SALAM ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA,
TAREHE 31 DESEMBA, 2011 
Ndugu Wananchi; 

Leo tunauaga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka 2012. Naungana nanyi Watanzania wenzangu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na bahati ya kuiona siku ya leo. Wapo ndugu, jamaa na marafiki zetu wengi ambao hawakujaaliwa kuwa nasi kwa kuwa wametutangulia mbele ya haki. Tuzidi kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awape mapumziko mema na sisi tuendelee kumuomba Mola wetu atujaalie rehema na neema tele katika mwaka ujao. 

Mapitio ya Mwaka 2011 na Matarajio kwa Mwaka 2012


Miaka 50 ya Uhuru


Ndugu wananchi; 

Mwaka 2011 ulikuwa mwaka wa aina yake na wa kihistoria kwa nchi yetu na wenye mchanganyiko wa mambo. Kulikuwa na matukio ya furaha na majonzi na ulikuwa mwaka tuliopata mafanikio mengi na changamoto mbalimbali. Tumeweza kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa heshima stahiki kama nilivyoelekeza katika hotuba yangu ya kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011. Tumezitumia vizuri sherehe hizo kufanya tathmini ya maendeleo tuliyoyapata tangu Uhuru mpaka hapa tulipo sasa pamoja na kutambua changamoto zilizo mbele yetu.

Hakika tumepata mafanikio makubwa sana katika miaka 50 hii ya Uhuru wetu kuliko yale yaliyopatikana katika miaka 77 ya ukoloni wa Wajerumani (miaka 34) na Waingereza (miaka 43). Pamoja na mafanikio hayo tuliyoyapata bado nchi yetu ni miongoni mwa nchi maskini sana duniani hivyo bado tunayo kazi kubwa sana ya kufanya mbele yetu. Katika tathmini iliyofanywa na kila Wizara na Idara za Serikali, mambo yanayostahili kufanyika miaka ijayo pamoja na mikakati ya kufikia malengo hayo, yameainishwa vizuri. 

Mpango wa Maendeleo

 
 
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF- Chama Cha Wananchi)

Office of the Secretary General
Party Headquarters, P.O. Box 3637, Zanzibar, Tanzania

Tarehe : 31/12/2011 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati ya Utendaji ya Taifa ya Chama Cha Wananchi (CUF) imefanya kikao chake cha kawaida cha siku mbili mjini Zanzibar tarehe 30 – 31 Desemba, 2011 chini ya Katibu Mkuu wa Chama, Maalim Seif Sharif Hamad.

Pamoja na kujadili ajenda kadhaa za kawaida kuhusiana na mambo ya utendaji katika Chama, Kamati ya Utendaji ya Taifa pia ilipata nafasi ya kupokea taarifa ya kina kuhusu hali ya kisiasa ndani ya Chama kutoka kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Chama kupitia Kamati yake Ndogo ya Nidhamu na Maadili. Taarifa hiyo ilijikita zaidi katika njama zinazoendeshwa na wanachama 14 wakiongozwa na Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed zenye mwelekeo wa kutaka kukivuruga Chama.

Kamati ya Utendaji ya Taifa imeridhika kwamba kuna hoja za msingi na ushahidi wa kutosha dhidi ya wanachama hao 14 unaoonesha kuhusika kwao na njama hizo. Wanachama hao ni:

1. Hamad Rashid Mohamed
2. Doyo Hassan Doyo
3. Shoka Khamis Juma
4. Juma Said Saanani
5. Yasin Mrotwa
6. Mohamed Albadawi
7. Mohamed Masaga
8. Doni Waziri
9. Yusuf Mungiro
10. Haji Nanjase
11. Ahmed Issa
12. Tamim Omar
13. Amir Kirungi
14. Ayubu Kimangale

Kwa mujibu wa Katiba ya Chama, kifungu cha 63 kinachozungumzia Wajibu wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, kifungu cha 63 (1) (d) kinafafanua wajibu huo kuwa ni “kulinda na kuendeleza heshima ya Chama na Serikali zote halali za nchi.” Kifungu cha 63 (1) (j) kinaelezea wajibu mwengine kuwa ni “kuwachukulia hatua za nidhamu viongozi na wanachama wanaoshutumiwa kwa makosa mbali mbali kwa kufuata masharti ya Katiba hii na kanuni zitakazotungwa mara kwa mara kwa mujibu wa katiba hii.”

