Barabara ya "Asante Pinda" Sumbawanga-Mpanda 30/09/2010
Ipo katika ujenzi. Ni barabara ya Sumbawanga-Mpanda, Rukwa. Mkandarasi amekwishaanza kazi, anatarajia kuikamilisha ndani ya miaka mitatu. Picha imepigwa na Muhidin Sufiani. 2 Comments Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) imesema kuanzia wiki ijayo itaanza kupokea awamu ya pili ya maombi ya wanafunzi wanaotaka kujiunga na taasisi za elimu ya juu kupitia mfumo mpya wa udahili wa wanafunzi. Afisa uhusiano wa TCU, Edward Mkaku alisema kuwa zilikuwepo kasoro nyingi kwenye awamu ya kwanza ya udahili na kusababisha waombaji wengi kukosa nafasi, hivy, baada ya kukamilisha kutoa matokeo ya wanafunzi waliochaguliwa, watafungua tena mitambo ya udahili ili wenye matatizo waombe upya. Siwezi kusema utaanza siku gani na kutakuwa na awamu nyingine zaidi kumaliza matatizo yaliyopo - Mkaku.
Kwenye ofisi za TCU juzi, wanafunzi wengi walikuwa wakilalamika kutochaguliwa na wengine kuchaguliwa kwenye kozi ambazo hawakuziomba. “Mimi nimetoka Arusha nimekuja hapa kujua hatma yangu, kwa sababu matokeo yangu ya kidato cha sita yalikuwa mazuri tu lakini sikuchaguliwa na rafiki yangu niliyempita, amechaguliwa kwenye kozi kubwa kuliko ufaulu wake,” alisema mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina la Rahim Bendera. Mmoja alidai amekuta jina lake lakini namba siyo; mwingine alikuta namba yake, ila jina silo. credit: Hussein Kauli/Mwananchi Mwandishi Francis Godwin atishiwa maisha re: "RIDHIWAN KIKWETE AVAMIWA NA VIJANA WA CHADEMA..." 30/09/2010
Mimi Francis Godwin, mmiliki wa blog na mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, napenda kuelezea masikitiko yangu kwa wale wote ambao wameendelea kunipigia simu za vitisho kuhusiana na habari ya "RIDHIWAN KIKWETE AVAMIWA NA VIJANA WA CHADEMA ASHINDWA KUFANYA KAMPENI". Ijapokuwa sijapokea simu ya wahusika wenyewe, wapambe wa nje wameendelea kuwa na nguvu hata kutoa vitisho dhidi yangu kuwa iwapo nitaendelea kujifanya mkweli siku zangu zinahesabika. ![]() Francis Godwin Napenda kupingana na wote walionipigia simu nakutoa vitisho kama hivyo huku nikiamini kuwa kifo kwangu ni mipango ya Mungu na sitaogopa wala kuingia katika dhambi ya kusema uongo kwa jambo la ukweli, hivyo ni heri kuteswa hata kufa kwa kusema ukweli kuliko kuliangamiza Taifa langu kwa kuendekeza rushwa na kusema uongo kwa faida ya wachache. Pia ninapenda utambue kuwa habari hii iliyopewa nafasi ya mbele katika gazeti la Tanzania Daima la Septemba 30, 2010 huu ndiyo ambayo imeonekana watu hata wale ambao ni rafiki zangu wakubwa na viongozi wangu ninao waheshimu zaidi kuninyoshea vidole na bila uchunguzi wakinituhumu kuwa mimi ni CHADEMA. Japo si dhambi kuwa CHADEMA wala chama chochote cha siasa kwa Mtanzania, ni vema watambue kuwa mimi ni kada wa CCM na nimepata kugombea ubunge kupitia CCM na ni mjumbe wa halmashauri ya CCM wilaya ya Iringa Vijijini. Taaluma yangu haina chama, dini wala kabila. (Endelea kusoma zaidi katika blogu yake - bofya hapa) Yatokanayo... wavuti.com inakemea na kulaani vikali tishio lolote kwa raia yeyote wa nchi hasa kwa wanataaluma, hususan, wanataaluma ya habari ikiwa habari wanazoziandika ni za ukweli. Tumeshuhudia waandishi wengi wa habari toka Afrika, Asia, Ulaya na Urusi, wakitiwa katika misukosuko na wengine wao wakipoteza uhai, kwa kuwa tu wameripoti na kuchapisha habari zisizopendwa na baadhi ya watu. Tunakemea jambo hili na