wavuti
 
Nimefurahishwa na hatua hii ambayo kwa namna fulani, pengine itatia msukumo na kuchangia katika kuhimiza uangalifu kwa wamiliki wa vyombo vya safari na waendeshaji vyombo kuwa makini na kujali uhai wa binadamu.

Mwandishi Richard Konga kutoka Arusha anairipotia Majira.co.tz kuwa Kampuni ya kutetea wasafiri yaanzishwa. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Haki za Wasafiri na ajali Bw. Godson Kirita amesema ameanzisha kampuni hiyo ili kutetea haki ya wasafiri wa ndani na nje ya nchi mara wapatapo ajali na wakati huo kukosa chombo cha kuwatetea. Akizungumza na Majira Bw. Kirita alisema ajali zinazotokea mara kwa mara husababisha familia nyingi kuwa yatima na wajane na wengi wao kuwa na vilema vya maisha hivyo kuwa mzigo kwa jamii, pia husababisha ongezeko la watoto wa mitaani. Akitoa mifano ya ajali zilizotokea hivi karibuni katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Bw. Kirita alisema ajali hizo zimepoteza maisha ya watu wengi wasio na hatia ambao, ndio nguvu kazi ya Taifa, wakati huo huo hakuna chombo kinachojishughulisha kuwatetea watu hao ili kupata haki zao. Alisema amekuwa akifarijika na jitihada za serikali katika kushughulikia masuala ya usafirishaji wa abiria lakini amesikitishwa na madereva wazembe wasiotekeleza, maagizo ya serikali hususani juu ya mwendo kasi wa magari yao na kuiomba serikali kurekebisha sheria ya usalama barabarani. Wananchi wakiwemo wafanyabiashara wameonesha kufurahishwa na chombo hicho walichokiita mkombozi wa usafiri wakati wa majanga ya ajali na kwamba kitawasaidia kutetea haki zao.
 
 
Picture
Timu ya Simba Sports Club leo imefanikiwa kuendeleza dozi zake kwa kuifunga Toto Afrika katika uwanja wao wa nyumbani goli 2 kwa nunge. Hadi kipindi cha kwanza kinakwisha, timu zote zilikwenda mapumziko kwa suluhu ya kutokufungana. Kipindi cha pili dakika ya tano, Mussa Hassan 'Mgosi' alifungua darasa la magoli akifuatiwa na Ramadhani Chombo 'Redondo' aliyefunga kitabu cha magoli dakika nne baadaye. Hadi mwisho wa mtanange huo, Simba 2 Toto Afrika 0.

Hongera Simba kwa kuondoa aibu ya mwaka jana kwa kufanya malipizi ya aina yake kwa mwaka huu!

Na katika mechi zilizochezwa kwingineko duniani,
Mshindi wa kombe la mpira wa miguu kwa Mataifa ya Afrika amekuwa Misri baada ya kuitandika Ghana bao moja ambalo lilifungwa dakika ya 85. Hivyo hadi mwisho wa mechi, Misri 1 Ghana 0. Nchi ya Misri inaweka rekodi ya kuwa nchi iliyonyakua kombe hilo mara nyingi zaidi kuliko nchi nyingine yoyote.
Na kisha huko Uingereza matokeo ni Manchester United 3 Arsenal 1.

 
 
Patrick Lusato of Tanzania won the Nagpur International Marathon, which was held on Sunday to mark the death anniversary of Mahatma Gandhi. Patrick crossed the finish line with a timing of 2:13:06 to win the title plus a prize money of Rupees 1.25 lakh in the Full Marathon. Oswald Kahanuzi of Tanzania, came in second with a timing of 2:13:07, winning a prize of Rupees 2.25 lakh. Benson Yator of Kenya clocked 2:13:54 to win the third spot and a prize money of Rupees 2 lakh.

Helen Musyoka of Kenya won the Half Marathon for women, clocking 1:11:27 and winning Rupees 1.50 lakh in prize money. Restituta Kemi of Tanzania came in second (1:12:39, Rupees 1.25 lakh) and Dehninet Jara of Ethiopia third (1:13:00, Rupees 1 lakh).

