Profesa David Mwakyusa akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya bi Blandina Nyoni na Mganga Mkuu Kiongozi katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya NMR aliyoizindua leo. Wajumbe wa bodi hiyo mpya ni pamoja na Mbunge wa Mbozi Magharibi Dk. Luka Siyame, Dk. Hassan Mshinda, Dk. Edith Ngirwamungu, Jonathan Tangwa, Dk. Alaick Abdallah Juma, Profesa Eligius Lyamuya, Dk. Catherine Kuwite, Bi. Elli Pallangyo, Elisa Mjema, Dk. Salim Mohamed Abdullah na Dk. Mwele Malecela, ambaye ndiye Katibu wa bodi. NIMR ni kifupi cha National Institute for Medical Research (Taasisi ya Taifa ya Utafiti katika Tiba) (Picha kwa hisani ya blogu ya John Bukuku - Full Shangwe) Add Comment Pichani ni mwanamuziki mkongwe wa muziki Bi Kidude akiwa na mwanamuziki Babu Ayoub, wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu onesho lao la kupambana kwa sauti 'Mtanange wa Masauti' litakalofanyika kwenye Ukumbi wa hoteli ya Travertine iliyopo Magomeni. Mpambano huo utafanyika siku ya Jumapili na utasindikizwa na kundi la Taarab la Jahazi. Picha na taarifa kwa hisani ya blogu ya Sufiani Eti nini? Una... 26/02/2010
Have you ever wondered how the world of technology will be transformed with gadgets and devices in say - ten years from now? me too. Just at the end of 2009 we were wondering if there is still anything let to discover. Probably we do not call it a discovery anymore, but an invention. A world of tech and invention where people invent instead of discover. Currently, somebody has invented a roll-on laptop. Click on the photos below to see this concept laptop and watch the video (1:30 min) by clicking here. ![]() David Mathayo David Gazeti la Nipashe linaripoti kuwa baadhi ya Mawaziri, Naibu Mawaziri na Wabunge wanaodaiwa kuwa mafisadi wa elimu, hawajapeleka vyeti vyao katika Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kwa ajili ya uhakiki. Mkurugenzi Mtendaji wa TCU, Profesa Mayunga Nkunya, alisema hadi jana ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dk. David Mathayo David, ndiye aliyekuwa amewasilisha vyeti vyake ambavyo vimethibitisha kuwa ana fani alizosomea. Naye mwanaharakati Kainerugaba Msemakweli amesema hujuma dhidi ya harakati za kupambana na ‘ufisadi wa elimu nchini’, unaodaiwa kufanywa na baadhi ya vigogo nchini, zimepamba moto, baada ya mpango wake wa kuanika zaidi kashfa hiyo kupitia mabango kukwamishwa. “Nimehujumiwa. Maana tarehe 18 (mwezi huu) watu wanne walikwenda kampuni ya mabango na kuwatisha kuwa wakikubali niweke mabango watachunguzwa kodi zao na mabango na wamejenga kwenye hifadhi za barabara. Naandaa kuwafungulia kesi kwa kuvunja mkataba na mimi”. Mabango hayo ilikuwa yawekwe katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na kwenye majimbo yanayowakilishwa na wanasiasa hao, ikiwa ni hatua ya tatu ya mapambano aliyoyaanzisha dhidi ya ufisadi wa elimu nchini. Jijini Dar es Salaam yangewekwa katika daraja la Salender, Jangwani, makutano ya barabara za Nyerere na Kawawa na Barabara ya Kilwa karibu na bandarini. Kabla ya hujuma dhidi ya mabango hayo, Msemakweli alilalamikia kufanyiwa hujuma vitabu alivyochapisha vinavyoelezea kashfa ya vigogo hao jijini Dar es Salaam na mkoani Mwanza, ambapo mtu mmoja alionekana akinunua nakala zaidi ya 600 kwa mkupuo mmoja bila kujulikana anakozipeleka. Kwa habari kamili, jisomee gazeti tando la NIPASHE kwa kubofya hapa CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA UINGEREZA SHEREHE YA KUZALIWA KWA Chama Cha Mapinduzi (CCM) MIAKA 33 YA CCM Wanachama Wote - C C M Wakereketwa Wote - C C M Wapenzi Na Wana-Mapinduzi Wote Tarehe: 06/03/2010 Saa: 10 jioni Hadi Saa 5 usiku WAPI: UKUMBI WA: THE WAREHOUSE 1 CUMBERLAND ROAD READING RG1 3LB Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara: Mhe Pius Msekwa Watanzania ambao wangependa kujiandikisha, mnaombwa kuleta picha zenu za passport size mbili na paundi kumi na tano (paundi tatu kwa kadi, halafu paundi kumi na mbili kwa ada ya uanachama ya mwaka mzima). Kwa ufafanuzi zaidi, tafadhali wasiliana na: Moses Katega - 07727475313 Victor Mgoya – 07501083328 Maira Migire – 07799212095 Wote Mnakaribishwa – Kutakuwa na Vinywaji, Vitafunio, na Muziki Baada ya Shughuli Zote. Kiingilio – BURE!!! ![]() Hasheem Thabeet Habari zilizoandikwa hivi karibuni mtandaoni kumhusu Mtanzania mwenzetu, kijana Hasheem Thabiti ambaye ni Mtanzania wa kwanza kucheza mchezo wa kulipwa wa mpira wa mikono katika ligi ya nchini Marekani maafuru kama NBA, si za kufurahisha. Hasheem alinyakuliwa