Baadhi ya madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam, wanadaiwa kutoa taarifa za uongo kwamba mtoto aliyezaliwa amekufa, lakini muda mfupi baadae alibainika kuwa yu hai. Tukio hilo lililoacha maswali mengi lilitotokea juzi saa moja usiku, ambapo uongozi wa hospitali hiyo ulithibitisha kutokea, huku ukitia shaka juu ya mazingira yake. Habari zilizopatikana hospitalini hapo zilidai mjamzito aliyejifungua mtoto huyo alifikishwa hospitalini hapo kichanga hicho cha kiume kikiwa kimeanza kutoka. Ilidaiwa baada ya mjamzito huyo kusaidiwa na kumaliza kujifungua, alielezwa mwanawe amekufa, hivyo walikabidhiwa kichanga hicho kwa ajili ya maziko. Kwa mujibu wa chanzo cha habari, baada ya kufika nyumbani wakijiandaa na mazishi ya mtoto huyo, baba yake alipewa taarifa za kifo na aliomba asizikwe hadi atakapofika. Ilidaiwa baada ya baba huyo kufika nyumbani, mtoto huyo aliyekuwa amefunikwa nguo alipofunuliwa alionyesha dalili za kuwa hai, huku akijinyoosha, jambo lililowafanya wamrudishe hospitalini hapo. Chanzo hicho kilidai baada ya kufikishwa hospitalini, kichanga hicho kiliwekwa kwenye kifaa maalumu kinachotumika zaidi kwa watoto njiti. Imeelezwa kuwa kichanga hicho kilikaa katika kifaa hicho kwa saa tano, kabla daktari kueleza kuwa kimekufa. Habari zaidi zilidai baada ya uongozi wa hospitali kupata taarifa za kifo hicho, ulimrudishia mama mzazi sh. 400,000, fedha alizotoa kwa ajili ya huduma za kujifungua. Akizungumzia suala hilo jana, Dk. Kaushik Ramaiya, alisema walipata taarifa za tukio hilo juzi kutoka kwa daktari aliyekuwa zamu. Dk. Kaushik alisema mama huyo alifika hospitalini hapo akitokea hospitali ya Dar Group, akiwa katika hatua za mwisho za kujifungua. Alisema mama huyo alihudumiwa na daktari aliyemtaja kwa jina moja la Dk. Charles. "Baada ya mtoto kuzaliwa alionekana hana dalili za kuwa hai, wauguzi walitumia njia zote na walipothibitisha amefariki waliamua kumweleza mzazi kuwa mtoto amekufa. Nilishangaa kusikia baba na shangazi wa mtoto huyo walisema walipofika nyumbani waliona mtoto anaanza kupumua na kumrudisha ambapo wauguzi walikiri anapumua na kumweka katika mashine,” alisema Dk. Kaushik. Hata hivyo, alisema tukio hilo ni la ajabu kwani halijawahi kutokea tangu aanze kazi ya udaktari miaka 29 iliyopita. Alisema wauguzi na daktari aliyekuwa zamu wakati wa tukio wametakiwa kutoa maelezo na kwamba uchunguzi unaendelea. Kuhusu mzazi kurudishiwa fedha, Dk. Kaushik alisema walifanya hivyo kwa ajili ya ubinadamu na si kwa nia nyingine yoyote. Chanzo: tovuti ya gazeti la Uhuru Sam Bed Net ni neti zilizotengenezwa ili kupunguza usumbufu utokanao na kuchomeka vyandarua vya kupambana na mbu wanaosababisha malaria na wadudu wengine wenye kusambaza vimelea vya magonjwa. Waweza kubofya picha kutizama namna ya kuzichomeka au bofya hapa kutizama video fupi kabisa. Kwa mahitaji, wasiliana na SamBedNet kupitia sam@sambednet.com na tovuti ni www.sambednet.com Hongera Yasinta Ngonyani kwa kushiriki kisa hiki. Ni kisa kingine tena toka kwa Mtanzania mwenzetu baada ya kusoma kile alichoandika Prof. Matondo kuhusiana na huduma ya afya nchini Tanzania. Kwangu mimi, hii inanidhihirishia ukomavu uliopo sasa kwa baadhi ya Watanzania kuanza kutumia TeknoHaMa kwa njia ya blogu kuandika zaidi matukio ambayo yanamgusa mwandishi mwenyewe na hatimaye kundi la hadhira na mwishowe, kufikisha ujumbe kusudiwa. Katika visa vyote hivi viwili, niliyoyaona kwa ukaribu ni pamoja na:
