Jana nilikuwa mmoja wa watu wenye furaha baada ya kuiona TBC hewani, lakini kwa bahati mbaya tabasamu langu halikukawizwa kutiwa nyongo mara mbili.
Basi itakuwa ni kiherehere changu tu kimenizodoa sasa inabidi nitulie mpole ka maji ya mtungini alfajiri. Suala la matumizi ya habari ya aina yoyote ile lina sheria zake na taratibu za kufuatwa kabla ya kutumika. Aidha, yapo makubaliano maalumu baina ya mtoa taarifa na yeyote ambaye angependa kuitumia taarifa hiyo, iwe ni taarifa kwa njia ya picha, maandishi ama sauti alimradi ni ya kidigitali, basi huwa inalindwa na sheria za World Intellectual Property Organisation kifupi WIPO na Digital Copyright Millenium Act, kifupi, DCMA. Zipo haki ambazo mmiliki huzitoa kwa kuridhia makubaliano ya Creative Commons (CC) au maelezo ya Terms and Conditions au Privacy au Disclaimer nk. Yeyote anayetumia kazi hizo hupaswa kuonesha shukrani kwa kueleza alikoitoa habari kwa namna yoyote ikiwa ni pamoja na kumtaja mwenye habari au kuweka linki ya ilikotoka habari (chanzo cha habari). Inapotokea hali ya wizi au matumizi yasiyo ya haki ya habari, mwenye habari anahaki ya kumwandikia aliyetumia kazi yake isivyo, na kumtaka airekebishe au aombe samahani ama aiondoe habari hiyo (na wakati mwingine afanye mawili kati ya hayo) vinginevyo, ni rahisi sana kumburuza mtu huyo mahakamani. Zipo sheria zinazotuatwa na nchi kadhaa zimeridhia na kukubaliana na sheria hizo. Kadiri matumizi ya intaneti yanavyoongezeka, ndivyo sheria hizi zinavyozidi kuboreshwa na kutumiwa katika nchi mbalimbali. Aliwahi kuniibia kazi zangu mtu mmoja na baada ya kukosa muafaka naye, ilinibidi kumripoti, na blogu yake ilifutwa kabisa mtandaoni mara moja. Nakubali kuwa nimewahi na huenda nitaendelea kutumia kazi za watu pasipo ridhaa zao rasmi, si kwa kusudio baya hata kidogo, aidha ni kwa kuwa ni vigumu kuwapata wahusika halisi wa kazi hizo, au itanichukua muda mrefu sana kusubiri kupata haki ya matumizi hayo, hivyo nimekuwa nikizitumia na kusema nilikozipokea na kisha inapobidi kuziondoa, huwa ninafanya hivyo punde tu ninapotakiwa kufanya hivyo na mmiliki husika. Tujifunze (mimi mmojawapo) kujali na kuheshimu itakikanavyo kazi za watu wanazozitokea jasho, kutokufanya hivyo tutawavunja moyo wengi na hivyo tukose mengi. Add Comment Habari zinasema kuwa siku ya Jumamosi, maafisa katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha mjini Philadelphia nchini Marekani wamefaulu kukamata paundi mbili za madawa ya kulevya aina ya hashish na ounce moja na nusu ya marijuana zilizokuwa zimefichwa katika kifaa cha mchezo wa chess. Maafisa hao waligundua siri ya urembo baada ya kustukia kibao cha chess kuwa na uzito usio wa kawaida. Msemaji wa kampuni inayohusika na kitengo hicho cha vifurushi, Steve Sapp alisema kuwa bangi hiyo ilisafirishwa toka Tanzania lakini hakusema ilitakiwa kumfikia nani. Polisi wanatathmini kuwa madawa hayo ya kulevya yatakuwa na thamani ya dola za Kimarekani $ 30,000. Madawa hayo yatateketezwa. Hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo. Ilikuwa siku siku ya kutabasamu baada ya kuweza kuona tovuti ya TBC mtandaoni. Ni matumaini yangu kuwa mwanzo huu mzuri utaendelezwa na kuifanya TBC kuwa kitovu kizuri cha habari za ndani na nje ya Tanzania ili kuitangaza nchi yetu katika anga za Kimataifa. Unaweza kubofya picha hapo na itakupeleka moja kwa moja kwenye tovuti ya TBC ambayo anwani yake ni http://www.tbc.go.tz Hongera timu nzima ya TBC kwa kuanzisha kwa vitendo jukumu hili! ATM card # skimming and PIN capturing 27/10/2009
Click HERE to see the videos (1. Demo 2. Actual real life stealing attempt). Pata ile kitu roho inapenda... 27/10/2009
