Elimu yetu ni misiba kwa Taifa 03/02/2012
Na Mohamedi Mtoi Hakuna maneno matamu zaidi ya kusema kuwa Elimu yetu iko kwenye mkwamo mkubwa sana kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya nchi yetu. Isipo kuwa ukisikiliza wanasiasa wakisifia idadi ya vyumba vya madarasa vilivyojengwa pamoja na idadi ya wanafunzi walio andikishwa shule unahamasika na kufarijika bila chembe ya shaka kuwa tumepiga hatua kubwa sana katika sekta ya elimu. Lakini ukweli mchungu unabaki kuwa Elimu yetu iko kwenye mkwamo mkubwa sana na hakika tunaandaa taifa la vilaza wenye vichwa nazi. uzuri wa bahati ni kwamba wakubwa wamelijua hili mapema sana ndio maana wao hawasomeshi watoto wao kwenye hizi shule za kina Kayumba zilizosheheni ukanjanja wa kila aina, Wao watoto wao wana wasomesha kwenye shule zenye mazingira bora kwa afya ya akili ya watoto wao ili waje kushika nafasi zao na kuendelea kuwatawala watoto wa maskini wasio kuwa na uwezo wa kupata elimu bora. Matatizo ni mengi kwenye sekta ya Elimu lakini kubwa ni namna ya kumpata na kumuandaa mwalimu bora atakae fungua milangao ya fahamu ya mwanafunzi. Walimu wengi wa sasa hasa wale wa shule za msingi ni walimu waliofauli kwa viwango vya chini (Div IV), hawa wamefeli na wanatakiwa kuandaa watoto watakao faulu, halika dhalika sekondari, mfumo wa kuandaa walimu kwa njia ya Vodafasta nao umekuwa na madhara makubwa kwani kwa kipindi cha mwezi mmoja au mitatu bado hakitoshi kumuuandaa mwalimu bora atakae kuwa mahiri kwenye nyanja zote za ufundishaji, kitakacho fuata hapo ni kushindwa kumudu mchakato wa ufundishaji na matokeo yake ufaulu duni wa watoto. Lakini pia baya zaidi kwa sasa ni la walimu kutokuwa na ari ya kufanya kufundisha kutokana na mazingira magumu na ki mshahara kidogo kisicho endana na gharama za maisha, Nina mfano wa Mwalimu aliye ajiriwa kwa ngazi ya Stashada tangu mwaka 2006 akianza na mshahara wa shilingi 124,000/= (take home) mpaka leo hii analipwa 280,000/= (take home) ana barua ya kupandishwa daraja mkononi lakini hajabadilishiwa ngazi ya mshahara na wako wengi wa namna hii. Hebu tujiulize, kwa shilingi 280,000/= Mwalimu huyu ataishi maisha ya namna gani kwenye mfumuko huu wa bei yeye na familia yake? Ari yake ya kufundisha kwenye darasa lenye watoto 70 - 80 itakuwaje? Mdororo wa elimu yetu unaanzia kwenye kuto kuwajali walimu kimaandalizi na ki-maslahi, majengo kwangu si tija maana mwalimu aliye andaliwa vizuri ki saikolojia na kimaslahi akipatiwa vifaa bora anaweza kufundisha hata kwenye darasa mithili ya banda la kuku kama haya tuliyo kuwa nayo na bado wanafunzi wakapata maarifa yaliyokusudiwa. Kinacho tugharimu leo ni kukosa viongozi wenye utashi wa dhati kusimamia elimu kwa dhati ya kusimamia na matokeo yake imekuwa vurugu mechi na uchakachuaji wa mitihani. Add Comment With thanks to the writer of the article below, I thought it was okay to share the message with wavuti.com readers/visitors because it concerns Tanzanians. Dear Subi. Thanks so much for continuing to provide Tanzanians with uncontaminated and relevant information through your blog. I would like to acknowledge your effort and those of who are doing the same in the threads posted and in other forums too. I would like to kindly request you to give me a space on your blog to share my personal appraisal of the situation at the moment. As a stakeholder in the health sector and so do you, improving the quality and safety of health services in