Nakumbuka mwaka 1996, kuna tukio la kushangaza kidogo lililotokea katika tasnia ya Michezo kule nchini Italia na kuushangaza ulimwengu. Tukio hilo lilimtokea mchezaji wa Kimataifa aitwae Nnwanko Kanu. Huyu alikuwa ni mchezaji wa Timu ya taifa ya Nigeria, ambaye alikuwa akichezea timu ya Ajax ya Uholanzi. Ni baada ya Kuiwezesha nchi yake kutwaa kombe la Olympic, hapo mnamo mwaka 1996, ndipo alipopanda kilele cha mafanikio na kununuliwa na timu maarufu ya kule Italia inayoshiriki ligi ngumu ya almaarufu kama Serial A. Mchezaji huyu alinunuliwa na timu ya Inter Milan na ni wakati alipokuwa akifanyiwa vipimo vya afya,(Medical Check Up) ndipo matokeo ya vipimo hivyo vilipoushangaza ulimwengu. Nnwanko Kanu aligundulika kuwa na matatizo ya moyo na alitakiwa kufanyiwa upasuaji haraka sana ili kunusuru afya yake. Ikumbukwe kuwa mchezaji huyo tayari alikuwa akishiriki ligi za kimataifa, akichezea timu ya Ajax ya Uholanzi pamoja na kuchezea timu yake ya Taifa ya Nigeria na kuiwezesha kutwa kombe la Olympic, lakini katika kipindi chote hicho haikuwahi kugundulika kuwa na tatizo hilo. Hata hivyo kulikuwa na kupingana kwingi kitaalamu kati ya madaktari wagunduzi wa tatizo hilo na wale wa Uholanzi, lakini hatimaye alifanyiwa upasuaji na kurejea katika anga za michezo na kupata mafanikio makubwa. Nimelikumbuka tukio hili kutokana na kile kilichomtokea mdogo wangu Asifiwe, huyu ni mdogo wetu wa mwisho kuzaliwa. Tukiwa tumezaliwa wanaume watano na wanawake wawili, yaani kati ya watoto saba wa Mzee Ngonyani na mama Ngonyani tuko watoto wakike wawili tu, yaani mimi na huyu mdogo wangu Asifiwe. Akiwa darasa la sita ndipo alipoanza kuugua, ghafla, na tatizo kubwa lililokuwa likimsumbua ilikuwa ni tatizo la kukosa nguvu ghafla na kubanwa na kifua, lilikuwa ni tatizo ambalo kule Songea katika Hospitali ya Peramiho hawakuweza kugundua kuwa ni tatizo gani lakini kwa juhudi za madaktari aliweza kupewa tiba ambayo hata hivyo ilimletea nafuu badala ya kumponyesha. Ni mwaka jana mwezi wa pili nilipokuwa nyumbani Tanzania ndipo nilipokata shauri tumpeleke katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya vipimo zaidi. Ni hapo ndipo tulipo shangawa na matokeo ya vipimo kuwa mdogo wetu Asifiwe anayo matatizo ya Moyo na anatakiwa kufanyiwa Upasuaji nchini India. Naamini hata wewe unayesoma hapa unaweza kuhisi ni kwa kiasi gani nilikuwa naumia kwa kile kilichomtokea mdogo wetu. Hata hivyo baada ya kushauriana na madakatari alipangiwa kuwa awe anakuja pale Muhimbili kwa ajili ya matibabu yaani kliniki huku mchakato wa kufanyiwa upasuaji nchini India ukiendelea. Kwa hiyo akawa anakuja Muhimbili na kurudi Songea (Ruhuwiko). Lakini mara hii ya mwisho yaani mwezi wa kwanza mwaka huu alipofika Kliniki aliandikiwa kufanyiwa upasuaji hapa hapa nchini na hivyo kulazwa pale Muhimbilli akisubiri kufanyiwa upasuaji. Ni katika kipindi hicho sala na maombi vilifanyika kumuomba mungu afanikishe upasuaji huo ili mdogo wetu apone na kurejea shule kuendelea na masomo. Mnamo tarehe 16/02/2010 mdogo wetu Asifiwe alifanyiwa upasuaji wa moyo na kwa uwezo wa Mwenye Enzi Mungu upasuaji ulikwenda vizuri na ijumaa tarehe 27/02/2010 ametolewa nyuzi zake na tarehe 01/03/2010 jumatatu ameruhusiwa. Leo napenda kumshukuru Mwenye Enzi Mungu, Madaktari, Manesi na watu wote kwa Juhudi zao katika kumuhudumia mdogo wetu Asifiwe, sisi tunasema kwamba kwa uwezo wake ameweza kuisimamia kazi hiyo ya madaktari na kufanikisha upasuaji huo.Pia shukrani nyingi sana kwa daktari Mushi wa kule Peramiho yeye ndiye aliyetupa ushauri wa kumpeleka Asifiwe, Kwanza katika kliniki moja hapa Dar ya Dr. Johnson M. Lwakatare. na ndipo tukapata rufaa ya kwenda Muhimbili . Sisi tunaamini ni mungu pekee kwa kupitia mikono ya madaktari wale pamoja na manesi ameweza kufanikisha upasuaji huo. Nakumbuka siku tatu kabla ya kufanyiwa upasuaji huo nilizungumza na mdogo wangu, na kwa huzuni alinijulisha kuwa watoto wawili wa kike ambao walitangulia kufanyiwa upasuaji kabla yake wamepoteza maisha, ni watoto ambao walikuwa wana umri wa chini ya miaka 10, na walihitaji bado kuishi lakini Mwenye Enzi Mungu aliwapenda zaidi, na