Add Comment Kwa nini unanichora? 04/02/2012
Hayo mamuvi yana mwanzo tu, mwisho... 01/02/2012
Kaa mbali! Jitahidi kukaa mbali kabisa maana ni ugonjwa mbaya kweli kweli. Unaambatana na sifa za kudharauliwa, kuchekwa, kuibwa, kuonwa juha, kusengenywa, kupewa makombo, kupewa kwa masharti ya kudhalilisha...yaani kwa ujumla ni ugonjwa mbaya mno! Jamaa anamtizama Mzee kiraka hapo anajiuliza sijui amzabue makofi fya fya fyaa, sijui amkung'ute hadi vumbi limtoke? au aliache tu liendelee kupiga kelele kama juha huku akilizunguka na kuliibia utajiri wake kisha kwa dharau na mkwara mzito, analigawia sehemu kwa mkopo wenye riba na masharti na dharau chungu tele! Unarudi kundini au niku-delete? 31/01/2012
Ni jambo la kusikitisha kuwa katika jamii yetu tunao wazazi na walezi ambao ama wanafanana na kibonzo hiki au wanakaribia kufanana nao, kwa maana kwamba, huikwepa familia yao, watoto wao wenyewe, kwa kuona kadhia, kero, bughudha na usumbufu mwingi. Wengine hata ikiwa hawatamki bayana kusumbuliwa, matendo yao yanatosha kujisemea. Wakikutana katika vijiwe vyao vya starehe kama klabu za pombe, kahawa, bao na gumzo, hadithi za "usumbufu" wa watoto na familia zao ni mojawapo ya ajenda. Ajabu, ni usumbufu wa kuonja tu, hawaujui kwa kina kwa kuwa wanaukimbia na kuwaachia wenza au yaya. Suala la kujiuliza ni, je, familia bora itajengwaje ikiwa unaikwepa? Kwa bahati mbaya, jamii nayo imebadilika, kwani mtoto siku hizi siyo kama "enzi za Mwalimu" kuwa mtoto ni wa kijiji, sasa ni nyakati ya changu ni changu na chako ni chako, usimrudi mwanangu hata ikiwa amekosea. Wazazi mlio na tabia ya kuzikimbia familia zenu jioni na wakati wa wikiendi, kisha mkirudi mnakuwa wageni kwa wanenu au 'wakali kama mbwa mwitu' timizeni ahadi na maamuzi yenu ya kutaka kuwa na familia mlipoamua kuwa na wenza. Usiwe mzazi ambaye akiingia ndani watoto wanatafuta mlango wa kutokea. Usitarajie kwa miujiza kuwa na familia bora, kwani familia bora hujengwa kwa juhudi, maarifa na ushirikiano. Usiache kuwasikiliza watoto kwani nao wanajifunza na wanapenda kusikilizwa na wazazi wao. Nilipokuwa mtoto mdogo nilikuwa ninaamini zaidi maneno ya wazazi, hata kama waliongopa, kuliko nilivyowamini majirani au ndugu baki. Watoto wanaoishi maisha ya kubahatisha na kushindwa kuzilea vyema familia zao wawapo wakubwa mara nyingi hutokana na wasiopata malezi ya wazazi wao wangali wadogo "samaki mkunje angali mbichi". Vunja mnyororo wa familia mbovu kwenye kizazi na ukoo wako utakaofuata, kwa kufanya marekebisho kwenye familia yako. Usipende kutunukiwa sifa usiyoifanyia kazi kwa hamu na gamu. Malezi ya familia ni ya wazazi, siyo mzazi. | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed