, lete nyama ya 'serekale', chwa chwa chwaaaa, haya, kichura chap chap elekea kwenye dawati na ole wako usimalize kusoma kitabu cha wavuti.com leo!
Reply
mpekenyuzi 22/08/2010 10:18am
Jaman ndugu zangu naomba hii video muitazame vizur kama na nyinyi mtagundua nilichogundua
Reply
wow 22/08/2010 4:42pm
Mtu kuanguka sio jambo la ajabu, kwanini mnapenda kukuza mambo? hata wewe unaweza kuangu kwabahati mbaya. Jiulize mara ngapi uliwahi kujikwaa ukanguka, huu ni mwili tufikirie kabla ya kusema. Mtu na kuanguka au kutokuanguka hakumfanyi mtu awe kiongozi bora hiyo ni falsafa ya wapi!
Reply
lapppt 22/08/2010 6:43pm
Nimeziona video leo bongoline.com.
Reply
Mdau 22/08/2010 7:30pm
"Inakuwaje Amiri Jeshi Mkuu, mtawala na mwanajeshi kitaaluma azidiwe na kudondoka mara kadhaa, halafu wasaidizi wake wanacheka cheka na kusema hakuna tatizo? Wanamdanganya yeye au wanatudanganya sisi?
Reply
Punda wa Pemba 23/08/2010 3:52pm
Msichanganyane Bureeeeeeeeee! Rais ni Muislamu na Usiku wa Kabla ya Tukio hakula DAKU hivyo ni vyanzo vya habari kutoka kwa MAMA Salma Kikwete First Lady Wetu ... Kwa mantiki hiyo alianguka kwa kuzidiwa na Njaa .. na ukitaka ushahidi alifikishwa ndani alipewa kinyaji cha nguvu akarejea kumalizia Usinduzi wa Kampeni hapo Jangwani....
Reply
Mgongofimbo 23/08/2010 8:18pm
Punda wa Pemba usitukebehi. Mimi nafunga Ramadhan kwa takriban miaka 20 sasa na ni mara nyingi nilipitiwa na usingizi sikula daku, sijawahi hata kupepesuka achilia mbali kuanguka. Ukianguka ni mgonjwa na siyo swaum. Pili, Rais kaanguka mara nyingi sana. Naamini tulizosikia au kuona kwenye vyombo vya habari ni chache tu kati ya nyingi. Hatumchukii wala kumtakia mabaya lakini uongozi wa nchi unahitaji afya bora. Kama afya yako mzozo kaa pembeni waachie wenzio...aliyesema viongozi wamekwisha nani??
Reply
Mpambe Kamuzu 25/08/2010 6:04pm
Kuanguka kwenye hutuba kuna sababu kuu tatu: 1)Unaumwa ugonjwa unaoathiri ubongo kama kifafa 2) ugonjwa unaoathiri shinikizo la damu kama magonjwa ya moyo au kisukari 3) mapepo, majini au majinamizi.
Reply
Comments are closed. | LIVEsports links
Myp2p.eu Iraqgoals.net Rajangan.net LiveScoreHunter.com Scorepage.com LiveTv.ru xScores.com NowGoal.com Vieo CategoriesAll Video Archive
April 2011 |



