Makao makuu ya kanisa la Kikatoliki Vatican imekubali hatua ya kujiuzulu kwa askofu wa Ireland aliyekuwa Nigeria kutokana na shutuma za kumdhalilisha kijinsia binti mmoja huko Niger Delta. ![]() Richard Burke, askofu wa mji wa Benin, amekubali kuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti huyo lakini amekana kwa binti huyo kuwa na umri mdogo uhusiano huo ulipoanza. Katika taarifa iliyotolewa kwenye gazeti la kikatoliki la Ireland amesema," Sababu ya kujiuzulu ni kutokuwa mwaminifu katika kiapo changu cha useja." Askofu huyo amejiuzulu baada ya madai hayo kutolewa mwaka jana. Dolores Atwood alidai kunyanyaswa kijinsia na askofu Burke wakati alipokuwa padri huko Warri kusini mwa Nigera kwenye mji wa Niger Delta. Hata hivyo, amesema uhusiano wao ulianza mwaka 1989 alipokuwa miaka 40 na binti akiwa na umri wa miaka 21. Amesema kwenye taarifa yake," Nilijibu haraka iwezekanavyo kwamba sijawahi hata siku moja maishani mwangu kumnyanyasa mtoto kijinsia. Huu bado ni msimamo wangu. Huu ni ukweli." Askofu Burke pia alimwomba radhi Bi Atwood na kuomba msamaha katika vituo vyake vya kanisa huko Warri na Benin. Kanisa hilo limesema limekubali kujiuzulu kwake ambapo pia limetaja jopo litakalochunguza udhalilishaji wa watoto uliofanywa na viongozi wa kikatoliki huko Ireland. Source: bbc.co.uk/swahili Add Comment Tanzania to issue a debut Eurobond soon 31/05/2010
Tanzania plans to issue a debut Eurobond soon after it gets a sovereign rating in the next seven to eight months, governor Benno Ndulu said. Tanzania shelved plans to issue a debut sovereign bond because of the global financial crisis, but revived the plan in January. In May, the finance minister said it would take at least 12 months to complete the process and Tanzania would plug a financing deficit with syndicated loans. ![]() image coutesy of traveller.org/currency “We are in preparation right now to restart the country rating, sovereign rating. We are procuring now an advisor for a sovereign rating and for working alongside us,” Bank of Tanzania Governor, Mr Benno Ndulu, said on the sidelines of the WEF Global Redesign Summit 2010 in Doha. “The rating, we hope in the next seven to eight months to have that out of the way and follow quickly with the issuance,” he said, without giving details about the size of the planned issue. Mr Ndulu also told Reuters Insider that central bank intervention to prevent the Tanzanian shilling weakening was not necessary and that an increase in Tanzania’s inflation rate in April was due to rising food and oil prices. Tanzania’s year-on-year inflation rose to 9.4 per cent in April from 9.0 per cent the previous month. “The cause of the rise is not actually monetary-based. It’s been essentially exogenous because of the increase in food prices and the increase in oil prices, which are both outside of the control of monetary policy,” Mr Ndulu said. “But what we have done is try to compensate for that by tightening slightly more our monetary policy so that the pressure on prices would be relieved,” he said. Food carries a heavy weighting in the basket of goods used to calculate inflation and a drought last year sent inflation rates soaring. Better harvests have since helped bring down the headline rate from 12.2 percent in December. Mr Ndulu said he expected the inflation rate to stay in the single-digit range. The government predicted last week it would slow to eight per cent by June this year. “We are just entering the harvest season for food, so my expectations is that food prices should decline in May and in June, which might in this case keep us still within the single digit inflation,” the central bank governor said. “Recently, the prices of oil have come down somewhat as a result of anxieties about a recovery in Europe, that I think also will be helpful in keeping prices at the pump down.” Mr Ndulu said intervention by the central bank to prevent the Tanzanian shilling weakening was not necessary. “Most of our selling of US dollars has been purely for liquidity management purposes. We