Video ya Kwanza ya sehemu ya Utangulizi, inapatikana Youtube, haijawekwa hapa kwa kuwa sauti haisikiki hivyo nimeweka sahemu ya Pili - Mawaziri na Manaibu wa Wizara wakitangazwa ambayo sauti inasikika.
credit : Mwanakijiji
 


Comments

Msuya
24/11/2010 1:33pm

Ninamsifu Rais Kwa baraza jipya la mawaziri hususani wizara ya Ujenzi pamoja na wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi

Reply
24/11/2010 2:47pm

mie mwenyewe na mpa big up mheshimiwa kwa kumrudisha MAGUFULI ujenzi.safi sana jamaa anafanyakazi na anadata za kuaminikika si mbabaishaji

Reply
mambo mambo
24/11/2010 3:10pm

kwa kweli Rais amejitahidi kuteua baraza la mawariri, lakini issue ya kumuacha aliyekuwa Waziri wa afya na ustawi wa jamii naona amepoteza hazina ya mtu mchapakazi. au waungwana mwaonaje hapo?

Reply
24/11/2010 3:18pm

Napenda kutoa pongez zangu kubwa kwa Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa na ngumu aliyokamilisha ya kulitengeneza baraza la mawaziri.Sina shaka na uteuzi huo,naamini kabisa wale wote waliopewa nafasi hizo watazifanyia kazi kwa maendeeo ya Tanzania wote.Hongear sana ila nikuombe uangalie pia nafasi ya Mratibu wa huduma ya viungo bandia katika ngazi ya wizara,nadhani tunahitaji kuwa na mwakilshi ,kwani huduma hiyo hapa nchini imekuwa ikitolewa tu bila ya unagalizi.Niwatakie wote kazi njema na umoja kamili

Reply
KADA
24/11/2010 4:06pm

Hongera sana Rais wetu Kikwete umefanya kazi nzuri sana. Wapinzani sasa tufanye kazi karibuni kushirikiana nasi

Reply
MAKUNGU
24/11/2010 4:42pm

Hongera JK kwa kumchagua Dk. Mwakyembe ili naye apambane na changamoto

Reply
Mwl. Ezekiah T. Oluoch
24/11/2010 4:49pm

Nawapongeza wote waliochaguliwa na Mheshimiwa Rais amefanya kile alichoweza isipokuwa Mheshimiwa Shukuru Kawambwa hatakabiliana na changamoto za elimu nchini, Mheshimiwa Hawa Ghasia ataendelea kumwangusha Mheshimiwa Rais kama alivyofanya kwa miaka mitano iliyopita. Matumaini yangu makubwa yako kwa Kaptain Mkuchika kwa kuwa atasaidiwa na Kassim Majaliwa kuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia Elimu. Kama Majaliwa hatawageuka walimu waliomlea toka amekuwa kiongozi wa Chama cha Walimu Tanzania hadi alipokuwa Mkuu wa Mkoa, walimu wa nchi hii watasonga mbele. Kama Mheshimiwa Mkuchika atakuwa msikivu kwa wafanyakazi bila ya kuleta ubabe, atakuwa Waziri atakayekuwa na mafanikio makubwa.
Nawatakia kila la heri katika kazi zao, tunahitaji tija na uwazi katika utendaji wa serikali na kuwatatulia watumishi wa umma kero zao ili watoe huduma inayokidhi mahitaji ya watanzania

Reply
Ery
24/11/2010 5:52pm

Kwaweli safari hii Rais amesikia kilio cha wananchi Baraza zuri sana;waheshimiwa Magifuli,Nahodha,Sitta Huseni mwinyi pamoja wengine wote kwa ujumla wake bila shaka wamewekwa mahali pake. Naona sasa kazi itafanyika namatumaini yanaanza kurudi. Big sana JK);

Reply
i
24/11/2010 6:02pm

kwa watu kama magufuli,mwakyembe, samweli sita,na wengine wachache wanafaa lakini wengine wote fiki kama vile ngeleja hakuka jipya,hawezi kazi hakuna alichokifanya zaidi ya ubinafsishaji ambao unanufaisha makaburu ambao wanabeba hadi mchanga.hata Rick,cuf,zaker osward wanalijua hilo.

