![]() Pata burudani hiyo kwenye ukurasa wa Audio (bofya hapa). Nyimbo hizo zilizopo kwenye kaseti ya 'UKUMBUSHO' utunzi wake hayati Hemedi Maneti akiwa na Vijana Jazz Band ni: SIDE A 1. Jiko limenuna 2. Najilaumu 3. Nilitaka iwe siri SIDE B 1. Unikubalie 2. Ndoa ni kuvumiliana 3. Madaraka kwenye bar Shukrani ya nyimbo: John B. mwenye blogu ya Likembe. NAKONDE border in Northern Province was yesterday temporarily closed following a riot by irate Tanzanian traders that left three vehicles damaged. The riot started at about 10:30 hours and by 12:00 hours both the Zambian and Tanzanian customs gates remained closed. An eye witness at the border said the riot was started by Tanzanian nationals who sell various merchandise on top of the Tanzania Zambia Railways (TAZARA) tunnel on the Zambian side after police confiscated their goods. Police had been trying to prevent people from trading on top of the tunnel. The irate traders started throwing stones and all sorts of missiles at the combined team of council and state police as workers at the clearing agencies near the area scampered for safety. Three new vehicles were damaged in the process before a reinforcement of police officers arrived on the scene. Heavily armed police officers have since been deployed to keep vigil at the scene. Nakonde district commissioner Billy Silwimba said the closure of the border was temporary. Silwimba said normal business was expected to resume anytime soon and that the confusion had been addressed. Silwimba, who described the riotous behaviour of the Tanzanian nationals as unfortunate, said importers and the local people should not panic as the situation was now under control. Source: www.postzambia.com ![]() Some of you have been looking for ways to save email addresses and contacts of your Facebook friends, however, there is no official way from facebook management on how to do that, but you can do a work around if you have a Yahoo or YMail address. Here is how you do it:
Tafakari kwa njia ya picha... Elimu! 03/12/2010
Nukuu ya leo toka kwa Mtanzania 03/12/2010
"WHO's new recommendations are excellent in theory, but they did not give us a practical way of implementing the guidelines - already we have shortages of drugs in trying to put people with CD4s below 200 on treatment," said James Kamau, coordinator of the Kenya Treatment Access movement. Africa Africa, when will you start to have priorities? You have money for political campaigns, money for elections, money for wars, money for military coups... but when it comes to your people, you start crying... you shout for international funding. You forget that the money comes after Subi and Dewo, Iverson, Liu Cheng, Albulmarik, Lee, Stephanie et al, have been squeezed to the last coin... Please Africa use your brain to think not your spinal cord! "Avoiding this will depend on the willingness of donors to make new commitments. Although this is not easy in today's financial environment, donor countries cannot back away from supporting the promise of universal access to treatment made five years ago." Africa, the dying are your people. Their well-being is your responsibility. The donors have other important things to do, mama wewe bado umekaa unawategemea tu??!! Let me ask you my mama, how much of your budget from your own resources goes to HIV/AIDS? Hakuna. ...but how much do you spend for corruption, wars, unnecessary trips of your leaders, military coups? A lot. One more before I let you go, how much of the funded money goes into the pockets of your corrupt, irresponsible leaders and health care authorities? How much of the funded monies is used for medications? Very little... but how much is used for the Shangingis? A lot. Ah Africa!! I have never heard an ARV by the name of Land