Niliicheki hiyo mechi siku hiyo, binafsi nakubaliana na Eto'o kumpa kichwa huyo Cesar. Ujue alimpiga ngumi ya usoni kwanza, na ukiachilia hapo kila mtu alikua anamchezea rafu kwenye mechi ile...sasa kumpiga kichwa kama Zidanne alivyofanya kwa Materazi kiasi flani safi (Japo inam-cost Eto'o kwa kufungiwa mechi 3, na timu itapata pigo kwa kutokuwepo uwanjani kwa mechi hizo).
Yahitaji juhudi za ziada kupingana na hasira zako ukiwa uwanjani. Tunaamini Eto'o utajirekebisha, unahitajika uwe mchezaji bora wa dunia kwa kiwango chako unachokionesha sasahivi kwenye ligi ya Italy na UEFA Champions League...hivyo nidhamu itakuongezea kura za kuwa mchezaji bora wa dunia hizi punde.