![]() Issa Michuzi akikabidhi fulana kwa Hassan Abdulla mjini Reading Habari kutoka kwenye blogu ya mwanabloga maarufu nchini, bwana Issa Michuzi 'ankal' au 'mzee wa libeneke' zinapasha kuwa, baada ya kuendeleza kazi ya kublogu kwa takriban miaka minne mfulilizo bila kuchoka, hatimaye fulana ya blogu ya jamii imechukuliwa rasmi kutoka kwa 'ankal' na kuwekwa pembeni tayari kwa kupigwa mnada ili kuchangisha pesa za maendeleo ya wadau. Kampuni ya usafirishaji mizigo ya Hillview Family Company Limited ya mjini Reading, nchini Uingereza, imeinunua fulana hiyo kwa pauni 1,000 ili kuinadi na kuchangia mabloga kuendeleza 'libeneke' kwa ufanisi zaidi. Siku ya mnada utaofanyika online itatajwa hivi karibuni, na mabloga wanaotaka kunufaika na 'libeneke la mnada wa ze fulanazzzz' wanatakiwa watume maombi ya msaada na anwani pepe zao kupitia issamichuzi@gmail.com ili kuweza kufikiriwa na jopo la blogu ya jamii na wataalamu wa Hillview Family Company. Jumla ya mabloga wachanga 10 watanufaika na mpango huu ambapo watapatiwa laptops, modem za internet pamoja na pesa za hewani za internet ya miezi mitatu ili kuwawezesha kuanzia kazi. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 10 Aprili 2010. Mpango huu unamhusu bloga yeyote mchanga popote alipo duniani. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea www.issamichuzi.blogspot.com Sisi wana wavuti.com tunatoa pongezi za dhati kwa Issa Michuzi na HillView Family Co LtD kwa kuweza kubuni na kutaka kufanikisha azma ya kuwasaidia wale wote wanaojitokeza kutaka kupasha habari kwa njia ya blogu. Ni matumaini yetu kuwa mpango huu utakuwa yenye manufaa. Add Comment Habari hii ni kwa mujibu wa blogu ya Beda Msimbe - Lukwangule Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Uomboni wilayani Moshi vijijini, Festo Kibonda (18), amekufa na wengine ishirin na nne (24) kujeruhiwa katika ajali baada ya basi la Ngorika kuiparamia Hiace(Kipanya) waliyokuwa wakisafiria wanafunzi hao kutoka shuleni. Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko alisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 3.30 asubuhi katika eneo la njia panda ya Himo wilayani humo. Alisema katika ajali hiyo basi hilo la Ngorika lenye namba za usajili T 154 AHF aina ya Scania lililokuwa likindeshwa na Abbas Maeda likielekea mkoani Tanga ambapo wakati likitokea mizani liliigonga Hiace hiyo yenye namba za usajili T 810 AFK. “Baada ya ajali wasamamaria wema wakishirikiana na askari wa usalama barabarani waliwakimbiza majeruhi katika hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi lakini, Festo alifariki wakati akipatiwa matibabu”alisema. Kamanda alisema wakati Ngorika ikitoka eneo la mizani huku dereva wake bila uangalifu aliiparamia Hiace hiyo iliyokuwa imebeba wanafunzi ikitokea shuleni kwao eneo la Marangu Kiraracha Wilayani Moshi vijijini. “Hii ni ajali mbaya na ilisababishwa na uzembe wa dereva wa Ngorika ambaye hakuwa mwangalifu kwani eneo la mizani ni dogo na halikustahili kwa gari yoyote kutoka kwa kasi… tunamshikilia ili tumfikishe mahakamani hapo badaye” alisema. Alisema baada ya Ngorika kutoka kwa kasi liliigonga Hiace iyo kwa ubavu na kusababisha mwanafunzi mmoja kufariki huku wengine wakijeruhiwa vibaya ambapo wanafunzi watatu miongoni mwao akiwamo Mwalimu wao hali zao ni mbaya. Aliwataja wanafunzi waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC na hali zao ni mbaya kuwa ni Innocenti Kibonda(18) ambaye ni pacha wa marehemu katika ajali hiyo, Levina Assey (17) na Mwalimu wao Charles Bantalome (26). Alisema majeruhi wengine 21 katika ajali hiyo wamelezwa katika hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi huku ikiripotiwa kuwa hali zao si mbaya na wanaendelea na matibabu. Hata hivyo dereva wa Hiace aliyejulikana kuwa ni Tumaini Rwaito amelazwa katika hospitali ya Kilema wilayani humo na hali yake inaendelea vizuri. MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI Kama nilivyoandika jana, narudia kauli hiyo kuwa hakuna jipya la kusema wala kushauri hadi yale yaliyokwisha kusema na kushauriwa yafanyiwe kazi ifahamike kipi kinatekelezeka na kipi hakitekelezeki na tufanye nini. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bwana Ludovick Utouh akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete ripoti za ukaguzi wa matumizi ya fedha za Serikali na Taasisi zake Ikulu jijini Dar es Salaam. Aliyesimama kushoto kika picha ya kwanza ni Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu Bwana Atanas Tarimo. Photo credit: Mroki Mroki blog Rais Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 31 Machi 2010 alimepokea ripoti za Ukaguzi wa Matumizi ya Fedha za Serikali na Taasisi zake za mwaka 2008/2009 kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bwana Ludovick Utouh. Ripoti alizopokea Rais ni za Ukaguzi wa Taarifa za Fedha ambazo zinahusu Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na za Mashirika ya Umma. Ripoti nyingine ni za Ufanisi ambazo ni ripoti ya jumla ya Ukaguzi wa Ufanisi, ukaguzi wa ufanisi na thamani ya Fedha kwenye sekta ya ujenzi wa Barabara. Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, iliyorekebishwa mwaka 2005, pamoja na sheria ya Ukaguzi wa Umma ya mwaka 2008 na Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 iliyorekebishwa mwaka 2000, mara baada ya kupokea ripoti hiyo anatakiwa kumwagiza Waziri mwenye mamlaka husika kuziwasilisha ripoti hizo Bungeni. Katika mazungumzo hayo Bwaba Utouh amemueleza Rais Kikwete juu ya mafanikio mbalimbali ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kutoka mwaka 2005/2006 hadi za 2008/2009 na kuonyesha kuridhishwa nazo. Baadhi ya mafanikio hayo ni uwezo wa ofisi yake kuwakilisha ripoti 4 kwa mwaka huu 2008/2009 kutoka ripoti 2 mwaka uliopita wa 2005/2006. Itakumbukwa kuwa Ripoti za mwaka 2005/2006 zilijadiiwa chini ya Uenyekiti wa Rais Kikwete katika vikao muhimu vitatu ambacho ni kikao cha Baraza la Mawaziri, Kikao cha viongozi wakuu wa Serikali Kuu kilichofanyika na kikao cha Viongozi Wakuu wa Serikali za Mitaa vyote vilifanyika Aprili , 2007. Bwana Utouh pia ameeleza kuwa tofauti na ripoti za mwaka 2005/2006 ambazo uandaaji wa taarifa za Serikali Kuu na Serikali za Mitaa ulitumia viwango na miongozo ya ndani ya nchi, uandaaji wa ripoti hizi mpya umetumia viwango vya kihasibu vya Kimataifa. Hatua nyingine kubwa iliyofikiwa na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ni kuwa ukaguzi wa Balozi za Tanzania za ripoti iliyopita ulifanyika kwa kutumia sampuli chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakati ripoti hii ya leo ukaguzi umefanyika kwa Balozi zote na kila Balozi kupewa hati yake ya Ukaguzi na katika ukaguzi mzima hati za mwaka huu zinaonyesha kuboreka zaidi kuliko za kipindi kilichopita. Akipokea Ripoti hizo Rais Kikwete ameishukuru ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kazi hiyo na kuahidi kuijengea ofisi hiyo ili ifanye kazi vizuri zaidi.“ Tutafanya jitihada ya kuwawezesha zaidi, ni muhimu kuongeza watumishi, mishahara, vitendea kazi ili mfanye kazi vizuri zaidi”. Amesema Rais na kusisitiza kuwa nidhamu kwenye matumizi ya fedha ni muhimu na kwamba tangu serikali ilipoelezea na kukuza uelewa na umuhimu wa nidhamu katika matumizi ya fedha kwa viongozi na watendaji, nidhamu imeanza kuonekana na hivyo hakuna budi kujenga nidhamu zaidi. Story credit: Beda Msimbe's Lukwangule blog Dear All, The Second Mwalimu Julius Intellectual Festival is two weeks away. As the attached programme shows, it promises to be such a great public event, graced by the likes of Samir Amin, Samia Nkrumah, Salim Ahmed Salim, Utsa Patnaik and Marcelinho dos Santos! Plan early to, and do, attend! Best Regards, Chambi Please click on the attachment below to download a copy of the program.