Nearly one lakh runners took part in the marathon in various events, which included the full marathon, half marathon, 12 kilometres for boys, 10 kilometres for girls, 5 kilometres for boys under 18, 3 kilometres for girls under 18, besides an event for wheelchairs. The 'Ahimsa Daud' (The Run for Non-Violence) attracted thousands of entries and saw enthusiastic participation from the residents of the second capital from all walks of life. The events were flagged off by former India cricketer Mohammed Azharuddin, Maharashtra ministers R R Patil, Anil Deshmukh and Suresh Shetty, besides Mayor Archana Dehankar. Bollywood stars Arshad Warsi and Vidya Balan were among the guests for the concluding and prize distribution ceremonies.

Source: news.webindia123.com
 
 
A vaccine to protect HIV patients from contracting tuberculosis (TB) and ultimately dying of it has finally become a reality.   After a seven-year-long trial in Africa, scientists have for the first time developed a vaccine that was succesful in reducing the rate of definite TB infection by almost 39% among 2,000 HIV-infected patients in Tanzania. TB is the biggest killer of HIV-infected patients in the world.

Scientists from Dartmouth Medical School (DMS) have reported results of their clinical trial of this new vaccine against TB -- Mycobacterium vaccae (MV) -- in the January 29 online issue of the journal AIDS. The study will be published in the March print issue of the journal. Principal investigator Ford von Reyn from DMS said, "Since development of a new vaccine against TB is a major international health priority, especially for patients with HIV infection, we and our Tanzanian collaborators are very encouraged by the results of the study." The vaccine is a type known as an inactivated, whole-cell mycobacterial vaccine and is expected to be economical to produce and distribute. Von Reyn described the trial as a "significant milestone -- the first to demonstrate that any type of vaccine can prevent an infectious complication of HIV in adults". He added that the next steps are to improve the manufacturing methods to support the production of the larger quantities of the TB vaccine needed for further studies and subsequent clinical use.

Since newly-infected HIV patients risk contracting TB almost immediately, investigators are targeting a strategy for immunization with MV before patients need to start taking antiretroviral drugs. The scientific team at Dartmouth began Phase-I human studies with MV in the United States in 1994 and demonstrated that a multiple-dose series of MV was safe in both healthy subjects and patients with HIV infection. The group then conducted Phase-II studies in larger groups of adults in Zambia and in Finland. In the Zambian trial, researchers found that MV boosted immune responses against TB that had first been primed in childhood with the current TB vaccine, BCG. Subsequently, the DarDar group received NIH funding to conduct the large Phase-III efficacy trial among HIV-infected patients with prior BCG immunization in Tanzania.

HIV patients are particularly vulnerable to TB because their immune systems are compromised. The vaccine works by boosting the immune responses of patients who have already been given the BCG vaccine earlier in life. 

Read all of this story at: timesofindia.indiatimes.com
 
 
You need to do it more often. Updating your drives makes your computer perform at an ultimate level, it also helps keeping away bad-wares from taking advantage of your old system. Some manufactures protects their drives and software products from threats by releasing updates that you need to install in your computer. We often forget to do that but there is a simplified way.
Picture
Device Doctor is a FREE Windows application that scans your computer hardware and checks to see if there are new driver updates available for your devices. It also locates drivers for "unidentified devices" in the Windows Device Manager.

Just click on 'Begin Scan' to detect your hardware; Device Doctor queries manufacturer driver database and immediately fetches the correct driver files for your computer.

System Requirements:  Windows XP, Vista, 7 (64-bit or 32-bit) and 10 MB Hard Drive Space.