hivyo kuwatwaa. Ila namsifu Asifiwe, yeye hakuwa mwoga isipokuwa hakupenda kama ingetokea bahati mbaya kutuacha sisi nduguze. Tulifanya maombi kwenye simu na nilimpa moyo mdogo wetu kuwa yote tumuachie Mungu kwani tunaamini atatenda miujiza. Lakini hata hivyo upasuaji uliahirisha tena kutokana na ziara ya ghafla ya mheshimiwa Raisi Jakaya Kikwete alipotembela hapo hospitali ya Muhimbili kuzungumza na madaktari. Leo hii kwa niaba ya familia ya mzee Ngonyani napenda kuchukua nafasi hii kusema Ahsante Mungu kwa kuitendea familia ya Mzee Ngonyani Muujiza, Pia ningependa kuwashukuru wote mliokuwa nasi katika sala, katika kutupa moyo wakati tulipokuwa na mawazo. Na shukrani nyingi zimfikie kaka yetu Ngonyani na mkewe wa pale Kinondoni Kinondoni Mkwajuni kwa kuwa karibu nasi wakimhudumia mdogo wetu katika kipindi chote alipokuwa akija kliniki na hata wakati wa kufanyiwa upasuaji. Ninawashukuru kwa kuwa walitumia muda wao mwingi kwenda na kurudi Muhimbili ili kuhakikisha mdogo wetu Asifiwe hajisikii mpweke. Na pia napenda kumpongeza yeye mwenyewe Asifiwe kwa kutoonyesha uoga. Chanzo: Blogu ya Yasinta Ngonyani - Ruhuwiko|Maisha A 12-year-old Tanzanian died at the international airport in Ahmedabad early on Tuesday morning after she allegedly suffered a heart attack. A team of doctors from Apollo visited her but by that time she had already succumbed to death. According to CEO of Apollo Hospitals, Ahmedabad, Dr Praful Pawar the 12-year girl was from Tanzania and was suffering from congenital heart defect. "Therefore, she was brought to Apollo and was under medication for the past 11 days. However, as she was unfit to be operated upon, the authorities refused to let her undergo a surgery." The doctors at the hospital refused to disclose the name of the girl. "She was also examined to see if she was fit to fly and was accompanied by her mother for the journey," said Pawar. He said initially the girl had breathing troubles and the doctors at the Apollo clinic at the airport rushed to the spot but she suffered a cardiac arrest and died. According to CISF sources at the airport the girl fainted inside the building early in the morning while waiting for her flight. According to sources a couple of days back a 55-year-old passenger had a heart attack in a flight. However, unlike the Tanzanian girl, the man was saved. A senior official of CISF told DNA that the girl even boarded a flight but was brought back when she could not breathe properly inside the aircraft. Tohara kwa njia ya pete 03/03/2010
Ni kifaa aina ya pete kilichofanyiwa utafiti ili kiweze kutumika katika kutahiri wanaume bila maumivu makali. Sikiliza kipande cha habari hii kwenye audio kwa kubofya kifute cha 'play'. Eti we mwoga wa mende kama huyu? 03/03/2010
Humu duniani watu tunatofautiana kiwango cha ujasiri. Lakini wapo watu wengine japo wawe jasiri kiasi gani, ikiwa wana ugonjwa wa kuogopa, baadhi ya vitu (phobia) ujasiri wake ni kazi bure katika nyakati fulani. ![]() bofya pichani utizame video hii fupi Ninakumbuka nilpokiuwa Sekondari dada mmoja alikuwa mwoga sana wa wadudu kama vile sisimizi, nyenyele, maji ya moto nk. Mwanzoni nilidhani ni utani kwa kuwa umbo lake lilikuwa kubwa kuliko wanafunzi wengi, na hivyo tulitarajia mtu mkubwa asiweze kuogopa kidudu kidogo hata siku moja. Tena, nilipokuwa chuoni, nilisoma na dada mwingine ambaye ni rafiki yangu pia, naye alikuwa mwoga wa wadudu hasa aliyekuwa akimtikisa maini alikuwa mdudu mende. Halafu hivi vidudu bwana hata sijui vinakuwa vimetumwa na nani kwani hisia zao huwa ni kali na mara moja huwapeleka kwa yule mtu mwoga. Hii nadhani ni kutokana na msisimko (stimulation) zinazosababisha kemikali fulani kuzalishwa mwilini na mtu huyu baada ya kumwona mdudu au kiumbe anayemwogopa. Siku moja hivi tupo