Baada ya taarifa ya jana kuwa VodaCom wamekuja na shilingi moja siku nzima kwa siku zote, tiGO wameibuka leo na thumni kwa kila sekunde baada ya dakika ya kwanza kwa saa ishirini kwa siku (kasoro saa kumi na mbili jioni hadi nne usiku). Tanzania telecommunication company, tiGO announces the launches of another most affordable tariff for tiGO pre paid subscribers which will be available for every Tigo subscribers from now onwards every single day. Mbando akiwa na Masanja wakishikilia mabango yao ya Nusu shilingi. Speaking in the press conference tiGO PR Executive Jackson Mmbando said “This new tariffs wants to encourage tiGO subscribers to make calls for lower prices at Tshs ½ after the 1st minute, 20 hours a day except between 6pm to 10 pm at night. Our new tariff services will be known as Tigo Thumni / Ongea kama Zamani. Which means with tiGO Thumni it’s like in the old days when currency had much value. Talk as much as you want for only ½ Tsh per second after the 1st minute, 20 hours a day except from 6pm to 10 pm, Jackson insisted, for this we want to grant our customers with enough freedom to access today’s world in a simple manner by giving them thumni as a special tariff they can afford and manage to strive against the social life. We are sure that this will give enough opportunity to every one using tiGO to interact and share their professional experiences in a truly different way.” Now lets every one talk and enjoy Kama Zamani with only ½ Tsh per second after the first 60 seconds of each call to other tiGO subscribers. Just to remind you with this tariff there is no registration requirement of any kind. The user just needs to have a tiGO pre-paid sim card, and good enough thumni tariffs will not affect home zone tariffs of ROBO shillings per second after the first minutes while in Zanzibar. We real encourage our subscribers to continue enjoy our best price ever now. tiGO with our introduction of Longer longa, XTREME services, Usipimes , Xtreme SMS and today tiGO Thumni I believe it explain tiGO Brand as most affordable, thus means consider our subscribers situation and we own the spirit of simplicity, uncomplicated, open, assessable and always there when needed. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amewapandisha vyeo maafisa 42 wa Jeshi la Polisi kutokana na utendaji wao mzuri wa kazi. Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika, imesema kuwa waliopandishwa vyeo kuanzia Machi 16, mwaka huu ni pamoja na Makamanda wa Polisi wa mikoa tisa, Makamanda watano wa vikosi na Wakuu wa Vitengo mbalimbali vya Jeshi hilo waliopo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam na Zanzibar. Kamanda Mssika amesema kati ya hao wapo Maafisa wanne wakuu ambao wamepandishwa vyeo kutoka vyeo vyao vya zamani vya Makamishna Wsaidizi Wandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Manaibu Makamishna wa Polisi (DCP). Walipandishwa kuwa Manaibu Kakamishna wa Polisi (DCP’s) ni Mkuu wa Huduma za Polisi Jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi SACP Isaya Mngulu, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Afya nchini SACP Neven Mashayo, SACP Rashid Omari Ali, wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACPO Suluiman Kova. Kamanda Mssika amewataja Makamanda 38 wakiwemo Makamanda wa Polisi wa Mikoa tisa ya Tanzania Bara na Visiwani kutoka Vyeo vya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP ambao sasa kila mmoja anakuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) ambao ni Makamanda Thobias Andengenye wa Morogoro, Henry Salewi wa Kagera, Bi Celina Kaluba wa Singida na Kamanda Lucas Ng’hoboko wa Kilimanjaro. Wengine ni Kamanda Absalom Mwanyoma wa Pwani, Simon Sirro wa Mwanza, Isuto Mantage wa Rukwa, Michael Kamhanda wa Ruvuma na Yahaya Rashidi wa mkoa wa Kaskazini Pemba. Kamanda Mssika amewataja Makamanda wa Vikosi waliopandishwa vyeo kuwa ni Mohammed Mpinga, wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Tresphory Anaclet wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia nchini (FFU), Sospeter Kondela, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Ujenzi, Geofrey Nzoa Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na kupambana na Madawa ya Kulevya na Mkuu wa Chuo cha Polisi cha Dar es Salaam Bi. Alice Mapunda. Wengine ni Mkuu wa Shirikisho la Polisi wa Kimataifa Interpol hapa nchini Kamanda Hussein Nassoro Laizer, Mkuu wa Bohari Kuu la Polisi nchini Kamanda Adriano Magayane, Mkuu wa Kikosi cha Usafirishaji cha Jeshi la Polisi nchini Kamanda Kamanda Ali Mlege na Mkuu wa Kitengo cha Fedha cha Jeshi la Polisi nchini Kamanda Jonas Mgendi. Wengine ni Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Tanzania kwenye Ofisi za Interpol Kanda ya nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika Kamanda Goodluck Mongi, Mkuu wa Kitengo cha Picha na Maabala ya Uchunguzi wa Vielelezo vya Makosa ya Jinai nchini (FB) Kamanda Hezron Gyimbi. Wengine ni Kamanda Jamal Rwambow, Kamanda Lucas Haule na Kamanda Donald Ludamila wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Makao Makuu, Mkuu wa Kitengo cha Maboresho cha Jeshi la Polisi nchini Kamanda Lucas Kusima, Kamanda Saidi Juma Hamis kutoka Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Makao Makuu. Kamanda Mssika amesema kuwa wengine walipandishwa ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mifumo ya Mitangao ya Kompyuta ya Jeshi la Polisi nchini kamanda Anyisile Kyoso, Kamanda Renatus Chalamila, Mwanasheria wa Jeshi la Polisi nchini Kamanda Donald Kaswende na Kamanda mwanamke Adolfina Chialo. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo cha Jeshi la Polisi nchini Kamanda Abdulrahman Kaniki, Msaidizi wa Mkuu wa Operesheni Maalum nchini Kamanda Hezron Kigondo, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zananzibar Kamanda Mussa Alli Mussa na Kamanda Hamdani Makame wa Ofisi ya Kamishna wa Polisi Zanzibar. Mkuu wa Mipango Kamanda Ernest Mangu, Kamanda Makame Ali Makame, Kamanda Mwalim Ame na Kamanda Mpinga Gyumi ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko Makao Makuu ya Jeshi la Polisi. Habari hii ni kwa mujibu wa Mohammed Mhina na Athumani Mtasha wa Jeshi la Polisi Kastama Kea au Kastama Kero? 31/03/2010
Tafadhali maofisi husika na watoa huduma bila kujali kama ni sekretari, muuguzi, daktari, injinia, postamasta, dereva, utingo, tandiboi, muuza nguo, mama ntilie, baba lishe na kazalika, end of thinking kapasiti, tafadhali sana heshimuni kazi, wajibu wenu na ofisi zenu. Tusizinguane bila sababu ya msingi! Nasi 'wadau' tukiyaona haya ya 'ndivyo sivyo' tuyakemee kiviiiile. Senkyu. Vietnam President Nguyen Minh Triet said Vietnam is ready to share experiences and help Tanzania in agricultural development. The state President while receiving Tanzanian Prime Minister Mizengo Peter Pinda in Hanoi on March 30 valued the visit, which takes place on the occasion of the 45th anniversary of the establishment of diplomatic ties between the two countries, as an important milestone that helps further strengthen the friendship and cooperation between Vietnam and Tanzania . He thanked the Tanzanian people for their support for Vietnam during its struggle for national independence and affirmed that Tanzania is seen as a steadfast friend of Vietnam. Regarding cooperation in economics, trade and investment, President Triet said that Vietnam and the countries of Africa, including Tanzania, should speed up cooperation to achieve the prosperous development of each country and improve the living standards of their peoples. He said he wished that the ministries and agencies of the two sides would soon implement specific measures to boost cooperation in areas of potential, especially agriculture, irrigational construction, food processing, health care and education. For his part, PM Mizengo Peter Pinda affirmed that Tanzania values its ties with Vietnam and wishes to further boost their friendship, solidarity and cooperation, particularly in agriculture, health and education. Read more at www.vnnnews.net/vietnam-offers-assistance-to-tanzania Gavana wa Jimbo la Zhangdong nchini China bw. Sun Liang akizungumza na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Profesa David Mwakyusa kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo. Mgeni huyo pamoja na ujumbe wake walifika Wizarani hapo kwa mazungumzo mafupi juu ya mkakati wao wa kujitolea kujenga kituo cha kutibu magonjwa ya moyo na upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Photo credit: Issa Michuzi blog Jiwe la Msingi la Taasisi ya Tiba ya Moyo Muhimbili lasimikwa rasmiRais Jakaya Mrisho Kikwete (wanne kushoto) na Balozi wa China nchini Bwana Liu Xinsheng (watatu kushoto) wakiweka udongo katika jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi kwa ujenzi wa Taasisi ya Tiba ya Moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili MNH tarehe 31 Machi 2010. Wengine katika picha ni Waziri wa Afya Profesa David Mwakyusa(watano kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bwana Adolar Mapunda, wapili kushoto ni kiongozi wa ujumbe wa Jamhuri ya watu wa China bwana Sun Liang Photo credit: Freddy Maro/Ikulu Ni swali alilouliza Paul Misalaba siku chache zilizopita kwenye kisanduku cha maoni na bado halijapata jibu. Swali: Tusaidianeni katika kunyosha utata huu katika sentensi ifuatayo JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA na JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA. Ipi ni sentensi sahihi kati ya hizo sentensi mbili? Paul | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 | ||||||













RSS Feed