Kwa kuzingatia hali hiyo, Kamati ya Utendaji ya Taifa imeridhika kwamba kuna haja ya kutumia uwezo iliopewa chini ya kifungu cha 62 (1) cha Katiba ya Chama kuitisha kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama ili kutafakari hali hiyo, kusikiliza tuhuma zinazowakabili wanachama hao, kuwapa nafasi ya kuwasiliza na kujitetea na kisha kuchukua hatua kama litakavyoona inafaa.

Kikao hicho cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kitafanyika Zanzibar, tarehe 04/01/2012, katika Ukumbi wa Hotel ya Mazson.

Kamati ya Utendaji ya Taifa inawaomba wanachama na wapenzi wote wa CUF kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki na kutoa nafasi kwa vikao vya Chama kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba ya Chama.

HAKI SAWA KWA WOTE

JULIUS MTATIRO
NAIBU KATIBU MKUU (TANZANIA BARA)

KATIBU WA KAMATI YA UTENDAJI TA TAIFA (CUF NATIONAL CENTRAL COMMITTEE).
31 Disemba 2011,
ZANZIBAR. 
 
 
Four years ago, I joined graduates.com (the name is self explanatory), but my profile's been dormant ever since. 

So today, I just did to it what I did to my then Hi5 and Zorpia accounts, i.e. delete and get rid of them.

Just in case you need to do the same, here is the link: graduates.com/ProfileRemove.aspx

You have to login first with the username and password used to register the time you opened the account (follow instructions on the site in case you forgot your credentials), then you will be presented with a window (see screeshot below) to complete the deletion process.
 
 
Tanzania Music Television (TMTV) ni TV ambayo unaweza kuiona Online na pia ktk DECODER.

TMTV itazinduliwa hivi karibuni pindi maandalizi yatakapokuwa tayari. Kwasasa waweza kuendelea kuangalia Chanel hii bure kupitia computer yako kwa linki hii www.tmtv.co.tz.

Mauzo ya DECODER yataanza pindi decoder zitakapo kamilika.Ili watu waweze kuona TMTV kupitia TV zao za majumbani.

Vile vile ni TV ambayo inarushwa kwa teknonlojia mpya ambayo unaweza kuangalia TMTV kupitia, MOBILE, GAMES Kama XBOX360, SMATPHONES aina zote kama za mobile kama Nokia, Motorolla, Samsung, LG Zenye 3G n.k pia kupitia Android na Decoder TRU SATTELITE. 

TMTV ni kwa ajili yetu sote, isitoshe ni ya kijanja na imelenga kutuburudisha kokote tulipo kupitia simu zetu na computer zetu. Ikiwa kama MTV chanel.

TMTV ni music chanel ambayo inaonyesha music ya kibongo mchanganyiko 24/7. 

TMTV ina vipindi 10,

BENDI ZETU
SWAHILI HIP HOP
ZILIPENDWA
TAARABU
NYIMBO ZA ASILI
NYIMBO ZA DINI
SALAMU BOX
BONGO BOX
TMTV TOP 10
VIPAJI na
MUSIC NEWS

Tusiogope kuisapoti bidhaa yetu ya nyumbani kabisa. Tuipe ushirikiano wa kutosha. 
Link www.tmtv.co.tz Downlod microsoft Silverlight itajitokeza ktk screen, kama haijafunguka yenyewe.
Email. info@tmtv.co.tz 
 
 
Kamati  ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es Salaam, imeunda kamati ya kuchunguza sababu za kushuka kwa ukusanyaji wa kodi mbalimbali ikiwemo ya majengo iliyoshuka kutoka Shilingi Bilioni 2  mwaka 2009/10 hadi kufikia Shilingi Milioni 500 mwaka 2010/11.

Hayo yalijitokeza  katika kikao  cha kamati hiyo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali.

Hoja kuhusu mapato ilikuja baada ya wajumbe kuanza kujadili mapato yatokanayo na kodi inayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa niaba ya manispaa za Jiji la Dar es Salaam.