this country and wherever else, requires meeting the needs and expectations of both internal [healthcare workers] and external [patients and community] customers. These needs and expectations are variable but at the end of the day they are all determinant factors for success. My analysis of this situation, doctors are for the first time in history demanding for both internal and external customers rights, expectations and needs. I am a bit disappointed by the breeze of the discussion in the sense that everyone is so focused on that doctors should return as the government should be addressing their needs. One could argue that this is possible, but think about hepatitis B vaccine – such a crucial but affordable intervention. Currently the Ministry is not providing for this and it is truly unacceptable. What about medical insurance for doctors? In several occasions I have been approached by colleagues that we make a contribution for fellow doctors who are admitted at Muhimbili Orthopedic Institute and other private hospital, and yet these are the key providers of the service in the country. I can not over-emphasize how the wages are a total mismatch with what these individuals do, bearing in mind current inflation rates and the like. The external ones are more important and I bet if the community could have understood about this, may be they could be the ones denying to go to facilities. These doctors have been complaining about lack of infrastructure, materials, supplies and equipment, factors of which truly compromise the safety and quality of the services offered to patients, albeit doctors presence in the facilities. There are some anecdotal reports on the lack of stuff listed hereunder in a number of reputable hospitals in the country:
These are just examples, but my point is, I am not seeing a clear strategy in trying to address these issues, and it is high time that the government take care of the internal clients needs and promptly work together in addressing the external clients needs starting with the most life-threatening ones. There are people in the country who could work with the government in coming up with solutions if given opportunity. I submit. Bunge halina mguso na Wananchi ‘out of touch’ - Zitto KabweInasikitisha kwamba Bunge laweza kukaa wiki nzima na kujadili masuala mbalimbali bila kutoa muda kujadili suala la mtikisiko katika sekta Afya. Siku ya kwanza ya Bunge nilisimama kutaka taarifa ya serikali kuhusu mgomo wa madaktari na taarifa hiyo ijadiliwe na Bunge. Spika akalojulisha Bunge kwamba Serikali imempa taarifa na itawasilishwa. Bunge likaahirishwa siku bila kurejea. Kamati ya Uongozi ya Bunge ilipohitaji taarifa ya Serikali, Serikali haikuwa na taarifa. Kwa hiyo walifanya ujanja ujanja kuzuia mjadala wa mgomo wa madaktari. Leo wabunge kwa mara nyingine wamesimama kutaka mjadala huu wa dharura. Naibu Spika wa Bunge akatumia sababu za kiufundi kuzuia mjadala. Inawezekana wabunge hawakuwaandaa wabunge kusimama kuunga mkono hoja, lakini ni jukumu la Kiti kuona umuhimu na udharura wa mijadala. Hii inadhihirisha kwamba sasa Bunge kama Mbunge mmoja mmoja au kwa ujumla wake na Taasisi ya Bunge imekosa mguso na Hali ya wananchi (out of touch). Hali hii ni hatari sana. Wananchi wanapoona chombo kinachowawakilisha hakitoi nafasi kwa masuala yanayowagusa, watachukua hatua zao wao wenyewe na hivyo kuhatarisha utulivu wa nchi. Bunge liache shughuli