Download Device Doctor Free Driver Updater version 1.0:
- Installation Download HERE (4.6 MB)
- Standalone/Portable Download HERE (carry it in flash drive, use it on multiple computers, no installation)

Website: www.devicedoctor.com

 
 
Have you ever liked a song so much that no matter how many times you listen to it, you seem to never get over it? Yeah, that cool, almost refreshing feeling is what I am talking about. It's what I have with one of Celine Dion's songs. A song she performed at the Opening Ceremony of the 1996 Olympic Games (Atlanta, Ga, USA). It is absolutely one of my favorite songs ever. Each time I read the lyrics of this song, I get overcome with emotions - incredibly powerful (?song ?emotion ?lyrics). We are human beings, right? and human beings have emotions, right? and sometimes we fall victims of our own feelings and emotions, right? please excuse my insanity. Ladies and Gentlemen, the one and only singing bird of a time, Celine Dion:
Deep within each heart, There lies a magic spark
That lights the fire of our imagination,  And since the dawn of man
The strength of just "I can", Has brought together people of all nations
There’s nothing ordinary, In the living of each day
There’s a special part, Every one of us will play

Feel the flame forever burn, Teaching lessons we must learn
To bring us closer to the power of the dream, As the world gives us its best
To stand apart from all the rest, It is the power of the dream that brings us here

Your mind will take you far, The rest is just pure heart
You’ll find your fate is all your own creation, Every boy and girl
As they come into this world, They bring the gift of hope and inspiration

Feel the flame forever burn, Teaching lessons we must learn
To bring us closer to the power of the dream, The world unites in hope and peace
We pray that it will always be, It is the power of the dream that brings us here

There’s so much strength in all of us, Every woman child and man
It’s the moment that you think you can’t, You’ll discover that you can

Feel the flame forever burn, Teaching lessons we must learn
To bring us closer to the power of the dream, The world unites in hope and peace
We pray that it will always be, It is the power of the dream that brings us here

Feel the flame forever burn, Teaching lessons we must learn
To bring us closer to the power of the dream, The world unites in hope and peace
We pray that it will always be, It is the power of the dream that brings us here

The power of the dream, The faith in things unseen
The courage to embrace your fear, No matter where you are
To reach for your own star, To realize the power of the dream

Written By: David Foster, Babyface
Lyrics By: L. Thompson
Produced And Arranged By: David Foster for Chartmaker Inc.
Co-Produced By: Kenny "Babyface" Edmonds
Published By: One Four Three Music, admin. by Peermusic Ltd./Sony/ATV Songs LLC/ECAF Music/Warner-Tamerlane Publishing Corp. o/b/o Brandon Brody Music (BMI)
 
 
Nakumbuka ni jana tu hapa niliandika habari ya 'penye miti hakuna wajenzi' kuhusiana na Waingereza kuchukua hatua ya kutufundisha michezo yetu wenyewe ili kutusaidia kuiweka katika hadhi na ngazi ya Kimataifa zaidi.  Leo nimesoma habari katika tovuti ya BBC inayohusu jirani zetu wa Kenya kuwa wamechukua michoro ya tingatinga na kiweka katika kiwango cha zaidi ya mchoro tu.
Picture
bofya picha kutizama video
Hivi sasa wenzetu hao si kuwa wanachora kwa ajili ya kuuza na kujipatia kipato, bali wanaitengenezea michezo ya katuni zinazoonekana katika runinga. Wamepiga hatua na kuwakilisha kazi zao katika mashirika makubwa ya utangazaji na sanaa hii kama vile shirika la Taifa la Utangazaji la nchini Uingereza (BBC) na kampuni kongwe katika sanaa ya katuni ya Disney.

Hatua waliyoipiga si ndogo kwani yahitaji utaalamu na umakinifu katika uchoraji na utengenezaji picha kuwa katika uhalisia. Nilichojiuliza ni, ikiwa majirani zetu hawa wameona na wamejaribu na wanaweza,
je! sisi tulio asili na chimbuko la michoro ya Tinga Tinga, chatushindani?

