Tumepiga kelele, jirani wanatubia Mlima Kilimanjaro, wanajisifia Serengeti wameiba Tingatinga, haya, baada ya kelele hizo yaelekea wamesema isiwe taabu, wanatizama vyao.

Utakubaliana nami baada ya kutizama video hii ya dk. 13 hasa dakika 4 za mwisho utakapoona vivutio vyote vikubwa vya asili vya nchini kenya vikoneshwa ndani ya dakika moja katika tangazo la kampuni ya simu ya SafariCom wakati wa maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo.

Kwa mwendo huu, hata ikiwa wameiga hapa na pale, sidhani kama hiyo inawaondolea sifa ya pongezi na sidhani kama uko ubaya katika kuiga na kuboresha chako. Hongera sana Wakenya.
 


Comments

Kenny
13/11/2010 7:36pm

Hakika, nimetazama video hii, Kenya walituacha mbali muda mrefu. Hata shirika lao la ndege-Kenya Airways lina nguvu wameungana na KLM au British Airways. Tanzania tuna vivutio vingi kuzidi nchi yoyote duniani lakini....!

Reply
Vumbi
13/11/2010 8:30pm

Hongera jirani, unatuonyesha tunasafari ndefu ilituweze kukufikia. Ila tunashukuru kwa changamoto ninaimani zitatusaidi kubadilika.Tanzani tunatatizo la elimu, elimu yetu haina kiwango cha kukabilana na hali ya ushindani uliopo dunia kwa sasa. Pia idadi ya watanzania waliopata elimu ya juu ni wachache sana. Lazima taifa likubali kuwekeza kwenye elimu vinginevyo tutabaki nyuma sana.

Reply
Mfuko
14/11/2010 5:05am

Tz tunahitaji watu makini zaidi kwenye sera ya utalii,na utangazaji wa vivutio vyetu pia tic iwabane wawekezaji kwenye matangazo yao ya biashara yazingatie mandhari ya kitanzania zaidi na si nje .sioni kitu kwenye hili tangazo ambacho watz hatuwezi au hatuna.

Reply

Comments are closed.