nyingine zote na kutoa fursa ya kupokea taarifa ya serikali kuhusu madai ya Madaktari, kuijadili na kuazimia kwa kuelekeza hatua za kutekelezwa na serikali. BUNGENI LEO: Mgomo wa Madaktari na Sheria ya Bodi ya Mikopo - John Mnyika Asubuhi ya leo Naibu Spika Job Ndugai alitumia kanuni vibaya kuzuia hoja ya dharura bungeni kuhusu mgomo wa madaktari. Kimsingi, sikuwasilisha hoja ila niliomba muongozo wa Spika ili niweze kupatiwa nafasi ya kuwasilisha hoja ya dharura. Kwa kuwa hoja kama hiyo iliwasilishwa juzi na ikaungwa mkono lakini Spika akasema ameshakubaliana na serikali kuwa ingewasilisha kauli. Hata hivyo, jana hakukuwa na kauli ya serikali huku wananchi wakiendelea kupata madhara ya mgomo. Hivyo nikata muongozo kwa kuwa Spika alitumia kanuni ya 49 (2) ambayo kimsingi inatoa mwanya kwa kauli ya serikali kuwasilishwa kwenye wakati atakaoona yeye kuwa na unafaa juu ya jambo linaihusu serikali na lisilozua mjadala. Nilitaka kanuni hiyo isitumike badala yake wabunge tutimize wajibu wa kuisimamia serikali kwa kutumia kanuni ya 47 kuhusu hoja ya dharura. Kwa kuwa ilikuwa muongozo hakukuwa na hitaji la kikanuni la wabunge wengine kuunga mkono lakini akaamua kuilinda serikali kwa kuwa hawakuwa wamejiandaa. Lakini mwishoni ameahidi kuwa kauli ya serikali itatolewa kesho. Wabunge wana kigugumizi au...? - Beda Msimbe/Lukwangule KATIKA hali ambayo haikutarajiwa na wachambuzi wa mambo leo katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu suala la madaktari na posho za wabunge zinazowaumiza vichwa hayakupata nafasi ya kuulizwa. Waandishi wa habari waliokuwapo katika chumba cha kufuatilia mijadala ya bunge walijikuta wakisemezana imekuwaje baada ya maswali manane kwa waziri mkuu yote kukosa swali kuhusu tatizo la madaktari na posho. Huenda tatizo la madaktari kwa kuwa linangoja tamko la mawaziri husika, lakini suala la posho bado lingeweza kuulizwa kwa kuwa kuna kutupiana mpira kati ya Ikulu na ofisi ya Spika juu ya kuridhiwa kwa posho hizo. Maswali aliyoulizwa waziri Mkuu jana mengi hayakuwa ya kisera na kumfanya Spika wa Bunge Anne Makinda kuwakumbusha wabunge kwamba Waziri mkuu anahitaji maswali ya kisera na wala si ya kiutendaji, mambo ambayo yanatakiwa kujibiwa na mawaziri. Lakini hata kabla spika hajasema hayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda naye alisema kiungwana kwamba maswali ambayo ni specific (mahususi) hawezi kuyajibu kwa kuwa yeye atakuwa anajua masuala ya kijumla ambayo yanagusa sera. Katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo wabunge wengi walizungumzia majimbo yao na matatizo binafsi kuliko masuala ambayo ni ya kitaifa na yenye mwelekeo wa kuchanganua sera zilizopo. Hata hivyo Waziri Mkuu ambaye alijibu maswali kutoka kwa wabunge wanane kati ya 26 walioomba kupewa nafasi kwa Spika, aligusia tatizo la kuyumba kwa uchumi ambako alieleza ni kwa dunia nzima. Akijibu swali la mbunge Diana Chilolo (Viti maalum - CCM) kuhusu mkakati wa serikali wa kukabiliana na tatizo la kuharibika kwa uchumi wa nchi Waziri Mkuu alisema taifa lipo katika msukosuko mkubwa unaotokana na mfumuko wa bei unaosababishwa na bei kubwa ya chakula na mafuta. Aliwatafadhalisha watanzania kutambua kwamba tatizo la kuyumba kwa uchumi si la watanzania pekee bali ni la kidunia ila kinachostahili ni kutekeleza mipango itakayowezesha kuongeza tija na kuboresha uchumi. Pia alizungumzia uboreshaji wa kilimo ambapo alisema serikali inajitahidi kilimo kuwa