Mbunge wa Ilala Azzan Zungu alikuwa mjumbe wa wa kwanza kuchangia  hoja hiyo ambapo  alisema kabla ya kurekebishwa kwa  sheria, ukusanyaji wa mapato ya Jiji yalikuwa yanafanywa na halmashauri za manispaa ambazo kwa pamoja ziliweza kukusanya wastani wa Bilioni 2/= kwa mwaka lakini sasa, wakati kazi hiyo ikifanywa na TRA  mapato yamekuwa hayafikii hata robo ya makusanyo ya awali, “Hapo mwanzo halmashauri zilikuwa zinapata mapato ya kutosha na kuweza kujiendesha ipasavyo lakini tangu TRA ilipopewa jukumu hili hali imekuwa tofauti, nadhani kuna haja ya kurudisha majukumu haya kwa halmashauri kama ilivyo kuwa mwanzo,” alisema Zungu.

Kwa upande wake, Mbunge wa Segerea, Dk. Makongoro Mahanga, alisema hakusa sababu za msingi kwa mapato kushuka, “Cha msingi hapa ni kurudisha majukumu kwa halmashauri kwa sababu sasa tunashindwa kuendeleza miundombinu, elimu, afya na huduma nyingine kwa sababu ya  kukosa fedha ambazo kama tutazisimamia vizuri tunaweza kuzipata,” alisema Dk. Mahanga.

Hata hivyo Mwenyekiti wa kikao hicho Saidi Meck Sadiki, alisema kama hiyo haina uwezo wa kurejesha kwa halmashauri, jukumu la kukusanya mapato na kwamba mamlaka hayo ni ya Bunge. Alisema jambo linaoweza kufanywa na kamati yake ni kuangalia taratibu nyingine za kushughulikia tatizo hilo.

Mbunge wa Ubungo John Mnyika, iliiomba kamati ikubali kuunda kwa kamati ya kuchunguza kiini cha kushuka kwa mapato,“Tusikimbilea kurudisha majukumu kwa halmashauri wakati tatizo hatulijui  naomba iundwe tume itakayochunguza tatizo hili,” alisema.

Mwenyekiti wa kikao hicho, alikubali hoja ya Mnyika ambayo iliungwa mkono na wajumbe.

Kamati hiyo itaongozwa na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda na wajumbe ni Mnyika, Zungu, Mbuge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile, Mkurugenzi wa Manispaa ya  Ilala Gabriel Fuime na  Meneja wa TRA Matrida Kunenge.

via Mwananchi
---

Kujua ni kwa nini "nimekurupuka kukimbilia" kusema "huu ni wizi tu" soma barua ya Mbunge wa Kigamboni kwa Waziri husika kuhusu kinachofanyika pale feri, ambapo ni sehemu ya Jiji hilo hilo lililopungukiwa mapato. Hiyo ni sababu mojawapo,  nyingine ni uzembe/kukosa umakini na kuachia mianya ya kukwepa ushuru.
 
 
BUNGE LA TANZANIA

OFISI YA MBUNGE WA JIMBO LA KIGAMBONI

Kumb na: KIG/KVK/VOL.1/4                                                                                                                                  29 Disemba 2011

Mhe. Dkt John P. Magufuli (MB)
Waziri Wizara ya Ujenzi
Dar es Salaam

YAH: KUSUDIO LA ONGEZEKO LA VIWANGO VYA NAULI KATIKA KIVUKO CHA KIVUKONI-KIGAMBONI 

Kichwa cha habari hapo juu chahusika.

Wananchi wa Jimbo la Kigamboni wamepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kusudio la kuongeza nauli za abiria, magari na vyombo vingine vinavyotumia huduma ya kivuko kati ya Kigamboni na Kivukoni kuanzia tarehe 1 Januari 2012. 

Kivuko hiki ni kiungo muhimu kwa wananchi wanaoishi upande wa Kigamboni ambao wengi wao ni watu wa kipato duni na hawana ajira za kudumu. Ongezeko la nauli kwa asilimia 100 ni kubwa sana na litawaathiri kiuchumi. Nimepigiwa simu nyingi na kuletewa malalamiko mengi katika siku ya leo kuhusiana na mpango huu wa kuongeza nauli. Wananchi wanataka kujua ni vigezo gani vilivyotumika kufikia nauli hizi mpya; vyombo gani vilivyopendekeza, kupitisha na kuidhinisha nauli hizi na wanataka kujua kwa nini hawakushirikishwa katika mjadala wa nauli mpya. 

