Audio: NjiaPanda na Langa - Kabla, Wakati na Baada ya dawa za kulevya, Inawezekana kuacha! 14/08/2011
![]() Langa Ifuatayo ni audio ya kipindi cha Njia Panda kilichorushwa hewani na Dk. Isaac Maro (akishirikiana na Dk. D. Maro) siku ya Jumapili Agosti 14, 2011 kupitia Radio Clouds FM. Kwenye kipindi alialikwa Langa Kileo ambaye habari yake tuliisoma wiki iliyopita katika vyombo mbalimbali vya habari (unaweza kubofya hapa kuisoma tena) pamoja na mwanamuziki kwa jina la kisanii "Kala Pina". Katika kipindi hiki, Langa na Kalapina wanazungumzia juu ya matumizi ya dawa za kulevya, ilivyoanza, mwendelezo wa kuzitumia na hatimaye kufikia hatua ya kutaka kuachana na dawa hizo. Wanagusia magumu waliyoyapitia katika kujidahidi kuziacha dawa, mafanikio na mbinu za kuendelea kushinda. Langa anatoa dondoo za kilichomwezesha kutimiza miezi 4 hadi sasa bila ya kutumia dawa hizo. Vile vile anaelezea malengo na mikakati yake ya mbeleni katika kuwasaidia vijana wanaotaka kuachana na dawa za kulevya. 7 Comments Wiki iliyopita tulisikiliza kisa cha kusikitisha cha kukanganya kabisa cha binti aliyebakwa na Baba yake mzazi, binti ambaye ni uzao wa tendo la ubakaji la mtu huyo huyo kwa mama mzazi wa mtoto. Ikiwa hukusikiliza kipindi hicho, unaweza kurejea kukisikia kwa kubofya hapa. Ifuatayo ni audio ya kipindi cha mwendelezo wa kisa hicho, kipindi kimesikika Jumapili Agosti 7, 2011 na kurekodiwa, japo audio inakuwa 'fast' kidogo, lakini utaweza kusikia kila kilichoendelea. Tuvumiliane kwani kinasa sauti ndiyo kiliamua kukata nafasi na kuamua kuunga maneno, hivyo mtu anasikika kama anaongea kwa kukimbia au 'mcharazo'. Kipindi cha Njia Panda kilichorushwa hewani siku ya Jumapili tarehe 31 Julai 2011. Ni kipindi ambacho kimefanya mahojiano baina ya mwendeshaji wa kipindi Dk. Isaac Maro na Mama Mdogo wa Binti ambaye alibakwa na baba yake mzazi na kupata ujauzito. Binti alimzaa mtoto, mtoto ambaye naye alibakwa na baba/babu. Ndiyo kusema, Baba alimbaka mwanaye, akampa ujauzito, kilichozaliwa katika ujauzito huo, miaka 10 baadaye, akakibaka. Kambaka mtoto na mjukuu damu yake. Aliyelivalia njuga suala hili, ametishiwa kuuawa na Baba mbakaji. Baba aliyebaka ametoroka nyumbani na hivi sasa anatafutwa na Polisi kwa ajili ya kufikishwa mahakamani. Mwanasheria naye alikuwepo studioni kutoa ufafanuzi wa kisheria kuhusiana na suala hili. Bofya kifute cha play usikilize, dakika 18 za mwanzoni utasikia kipindi cha spoti na habari za michezo kikifikia ukingoni ndipo kiache nafasi kwa kipindi cha Njia Panda kuanza, hivyo vumilia hadi dakika ya 19. Kipindi hiki kitaendelea tena wiki hii kwa kuwashirikisha Mama mzazi wa Mtoto, Mjumbe wa mtaa na Polisi. Ukitaka kusikiliza basi usikose kuwa kando ya redio siku ya Jumapili tarehe 7 Agosti 2011 kuanzia sasa nane alasiri hadi kumi jioni. Unaweza kusikiliza redioni au (bofya hapa). Hiki ni kisa cha kusikitisha sana. Ni kisa ambacho kila anayejali utu wa binadamu anapaswa kukisikia ili kupata changamoto ya namna atakavyotumia juhudi binafsi kuzuia ukatili huu ambao unaweza kumpata mwanaye, mdogo wake, mkewe, mama yake, bibi yake, shangazi yake, mkwewe, shemeji yake, wifi yake, au ndugu yaye yeyote wa kike, zaidi sana, matukio haya yamekuwa yakiwahusisha hata vijana wadogo wa kiume. Jamii hujengwa na sisi. Kisa kimemtokea Binti wa miaka 