know that the decline of the shilling against the dollar is in some ways also offset by the strengthening of the shilling against the euro and the pound.” “(With) the dollar strengthening against all currencies, an intervention wouldn’t make much sense. And in any case our best principle is only intervening when the currency gets way, way out of proportion,” he said. The governor also said the government would be able to plug a gap after donors pledged to cut funding for Tanzania’s 2010/11 (July-June) budget by $220 million to $534 million due to concerns about the slow pace of reforms. “The country is organising itself to fill the gap without recourse to our macroeconomic stability and more efforts will be put into raising revenues. Also, a better look at our expenditures and that combination should be able to fill the gap,” Ndulu said. TUCTA watatoa tamko Juni 5 kuhusu mgomo 31/05/2010
Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA), linatarajia kutoa tamko la kuhusu kugoma ama la tarehe 5 Juni 2010, baada ya kikao kinacho cha majadiliano kinachotarajiwa kufanyika Juni 4. Hatua hiyo inafuatia Serikali kushindwa kutoa tamko la makubaliano yao ya kikao cha tatu kilichofanyika Mei 8 mwaka huu, ambapo kwa mujibu wa sheria, Waziri wa Kazi-Ajira na Maendeleo ya Vijana, anapaswa kutoa taarifa ya kikao hicho ndani ya siku 21. Naibu Katibu Mkuu wa TUCTA, Nicholas Mgaya amesema kutokana na Serikali kushindwa kutoa taarifa yoyote ndani ya siku hizo, baraza linaloratibu mgomo litatoa tamko lake. Wafanyakazi wamekuwa kimya kutokana na kusubiri tamko la Serikali kuhusiana na kikao chao hicho, ambapo mpaka sasa Waziri ameshindwa kutoa taarifa yoyote kutokana na hali hiyo watakaa kikao hicho kwa ajili ya kujadili hatua zitakazofuatwa na wafanyakazi hao. "Tunatarajia kufanya kikao cha mwisho siku ya Ijumaa, ambacho kitatoa mwelekeo wa wafanyakazi kufanya mgomo au la, kwa sababu tulikuwa tunasubiri tamko la makubaliano kutoka Serikalini, lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika badala yake waziri amekaa kimya,"alisema Mgaya. Aliongeza kutokana na hali hiyo baraza hilo limesikitishwa na hatua hiyo, kwa sasa wanaendelea na mikutano ya ndani kwa ajili ya kupanga utaratibu watakaotumia wakati wa kutoa tamko hilo. "Wafanyakazi ndio wanaokuza uchumi wananchi, lakini wanarudishwa nyuma na baadhi ya viongozi kwa kuwadharau na kutosikiliza matatizo yao, jambo ambalo linawafanya waingie kwenye mgogoro mkubwa namna hii na serikali," anaongeza. Kwa mujibu wa Mgaya, mbali na tamko hilo pia, siku hiyo hiyo shirikisho hilo litatoa taarifa za kutaka kumshitaki Waziri huyo kutokana na kutangaza mishahara yenye mapungufu katika baadhi ya vipengele. credit: Patricia Kimelemeta/Mwananchi Said Kalembo amsimamisha kazi Majuto Mbuguyu 31/05/2010
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Meja Jenerali mstaafu Said Said Kalembo amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tanga Majuto Mbuguyu kufuatia ukengeufu katika ukarabati wa barabara Bombo, Tanga. ![]() Mej. Jen. Said S. Kalembo (picha ya maktaba) Meja Jenarali Kalembo amemsimamisha kazi Mkurugenzi huyo kutokana na kukiuka agizo la Bodi ya barabara ya Mkoa iliyomtaka kusimamisha marakoja kazi ya ukarabati huo wa barabara katika eneo la Mkonge - Raskazoni kwa kiwango cha lami. Kazi hiyo ya ukarabati wa Barabara yenye urefu wa kilometa mbili na nusu, hadi kukamilika ilitarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 575. Taarifa za mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo unamuelekeza Mkandarasi huyo kukwangua tabaka la juu na kisha kushindilia kabla ya kuweka lami jambo ambalo hata hivyo limefanyika kinyume kwa kuchimbua mawe yote na kuweka kokoto. "Tofauti na mkataba unavyosema na hata maagizo ya Bodi ya Barabara, mkandarasi ameendelea kuchimba barabara na kutoa mawe, hii ni dharau kubwa", alisema Kalembo. Kalembo pia aliwaweka mahabusu kwenye Kituo cha Polisi Chumbageni Tanga, mkandarasi wa kampuni inayojenga barabara hiyo Ediya Mwalusya, Mavumira Bori, Dereva wa trekta Ayub Yakub pamoja