Pamoja na ongezeko kubwa la wakazi na magari yanayotumia huduma ya kivuko, cha kushangaza ni kwamba mapato kwa siku yamekuwa ni takribani Tsh 8 milioni kwa siku kwa muda mrefu sasa. 
Ni dhahiri kumekuwa na upotevu mkubwa mikononi kwa watumishi wasio waaminifu wa kivuko. Mapato mengi yanapotea kwa njia zifuatazo:

1. Baadhi ya watumishi wa kivuko kukatisha risiti hususan za magari kwa kutumia vitabu bandia.
2. Baadhi ya watumishi kuziuza tena tiketi zilizotumika badala ya kuzichana.
3. Baadhi ya watumishi na askari wanapitisha magari na abiria baada ya kupokea malipo ya pembeni.

Vilevile mafuta ya vivuko huuzwa kwa wavuvi wadogo wadogo katika maeneo ya Feri.

Mambo haya yote yanafanyika pasipo kificho, binafsi nimeshawahi kushuhudia yote niliyosema hapo juu yakifanyika na kuyatolea ripoti kwa uongozi wa kivuko.

Ninaamini kuwa hatua zifuatazo zikichukuliwa mapato ya kivuko hiki yanaweza kufika zaidi ya Tsh 13 milioni kwa siku:

4. Kudhibiti uuzaji wa tiketi za abiria na magari.
5. Kudhibiti ununuzi, utunzaji na matumizi ya mafuta yanayotumika kwenye vivuko.
6. Kudhibiti idadi ya watu na magari yanayovuka bila kulipia huduma hii.
7. Kupunguza gharama za uendeshaji ikiwa ni pamoja na kupunguza idadi ya vibarua.

Kutokana na unyeti wa suala hili, nashauri zoezi hili lisitishwe ili kutoa fursa ya kujadiliana kuhusu upandishaji wa nauli na maboresho ya huduma hii kwa kushirikiana na wadau na wawakilishi wa wananchi katika Jimbo la Kigamboni.

Natumaini mapendekezo haya yatafanyiwa kazi ili kuepuka kuwabebesha mzigo wa gharama za uendeshaji wakazi wa Kigamboni wanaotumia huduma ya kivuko pale Feri.

Naambatanisha nakala ya barua yangu ya tarehe 19 Januari 2011 yenye kumbukumbu namba KIG/KVK/VOL.1/1 kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa TEMESA ambayo ilitoa mapendekezo ya njia ya kuboresha huduma na vile vile kutaka ushirikishwaji wa wadau katika suala la ongezeko la nauli. Barua hii haijajibiwa hadi hivi sasa.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.
Wako katika ujenzi wa Taifa

Mhe. Dkt Faustine Ndugulile (MB)
MBUNGE
 
Nakala:

1. Mhe. Mizengo Pinda (MB)-Waziri Mkuu
2. Mhe. Mecky Sadick-Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam
3. Waheshimiwa Madiwani wote-Jimbo la Kigamboni
4. Wenyeviti wa Serikali za Mitaa-Jimbo la Kigamboni
5. Mkurugenzi Mkuu-TEMESA 
 
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Kilimanjaro, imemuachia huru, Padri wa Parokia ya Kilema ya kijiji cha Lego wilayani Moshi Vijijini ya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, Stanslaus Sala, baada ya kukutwa hana hatia ya kesi ya kumlawiti mtoto wa miaka 16.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Simon Kobelo, baada ya kusikiliza ushahidi wa mashahidi wanne akiwemo baba wa mtoto huyo na mlinzi wa Parokia ya Mtakatifu Theresa Kilema ambaye ndiye wa kwanza kuelezwa tukio hilo na mtoto huyo.