chepesi na chenye manufaa ili vijana wasikimbilie mijini na pia kutanua sekta nyingine kwa kuwa na mazao ya kusindika na kuyaongezea thamani. Alisema ni kweli kuwa ni wajibu wa serikali kuweka mazingira mazuri ya uzalishaji mali lakini pia ni wajibu wa wananchi kuwajibika. “Serikali imejitahidi kusaidia… tumeshusha bei ya matrekta kutoka India kati ya asilimia 15-30 ili kukiinua kilimo” alisema waziri Mkuu. Wakati huo huo Waziri Mkuu amesema kwamba mradi wa ujenzi wa mji wa kisasa wa Kigamboni na Kurasini unachelewa kutokana na haja ya wananchi kushirikishwa. Akijibu swali la Mriam Kisangi (viti maalumu – CCM) aliyetaka kujua miradi hiyo inaanza lini kwa kuwa inawachelewesha wananchi kupata mikopo katika benki kwa kukosa hati, alisema kamati imeundwa ili kuzungukia wananchi. Akizungumzia suala la fidia Mabwepande, Waziri Mkuu alisema kwamba serikali inajipanga ili wale wanaostahili kulipwa waweze kulipwa fidia zao. Aidha alisema kwamba mpaka sasa viwanja 300 vipo tayari kwa ajili ya waathirika wa mafuriko na kwamba watu waliokusudiwa ni kaya 500. Alisema hata hivyo wanachangamoto kubwa ya kuwapatia viwanja wapangaji kama Rais Jakaya Kikwete alivyoelekeza. Taarifa ya mambwepande ilitokana na swali la mbunge wa Kawe Halima Mdee (CHADEMA). Akizungumzia masuala ya magari ya serikali kuwekewa bima, Waziri Mkuu alisema kwamba kupanga ni kuchagua na kusema zipo sababu kwanini magari yote hayo hayawezi kuwekewa bima. Swali la Bima liliulizwa na mbunge wa Ole, Rajab Mbarouk Mohamed (CUF). Swali jingine ambalo liliulizwa lilikuwa la wastaafu ambalo nalo lilikuwa mahusisi na Waziri Mkuu kumtaka mbunge awasiliane na waziri wa mambo ya ndani. Wabunge wengine ambao waliuliza maswali mahsusi ni mbunge wa Vunjo Agustino Mrema (TLP) aliyeulizia soko la Himo, Profesa Kulikoyela Kahigi (CHADEMA) aliyeuliuzia wastaafu jimboni kwake, mbunge wa Kasulu Mjini Moses Machali (NCCR-Mageuzi) na mbunge wa Kilwa kaskazini, Muntazi Ali Mangungu (CCM). Taarifa ya habari Clouds FM saa 12 jioniSehemu ya kipindi cha Jungu Kuu TBC Nashindwa niandike nini na niache nini, na hata nitakachoandika hapa kama kitaleta maana yoyote; Kwa kuwa nimejawa na huzuni isiyo kifani; Huzuni kiasi cha kushindwa hata kufanya shughuli za kawaida. Namaanisha hata kula, hamu sina. Kila mara inanijia kichwani picha moja baada ya nyingine ya ama mtoto, au mwanamke au mwanaume, amelala katika kitanda cha wagojwa Muhimbili, Mbeya, Moshi, Morogoro, Mwanza n.k. anapumua ile pumzi ya mwisho "gasping for air" ya kiumbe hai anapokaribia kukata roho. Nina huzuni kubwa zaidi kutokana na jinsi ambavyo viongozi na watu wenye dhamana wameshindwa kabisa kufikia muafaka wa kuokoa roho za Watanzania ambao ndiyo wanasema wanawaongoza na kujali maslahi yao. Maslahi makubwa kuliko kuunurusu uhai pale inapowezekana siyafahamu. Ni nyakati kama hizi unafikia hatua ya kujiuliza Mungu yupo wapi na kama anaikumbuka Tanzania. Nyakati za kuwaza kama kufa ni jambo baya kama wengi tulivyoaminishwa, au ni jambo zuri na la kawaida kabisa isipokuwa tu tunatengana na wenzetu wanaotangulia kwenda ambako walio hai hawawezi kwenda hadi wafe. Nyakati kama hizi nawaza kuwa Mungu anaikumbuka Tanzania kweli na anaipenda isipokuwa ameruhusu yanayotokea yatokee kwa kuwachukua waja wake wamrejelee kwa maana hata uhai wao ungeokolewa kwa siku kadhaa na Madaktari au/na Wauguzi, bado maisha yake yangeendelea kuwa ya taabu na maumivu. Kumbe pengine kufa ni pumziko