Cruiser. Sasa unalia nini Africa? Afrika umejilaani mwenyewe, hujalaaniwa na mtu wala Mungu. Africa achana na ujinga wa utegemezi, una kila kitu umekikalia tu unalilia donors. Amka! Ingawa najua kamwe hautaamka. Unaniboa Afrika. Monsignor in China. (reacting to www.irinnews.org) Ripoti tuliyoipata inasema kuwa basi la kampuni ya Shabiby lililokuwa likitoka Dar Es Salaam kuelekea Dodoma limepata ajali mbaya sana eneo la Ubena baada ya kugonga nyuma ya lori. Taarifa inasema kuwa miili ya watu imetapakaa barabarani. REKEBISHO Kwa mujibu wa blogu ya Maggid Mjengwa, ajali ni ya basi la Shabiby lilolokuwa likitokea Arusha kwenda Dodoma. Ajali ilitokea majira ya saa kumi. Mabasi ya Shabiby na Mohamed Trans inasimuliwa na abiria kuwa yaliendeshwa katika mwendo wa 'mashindano'. Kwenye msitu wa Mwidu ikatokea hali iliyosababisha dereva wa basi la Shabiby kushindwa kumalizia ovateki na hivyo kulivaa lori. Picha zinazoonekana (bofya kuzikuza) ni kwa hisani ya blogu ya Mjengwa; ziada tafadhali bofya hapa. ![]() Pius Msekwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Mheshimiwa Pius Msekwa amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi ndiyo chama cha siasa pekee kinachoweza kujizalisha ki muundo, itikadi na sera ili kukidhi mahitaji ya watanzania wengi kwa nyakati tofauti. Akihutubia umati mkubwa wa wana CCM waliohudhuria kuadhimisha sherehe za miaka 33 ya CCM huko Reading, Uingereza, Mheshimiwa Msekwa alisema azimio lililounda CCM mwaka 1977 linabaki imara kutaka CCM kiwe chombo madhubuti kwa muundo, fikra na vitendo vyake ili kumkomboa mwananchi na kuinua maendeleo ya Taifa. Alisema CCM imezidi kunufaika kifikra kutokana na kuendelea kuboresha muundo wake ikijumuisha pia matawi ya wasomi wa elimu ya juu na yale ya nje ya nchi. Mheshimiwa Msekwa alitahadharisha kuwa Azimo la Zanzibar la Februari 1991 halikuvunja Azimio la Arusha isipokua lilitazama upya masharti ya uanachama wa CCM na hasa ibara ya 8(7) ya katiba ya CCM toleo la 1987. Azimio la Zanzibar liliondoa miiko ya uongozi iliyowabana halaiki ya wanachama walio wakulima na wafanyakazi wa kawaida hasa baada ya mabadiliko ya uchumi na siasa ya vyama vingi. Hivyo alionya kuwa CCM na serikali yake haitawavumilia watovu wa maadili wanaokighilibu Chama na kuhujumu uchumi kwa kutumia mwanya wa CCM kujisahihisha, kujiboresha na kujiimarisha. Mheshimiwa Msekwa aliyeonyesha uwezo mkubwa wa kukifahamu Chama, Bunge na Serikali, alijadili kwa kina changamoto mbali mbali ambazo CCM imepitia baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi. Akizungumzia mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, Mhe Msekwa alisema mfumo wa uchaguzi uliokuwepo ulitoa mwanya wa rushwa kwa watu wasio waadilifu na wenye uwezo mkubwa wa fedha kununua kura. Huku akishangiliwa umati wa Watanzania, Mhe Msekwa alibaini kuwa ukiukwaji wa maadili utakwisha baada ya CCM kupanua wigo wa demokrasia katika uchaguzi na kupitishwa kwa sheria mpya ya gharama za uchaguzi mwaka huu. Awali akimkaribisha Mheshimiwa Msekwa, Mwenyekiti wa CCM Tawi la UK ndugu Maina Owino alisema hatua za makusudi zinazo chukuliwa na CCM kuboresha, muundo, fikra na sera ili kukidhi mahitaji ya watanzania wa jinsia zote ni wa lazima kwa nyakati na uimara wa chama. Alisema Serikali ya CCM ni lazima iwajibike kikamilifu na kwa ufanisi ili kusanifisha ridhaa na dhamana iliyopewa na wananchi. Ndugu Owino alikumbusha kuwa watanzania wanaoishi nje ya nchi wamekuwa wanachangia maendeleo ya Taifa kwa muda mrefu hususan katika sekta za kilimo na usafirishaji, vifaa vya elimu na utaalamu, afya na michezo na sasa umefika muda serikali iwatambue na kusajili rasmi mchango wao. Alidokeza kuwa Watanzania wa ughaibuni wanakwamishwa na ukiritimba usio wa lazima na kusababisha kupoteza vifaa vingi, kulipa gharama ambazo zisingekuwa