Hakimu huyo alisema mshitakiwa huyo hana kesi ya kujibu kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kumleta mahakamani motto aliyetendewa kitendo hicho, daktari aliyempima mtoto huyo na PF3 ya kuonyesha kuwa tukio hilo liliripotiwa polisi na mtoto kwenda kutibiwa, “Pamoja na ushahidi ulitolewa na mashahidi wanne walioletwa mbele ya Mahakama hii, lakini aliyetendewa kitendo hicho ambaye ni mlalamikaji hajafika kutoa ushahidi wake, daktari aliyempima na hakuna PF3 hivyo Mahakama inamuachia huru mshitakiwa huyo kwa mujibu wa kifungu namba 239 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai,” alisema Kobelo.

Wakili wa serikali, Javelni Rugaihuruza, alidai kuwa baba wa mtoto huyo, Amathy Lyamuya alidai kuwa hakumkagua mtoto wake na wala hakuwahi kujua kuwa alifanyiwa kitendo hicho na kwamba alilazimishwa kwenda kutoa taarifa polisi juu ya tukio hilo.

Naye, mlinzi wa Parokia hiyo, Paul Munga, alidai mahakamani kuwa siku ya tukio, Padri huyo alimtuma kwenda kumuita mtoto huyo baada ya kuondokana naye awali na kwenda naye kusikojulikana kwa madai anakwenda kumwadhibu na ndipo mtoto huyo alipomueleza juu ya kitendo alichofanyiwa na kwamba hakumuona akimfanyia kitendo hicho.

Awali, katika maelezo ya awali yaliyowasilishwa mahakamani hapo, ilidaiwa kuwa kuwa kinyume na kifungu namba 154 (1) (a) sura namba 16 ya sheria ya kanuni ya adhabu kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, mshtakiwa huyo alimlawiti kijana huyo ambaye alikuwa mtumishi wa kutunza mifugo kwenye parokia hiyo.

Ilidaiwa kuwa tukio hilo liliokea Oktoba 30, mwaka huu majira ya saa 2:00 Usiku ambapo kijana huyo alikuwa amelala chumbani kwake ambako mlinzi wa Parokia hiyo alimfuata chumbani na kumuamsha na kumweleza kuwa anaitwa na padri huyo.

via  Nipashe
 
 
Katika hatua nyingine, Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), kimesema kuwa kinafanya mazungumzo na  Kafulila kuangalia uwezekano wa kufungua kesi ya kupinga wabunge kupoteza nafasi ya ubunge wao pale wanapofukuzwa kwenye vyama.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Rais wa TLS, Francis Stolla, alisema kitendo cha chama au watu wachache kumfukuza uanachama mbunge aliyepigiwa kura na wananchi walio wanachama na wasio wanachama, ni kukiuka misingi ya demokrasia, “Sisi kama wanasheria tuna mpango wa kulifikisha suala hili mahakamani, ili kuitaka serikali iweke kifungu cha sheria kinachozuia mbunge au kiongozi yeyote aliyechaguliwa na wananchi kupoteza nafasi yake pale anapofukuzwa uanachama,"alisema Stolla.
 
Alisema kuwa katika marekebisho ya sheria, panatakiwa Bunge liweke kanuni za kumfukuza mbunge, siyo chama. 

Kuhusu mabadiliko ya katiba, alisema hana imani nayo kama kweli yataleta tiba ya tatizo hilo ila alisema ni miongoni mwa mambo watakayoyapigia kelele katika harakati zao. 

Wakati TLS ikijipanga kusimamia mkakati huo, wanasheria wengine na wataalamu wa siasa nchini , wamekosoa uamuzi wa NCCR- Mageuzi kumfukuza Kafulila wakisema kuwa umetokana na mfumo mbovu wa sheria.

Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Harold Sungusia,  amesema kuwa hali hiyo inatokana na tatizo la sheria zinazowalinda wanasiasa walioko madarakani kuliko wananchi, “Tuna tatizo katika mfumo wetu wa sheria, zinajichanganya zenyewe. Lengo la sheria ni kuleta utawala wa demokrasia, lakini inajichanganya kwa kuwazuia wananchi. Mfumo huo unawafanya watu wachache kuhodhi madaraka kama vile ilivyokuwa enzi za chama kushika hatamu,”alisema Sungusia. 

Akasema sheria hizo zilitungwa katika mfumo wa chama kimoja ili kulinda maslahi ya wachache ndani ya chama. 