Hii kanitumia rafiki anasema: Kama Roho yako inapenda Gari la Kifahari …..Why are you going for the expensive House !! Na Kama Roho yako itapenda kuwa na DSTV … Why should you build a good house while you have somewhere to lay down your ribs!! Satisfy your Soul First and your Soul will satisfy you in turn!! ![]() mfano wa panels za umeme jua Mdau na rafki yangu anaomba mawasiliano yoyote ya Kampuni, Kikundi au Watu wanajishughulisha na nishati ya umeme itokanayo na jua nchini Tanzania hasa katika mkoa wa Dar Es Salaam. Shukran! Mdau mmoja wa kundi pepe fulani ametoa mawasiliano haya: Francis wa Rex Investment, the owner; 0713607533 I received this pictorial analysis from a good friend of mine, Dr. Kiva showing how Fernando Torres and the team mates managed goal defeat their rivals on a match that was staged as 'Clash of the titans' I think it was a wonderful goal and really a superb work by Fernando Torres. Winning 2 - 0 against Manchester United brought a very good feeling to the kopites, even the rivals were happy just to see ManU torn down. I guess 'dislike' is the price you get paid for being big and tough. Sorry ManU, we won and you lost, I don't know what to say of the referee but whatever it was, it helped us. Liverpool 2009/10 needs to pull up their socks this season or else, we are a punching bag and laughing stock! Soga za momi wa kijiweni... 26/10/2009
Juzi ile, nanihii alisema stima itakuwa kwishnei kwenye vijumba sita hivi vya hapa kijiweni. Ujue jamaa mi n'lishindwa nimshangaeje, maana ndo nlikuwa nasubiria tu lini atasema hivyo, mwaka ndo unakaribia kukatika huu. Sijui cha juu safari hii anapata nani. Si unajua siye kijiweni kazi yetu kupokea tu taarifa, utauliza vipi? na hata ukiuliza unadhani utakosa jibu? ah, tena unapewa majibu mwenyewe unakubali na kuchangia kwenye jibu, ama vipi unapewa mengi unaambiwa uchague la kukubaliana nalo kisha jivute. Stori za mwaka elfu mbili na nne umezisahau? enzi hizo wamelipua kisemo kigeni 'la nina'? Basi keleleee kelele wakati huo ni ukamee, ukame, ukamee, ukame, yaani kero tupu! si umeme hamna shauri ya ukame mabwawa hayana maji?! Kulaleki walahi, si mwaka elfu mbili na tano ikatokea 'el nino'? mvua hiyo babake kuku hatoki bandani lakini umeme hakuna! Usichekelee, umeme ulikatika. sababu? si mabwawa yalijaa matope! Ebo, 'asa we unategemea matope yale yakiingia kwenye mashine itafanya vipi kazi? unakuwa na akili ka za ukutiukuti bwana? Mashine ya kunyonyea tope haijagunduliwa bado we dogo, usijifanye mjuaji. Eti? ...! Rudia tena? ...ndi! tuna mafundi? mafundi gani? waliosoma injiniaring au? we bwana usitake kuleta msala hapa Skiza, mvua iwepo isiwepo umeme kukatika Tanzania ni ada, sawa dogo? Kuna sababu chungu mbovu za kwa nini umeme ukatike na kama akili zako nyingi za kushauri eti tufanye hivi na vile ndo umeme usikatike, dogo, hizo dili kama hazina namna ya kuchomeka ten pasenti hapo utakuwa umefulia. Ebu tufanye dili la maana. We si unaenda kusoma USAgara? alaaa, samahani, kumbe ulimepata mchongo wa UKerewe kwa Bi Mkora? okei, sasa halijaharibika jambo, fanya hivi, utafute wawekezaji wa kitasha huko..., alimradi si kwenye suala la umeme, pengine nishati nyingine, tuna maji, gesi asilia, jua miezi sita, na nini na nini... Wao waje kuwekeza na kwingine tu, kuna vitega uchumi kibao! Kwanza we si umesoma jografia? na historia? si unaijua nchi? sasa wasomeshe hao watasha, 'afu wao wakija hapa miradi yao hiyo ya kiwekezaji inabidi wanunue jenereta! Sasa hapo ndo kwenye dili yenyewe, wananunua majenereta ya hapa hapa dukani kijijini kwetu kwa mshikaji Sefu yale yake kayanunua Dubaiii... Dili hilo mwanangu, 10% ya kutesea ughaibuni na mabinti wa kitasha hukosi, au vp? Hapo shwari mkubwa. Chakarika dogo... Poa! This is what I read... 25/10/2009
I read a lot of stuff online yesterday, and this is among my top picks for the day...
What are you reading? What are your picks? ...else you can read my pick. 2009 Diwali Celebrations 24/10/2009
See some more photos at Boston.com's Big Picture | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |






















RSS Feed