16 alipofukuzwa toka nyumbani kwa Mama Mwenyenyumba ambaye alikuwa amemwajiri kwa ajili ya kumfanyia shughuli za ndani. Binti anaeleza kuwa chanzo cha kufukuzwa siku hiyo pamoja na kuwa alishafanyiwa ukatili mara kwa mara, ilikuwa ni kosa la kutumia mafuta ya marashi "lotion" ya Mwajiri wake. Binti anatokea Kigoma. Anaelezea historia yake ya kuwa kitinda mimba na mtoto pekee wa kike kati ya 11 waliozaliwa na Mama mmoja na kwa Baba (ambaye alikuwa na wake wawili). Binti huyu alikwenda Jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kumtafuta Dada yake baada ya kushindwa kuendelea na masomo alipokuwa kidato cha Pili kwa kile kilichoelezwa kuwa ni "kurukwa na akili katika mazingara" na hivyo kushindwa kumalizia masomo ya Sekondari. Kwa bahati mbaya, binti hakufanikiwa kumpata dada yake na hivyo akaishia kutafuta pa kufanya kazi za ndani na ndipo alipojikuta ameajiriwa huko alikofukuzwa. Dk. Isaac Maro katika kipindi cha Njia Panda kinachorushwa na Clouds FM radio siku za Jumapili mchaa saa 8 alasiri hadi 10 jioni , alikuwa na binti huyu ambapo alimhoji na kupata maelezo ya jinsi alivyoshambuliwa kikatili katika tendo la ubakaji. Kwa bahati mbaya, kutokana na histori ya yaliyomtokea maishani, binti huyu anashindwa kueleza kisa na mkasa lakini kwa usaidizi wa Dk. Isaac, anaweza kuelelezea kilichotokea siku ya tukio. Ni kisa cha kusikitisha na kukerehesha sana. Alinitoa machozi aliposema kwa huruma, "walinibaka mdomoni"....! Bofya kifute cha pleya iliyopachikwa hapo chini usikilize kipindi hiki ambacho hakijahaririwa. Studioni walikuwepo wataalamu wa Afya, Saikolojia na Sheria waliozungumzia madhara ya tendo hili na adhabu ya sheria iliyopo na inayowakabili wahusika kuhusiana na tendo hilo. Audio iliyopachikwa hapo ni ya kipindi cha pili cha Njia Panda ambacho ni mwendelezo wa "Uponyaji wa Loliondo" kilichorushwa na redio Clouds FM Jumapili ya tarehe 10 Aprili 2011. Katika kipindi hiki, utayasikia majibu baada ya kupimwa ili kuthibitisha kauli ya dada aliyehojiwa katika kipindi kilichotangulia na kutamka kuwa anaamini amepona baada ya kunywa dawa kwa Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Ambilikile Masapila huko Loliondo kijijini Samunge. Pia utayasikia majadiliano baina ya wataalamu wa sekta mbalimbali walioalikwa studioni ili kuzungumzia sekta husika zilizoguswa na 'uponyaji' wa dawa ya Mch. Masapile. Mwendesha kipindi ni Dk. Isaac Maro. Bofya kifute cha play hapo upate kusikiliza. Audio zipo mbili ili kutoa uchaguzi zaidi ikiwa moja italeta usumbufu wa kutokusikika. Ikiwa huwezi kusikiliza, tafadhali bofya hapa kujipakulia audio hiyo. Audio: Njia Panda - "Uponyaji" wa Loliondo 30/03/2011
Audio iliyopachikwa hapo ni ya kipindi cha Njia Panda kilichorushwa na redio Clouds FM kila siku za Jumapili. Kipindi kilichorushwa hewani tarehe 27 Machi 2011, kilihusu "uponyaji" unaotamkwa kuwa unapatikana Loliondo kijijini Samunge kwa Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Ambilikile Masapila ambaye anasema alioteshwa na Mungu ndotoni kuwa tiba hiyo itaponya magonjwa sugu ya VVU/UKIMWI, Kisukari, Pumu na Shinikizo la juu la damu. Mahojiano katika kipindi hico kiliwashirikisha wataalamu wa Afya, Mmoja wa wagonjwa aliyekunywa dawa na kudai anajisikia kupona na Wachungaji wawili wa madhehebu tofauti ya Kikristo. Mwendesha