Ama kweli penye miti wajenzi hamna'ga. Ndiyo yale yale, Mlima Kilimanjaro upo Tanzania, wanaofaidi Wakenya, siye tuendelee kulalamika, 'oh ni wetu, ni wetu', 'waongo, waongo'. Sawa ni wetu, halafu? Yaani ukisha kuwa wenu ndo' basi yatosha?

 
 
Picture
Twit a file. TwitLoad is a free file hosting and sharing site made specifically for Twitter. All you have to do is login with your Twitter account, upload a file and share it with twipple in twiland via a status update. Head on to www.twittload.com and twit your file.

 
 
Nasema hivi baada ya kusoma habari iliyoandikwa katika kazeti la Majira (isome hapo chini) kuhusiana na Wageni kuona tukizembea katika michezo ambayo wao wanaona ingeendelezwa huenda ingewatoa watu kimasomaso. Ninapokubaliana na kauli ya wahenga kuwa penye miti hakuna wajenzi ninamaanisha kuwa, vyote vya thamani vya asili na vya kiutamaduni hatujajua bado kuvitumia kwa faida ya sote hadi aje mgeni atuoneshe umuhimu wake.

Nilishangaa zaidi wakati fulani nilipopata safari ya kutembelea miji ya Pwani na Visiwani Zanzibar kuona majengo yakiporomoshwa ati kupisha ujenzi mpya tofauti na nilichokiona wakati fulani mjini Roma nchini Italia ambapo wenzetu hao wanakarabati vyao vya zamani. Katika nchi hiyo watu wengi wamejipatia ajira binafsi baada ya kusoma masuala ha hisroria na miji ya kale katika nchi yao na hivyo kuwa waongozi wa watalii. Sisi badala ya kuiga mazuri wanayoyafanya wao na kusababisha ajira kwa wahitimu wetu, tunabomoa na kukazana kujenga wenyewe twaita, 'kisasa' na bado 'ukisasa' wenyewe si hili wala lile bali kila siku kusikia habari za kuanguka majengo yanayojengwa mapya ama yale ya kale, na hata yakajeruhi ama kuua.

"Waingereza waanza kutoa kozi ya mdako, kombolela" - Adolph Bruno, majira.co.tz

Walimu wa Shule za Msingi sita za Wilaya ya Temeke, juzi walianza kupata kozi ya siku nne inayotolewa na shirika la michezo la Uingereza la Uk Sports Inter, kwa ajili ya kuwapa ujuzi wa kuwafundisha watoto michezo shuleni ambayo inafanyika katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Shule zinazoshiriki kozi hiyo ni Mgulani, Mtoni, Shalom, Muungano, Kibasila na Yemeni ambapo michezo inayoibulia ni pamoja na kuvuta kamba, mdako, kukimbia na vijiti, kombolela na kukimbia kwa magunia.

Akizungumza Dar es Salaam jana Ofisa Habari wa Shirika hilo kanda ya Dar es salaam, Mohamed Mvumbagu alisema kozi hiyo ni miongoni mwa kozi zinazoendeshwa na shirika hilo kwa lengo la kukuza michezo isiyo ya gharama shuleni. "Kama ilivyo kawaida tumeanza jana (juzi), kutoa mafunzo ikiwa hii ni mara ya pili, tangu tulipotoa katika shule ya Chang'ombe na tuliweza kufanya vizuri kwa kufaulisha walimu wengi, ambao sasa wataendeleza mafunzo hayo shuleni," alisema Mvumbagu.

Alisema kozi hiyo itamalizika keshokutwa ambayo itafungwa kwa bonanza kubwa litakalofanyika katika Uwanja wa uhuru, Dar es Salaam litakalowezesha kujua jinsi mafunzo yalivyopokelewa na walimu hao.
 
 
Tumaini Makene analiripotia gazeti la Majira kuwa:

MUSWADA wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya mwaka 2009, umedaiwa kushindwa kugusa maslahi wala kuonesha thamani ya wauguzi hasa kwa kuangalia kazi ngumu na mzigo mkubwa walionao na mazingira magumu na hatarishi wanayofanyia kazi.
 