na Mhandisi wa Barabara wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Arafat Kaniki waliokutwa wakisimamia kazi katika eneo la Barabara hiyo. Mkuu huyo wa mkoa aliyekuwa ameongozana na Katibu Tawala mkoa wa Tanga, Paul Chikira na Mkuu wa wilaya ya Tanga Dk. Ibrahimu Msengi aliamua kufanya ziara ya ghafla kwenye eneo hilo baada ya kubaini kuwa agizo lililotolewa na Bodi ya Barabara mapema mwezi Mei mwaka huu limekiukwa. "Hivi inakuaje agizo litolewe na Bodi ya Barabara ya mkoa ambayo Mwenyekiti wake ni Mimi mwenyewe Mkuu wa mkoa likiukwe, yaani mpaka leo mnaendelea kuchimba hivi mnadhani sisi wote hatujasoma eeeh...?", RAS andika barua DED namsimamisha kazi kuanzia leo. Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa mkoa, Ofisi yake iliandika barua ya kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji kusimamisha kazi hiyo mara moja. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji, Majuto Mbuguyu alisema kuwa alitoa taarifa za mdomo kwa mkandarasi huyo na kwamba hata yeye haelewi sababu za mkandarasi kutotii maagizo ya bodi na kuendelea na kazi. "Mimi nilimwambia kwa mdomo tu tena niliongea na yule mkurugenzi na walisimama, lakini, nashangaa kwa nini wameendelea kuchimba Barabara, hata mimi Mheshimiwa sielewi?", alisema Mbuguyu. Hivi karibuni katika kikao cha Bodi ya Barabara, Kalembo alimsimamisha kazi na kumfukuza kwenye kikao Mhandisi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Rickson Lema kwa madai ya kushindwa kutoa maelezo ya kitaalamu kuhusiana na ujenzi wa Barabara hiyo. Mawe yaliyokuwa yakiendelea kutolewa katika Barabara hiyo yameanza kuibwa na watu wasiojulikana. credit: Mwananchi Wanafunzi Chuo Kikuu Kishiriki Mkwawa Wagoma 31/05/2010
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) wamegoma kuingia madarasani kwa siku nzima ya leo, Mei 31 wakishinikiza Serikali kuwapa fedha za malazi na chakula kiasi cha shilingi 300,000. Wanafunzi hao wameeleza kusikitishwa kwao na hatua ya Serikali kuileta timu ta Brazil kuja kucheza na timu ya taifa (Taifa Stars) kwa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 3 huku wanafunzi wa vyuo vikuu wakiendelea kulia njaa kwa kushindwa kupewa fedha zao hizo kama walivyoahidiwa. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi jana wanafunzi hao walisema kuwa mgomo wao ni mgomo wa amani na hata maandamano yao waliyoyafanya yalikuwa ni ya amani ila wanashangazwa na hatua ya uongozi wa chuo hicho kuwaita askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) kuja kuyayawanya waandamanaji chuoni hapo. Wageni wa mwaka wa kwanza ilipaswa kupewa fedha ya kujikimu kiasi cha shilingi 350,000 pamoja na shilingi 300,000 ambazo wanafunzi wote walipaswa kupewa. Wakielezea juu ya tukio hilo kwa sharti la kutotaja majina yao wanafunzi hao walisema kuwa mgomo huo ulianza majira ya saa tatu asubuhi kabla ya FFU kufika chuoni hapo majira ya saa 5 asubuhi. Walisema kuwa kutokana na mgomo huo kutokuwa na vurugu zozote askari hao hawakuweza kufyatua risasi kama ilivyo siku nyingine japo bado waliendelea kupiga kambi katika eneo hilo la chuo ili kupambana na wanafunzi hao iwapo wangefanya vurugu. Pia wanafunzi hao walihoji sababu ya uongozi wa chuo hicho pamoja na bodi ya mikopo kuendelea kuchelewesha malipo yao pamoja na yale ya mwaka wa kwanza wakati vyuo vingine vya umma wamepewa malipo hayo. Hivyo waliahidi kuendelea na mgomo huo hadi pale watakapotimiziwa madai yao. Wanafunzi hao pia walieleza kusikitishwa na uongozi wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo kwa kujitenga kwao na mgomo huo na kuwa iwapo watatimiziwa madai yao hawapo tayari kuendelea kuongozwa na viongozi hao ambao wapo kwa maslahi ya viongozi wa chuo. Mkuu wa chuo hicho Profesa Philimon Mushi akizungumza na mwandishi wa habari hii kwa njia ya simu kuhusiana na mgomo huo alikiri kucheleweshwa kwa wanafunzi hao madai yao na kuahidi kuwa wataanza kulipwa madai yao kuanzia alhamisi wiki hii. Alisema kuwa checki kwa ajili ya malipo hayo imekwisha tolewa na ipo benki kuu kwa ajili ya kumalizia taratibu za mwisho ili wanafunzi hao waweze kuingiziwa fedha zao. Hivyo aliwataka wanafunzi hao kuingia madarasani na kuendelea na masomo kama kawaida wakati mchakato huo ukiendelea. Kwa upande wake kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa (ACP) Evarist Mangalla alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kuwa hakuna mwanafunzi aliyekamatwa wala hakuna uharibifu wowote uliofanywa na wanafunzi hao. Credit: Francis Godwin Nukuu ya leo toka kwa Mtanzania... 30/05/2010