koridoni, nje ya milango ya vyumba vyetu ambavyo vilikuwa vinatenganishwa na uwazi wa kuelekea bafuni, alikuwa akijipita mende katika harakati zake za pengine kutafuta chakula. Ghafla, rafiki yangu ambaye kwa wakati huo alikuwa amesimama kati ya mlango wa chumba chao na kile cha kwetu huku akiukabili mlango wa bafuni, ghafla alipiga ukelele wa nguvu mara moja. Ndipo tulipostuka na kumwuliza, 'nini?' huku akinyoosha mkono akawa anasema, 'yule, yule', siye kumtizama ni mende, mimi mawazo yangu nilidhani kamwona nyoka ama ng'e ama pengine sijui kidudu gani cha kutisha. Loh, kumbe alikuwa akimwogopa mende. Alitetemeka, akamkamata mmoja wetu bila ya kumwachia akisema, 'mwue, mwue' nasi kwa kuwa tuliona kichekesho, hatukumwua, ndipo yule mende ghafla aligeuza akashika njia kuelekea upande alikokuwa amesimama yule dada muda wote akimshikilia mwenzie. Kuona vile, yule rafiki yetu huyu akaanza kujisogeza nyuma zaidi kadiri mende alivyomkaribia. Mende alipomkaribia kabisa yule dada aliyekuwa ameng'ang'aniwa, ndipo rafiki yetu alipiga hatua moja kuelekea nguzo iliyokuwa imeshikilia dari, la haula, mende anaye. Mende kama katumwa, akamfuata katika ile nguzo, ndipo rafiki yetu akapiga tena ukelele wa nguvu, 'nakufaaa...' Utaniuliza, 'kwa nini hakukimbilia chumbani kwake?'. Ni hivi, alishindwa kuwahi kuufungua mlango wake; vile vile, alitaka kuhakikisha kuwa mende anauawa ili apate amani kuwa hatamfuata chumbani kwake usiku. Ilibidi mmoja wetu amwue (sikumbuki alikuwa nani kati yetu) ili kuepusha watu kujaa na kutaka kujua kulikoni mtu 'anakufa' vile vile kutaka kuondoa ile aibu yakuwa dada fulani ni mwoga wa mende. Muda wote huo tulikuwa tunashikilia mbavu kwa kicheko (adabu zetu ndogo wakati huo, tunacheka msiba). Ilikuwa ni 'full' kuelewa somo la saikolojia ilipofika siku ya kufundishwa kipengele cha 'phobia' kwa maana kila mmoja aliikumbuka ile songombingo ya mende koridoni. Ndipo tulipong'amua kuwa alaa, kumbe ni ugonjwa. Na hapo ndipo nilipomkumbuka dada yuleee, wa Sekondari. Ama kwa hakika, usilolifahamu ni kama usiku wa kiza. Bofya hapa umtizame mtangazaji mmoja wa hali ya hewa akiteswa na mende studioni. ![]() Habari ya kusikitisha toka Uganda inasema kuwa daktari mmoja ambaye kwa sasa ni marehemu aaliyefariki dunia kwa UKIMWI aliacha orodha ya majina ya watu wapatao 782 ambao aliwaambukiza Virusi Vya UKIMWI (VVU). Daktari huyo kwa jina Byarugaba alikuwa na kliniki yake katika eneo la Nakulabye mjini Kampala. Alifariki wiki iliyopita na kuzikwa katika Wilaya ya Kanungu huko Magharibi ya Uganda. Ameacha orodha hiyo aliyoiandika katika daftari ambamo aliandika majina ya watu hao pamoja na namba zao za simu. Inasemekana kuwa aliugua UKIMWI kwa miaka mitano na kabla ya kifo chake alimfahamisha rafiki yake kuwa amewaambukiza wagonjwa wote wanawake ambao walihudhuria katika kliniki yake kwa huduma za utoaji mimba au kwa matatizo mengine yoyote ya kiafya. Pia alisema aliwaambukiza wanawake wengine katika kumbi za starehe na muziki, kwenye baa, mahotelini na katika migahawa. Inasemekana wengine walibakwa baada ya kulazwa kwa dawa ya usingizi (Chloroform) na kwamba baadhi yao hawafahamu kama wameambukizwa VVU. Taarifa hii inakuja wakati ambapo Serikali ya Uganda inandaa mswada utakaowaadhibu wale wote watakaogundulika ama kuthubutu kujaribu tu au kufanikiwa kitendo cha kuambukiza kwa makusudi VVU watu wengine. Kwa habari zaidi, soma mtandao wa 256news.com ama blogu ya Dk. Faustine From: Julie I thought I would share this with parents teenagers. Sometimes they do things we wouldn't expect them to do but without really knowing why they did what they did, we can't rescue them. Sometimes we have to open the door for them to confide in us about their fears, worries, and uncertainties. if one creates conditions that