kipindi ni Dk. Isaac Maro. Bofya kifute cha play hapo upate kusikiliza. Ikiwa huwezi kusikiliza, tafadhali bofya hapa kujipakulia audio. NB: Kipindi kimewekwa vivyo kilivyorushwa, hakuna editing yoyote iliyofanyika ili upate picha kamili ya kilichojiri siku hiyo. Siku ya Jumapili, tarehe 9 Mei 2010 kipindi cha Njia Panda kilikuwa na mgeni Dk. Jumanne kutoka 'Medicinal Plant Open Academy' ambaye alizungumzia suala la jinsi ya kuandaa vyakula na lishe muafaka kwa ajili ya afya ya Mama na Mtoto kwa kutumia vyakula asilia. ![]() Dk. Isaac Maro Bofya kifute cha play usikilize rekodi ya kipindi hiki. Ili kupata rekodi nyingine za NjiaPanda, bofya neno 'Dk. Isaac Maro' kwenye category hapo kulia mwa ukurasa au kwenye ukurasa wa audio. Kipindi cha Njia Panda kinachoendeshwa na Dk. Isaac Maro na kurushwa na Radio Clouds FM kila siku ya Jumapili muda wa saa nane mchana hadi kumi alasiri (8 mch. - 10 ala.) na kimekuwako hewani tangu mwaka 2001 na inakadiriwa huwafikia wasikilizaji wapatao milioni tatu na nusu waliopo ndani na nje ya Tanzania. Siku ya Jumapili, tarehe 25 Aprili 2010 kipindi cha Njia Panda kilikuwa na mgeni kutoka 'Medicinal Plant Open Academy' ambaye alizungumzia suala la matatizo ya uzazi, utasa, ugumba na kutokutunga mimba na uhusiano wake na lishe asilia. ![]() Dk. Isaac Maro Bofya kifute cha play usikilize rekodi ya kipindi hiki. Ili kupata rekodi nyingine za NjiaPanda, bofya neno 'Dk. Isaac Maro' kwenye category hapo kulia mwa ukurasa au kwenye ukurasa wa audio. Kipindi cha Njia Panda kinachoendeshwa na Dk. Isaac Maro na kurushwa na Radio Clouds FM kila siku ya Jumapili muda wa saa nane mchana hadi kumi alasiri (8 mch. - 10 ala.) na kimekuwako hewani tangu mwaka 2001 na inakadiriwa huwafikia wasikilizaji wapatao milioni tatu na nusu waliopo ndani na nje ya Tanzania. Siku ya Jumapili, tarehe 18 Aprili 2010 kipindi cha Njia Panda kilikuwa na mgeni kutoka 'Medicinal Plant Open Academy' ambaye alizungumzia suala la matatizo ya lishe na namna ya kupambana nalo kwa lishe asilia. ![]() Dk. Isaac Maro Bofya kifute cha play usikilize rekodi ya kipindi hiki. Ili kupata rekodi nyingine za NjiaPanda, bofya neno 'Dk. Isaac Maro' kwenye category hapo kulia mwa ukurasa au kwenye ukurasa wa audio. Kipindi cha Njia Panda kinachoendeshwa na Dk. Isaac Maro na kurushwa na Radio Clouds FM kila siku ya Jumapili muda wa saa nane mchana hadi kumi alasiri (8 mch. - 10 ala.) na kimekuwako hewani tangu mwaka 2001 na inakadiriwa huwafikia wasikilizaji wapatao milioni tatu na nusu waliopo ndani na nje ya Tanzania. Siku ya Jumapili, tarehe 2 Mei 2010 kipindi cha Njia Panda kinachoendeshwa na Dk. Isaac Maro na kurushwa na Radio Clouds FM kilikuwa na wageni ambao ni wanaume wanaojishughulisha na mapenzi ya jinsia moja. ![]() Dk. Isaac Maro Kwa ujumla kipindi kilizungumzia juu ya hali halisi ya maisha ya wanaume hawa pamoja na suala zima la kupambana na maambukizi ya VVU na UKIMWI katika jamii, hasa kwa kuwa wanaume hawa hujishughulisa na biashara ya mapenzi, kitendo ambacho ni kinyume na sheria za nchi. Bofya kifute cha play usikilize rekodi ya kipindi hiki. Ili kupata rekodi nyingine za NjiaPanda, bofya neno 'Dk. Isaac Maro' kwenye category hapo kulia mwa ukurasa au kwenye ukurasa wa audio. | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |









RSS Feed