kuwakumbusha wale wote wenye mawazo ya kuficha ukweli kwa vitisho kuwa kamwe haitawezekana kuuzuia ukweli. Kutisha au kuua mtu si suluhisho. Watanyanyuka wengine. Waliotishwa na hata kuuawa, haikuwa mwisho wa kuripoti habari. Watakapoondoka hao, watainuliwa wengine na kuchipua. Ni roho iliyo hai. Kamwe haifi, bali hunyanyuka kwa mwingine. Hilo mlifahamu. Pole sana Francis Godwin kwa usumbufu unaoupata. Inshaallah, twashukuru kuwa hukumu ya haki hutoka kwa Mwenyezi Mungu. Akiendelea na mikutano ya kampeni katika mikoa mbalimbali, akiwa mkoani Tabora katika Jimbo la Urambo Magharibi, Jakaya Kikwete amewataka Watanzania wamkumbuke kwa mambo 8 atakapoaga Ikulu 2015. "Nimesema kuna mengi nayafanya, lakini nikimaliza kipindi changu nataka watu wanikumbuke kwa mambo nane... waseme Mungu amrehemu, yule bwana acha tu, amefanya kitu." ![]() Jakaya Mrisho Kikwete Mambo hayo aliyataja kuwa ni:
Akasema, mengi yanahitaji misaada ya wahisani, yamo ujenzi wa barabara na miundombinu ya kisasa ya maji. Ndipo akapata na fursa ya kugusia malalamiko ya safari zake nyingi za nje ya nchi. Alisema: "Wapo wanaosema nasafiri sana, sasa ningekaa pale nyumbani kwangu nikamwangalia mke wangu Salma halafu nimwambie aisee ulivyopendeza, Watanzania wangekufa njaa na Wajapani wanaotaka kusaidia, leo hii wasingeijua Kaliua... "Sasa kuyapata yote haya, lazima nisafiri. Nilikuwa Marekani, nikakutana na wahisani mbalimbali; wenyewe wananiuliza wanataka wanisaidie wapi, mimi nasema hapa na hapa na pale... kuna watu wanapesa nyingi tu." Soma habari nzima katika gazeti la Mwananchi Phillip Nyanchini MOGENDI anaiomba kura yako 30/09/2010
![]() Phillip N. MOGENDI Naomba upost hii katika blog yako Mjue Mgombea Ubunge Kinondoni kwa tiketi ya CHADEMA Bw Phillip Nyanchini MOGENDI Tembelea tovuti yake hapa phillipmogendi.com Asante! This summer, president Jakaya Kikwete was in Bukoba to attend the 100th anniversary of the Lutheran Church in the area. As part of those festivities, Josiah Kibira University College was dedicated. In his speech, Kikwete noted that it was about time for Bukoba to have a university since Bukoba people are known to be "Nshomile" (Booksmart) and yet had no University in the area. The comment was all in good fun, the crowd reciprocated with a weak cheer and laughter. See the short version of that speech CLICK HERE or HERE. To read more on the college, CLICK HERE. -- Josiah Kibira Leo tena nimejifunza jambo toka kwa KK, kwamba zaidi ya bwawa la Mtera kuwa chanzo kikuu cha nishati ya umeme nchini Tanzania, bwawa hilo pia hutumika kama kivutio cha utalii kwa wageni. Pichani ni baadhi ya watalii na wanavijiji wakiwa katika usafiri wakitalii bwawani. Mdau wa tembeatz blog, Tom wa Kimasafaris anasimulia kuwa safari huanzia kwenye mkokoteni unaosukumwa na punda. Hii ni muhimu kwani kina cha maji pembeni mwa bwawa la Mtera ni kifupi hivyo maboti hayawezi kufika pembezoni mwa bwawa na kuchukua abiria. Baada ya kufikishwa katika eneo lenye kina kirefu cha maji ambapo boti imetia nanga, ndipo watalii hushuka na kupanda kwenye boti tayari kwa ziara ya kutalii bwawani. Ili kuona picha zaidi, mtembelee KK katika blogu yake ya tembeatz.blogspot.com Matibabu ya bure CCRBT wenye fistula 30/09/2010