would make them not trust us, the result can be devastating. Read what was written by and 8th grader named Jessica Arlia below. Julieth K., Date: Mon, 22 Feb 2010 08:34:26 -0700 Message from Jessica Arlia: If only adults lived our lives. Life today for teenagers is more difficult than most think. I know that most adults think that our only problems are what we're going to wear the next day or whether we're in the cool crowd, but some of us have it much more difficult than that. What adults don't know is that so many kids are dealing with depression, cutting themselves, being beaten, raped or sexually harassed, and even suicide. that's when they turn to drugs, alcohol, sex and crime. I know people in every one of those categories and something needs to be done. To help these kids, one of the best things parents can do is to be there for us. Don't be mad at us for acting rashly when you know there are reasons for it. Try to understand what we're going through and see what you ca do to help. Our irresponsibility is usually a silent cry for help. We want help even if we don't admit it. So please, just be there for us when we need it most. Jessica Arlia From: Edith The worst thing as a parent you can do to your teenager is to shut them out, not listening to them. You may not like what they are saying but open the lines of communication that way if you are lucky they will confide to you their worst fears and worries instead of their buddies. The way you react to some of these talks makes the difference whether they are going to confide to you again or not. So keep your cool even when you want to scream, Its a very thin line we walk as parents, so you walk it with care. And pray that God will guide them whatever mistake they make is a learning process and not the end of the story. God Bless us all, there a are no books out there that will make it easy you write it as you go. Edith K., Date: Mon, Feb 22, 2010 at 12:10 PM ![]() For the past two and a half years, there has been advancement in the world of science and technlogy in the medicine filed than the history of man, says Eric Topol in one of many TedMed presentations. The stethoscope was invented in the year 1816. It is expected that in 2016, doctors (and healthcare workers who are directly involved in client's care) will no longer have to carry this equipment. Instead, Eric Topol says medics and the general population will be using smartphones to monitor vital signs and chronic conditions. From physiology to imaging, we will be able to track and see the following on our phones:- - Electrocardiogram - ECG (EKG) - The vital signs (Blood Pressure, Temperature, Respirations, Heart Rate, Oxygen Saturation) - Contractions (in pregnant and expectant mothers) - Blood sugar - Sleep pattern (useful in determining sleep apnea) - Calorie intake in real time (useful in weight management) - Ultra Sound e.t.c. ![]() The tool is going to be able to help predict for example, who is going to get Diabetes type 2, Breast Cancer, Atrial fibrillation, Sudden Cardiac Arrest etc in the future, based on their genetic makeup. if you click on the series of photos embedded below, you will see one with the Top Ten diseases that at the moment can be tracked. The list is based on the percentage and distribution of some chronic diseases in the general population of the USA. While appreciating all this power of technology, my thinking was embeded on how we can apply it in our settings and be able to benefit Africa in the light of common and chronic diseases such as Malaria, HIV/AIDS, TB and now Diabetes, Hypertension etc. Click here to watch this video on the videos page. Pata elimu kwa njia ya katuni 02/24/2010
Bofya picha kuzikuza kwa muonekano mzuri zaidi na maandishi yanayosomeka. |