Hayo yalidhihirika jana katika Kikao cha Pili cha Mkutano wa 18 wa Bunge, ambapo wengi waliochangia walikuwa wakitilia mkazo suala la maslahi ya wafanyakazi waliko katika sekta hiyo nchini.
 
Kutokana na michango ya wabunge hao, serikali imeshauriwa kuhakikisha kuwa mswada huo unawathamini wakunga na wauguzi nchini, walioko katika sekta ya umma na binafsi, kwa kuongeza mishahara yao, kuwapatia posho za mazingira magumu ya kazi na posho za kufanya kazi hatarishi.
 
Akiwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani Bungeni juu ya muswada huo, Msemaji Mkuu wa kambi hiyo katika masuala ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Ali Tarab Ali alisema kuwa, muswada huo hauoneshi kifungu chochote ambacho kinatoa motisha kwa Wauguzi na Wakunga katika utendaji kazi wao.
 
"Hali halisi ya tasnia ya afya inaendeshwa na fani ya uuguzi na ukunga, lakini jambo ambalo mpaka sasa Serikali bado haijaligundua au imeligundua lakini inashindwa kulitekeleza ni mazingira ya kazi na maslahi duni kwa wanataaluma wa fani hii. Jambo hili limekuwa ndicho kikwazo kikubwa cha adui namba mbili wa nchi hii (maradhi) anaondoka.
 
"Mh. Naibu Spika muswada huu hauoneshi kifungu chochote ambacho kinatoa motisha kwa Wauguzi na Wakunga badala yake umesheheni vifungu vya kuwadhibiti Wauguzi na Wakunga katika utendaji kazi wao.

Kambi ya upinzani inaona pamoja na nia nzuri ya Serikali tunayoambiwa, lakini jambo hili litazidisha uhaba na upungufu wa wataalamu katika fani hii, jambo ambalo ni hatari katika mustakabali wa nchi yetu, kumbuka
kuwa hata kama tutakuwa na madaktari wengi kiasi gani bila Wauguzi bado hatujafanya kitu," alisema Bw. Tarab.
 
Akichangia muswada huo ambao uliwasilishwa bungeni jana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Bi. Aisha Kigoda, Mbunge wa Mji Mkongwe (CUF), Bw. Ibrahim Muhammad Mnyaa alisema kuwa muswada huo badala ya kuonesha kuwajali watu wanaofanya kazi ngumu za Uuguzi na Ukunga na kuthamini kazi zao, umejaa vitisho vya adhabu na kuwaonya katika jambo moja na jingine.
 
"Mswada haungalii thamani ya Wauguzi, hakuna priviledges zozote, unaongelea adhabu tu, hakuna risk allowance, hakuna hardships allowances, watu hawa hawalipwi mafao kulingana kwa mujibu wa taaluma, hii siyo sawa, maana kama wachache tulionao hatuwaridhishi halafu wakati huo huo tunaambiwa kuwa kuna maombi mengi yanawahitaji kutoka nje sijui tunafanya nini," alisema Bw. Mnyaa.
 
Hali hiyo pia iliwagusa Wabunge wengine waliochangia mswada huo wakitanguliwa na Profesa Idrisa Mtulia (Rufiji, CCM), George Lubeleje (Mpwapwa, CCM), Job Ndugai (Kongwa, CCM), Jenista Mhagama (Peramiho, CCM), Anna Lupembe (Viti Maalumu, CCM) na Pindi Chana (Viti Maalumu, CCM).
 
Mapema akiwasilisha muswada huo, Bi. Kigoda alisema kuwa muswada huo umekusudia kutungwa Sheria ya Uuguzi na Ukunga ambayo itainua na kudhibiti huduma za uuguzi na ukunga.
 
"Kutokana na mtazamo huo, muswada huu unakusudia kuifanya taaluma kutambulika kuwa taaluma muhimu katika jamii ambayo inahitajika kupatiwa nguvu ya kisheria ili kusaidia utekelezaji wa majukumu yake," alisema Bi. Kigoda.