Mtu usiingie katika mapambano halafu, kama mbuni ujitahidi kuficha kichwa pekee ndani ya shimo, kisha mwenyewe ujione upo salama il hali kiwiliwili chote kipo nje.
Vile vile, tusisahau kuwa mtu uingiapo vitani, adui yako humchagulii silaha atakayokupiga nayo.
Hivyo video hizi nimeziweka makusudi kwa wasiofahamu wazione, na kwa wale wanaozifahamu, basi "warudishe mapigo" kuielimisha jamii ikiwa kinachotamkwa ni upotofu. Yawezekana ukawa mwenye akili na mwepesi kung'amua "mpunga" na "chuya", lakini usisahau wengine huhitaji "kupeta" au "kuchekecha" ama "kutafuna" kwanza kabla ya kujua ipi kweli "pumba" na ipi ndiyo "chuya", ndivyo tunavyotofautiana kiakili.
Tusijisahaulishe kuwa tunawalalamikia wananchi ati wanawachagua viongozi wasiofaa na papo hapo hatuwaelimishi. Ikiwa mawazo yao ndiyo kama yaliyomo kwenye video hizi au ni wepesi kuamini ujumbe uliopo kwenye video hizi, bila kutizama video na kuyafahamu, tutaanza vipi kumwelimisha huyu mwananchi? Tutamhubiria? Mbona wanahubiriwa sana tu Makanisanina Misikitini lakini maovu yanaenelea? Mi nadhani ili kutoa elimu maridhawa, inampasa mwelimishaji ajue awazacho mtu ndiposa ajue namna ya kuchukuliana na kumwelimisha yule wanayetofautiana mtizamo. Hapo ndipo malumbano ya hoja yanapokuwa sawia. Haya mnayoyaona kwenye video ni muhtasari na uwakilishi wa mawazo yaliyotanda katika jamii.
Tusiwe waoga wa kufahamu habari tusizozipenda. Tusipende kukaa kwenye "comfort zote" na kutaka habari za kutufurahisha tu. Kufanya hivyo ni kupoteza fursa ya kumsoma mpinzani wako anavyokuharibia.
Changamoto
Ikiwa kweli wapo wanaokerwa na video hizi, ni hatua gani wanachukua nao "kuwafukunyua" wapinzani wao? Nachelea kusema, mbinu ya "zuia isionekane" na "jidai hatufahamu", hiyo ni mbinu iliyofeli.
Hizi ni siasa za tit-for-tat. Stepping into the ring, means you are ready for a fight. If you have the potential to attack and destroy me, so do I. Dare to show me what you've got and I'll show you what I've got.