Huku akigusia kesi ya mgombea binafsi ambayo ilinguruma kwa muda mrefu na hatimaye serikali kushinda, alisema kwa mfumo uliopo sasa, wanasiasa wanawajibika kwa vyama siyo wananchi, “Kwa hali iliyopo sasa, wanasiasa wanatumikia vyama siyo wananchi waliowachagua, ndiyo maana wanaweza kumwondoa muda wowote wakitaka na mtu akishaondolewa kwenye chama anakosa sifa ya kuwa mbunge,”alisema.

Sungusia na kutoa mfano wa Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika ambaye aliamua kuhama chama chake baada ya kutokea kutokuelewana na wenzake, na  kuanzisha chama kipya .

Alisisitiza kuwa kinachotakiwa sasa ni  kuwepo, sheria inayoruhusu wanasiasa kuhama vyama na ubunge wao pale wanapokorofisha sehemu moja, “Kunatakiwa kuwepo na ‘crossing of the floor’ kwamba mtu akihama chama kimoja aruhusiwe kwenda chama kingine na ubunge wake. Kwa mfano Bingu wa Mutharika wa Malawi alipojiondoa kwenye chama chake kwasababu ya kupambana na rushwa alianzisha chama chake na bado akaendelea kuwa rais,”alisema Sungusia. 

Hata hivyo Sungusia alitilia shaka mabadiliko ya katiba ya sasa akisema kuwa siyo mwarobaini kwa kila kitu, “Mabadiliko ya katiba siyo mwarobaini kwa kila kitu, wakati mwingine mnaisingizia katiba kila kitu. Sina imani na mabadiliko haya kwasababu wanaoyaongoza hawataki mabadiliko, kwahiyo sidhani kama yatasaidia kutatua tatizo kama hili,”alisema. 

Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Gaudence Mpangala alipohojiwa, aliunga mkono hoja ya ubovu wa sheria akisema wananchi wamewekwa kando kwenye mfumo wa demokrasia, “Hilo ni tatizo la ubovu wa kisheria na ndiyo maana tunatakiwa kubadilisha katiba ili kupata nguvu ya wananchi,” alisema Profesa Mpangala na kuongeza; “Wananchi wanakwenda kujiandikisha, wanapiga kampeni, kisha wanapiga kura, halafu leo juhudi zote hizo zinakwamishwa na kikundi cha watu wachache tu ndani ya chama.” 

Profesa Mpangala alipendekeza kuangaliwa upya kwa suala la mgombea binafsi ili kuwapa nguvu wananchi, “Siyo lazima mwananchi achague mtu aliyependekezwa na chama. Inapaswa tuwe na mgombea binafsi ili watu wachaguliwe bila kujali vyama. Hilo lilipingwa vikali na CCM. Ingawa kesi ilikwenda mahakamani na kushinda, bado serikali imekata rufaa na kushinda,” alisema Profesa Mpangala na kuongeza; “Tulipoingia kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, ilitakiwa katiba ibadilishwe ili iendane na mfumo huo, lakini haikufanyika, hadi sasa mchakato wa mabadiliko ya katiba unaendelea kubanwa.”
 
Alishauri wadau wa sheria na siasa kuendelea kupiga kelele ili wananchi wapewe kipaumbele katika mabadiliko ya katiba, “Kinachotakiwa hapa ni kuendelea kupiga kelele tu, kama ni wanasheria, kama ni wanasiasa hata wana habari. Tukiliacha hili tutakuja kupata shida huko mbeleni,”alisema Profesa Mpangala.

via  Mwananchi
 
 
Katibu Mwenezi wa NCCR-Mageuzi Mkoa wa Arusha, James Ndarvoi na waliokuwa viongozi wengine 8 wa chama hicho, wamejiuzulu uongozi wakipinga kufukuzwa uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila. 

Viongozi hao sasa wametangaza kujiunga na CHADEMA, kwa madai kwamba ndicho chama pekee chenye nguvu na hoja za ukweli kuhusu upinzani, kikilinganishwa na vyama vingine vya upinzani. 

Ndarvoi alitangaza uamuzi huo jana alipozungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.