kwao. Ni nyakati kama hizi ninaamini ile kauli ya viongozi wetu wanazotoa punde zinapotokea ajali na majanga yakachukua roho nyingi za watu kuwa, "Ni mipango ya Mungu" "Ni mapenzi ya Mungu" basi huenda ni hayo hayo mapenzi na mipango ya Mungu kuwa mgomo wa wahudumu wa afya utokee na Viongozi wa Serikali wapungukiwe akili ya kutatua ili watu wafe. Kimya cha Jumuiya za Kimataifa na ukimya wa vyombo vya habari vya Kimataifa umeniongezea simanzi. Pengine ni kwa kuwa hii ni nchi ya bara la Afrika, bara ambalo hakuna jema lolote linalotarajiwa na hata watu mamia kwa maelfu wakipoteza uhai, si habari mpya masikioni mwao, wamezoea kusikia hahari za vifo, lipi jipya? Hivyo hawatilii maanani kwa kuwa hakuna umuhimu huo. Mkidharauliwa na hata viongozi wenu wenyewe mliowachagua, mwanadamu gani anapaswa kuwathamini? Mahakama ya The Hague huwa inahusika na vifo vinavyotokana na machafuko na vita baada ya chauguzi za kisiasa tu? Kwa hivyo "neglect" ya wananchi kupata huduma ya msingi ya afya haimhusu Ocampo sivyo? Mungu anaikumbuka Tanzania na anaipenda na mapenzi yake yanatimizwa! Amin. *Kwenye video ya pili, dakika ya 52, yupo mtoto wa afisa polisi anayetoa maneno ya uchungu mkubwa. Usikose! Hivi ni video zinazoonesha jinsi biashara ya mihadarati ilivyo na mtandao mkubwa. Biashara ambayo hata wewe usipokuwa makini unaweza kujikuta umehusika. Video inayotanabahisha maafisa wapelelezi wanavyoweza kuwa washiriki wakuu wa biashara hiyo, ama kwa kutaka au kwa shuruti, na jinsi ilivyo vigumu kutenganisha aliye mkweli na mwongo. Lipo tukio la kutisha kwa jinsi ambavyo askari polisi aliyepewa jukumu la kuhifadhi ufunguo uliokuwa wa sehemu ilikokoifadhiwa shehena ya mihadarati aina ya "cocaine", alivyouawa kinyama kwa kupigwa jumla ya risasi 22, ikipenya moja baada ya nyingine kwa takriban daika 15 katika sehemu mbalimbali za mwili wake, katika boma lake huku wanawe wawili wadogo, wakike na wa kiume wakishuhudia, ambapo mmoja anahadithia alichokiona. Video hii pia inaonesha jinsi watu waliopewa ajira ya kusafirisha bidhaa, walivyojikuta na wazo la kutaka kujua walichokuwa wakisafirisha mara kwa mara, ndipo walipofungua na kutambua ilikuwa ni mihadarati. Utaona vile vile jinsi ilivyo rahisi kwa askari na watumishi wazuia magendo wenye tamaa, ilivyo rahisi kujihusisha na biashara hiyo na kuwatisha askari na watumishi waaminifu wanaofanya kazi kuzuia mihadarati. Magari ya serikali na 'ambulance' zaweza kutumika kwa shughuli hii, jambo ambalo uongozi mkubwa unahusika kwani haiwezekani magari hayo kutumika bila ruhusa, ufahamu na notisi ya viongozi wa jeshi husika. Vile vile utaona jinsi ilivyo rahisi kwa watu waroho wa utajiri wa haraka wanavyoweza kujichomeka kwa nguvu katika mihadarati iliyokamatwa, ili tu wapate kiasi cha mihadarati hiyo kwa ajili ya kujipatia fedha. Mohammed Ali na kikosi cha wanahabari wadadisi wanaelezea matokeo ya uchunguzi wao. Maoni yatolewa kuhusu "Je wajua: Kwenda kutibiwa India inawezeka ni "biashara" ya watu fulani?" 01/02/2012
