Ziara ya 'Mtoto wa Mkulima' mkoani Singida 30/04/2010
Picha zikimuonesha Waziri Mkuu wa Tanzania bwana Mizengo Pinda "mtoto wa mkulima" pamoja na mkewe, Tunu, viongozi mbalimbali wa Kiserikali na wananchi katika shughuli mbalimbali za ufunguzi na ukaguzi. Waziri Mtoto wa Mkulima alifanya ziara hiyo mkoani Singida katika Wilaya ya Manyoni mwezi Aprili 2010. Add Comment Basi la Islam laua wanne Morogoro 30/04/2010
Habari nyingine za kusikitisha katika wiki hii zinatoka Morogoro zikisema kuwa basi la usafiri la kampuni ya Islam linalofanya safari zake kati ya mkoa jirani ya Dar Es Salaam na Morogoro limesababisha ajali na kuua watu wanne, akiwamo mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Gwata, Morogoro. Mwanafunzi huyo, Dotto Issa (16), alikuwa amepakiwa katika pikipiki iliyokuwa inaendeshwa na Karim Selemani ambaye pia alifariki dunia katika ajali hiyo. Kamanda wa Polisi mkoa, Thobias Andengenye amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea katika kijiji cha Lukole, wilayani Morogoro. Habari na Beda Msimbe. Picha ya kwanza wanaonekana Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Amani Abeid Karume, Balozi wa Marekani nchini, Alphonso E. Lenhardt, na wahusika wengine wakishuhudi utiaji saini mkataba wa kazi za ulazaji waya wa umeme, (Marine Cable) kutoka Ras Kiromoni Dar es Salaam hadi Fumba. Picha ya pili wanaonekana mtendaji Mkuu wa Millenium Challenge Tanzania, Bernad Mchomvu akibadilishana na kukabidhiana mkataba waliotia saini zao na mwakilishi wa Kampuni ya Viscus ya nchini Japan, Tesuji Onno. Picha na Ramadhan Othman Ikulu via Sufiani Mafoto. REMARKS BY H.E. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DURING THE CLOSING CEREMONY OF THE 3RD EAC INVESTMENT CONFERENCE Speke Resort, Munyonyo, Kampala, Uganda, 30 April 2010 Your Excellency Yoweri Museveni, President of the Republic of Uganda; Your Excellency Yves Sahinguvu, Vice President of the Republic of Rwanda; Your Excellency Bernard Makuza, Prime Minister of the Republic of Rwanda; Rt. Honourable Raila Odinga, Prime Minister of the Republic of Kenya, Honourable Chairman of the Council of Ministers; Honourable Ministers and Officials from the EAC Partner States; The Secretary General of the East African Community; Members of the Business community, Distinguished Guests, Ladies and Gentlemen, On behalf of all of us gathered here, and on my own behalf, I would like to thank H.E. Yoweri Kaguta Museveni, President of the friendly and sister Republic of Uganda, for hosting this important conference. We are enjoying every minute of our stay and we are grateful for, the customary warm reception and gracious hospitality of the people of Uganda. Excellencies, Ladies and Gentlemen, We have come to the end of the 3rd East Africa Investment Conference. By all accounts, this conference has been a resounding success. I have been informed that all the roundtables, the presentations, and the discussions that have taken place over the past two days have been up to speed and lived up to our expectations. This has indeed, symbolised another important step forward being taken in our regional integration endeavours and quest for improving the economic conditions of our region and its people. We should be proud of this unity of purpose. Ladies and Gentlemen, Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka ishirini Ngorongoro Heroers, imeifunga bao tatu dhidi ya moja, timu ya vijana wa chini ya umri huo kutoka Malawi. Mchezo huo ulikuwa wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana na ulifanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. kwenye mchezo uliofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Vijana wa Ngorongoro Heroers walipigana vikali kuhakikisha wanaondoka na ushindi mnono dhidi ya wamalawi hao waliokuwa wakicheza mpira wa kiwango cha juu japokuwa umaliziaji wao haukuwa mzuri mara kadhaa walipofika langoni mwa Ngorongoro Heroers. Iliwachukua dakika tatu tu vijana wa Ngorogoro Heroers kupata goli lililofungwa na mshambuliaji Omega Seme ambapo timu hiyo iliendelea kuleta madhara katika lango la Malawi na mara nyingine Thomas Ulimwengu aliipatia goli la pili. Magoli hayo yalifungwa kabla ya kipindi cha kwanza kwisha. Kipindi cha pili kilianza na kuendelea hadi dakika ya mwisho ambapo Malawi walipata goli la kufutia machozi katika dakika ya tisini kwa njia ya penati, mpira uliyopigwa Lastin Simkonda baada ya Heroes kufanya 'madhambi' katika eneo la Malawi. Goli hilo lilipandisha mori wa Ngorongoro Heroers ambapo ilicheza vizuri katika dakika za lala salama kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 91 pale Rashid Issa Rashid alipoukokota mpira mpaka wingi ya kushoto na kutoa pasi nzuri kwa Thomas Ulimwengu aliyeunganisha mpira huo na kuandika goli la tatu. Hivyo hadi mwisho wa mchezo ni Ngorongoro Heroes 3 na Malawi 1. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa nchini Malawi, timu hizo zilitoka sare ya kufungana magoli mawili kila moja. Kwa matokeo hayo basi, timu ya ngorongoro itakutana na timu ya vijana ya Ivory Coast wiki ya tatu ya mwezi mei ambapo mchezo wa kwanza utafanyika katika nchini Ivory Coast na baada ya wiki mbili timu hizo zitarudiana katika dimba uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Habari kwa mujibu wa John Bukuku na Picha kwa hisani ya Issa Michuzi. Kwa mujibu wa taarifa za habari kupitia Dira ya BBC na Radio CloudsFM, boti binafsi (?ya Marine Park) iliyokuwa ikisafiri mkoani Mtwara ikiwa imebeba watu wapatao ishirini na wanane (28) imepata ajali na inasadikiwa kuwa watu ishirini wamefariki dunia. Ripota wa CloudsFM aliyehojiwa na Gardner Habash na Ephraim Kibonde katika kipindi cha Jahazi, amesikika akisema kuwa boti ilibinuka na kumwaga kila kilichokuwamo na kwamba maiti nane walikuwa wameshapatikana. Baadaye, Kamanda wa Kikosi cha Polisi mkoani Lindi Steven Buyuya alisikika katika kipindi cha Dira ya BBC akizungumza na Mtangazaji wa habari wa BBC, Josephat Mwanzi, na kuthibitisha kuwa ajali hiyo imetokea hapo Mtwara wakati boti ilipokuwa ikivusha abiria kutoka Shangaji (mwendo wa km. mbili toka Mtwara bandarini) kwenda Msangamkuu, wengi wao wakiwa ni wavuvi na wafanya biasahara ndogo ndogo. Boti hiyo imesajiliwa kwa uwezo wa kubeba watu kumi na nane (18) lakini walikuwepo abiria kumi zaidi hivyo kufikia idadi ya watu ishirini na wanane pamoja na mizigo na baisikeli za wasafiri. Inasadikiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kuzidiwa uzito (overloading) na hivyo kukosa stamina. Mmiliki wa boti hiyo pamoja na baharia wake wamekimbia. Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa vifaa vya uokozi na kusaidia katika zoezi hilo. SAHIHISHO Sahihisho kidogo, nadhani kuna makosa kwenye uwasilishaji wa taarifa hii. Marine Parks ni taasisi ya Serikali (chini ya wizara ya mifugo na uvuvi), na haimiliki boti za kusafirisha abiria, ina boats zake kwa ajili ya surveillance and enforcement in the ''marine park'' boundaries. Na pia kwa maelezo yaliyotolewa hiyo boat imezama toka ''kivukoni landing site'' eneo ambalo liko Mtwara mjini nje kabisa ya mipaka ya ''marine parks''. Shukrani kwa Eliabu Thomas kwa kutoa rekebisho hili (kama inavyosomeka kwenye sehemu ya maoni). MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2010 YAMETOKA 30/04/2010