Akizungumza na  HabariLeo kwa njia ya simu, Ndarvoi alisema kabla ya kuchukua uamuzi huo, aliwasiliana na viongozi wake wa makao makuu kutaka kufahamu kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya NCCR-Mageuzi, kiliwakilishwa na wajumbe gani, kwani wa Arusha hawakuitwa kwenye kikao hicho, lakini alikatiwa simu, “Sasa kama wanakata simu wanafahamu ni kosa wamelifanya; huo uamuzi wa kumfukuza huyu mbunge aliyekuwa analeta chachu katika chama umefanywa kwa hila na umetushtua na kutusikitisha, kwa sababu ni batili na umefanywa na wachache kwa maslahi binafsi bila wajumbe wa mikoani,” alisema Ndarivoi. 

Ndarvoi alisema maamuzi yalichuliwa na Halmashauri Kuu ya NCCR -Mageuzi hayakuzingatia maslahi na uhai wa chama, badala yake yalilenga kulinda kundi na maslahi ya watu fulani, ndiyo maana hata baadhi ya wajumbe halali kutoka mkoani  kwake, akiwemo yeye kama Katibu wa Jimbo, hawakualikwa baada ya kuhisiwa kwamba wangepinga, “Mara baada ya kupata taarifa ya kuwepo kikao cha NEC kupitia vyombo vya habari, tulitarajia kupata mwaliko rasmi kama wajumbe. Lakini hatukupata, tulipojaribu kuhoji waliotuwakilisha, hatukupata majibu sahihi, hali inayotufanya tuamini pengine tuliwakilishwa na mamluki,” alisema Ndarvoi.

Ndarvoi aliendelea kusema kuwa Kafulila alikuwa na haki ya kuhoji kuhusu ruzuku inayoishia makao makuu, ila kwa sababu ya ufisadi wa watu wachache, hawakutaka kuhojiwa hilo na kuamua kumtimua. 

Alitaja viongozi wenzake waliojiengua na kujiunga na Chadema kuwa ni Katibu wa Kitengo cha Wanawake Wilaya ya Arusha, Hellen Kileo, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Arusha, Mzee Haji Ramadhani na Mary Mollel ambaye ni Mweka Hazina wa chama hicho Jimbo la Longido.

Wengine ni Mweka Hazina wa Jimbo la Monduli, Happy Ayub,  Mjumbe wa Kamati ya Ulinzi Wilaya ya Arusha, Gasper Kaaya, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Jimbo la Arusha, Stephen Daniel, Katibu wa chama hicho Kata ya Daraja II, Peter Samuel na mjumbe wake Joseph Tarangei, “Nyuma yetu wako zaidi ya wanachama 3,000 wa NCCR-Mageuzi watakaojivua uanachama na kutufuata kupinga uongozi wa kiimla unaoanza kujitokeza ndani ya chama ambapo viongozi na wanachama, hawapewi fursa ya kuhoji mambo yanayotokea au wasiyokubaliana nayo,” alisema Ndarvoi.

Kiongozi huyo ambaye pia mwaka jana aliwania Udiwani Kata ya Daraja II kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, alitaja baadhi ya mambo ya msingi yanayostahili kupatiwa majibu na uongozi wa juu wa chama hicho kuwa ni pamoja na matumizi ya fedha ya ruzuku inayotolewa na serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa lengo la kusaidia uendeshaji wa shughuli na kuimarisha vyama.

Alidai wagombea wa nafasi mbalimbali kupitia chama hicho kwenye uchaguzi uliopita, akiwemo yeye, hawakupata msaada wowote kifedha wala kupigiwa kampeni na uongozi wa juu, licha ya awali kuahidiwa na kutakiwa kuandaa bajeti yao ya kampeni na kuiwasilisha makao makuu ya chama, “Haya ndiyo mambo ya msingi ambayo Kafulila na wenzake walihoji. Hoja hizo  zilistahili kujibiwa si kufukuzwa. Hatuwezi kuimarisha chama iwapo ruzuku yote itaishia makao makuu kwa wajanja wachache. Tutaingizaje wanachama wapya na kufungua matawi?”Alihoji Ndarvoi.

Kuhusu kuhamia CHADEMA, alisema tayari wamefuata taratibu walizoelekezwa ikiwemo kuandika barua na kuiwasilisha kwa Katibu wa chama hicho Kata ya Daraja II, Solomon Kitashu kuomba kupokelewa na kupewa kadi za uanachama.