![]() Mimi sipendi sana kushabikia kufeli kwa nchi inayonihusu sana na ninayoipenda ila tuzichukue hizi takwimu kama changamoto ili tuweze kutimiza wajibu wetu kwa uaminifu pale tulipo na kupitia kazi mbalimbali tunazozifanya ili kuboresha sio tu maisha yetu binafsi bali hata kuinua hali ya uchumi ya Watanzania wenzetu. Kila mtu ajue sisi sio watazamaji bali ni mhusika mkuu katika maendeleo ya nchi yetu kwa hiyo kufeli au kufaulu yoyote kama haikugusi moja kwa moja basi ina mgusa ndugu yako au hata rafiki yako wa karibu. Badala ya kubaki tukilia kutokana na tunayoyaona naomba tuamke na kuwa chachu ya maendeleo ya nchi yetu kwa kufanya unachopaswa kufanya kwa uaminifu, juhudi na maarifa mahali popote au ofisi yoyote ulipo. Kwa kufanya hivyi mwisho wa siku utakuwa na ujasiri wa kusema MIMI NILIJITAHIDI KWA KADIRI YA NGUVU NA UWEZO ALIO NIPATIA MUNGU na utakuwa hudaiwi. - Wangaeli (akichangia kuhusu Takwimu za Tanzania) Raisi aenda Uganda kwa ajili ya ICC 30/05/2010
Raisi Jakaya Kikwete amewasili mjini Kampala, Uganda, kwa kuhudhuria mkutano wa kwanza wa nchi wanachama wa Mkataba Ulioanzisha Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (International Criminal Court - ICC). Raisi aliondoka jana kuhudhuria mkutano huo kufuatia mwaliko wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon. Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, mkutano huo unaanza leo na utamalizika Juni 11, 2010. Rais Kikwete atarejea nyumbani punde baada ya ufunguzi. Mkutano huo utapitia na kufanya marekebisho ya mkataba ulioanzisha ICC na orodha ya makosa yaliyoorodheshwa chini ya mamlaka ya ICC, kwa lengo la kuongeza au kuyatolea ufafanuzi zaidi makosa hayo. ICC ina mamlaka ya kuhukumu makosa manne ya mauaji ya halaiki, mauaji wakati wa vita, mauaji dhidi ya binadamu na visa vya uchokozi (ambalo halijapata tafsiri inayokubalika kimataifa katika mkataba huo). Mkutano huo pia utafanya tathmini ya shughuli za mahakama hiyo tangu ilipoanzishwa Agosti, 1998, mjini Rome, Italia na kupendekeza namna ya kuboresha shughuli zake. Credit: Freddy Maro via Issa Michuzi bog (picha); Gazeti la Uhuru (taarifa). Singida ndiyo mabingwa wa Kili Taifa Cup 30/05/2010
Timu ya vijana wa mkoa wa Singida ndiyo bingwa wa kombe la Kili Taifa Cup baada ya kuwabwaga Lindi kwa jumla ya mabao matatu kwa nunge (3-0). Mchezaji Kelvin Charles aliifungia Singida mabao mawili. ![]() Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi akikabidhi kombe la ubingwa wa Kili Taifa Cup kwa Kapteni wa timu ya Singida, Rajab Mohammed, na anayeshuhudia ni Kelvin Charles na anayeonekana kwa ishara ya kpiga makofi ni Rais wa TFF, Leodger Tenga (shati jeupe) na Mkurugenzi wa masoko wa TBL, David Minja (blue top, kulia mwa Lukuvi) (photo credit: Ahmad Michuzi/Jiachie blog) Raisi akutana na Wakuu wa Mikoa 30/05/2010
Rais J.M. Kikwete emekutana na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa. Kikao hicho kimefanyika Ikulu jijini Dar Es Salaam tarehe 30.5.2010. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (credit: Mroki Mroki) Msanii mkongwe wa maigizo ya redioni na kwenye runinga nchini Rajabu Hatia maarufu Mzee Pwagu alizikwa katika makaburi ya Kigogo majira ya saa saba mchana Mei 29, 2010. Waombelezaji wengi walikusanyika nyumbani kwa marehemu kigogo na baadae kuelekea makaburini kwa ajili ya maziko hayo. Wasanii wengi pia walijitokeza katika kumsindikiza katika safari yake ya mwisho. Apumzike pema Mzee Pwagu. Amin. Photo credit: Vincent Kigosi/RayTheGreates blog | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |































RSS Feed