Brenda Msangi kwa ushirikiano na Dina Marios alifika katika kituo cha redio CloudsFM kwa lengo la kuwahamasisha wakina mama wenye fistula kujitokeza popote walipo ili kutbiwa. ![]() Brenda Msangi, Mkurugenzi wa Programu ya jamii CCBRT Fistula ni tatizo linalojitokeza kwa wakina mama wanaopatwa na tatizo wakati wa kujifungua ambapo kwa bahati mbaya njia ya kibofu cha mkono chaweza kupata tundu au njia ya haja ndogo kuchanika kiasi cha kuungana na njia ya haja kubwa na hivyo kusababisha mama kushindwa kuzuia haja ndogo, madhara ambayo husababisha kutokwa na haja ndogo mfululizo bila ya kuweza kuizuia. Tatizo la fistula inatibika ikiwa mhusika atafika hospitali. Kutokana na asili ya tatizo hili, akina mama wengi hupatwa na soni na kushindwa kutafuta matibabu, hivyo ninaungana na Brenda, Dina na wengine wote katika kuwahimiza ndugu, jamaa na rafiki kuwashauri na kuwasaidia akina mama wenye fistula kwenda hospitali kwa ajili ya matibabu. CCBRT inajitolea kugharimia usafiri, malazi, chakula na matibabu bure kabisa. Ikiwa unalo tatizo, au unamfahamu yeyote mwenye tatizo hili, basi piga simu namba 0752 678263 POPOTE ULIPO na utaelekezwa jinsi ya kupata usafiri wa kufika hospitali ya CCBRT, Msasani, Dar es Salaam. credit: Dina Marios blog Is CHADEMA’s Education Plan a Hoax? 30/09/2010
Naomba upost hii article kwenye blog yako, asante!
CHADEMA's EDUCATION PLAN IS NOT A HOAX IT IS A LONG AWAITED In Response to Tayari's Article : Is CHADEMA’s Education Plan a Hoax? by Deus Valentine I am writing this in response to the article "Is CHADEMA’s Education Plan a Hoax?" dated September, 16 2010 by Emmanuel Tayari. I took my time considering how I would respond to it. Anyway I feel obliged to respond to it for I believe the arguments upon which the piece of work was based were somewhat hoodwinking. I am not a member of CHADEMA or any political establishment back home. But I have developed keen interest and have been trained in Economics and Diplomacy therefore it only makes sense for me to put a word where I believe the arguments are misleading. I am going to quote some of the particular lines from the aforementioned article to highlight what iIbelieve is obfuscation contained in the article. CHADEMA na viongozi wa dini wateta 30/09/2010
Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Dini inayosimamia masuala ya Rasilimali na Maadili, Askofu Mkuu Paul Ruzoka wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Tabora, na viongozi wengine wa dini waliokutana na CHADEMA wamekiasa chama hicho kufanya kampeni kwa misingi ya haki, utulivu na kukubali na kuheshimu matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, 2010. Viongozi hao wa dini walisema kuwa kukataa matokeo ni chanzo kikubwa cha uvunjifu wa amani na husababisha nchi kuingia kwenye matatizo makubwa kisiasa. Wakawaomba viongozi wa vyama vya siasa kuacha tabia ya kushambuliana majukwaani, badala yake wanadi sera na Ilani za vyama vyao. Dk. Slaa akizungumzia maombi ya viongozi hao wa dini kuwa wakubali matokeo yatakayotangazwa na Tume, alisema “tuliwaambia vurugu baada ya uchaguzi zinatokana na matokeo, nasi tumesema wao wasitwambie tu tupokee matokeo, ila wahakikishe taratibu za haki zinafuatwa katika kupata matokeo”. Tume hiyo imekuwa ikuzungumza na viongozi wakuu wa vyama vya siasa katika kipindi hiki cha kampeni za Uchaguzi Mkuu na tayari wameshakutana na Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na uongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Willibrod Slaa na John Mnyika. | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |















RSS Feed