Matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC yanasikika moja kwa moja mtandaoni kutoka Dar Es Salaam. NI matangazo maalum ya uchaguzi mkuu wa Raisi, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani. Yatakuwa yanasikika kuanzia asubuhi saa moja hadi usiku saa tatu majira ya Afrika Mashariki.

Unaweza kufuatilia matangazo haya katika radio washirika nchini Tanzania ambazo ni Radio One (ukiwa Unguja tega 94.1 na ukiwa Pemba tega 93.5), Radio Free Africa na Kiss FM.
 


Comments

29/10/2010 11:12am

hongera bbc kwa kuona ipo haja ya kutupatia matangazo ya moja kwa moja ya uchaguzi mkuu wa tanzania.
mungu ibariki bbc

Reply
ali omar
29/10/2010 11:30am

wagombea wa vyama vya siasa tanzania, tupigeni kampeni za kistarabu tuache matusi kwani yanaweza kuvuruga amani ya nchi.
kampeni za matusi zimepitwa na wakati sasa tuko katika kushindana kwa nguvu za hoja na sio hoja za nguvu.
juu ya yote hayo wananchi ndio waamuzi wa serikali wanayoitaka.

Reply
Mhina Ombeni
31/10/2010 12:08pm

Watanzania wenzangu, hiki ni kipindi muhim sana, tuchague kiongozi bora na sio bora kiongozi. Mungu bariki watanzania , mungu ibariki Tanzania

Reply
Olivia
01/11/2010 11:56am

Hongera BBC, Tusaidieni kufichua wachakachuaji.

Reply
Msendo
01/11/2010 4:59pm

Tanzania tunahitaji mabadiliko,vijana tuna tunahitaji mabadiliko,tumechoka.. chama kimoja toka Uhuru mpaka sasa na ufisadi ndani nchi inaburuzwa bila mwongozo sahihi, tunapoteza rasilimali zetu na chanzo cha mikataba zeki na hisiyo na maslahi ya kwa watanzania imefanywa na viongozi wasio na upeo wa kifirwa bila kuangalia wala kujua maoni ya watanzania.. Tumechoka tunahitaji mabadiliko tumechokakaaaaaaaaaa

Reply
Musa Ngarango
01/11/2010 5:26pm

Mimi nimefurahi sana, kwani kupitia Internet nawapata moja kwa moja, hongera sana BBC kwa kutangaza Uchaguzi wa Tanzania! Mko Juu!
From Musa Ngarango -DSM TZ

Reply
Peter
01/11/2010 5:27pm

Tume ya Taifa ya uchaguzi iheshimu matakwa ya wapiga kura wa Tanzania. Nashauri kwamba kusiwe na uchakachuwaji katika utowaji wa matokeo, Mungu ibariki Tanzania!

Reply
lutfia
01/11/2010 7:58pm

jamani mimi kma mtanzania nasema tumechoka na nguo moja ya ccm tayar ishachakaaaaaaaaa sasa tunataka mpya ambayo ni CUF,INSHALLAH KILALALA KHER

Reply
Peter
02/11/2010 9:21am

Natarajia kuiona Zanzibar mpya yenye umoja wa kitaifa chini ya Serikali ya mseto, naamini kwamba Zanzibar itakuwa chachu ya mabadiliko kwa Taifa zima la Tanzania katika medani za siasa. Mungu Ibariki Zanzibar, Mungu Ibariki Tanzania.

Reply
02/11/2010 11:32am

Wao wana fedha sisi tuna MUNGU kwa Imani tumeshinda!HONGERA LEMA Ubunge Arusha-mjini,hiyo ndio people's power.CHADEMA JUU.

Reply
Kelvin Msuya
02/11/2010 1:23pm

jamani jamani jamani kawe kunani kawe?mbona hivi.......watu wapo nje siku tatu wanasubiri matokeo....

Reply
Moses M.Ruhomela
02/11/2010 5:23pm

Ndugu watanzania wenzangu tuungane kuhamasisha uzalendo ili waliochaguliwa wote watangulize maslahi ya Taifa mbele kuliko ufisadi. Pia Ninaumia saaaaaana ninapoona kila chama kina sare yake na rangi zake, Napenda Wagombea wawe wanavaa nguo zakawaida tu huku wafuasi wao wakipeperusha bendela ndogondogo za Taifa letu siyo sare.

Reply
Kinyogoli
02/11/2010 10:04pm

Eti nini? Wabunge watangulize maslahi ya nani mbele? Mnachekesha! Mafisadi wakubwa Tz ni wabunge, kama hamuamini maneno yangu subiri wakishaapishwa tu cha kwanza, kulalamika kuwa posho haitoshi na kudai waongezwe. Hapo hakuna mimi sijui nina uchungu sijui nini wote watadai nyongeza ya posho, maslahi yao kwanza. Kinachofuata ni mashangingi, utafikiri sio wale walokuwa wakibeza ambulance za vibajaji na kuahidi kuleta ambulance za ukweli.

Kwanza cha ajabu hata kazi hawajaanza, wengine ni wapya lakini utasikia wanadai maslahi zaidi, na hakuna tena ya kujidai kutetea maslahi ya wafanyakazi ambao wamewatumia ka tambara la deki.

Eti maslahi ya nchi? Kawadanganya nani? Kungekuwa na fujo? Hiyo ni ajira na hamuwaoni tena majimboni mpaka 2015.

Reply
mwalimumpole
03/11/2010 9:52am

WASIMAMIZI WATATU WA UCHAGUZI CHUNYA WAMEWEKWA NDANI KWA TUHUMA ZA UCHAKACHUAJI, HABARI KAMILI ZINAMTAJA AFISA ELIMU KILIMO BWANA MBULULE NA AFISA UKAGUZI NA MHUSIKA MWINGINE AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WAMEWEKWA NDANI TOKA JANA JIONI KWA TUHUMA ZA UCHAGUZI. INASADIKIWA MATOKEO YALIYOKUWA YANAPIKWA NA YALE YANAYOTOKA MAENEO AMBAYO MPINZANI WA CCM NDUNGU SUNDAY SANGA ANAKUBALIKA ZAIDI. HATIMA YA MATOKEO YA CHUNYA HAIJULIKANI.

Reply
kiepe
04/11/2010 2:33am

BBC NAOMBA MFICHUE MAOVU YANAYOTENDEKA TANZANIA DHIDI YA WAPINZANI, CHADEMA WADHULUMIWA HAKI YAO, NA SIO CHADEMA TU BALI NA WANANCHI WAMEDHULUMIWA PIA HAKIZAO, TUMESHA CHOSHWA NA UFISADI HAPA NCHINI, TUNATAKA MABADILIKO

Reply
Pampula
04/11/2010 2:39am

NEC HAWATENDI HAKI KWA WANANCHI, UTENDAJI WAO NI MBOVU SANA, WANANCHI HATUNA IMANI NA MATOKEO YA URAISI NA BAADHI YA MAJIMBO WALIOCHUKUA CCM, HAKI HAITENDEKI, CHA KUSHANGAZA NEC INACHAGULIWA NA CCM KUNA HAKI ITAKAYO TENDEKA KWELI??????

Reply
IS-HAKA MOHAMED RUBEA
04/11/2010 10:24am

Hongera Dk Shein kwa kuapishwa na hongera Maalim Seif kwa uvumilivu wako japo kuwa matokeo yalichezewa ulikubali matokeo kwa maslahi ya Wazanzibari wote.

Reply

Comments are closed.