Yafutayao ni maoni ya Mashingo aliyoyatoa katika chapisho lenye kichwa cha habari, "Je wajua: Kwenda kutibiwa India inawezeka ni "biashara" ya watu fulani?" 1. tatizo la watanzania walio wengi ni kufuata mkumbo bila kutumia angalau dakika kadhaa kufikiri. kwa nini India? kwani hakuna nchi nyingine ya afrika ambayo ina huduma bora zaidi? sasa hivi mpaka internet wameanza kutangaza hospitali maalum kwa ajili ya watanzania. hamjiulizi mbona wahindi tulio nao hapa hawarudi kwao? ni ukweli kwamba ukireffer mgonjwa kuna commission. nikiwa kama mmoja wa waliopata 'bahati' ya kusindikiza wagonjwa India, niliahidiwa kupewa sponsorship na 'wenyeji wetu' iwapo ningefacilitate more refferals. Hawajifichi,hawa ni wafanya biashara sio ndugu zetu,so i don't blame them.Iits our own stupidity. kwenda kutibiwa nje sio kosa au dhambi. Lakini iwe kweli imeshindikana hapa kwanza. Sio hali ilivyo hivi sasa ambapo viongozi wa juu wana haki ya kwenda 'KUCHEKIWA AFYA' nje ya nchi wao na familia zao. Amiin nawaambia, kama hili halitapigiwa kelele na kufutwa,hali ya hospitali zetu hasa hizi ambazo ndio wengi wetu tunakwenda itazidi kuwa hovyo. Umeona wapi mtu akahangaika kuboresha nyumba asimolala! Hivi tunaonekanaje huko nje? 2. Sikatai kweli kuna vitu wametuzidi, lakini tungeweza kuvifanya hapa kwetu kama tukiamua. Na serikali zinazojali na kufanya kazi kwa kutumia akili na kuona mbali huwa unaleta wataalam au unapeleka wa kwako huko unakodhani wamekuzidi kimaarifa ili watu wajifunze sio kupeleka wagonjwa. Mbona kenya walikuja kujifunza tunaendeshaje Mfumo wetu wa bima ya afya. 3. Kingine ni kuingiliwa kwa fani ya utabibu. Leo hii Tanzania kila anayejisikia kujiita daktari anajiita tu na bila kujali uwezo wake anatibu watu. Sijui kama Watanzainia hata wanajua kutofautisha. Na hii matokeo yake ni kugeneralise kuwa hii fani ni ya wasanii. Ni nchi pekee ambayo mgonjwa akifika kwa daktari anamkabidhi kila kitu na kumuachia afanye maamuzi yake,bila hata kuulizia matokeo yatakua yapi. Ni wagonjwa wangapi huwa hata wanauliza aelezwe anachoumwa na wajadili njia za matibabu na pengine kukataa njia moja na kuchagua nyingine! Ni wangapi wamefanyiwa upasuaji bila hata kuuliza kama ndio njia pekee,au hata kujua kwa juu juu tu kinachoenda kurekebishwa au kutolewa? Na hili ni tatizo,kwani hata mgonjwa anapoelezwa tatizo lake na options za matibabu wengi huwa wanaona kama wapotezewa muda. Haya,with all due respect, hawa madaktari wanajeshi wanaopelekwa muhimbili wanatokea wapi? huko walikokua walikua wanareffer wagonjwa muhimbili kwa madaktari bingwa, sasa leo aliyekushindwa Lugalo ndio unamkuta muhimbili kitengo ambacho hata walio muhimbili kwenyewe sio wote wana utaalam nako. Ni kweli mtu yeyote anaweza akaitwa kutoka alikokuwa (jeshini, wizarani, mstaafu) na akaziba pengo! Sitaki kuamini kwamba ni rahisi hivyo. Na sidhani kama ni lazima sana wavae magwanda,ni wanajishi sawa, lakini pale ni hospitali,kuna maadili yake. Hata hospitali za jeshi huvai magwanda unapokua unatoa huduma. Au hawataonekana kuwa ndio waliopelekwa na serikali? 4. Dharau kwa vituo vyetu vya afya. Ni kiongozi gani alishawahi kwenda kwa mfano mwananyamala,au hata Muhimbili kwenyewe akapigwa picha akiwa kwenye foleni ya kusubiri tiba? lakini ni wangapi walipiga picha kwa babu wakinywa kikombe ambacho hata tafiti zake zimefanyika baada ya watu mamia kuwa wameshakunywa? na waziri wa ujenzi, Mh magufuli akatangaza kutenga tsh billioni 10 kwa ajili ya kumjengea barabara ili mkwanywe vizuri? ile ilipangwa kwenye bajeti? kama waliweza kumtengenezea mazingira mazuri ili mkanywe msichokijua,kwa nini wasifanye hivyo huku ambako wengi tayari angalau mna ufahamu nako na hata wasio na imani wanapona? Ili kupitisha dawa mpya inabidi ifanyiwe utafiti si chini ya miaka 10! hii ni kwa sababu kila dawa ina madhara ya muda mfupi na yale ya muda mrefu. Leo hii wangapi