za lazima au kujengewa mazingira ya rushwa katika maeneo ya mamlaka za bandari, viwanja vya ndege, kodi ya mapato na uhamiaji. Aidha aliziomba serikali na Bunge wazipokee na kuzifanyia kazi hoja za Diaspora bila walakini. Alimtaarifu mheshimiwa Msekwa kuwa wazaliwa wa Tanzania wenye uraia wa kufikia ughaibuni wanatambua kuwa mapenzi, malengo na hatima ya maisha yao yapo Tanzania. Idadi kubwa ya watanzania kutoka miji mbalimbali walijiunga na Chama Cha Mapinduzi na walifurahia kukabidhiwa kadi zao na mheshimiwa Msekwa. Mheshiwa Msekwa aliwaasa watanzania kuendeleza uzalendo, kuwa wabunifu na wajasiria mali. Na mwandishi wetu. Create passport size photos online for free 03/11/2010
![]() A friend of mine recently asked if I could create some passport size photos for his baby ready for official documents especially the passport for traveling. Luckily, I know three websites that can do the job and was able to help him immediately. I thought somebody could also need this tip. Here are the links: www.epassportphoto.com and www.idphoto4you.com and www.portraitbooth.com You may want to save this page for future references, just press CTRL+D (on your keyboard) to bookmark this page. Vibweka vya Kabwela na ulevi...! 03/11/2010
Baadhi ya madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam, wanadaiwa kutoa taarifa za uongo kwamba mtoto aliyezaliwa amekufa, lakini muda mfupi baadae alibainika kuwa yu hai. Tukio hilo lililoacha maswali mengi lilitotokea juzi saa moja usiku, ambapo uongozi wa hospitali hiyo ulithibitisha kutokea, huku ukitia shaka juu ya mazingira yake. Habari zilizopatikana hospitalini hapo zilidai mjamzito aliyejifungua mtoto huyo alifikishwa hospitalini hapo kichanga hicho cha kiume kikiwa kimeanza kutoka. Ilidaiwa baada ya mjamzito huyo kusaidiwa na kumaliza kujifungua, alielezwa mwanawe amekufa, hivyo walikabidhiwa kichanga hicho kwa ajili ya maziko. Kwa mujibu wa chanzo cha habari, baada ya kufika nyumbani wakijiandaa na mazishi ya mtoto huyo, baba yake alipewa taarifa za kifo na aliomba asizikwe hadi atakapofika. Ilidaiwa baada ya baba huyo kufika nyumbani, mtoto huyo aliyekuwa amefunikwa nguo alipofunuliwa alionyesha dalili za kuwa hai, huku akijinyoosha, jambo lililowafanya wamrudishe hospitalini hapo. Chanzo hicho kilidai baada ya kufikishwa hospitalini, kichanga hicho kiliwekwa kwenye kifaa maalumu kinachotumika zaidi kwa watoto njiti. Imeelezwa kuwa kichanga hicho kilikaa katika kifaa hicho kwa saa tano, kabla daktari kueleza kuwa kimekufa. Habari zaidi zilidai baada ya uongozi wa hospitali kupata taarifa za kifo hicho, ulimrudishia mama mzazi sh. 400,000, fedha alizotoa kwa ajili ya huduma za kujifungua. Akizungumzia suala hilo jana, Dk. Kaushik Ramaiya, alisema walipata taarifa za tukio hilo juzi kutoka kwa daktari aliyekuwa zamu. Dk. Kaushik alisema mama huyo alifika hospitalini hapo akitokea hospitali ya Dar Group, akiwa katika hatua za mwisho za kujifungua. Alisema mama huyo alihudumiwa na daktari aliyemtaja kwa jina moja la Dk. Charles. "Baada ya mtoto kuzaliwa alionekana hana dalili za kuwa hai, wauguzi walitumia njia zote na walipothibitisha amefariki waliamua kumweleza mzazi kuwa mtoto amekufa. Nilishangaa kusikia baba na shangazi wa mtoto huyo walisema walipofika nyumbani waliona mtoto anaanza kupumua na kumrudisha ambapo wauguzi walikiri anapumua na kumweka katika mashine,” alisema Dk. Kaushik. Hata hivyo, alisema tukio hilo ni la ajabu kwani halijawahi kutokea tangu aanze kazi ya udaktari miaka 29 iliyopita. Alisema wauguzi na daktari aliyekuwa zamu wakati wa tukio wametakiwa kutoa maelezo na kwamba uchunguzi unaendelea. Kuhusu mzazi kurudishiwa fedha, Dk. Kaushik alisema walifanya hivyo kwa ajili ya ubinadamu na si kwa nia nyingine yoyote. Chanzo: tovuti ya gazeti la Uhuru |