katika naasi ya pili 'Pick Number 2' na timu ya Memphis Grizzlies kwa ajili ya msimu wa NBA 2010. Habari zilizoripotiwa na kuandikwa katika mtandao wa Yahoo! na mitandao mingine zinasema kuwa Hasheem ameshushwa kutoka NBA na kupelekwa katika ligi ya D (Developmental League) ambapo mchezaji anayeshindwa kufikia viwango na malengo katika NBA hutakiwa kwenda kwa muda ili kujinoa zaidi. Kitakwimu, katika michezo yote 50 aliyocheza Thabeet msimu huu, ameweza kupata wastani wa pointi 2.5 tu ndani ya kila dakika dakika 10.3 za mchezo. Tayari amepoteza nafasi yake katika timu ya Grizzlies kwa Hamed Haddadi, kiungo wa kati aliyeichezea timu hiyo kwa miaka miwili sasa. Wakala wake, Bill Duffy, alifanya juhudi za kumhamishia kwenye timu ya Dakota Wizards ambayo ni washirika wa Grizzlies katika D-Legue na kusema, "I think he needs to play". Kwa kucheza D-League, Hasheem anakuwa mchezaji wa kwanza kabisa kushuka toka NBA hadi D-Legue kati ya wote waliowahi kunyakuliwa katika nafasi za juu za NBA draft. Hasheem anatarajiwa kuingia kiwanjani wakati Dakota itakapopambana na Erie siku ya Ijumaa. YATOKANAYO Waswahili tuna usemi wetu kuwa, 'kuteleza si kuanguka'. Kwamba kijana Hasheem bado anayo nafasi ya kufanya vizuri na kuwa mchezaji bora kabisa ikiwa atapata ushauri na maelekezo mazuri. Safari ya Hasheem alikotoka na alikofikia si ya lele mama hasa pale utakapoilinganisha na mamilioni ya watu, si tu wanaotoka nje ya Marekani, bali hata waliopo nchini Marekani kwenyewe. Historia ya Hasheem ya nyumbani Tanzania ambako mchezo wa mpira wa kikapu si nzuri kama ilivyo mchezo wa soka, anayo kila sababu ya kuangalia hatua na mafanikio aliyoyafikia. Kwa kuzingatia umri wake (16 Februari 1987), Hasheem bado anayo fursa ya kujinoa, kukata tamaa ni mwiko. Mara zote tunapoanguka au kupatwa na shida, yatupasa kuangalia chanzo cha tatizo, kisha tutafute mbinu sahihi za kulitatua na tena liwe somo ili tupate kujifunza kutokulirudia tena kosa. Binafsi nimejitahadharisha, 'usifurahie kujikwaa kwa mwenzio' ama 'usicheke ukunga na uzazi ungalipo'. Nimepitia magumu mengi, matatizo makubwa, na machungu tele, na bado mapambano yanaendelea, hivyo ninaelewa ilivyo mtu unapopatwa na hisia za uchungu na pengine aibu. Lakini huu si wakati wa kufikiria hayo, huu ni wakati wa kujua kuwa kadiri ya ukubwa wa jina lako, ndivyo utakavyokuwa ukubwa wa mlio wa mguno wako. Kijana jipe moyo mkuu, nyanyuka, simama imara, piga kifua mbele, safari na iendelee. Nasemaje, 'make it your STEPPING stone and not a STOPPING stone' - Subi, 25.02.2010. ![]() Kila mmoja anakaribishwa kwenye Nokia Care Service Tukio: Nokia Care Service Tarehe: Ijumaa, Februari 26, 2010 Muda: Kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni Eneo: Barabara ya Uhuru - Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa If you are in Dar es Salaam, Tanzania, you are invited to the Nokia Care Service Event: Nokia Care Service What: Flea Market Date: Friday, February 26, 2010 Time: 9:00am - 5:00pm Where: Uhuru Road-Benjamin Mkapa Sec School ![]() Downloading any text rich website or page for offline reading or printing can be done via the File --> Print or File --> Make available offline. But what happens when you don't want to sit in front of your computer all the time? or when you have to let somebody else use the computer at an inconvenient time? or how about when using office or internet cafe where time is limited? even better, how about wanting to read something while in the public transport or when waiting for something? Instead of staying idol, you can easily visit some interesting websites, convert the pages int simple PDF files, download them in your reader or print them for easy reading. To easily convert pages into PDF format, simply make use of either: pdfmyurl.com OR html-pdf-convert.com ![]() FOR WEB-BLOG owners, you can place the link in any page you want downloaded as PDF by just adding the url of the web, blog or page. Those with one page personal info i.e. online e-business card or an online resume/cv you can also do the same. Simply link the text or image you want people to use for downloading a specific page/url like this: http://pdfmyurl.com?url=www.wavuti.com e.g. <a href="http://pdfmyurl.com?url=http://www.wavuti.com/">downlaod this page as pdf</a> will create a text link that looks like this: downlaod this page as pdf Tafakari kwa njia ya katuni bin vibonzo... 25/02/2010
| Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |



































RSS Feed