Reply
sam
24/11/2010 6:07pm

soma hapo juu,i know utakubaliana na mimi.na kama ccm hamtaki kuchakachua sana so that next election msiloose kabisa attend to your promis mr president na watu wako.ila kama utafanya changes samweli sita mpe nafasi ya waziri wa sheria na katiba na ngeleja umpoteze kwa rasilimali endelevu kama vule madini.

Reply
Yusufu R.Masai
24/11/2010 6:14pm

Hakika Baraza jipya la mawaziri ni la kimapinduzi sana.Ukweli ni kwamba kuwa na vijana wengikatika uwaziri siyo mwarobaini kwa maswahibu yetu vijana.

Muda mwingi watatumia kujijengea majina na zaidi kujifunza wakati taabu zetu hazina subira.

Reply
ROBERT K.GEORGE
24/11/2010 7:42pm

NAMPONGEZA MH.RAIS KWA KUMALIZA KAZI YA UTEUZI WA MAWAZIRI ILA BAADHI WALIORUDI HAWANA JIPYA LA KUWAPA WATANZANIA KAMA MH. NGELEJA HANA JIPYA ZAIDI YA KUJINUFAISHA KWA UBINAFSISHAJI WA MALI ZA WATANZANIA KWA MAKABURU AMBAO HAWAWALETEI WATANZANIA MAENDELEO YOYOTE BALI KUWANYONYA KWENYE UDONGO WAO.

Reply
Dizo
24/11/2010 8:16pm

Madini=o%
Barabara 101%

Reply
kimera
24/11/2010 10:36pm

Nakupongeza sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg Jakaya M. Kikwete kwa kuunda Baraza nzuri la Mawaziri. Kwa baraza hili tunategemea maendeleo mazuri hasa barabara. Ushindo wa kishindo mwaka 2015. "kazi nzuri".

Reply
james godfrey
24/11/2010 11:22pm

nasifu muheshimiwa rais kwa kutangaza baraza la mawaziri makini waliojaa na hekima katika jamii. mungu amzidishie maisha mema na majukumu yake ya kuliongoza taifa letu

Reply
masangu LAMECK
24/11/2010 11:28pm

hilo ni baraza zuri sana! hongera sana rafikiyangu

Reply
ELIAS
24/11/2010 11:31pm

hongera sitta na magufuri najua mtashirikiana na rais kuleta maendeleo kwa watanzania! sina shaka na nyinyi eeeeeeti

Reply
mc
25/11/2010 6:17am

Na mshukuru sana muheshimiwa JK. ktk kumuweka magufuli kwenye hiyo nafasi na nina uhakika kazi itafanyika katika nafasi yake bila shaka wapenda wote waliko katika nafasi zao wasimamie kazi pasipo kuchekana katika kujenga taifa letu ili kusonga mbele daima. wote tushughulike katika kujenga mazingira safi ya taifa letu pasipo kuangalia upinzani wa vyama bali tukumbuke sisi sote ni watanzania na ni ndugu. USHIRIKIANO DAIMA, KAZI BORA, FIKIRIENI MAENDELEO YA NCHI, HAKI SAWA, UMASKINI TUUFUKUZE.

Reply
mukobo
25/11/2010 9:27pm

Dk Magufuli,anza kwa kasi ya ajabu kwanza kabisa foleni za barabarani dar kwa kujenga barabara zote za pembezoni ili zitumike hasa hii ya tegeta kupitia mpiji magoe hadi kibamba/mbezi luisi,
Pili,ondoa bumps zote zinazosababisha foleni hasa ile ya kimara over halifai kwani ungekuwepo wewe muda huo lisingewekwa pale...Hongera sana Mh Rais kwa kumpa hiyo nafasi Dr.Magufuli na Dr.Mwakyembe.

Reply
BETH KAANAEL
26/11/2010 8:46am

Hongera sna raisi Jakaya Mrisho kwa kuwaweka mawaziri makini kama Magufuli na Sitta kwenye wizara muhimu. Be blessed.

Reply

Comments are closed.