Ndarvoi alisema barua hiyo waliiandika na kuifikisha Ofisi za Chadema, Desemba 29 mwaka huu na sasa wanasubiri maelekezo mengine, ikiwemo siku rasmi ya kupokelewa na kukabidhiwa kadi ili washiriki kukiimarisha chama hicho alichodai kimejipambanua kuwa mtetezi na msimamizi wa haki na demokrasia licha ya vitisho kutoka serikalini na vyombo vya dola.

Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro, alisema milango iko wazi kwa viongozi hao pamoja na wengine kutoka vyama vingine kujiunga na chama hicho baada ya kufuata na kuzingatia taratibu, kanuni na katiba ya chama kulingana na maelekezo ya viongozi wa maeneo husika, “Siyo hao kutoka NCCR-Mageuzi pekee tunaowakaribisha, bali hata kutoa CCM na vyama vingine wenye mapenzi mema na taifa hili waje CHADEMA tuendeleze mapambano na harakati za ukombozi wa kifikra na mfumo kandamizi dhidi ya umma uliopo nchini,” alisema Nanyaro.

Hata hivyo, aliwaonya wote wanaotaka kujiunga CHADEMA, kutogeuza chama hicho sehemu ya kukimbilia baada ya kuharibu walikokuwa kwani hawatavumiliwa wakienda kinyume na taratibu, kanuni na katiba ya chama, akikumbushia jinsi chama chake kilivyowavua uanachama madiwani watano wa Manispaa ya Arusha, waliokaidi kutii maelekezo na maagizo ya vikao halali vya chama.
Aidha, alielezea kusikitishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini, kwani badala ya kujenga demokrasia komavu na upinzani imara, wanadidimiza kwa kujipendekeza CCM au kwa maslahi binafsi.

via MwananchiHabariLeo na  Nipashe
 
 
Picture
Mkazi wa mtaa wa Maisaka Sinai mjini Babati mkoani Manyara, amenusurika kuuawa baada ya kukatwa sikio na kulazimishwa kulimeza kutokana na kipigo cha kwa wananchi, akidaiwa kuiba mbuzi wawili na kutaka kuwauza. 

Daatho Kodi (20) alipigwa na wananchi juzi saa 10 jioni, kwenye mnada wa Gendi wilayani Babati na kukatwa sikio la kushoto na kulazimishwa kulitafuna akipewa na chumvi. 

Akizungumza kwa njia ya simu,mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Joseph Muray ambaye alikuwa mnadani hapo, alisema kama si jitihada za Mwenyekiti wa soko hilo, Sifael Mollel, hivi sasa Kodi angekuwa marehemu. 

Muray alisema Mollel alitumia askari wa mgambo mnadani kuzuia vurugu hizo na kuwaita polisi waliofika eneo hilo wakati Kodi ameshajeruhiwa kwa kipigo na kukatwa sikio. 

Alisema watu hao walimpiga mtuhumiwa huyo aliyedaiwa kuiba mbuzi wawili, beberu na jike, mali ya Safari Angali (24) mkazi wa mtaa wa Nakwa Barazani, Babati. 

Alisema baada ya kuiba mbuzi hao aliwapeleka mnadani hapo na wakati akitafuta mnunuzi, alikamatwa na kupigwa kwa silaha za jadi. 

Muray alisema alipokamatwa aliambiwa achague moja, kati ya kuuawa au kukatwa sikio na kulitafuna na chumvi na kulimeza, akachagua sikio likatwe, “Alipigwa kwa marungu na mapanga na kukatwa sikio na kupewa chumvi na kulitafuna na kulimeza hadi polisi walipoitwa,” alisema shuhuda huyo. 

Alidai kuwa, Kodi ni mzoefu wa kuiba mali za watu na amekuwa akikamatwa na kuachwa kutokana na kulindwa na ndugu na jamaa zake, “Walitaka kumuua na kama si Mwenyekiti kuita polisi wangemmaliza, kwani walidai wakimkamata huachiwa,” alisema. 

Kodi anaendelea kupata matibabu kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara) huku akiwa na pingu mikononi. 

via HabariLeo