wamejitokeza kuelezea madhara yaliyowakuta baada ya kunywa kile kikombe? Ni kweli hakuna,au ndio kila mtu na mzigo wake kwa sababu ulienda mwenyewe? Mwisho kabisa, ningependa kutoa mifano michache. Iwapo umelipia kampuni ya ulinzi ikuletee mlinzi,unatarajia mlinzi nyumbani kwako kama mlivyokubaliana. pale mlinzi asipotokea, utakachofanya ni kwenda kwa meneja au mwenye kampuni kudai mlinzi kama mlivyokubaliana. Timu yetu ya taifa hatupangi sisi watazamaji. Tunakabidhi majukumu yote kwa kocha na kamati yetu ya ushindi. Na kama haikutuletea matokeo mazuri, tutalaumu mchezaji fulani lakini anaebeba lawama zote na kuwajibishwa ni kocha kwa kuchagua watu ambao hawakutufikisha pale tulipotaka. Sasa kwa nini Watanzania tunaoteseka hatujaiuliza wizara na serikali kwa nini haiwawajibishi hawa watabibu ambao hawatoi huduma wanayotakiwa kuitoa? Ni ujumbe kutoka kwa mdau wa afya, unajieleza! Tafadhali tuachane na kuuliza "nani mjumbe" tukazie "nini ujumbe"! It is very possible that, private practice in India is driven by pay back system, you refer a patient to Apollo you get paid. I just don't have evidence but I am sure move za hospitali kukusanya wagonjwa na kuwapeleka India zitakuwa driven by this payment system, I bet our officials may also be involved. And these people are serious about that business, Apollo wanaanza kuwapa huduma wagonjwa Dubai, so from the airport you start getting services. And the practice is made in such a way unafanyiwa vipimo vingi kadiri inavyowezekana, including those you don't need, the aim being to maximize the cost. I am posted at Christian Medical College Hospital in India, this is a hospital which is not business oriented, but it is the best cardiology centre in India, it is one of the best nephrology centre in India also, iko Tamil Nadu km 120 kutoka Chennai. The cost of services here is 1/3 ya gharama za Apollo and the like, the cost is even cheaper as compared to cost of some services in Nairobi (kuna mgonjwa alikuwa na leukemia Nairobi, gharama ya matibabu Nairobi ilitosha kulipia usafiri, matibabu gharama za kuishi hapa Vellore na akabaki na change), but guess what, no one is referring patient to CMC even in India itself because this hospital does not entertain the system of pay back!!!!! It is very sad in deed! YATOKANAYO...Upo msemo mmoja ulivuma siku chache zilizopita, unasema, "ukiona manyoya, basi ujue keshaliwa" Kwa hivyo, ujumbe huu unaweza ukawa umetufungua macho wengine tuliokuwa tukikuna vichwa kujiluliza kulikoni? Vipi "kutiririka" kwenda India kwa matibabu kwa viongozi wetu kunashamiri na kushika kasi hivi? Mimi kwa mfano nilijiuliza: Je! Hii inatokana na wagonjwa hao kukosa imani na tiba toka kwa wataalamu wetu? Kwamba, wanahisi wanapewa tiba isiyo na kiwango? Au ni imani ya kasumba ya kujitakia au kufuata mkumbo tu kwamba matibabu ya "mzungu" au "mhindi" ama "mchina" yanaponesha vyema na haraka zaidi kuliko yale ya "mbantu" mwenzetu? Hatuamini wala kuuthamini utaalamu wa wataalamu wetu? Ikiwa madai yao kwamba wanakwepa huduma hafifu na mbovu, je, hawa viongozi wanaokuwa wepesi kutaka matibabu nje ya nchi, wanakosaje akili ya kuwawezesha wataalamu wetu kwa vifaa na mazingira bora ya kazi kwa kutumia fedha hizo hizo wanazozipeleka "India" ili nasi Watanzania tujivunie Watalaalamu wetu, wananchi wa kipato cha chini nao wasioweza kwenda "India" nao wapate nafuu ya tiba nzuri? Mbona tunadharauliana hivi? Umewahi kujiuliza ni kwa