![]() Matokeo nimeweza kuyaona kupitia www.necta.go.tz Zimetolewa tovuti mbadala ili kupambana na tatizo la traffic, hivyo jaribu katika mojawapo ya hizi zifuatazo: Linki Na. 1 www.necta.go.tz/matokeo_acsee/Alevel Linki Na. 2 admin.udsm.ac.tz/results/Alevel Linki Na. 3 matokeo.necta.go.tz/matokeo_acsee/Alevel Ijapokuwa katika matokeo hayo, wavulana wanaongoza katika kumi bora Kitaifa, lakini wastani wajumla unaonyesha wasichana wamefanya vyema zaidi ya wavulana. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako alisema ufaulu umepungua kwa asilimia 0.78 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2009 ambapo waliofaulu ni sawa na asilimia 89.64. Alisema watahiniwa wa shule waliofaulu ni 45,217, sawa na asilimia 93.76 ya waliofanya mtihani na watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu ni 10,547 sawa na silimia 74.57. Date: Saturday, May 22, 2010 Time: 8:30am - 9:00pm Location: Dar-es-salaam International Academy (DIA). Dar-es-salaam, Tanzania Wale wote mnaofuatilia mitandao jamii ya video mtagundua kuwa TED ni mojawapo ya mitandao bora kabisa elimishi katika jamii. Ni sehemu ambayo utapata kujifunza mengi ambayo hayajawahi kuzungumzwa jukwaani mahali pengine (ndiyo mojawapo ya misingi ya TED) katika maisha ya kila siku, tangu kuelezea mambo ya kihistoria hadi uvumbuzi mpya wa kisayansi, upigaji picha hadi utunzi wa mashairi. Katika tovuti hii tumekuwa tukiweka baadhi ya video zinazovutia na kuendana na mazingira yetu (unaweza kuziona katika ukurasa wa videos) na mojawapo maarufu sana ni zile za mwalimu Hans Rosling anavyopambanua takwimu mbalimbali za kimaendelo katika maisha ya binadamu katika mataifa ya dunia kwa miaka kadhaa. Habari njema ni kuwa, kwa mara nyingine tena TED watakuwepo Tanzania, ila safari hii si sawa na wakati walipokuja kama TED ambapo ilikuwa ni mkutano mkubwa, bali wanakuja kama TEDx kwa mfumo mpya wa kujigawa na kutembelea maeneo mengi zaidi. In the spirit of ideas worth spreading, TED has created a program called TEDx. TEDx is a program of local, self-organized events that bring people together to share a TED-like experience. Our event is called TEDx Dar "Pamoja Tunaweza!", where x=independently organized TED event. At our TEDxDar event, TEDTalks video and live speakers will combine to spark deep discussion and connection in a small group. The TED Conference provides general guidance for the TEDx program, but individual TEDx events, including ours, are self-organized. Soma zaidi kuhusu TEDxDar event kupitia: www.tedxdar.com Waziri wa Wizara husika ametangaza viwango vya kima cha chini cha mshahara na kutaja kima cha chini cha mishahara hiyo kwa sekta mbalimbali binafsi kama ifuatavyo, wafanyakazi wa:
Picha na Aron Msigwa wa Maelezo. Dhuluma dhini ya albino bado inaendelea 30/04/2010
Ni jambo la kusikitisha sana, kwamba baada ya kukemea, kufikisha washitakiwa mahakamani na hata hukumu kutolewa, pamoja na juhudi zote zinazofanyika katika kupambana na dhuluma hii ya kukata viungo ya miili ya binadamu wenzetu kwa imani potofu tu kutokana na rangi yao ya miili, inaendelea. Anayeonekana pichani ni mtoto Kabula Nkalango akiwa na dada yake Regina Cosmas baada ya kufanyiwa ukatili wa kukatwa mkono wake wa kuume na watu saiofahamika. Watu hao waliondoka na mkono huo. Ukatili huu ulifanyika katika kijiji cha Luhaga, kata ya Igwamanoni, wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Huu ni ushetani na wote wanaofanya hivi na kuamini hivi wanaongozwa na roho wa shetani. Picha kwa hisani ya Mroki Mroki. | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |











































RSS Feed