nini Watanzania wengi wanaohama nchi na kuajiriwa nchi nyingine wanasifika kwa uchapa kazi wao lakini wakiwa Tanzania walidharauliwa hata pale waliposhauri yaliyo ya haki? Ama ndiyo "Nabii hakubaliki kwao?" Fedha wanazolipwa viongozi wetu hawa si zinatokana na kodi za wananchi na rasilimali za mumu humu ndani jamani? Sasa badala ya kuzizungusha humu ndani, ni kwa nini zinapelekwa kunufaisha mataifa ya nje? Ama yote hayo hayana maana kwa kuwa fedha zenyewe, haziendi "nje" kweli bali zinazunguka na kurudi mifukoni mwao? Hii nchi hii, ukisikia "pa" ujue ndiyo hivyo tena...! LICHA ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutoa amri kwa madaktari wote wenye mikataba na Serikali kurejea kazini, bado wanataaluma hao jana waliendeleza mgomo baada ya kutia saini vitabu vya mahudhurio na kutoweka kusikojulikana huku wauguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wakitoa msimamo mpya kwamba hawako tayari kufanya kazi na madaktari kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ). Juzi, Waziri Mkuu Pinda alitoa onyo kwa madaktari hao akiwataka kurejea kazini kufikia jana kinyume chake ambaye angeshindwa angekuwa amejifukuzisha kazi na kwamba madaktari wa JWTZ wangechukua nafasi zao. Agizo hilo la kwamba wangewatumia madaktari kutoka JWTZ jana liliamsha hasira za wauguzi Muhimbili ambao walitangaza msimamo wao wa kutofanya kazi nao. Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania, Tawi la MHN, Paul Magesa alisema madaktari hao hawana uwezo wa kufanya kazi katika hospitali hiyo ya taifa ambayo ndiyo kubwa nchini kwa kuwa inahudumia wagonjwa walioshindikana katika hospitali wanazotoka. “Ifahamike kuwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ni ya rufaa na inapotokea wagonjwa walioshindikana katika hospitali nyingine inakuwaje leo wakaletwa madaktari kutoka katika hospitali hizo kuja kutibu?” alihoji Magesa na kuongeza: “Sisi tulishafanya kazi nao mwaka 2005 na tunawafahamu wengi hawajui mambo mengi, watakuja kutuuliza na kutuongezea kazi za kufanya... tunaomba katika hili Serikali isikwepe tatizo, ilishughulikie kwa maslahi ya taifa,” alisema. Hali mbaya Hali katika hospitali hiyo kuu ya nchini imezidi kuwa mbaya, kutokana na kuendelea kwa mgomo wa madaktari hao huku kukiwa na dalili nyingine za mgomo wa wauguzi kupinga kufanya kazi na madaktari kutoka jeshini. Habari zilizopatikana jana na kuthibitishwa na uongozi wa hospitali hiyo, zilisema kwamba madaktari wengi walifika na kusaini katika kitabu cha mahudhurio na kuondoka. Mmoja wa madaktari katika hospitali hiyo, Dk Azizi Keto aliyekuwa katika wodi ya Mwaisela alisema kauli ya Pinda dhidi ya madaktari imewakatisha tamaa na kuwavunja moyo wa kufanya kazi. Alisema hali ni mbaya ndiyo sababu hata waliofika asubuhi hawakujisikia kufanya kazi. Katika hospitali hiyo madaktari walioendelea na kazi ni wale washauri, wanaotarajia kustaafu na walioingia mkataba na Serikali mwaka 2005, walipoitwa wakati madaktari walipogoma. Vilio vilitawala jana katika eneo la nje ya Wodi ya Mwaisela huku waombolezaji wakidai kuwa kama si mgomo huo wa madaktari, ndugu zao wasingepoteza maisha. Mmoja wa waombolezaji alikaririwa akisema ndugu yake alipoteza maisha bila ya kupata huduma hospitalini hapo. Baadhi ya wagongwa waliowasili katika hospitali hiyo wakitokea hospitali mbalimbali, walirudishwa bila ya huduma. Muhimbili yakiri Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mgomo huo, uongozi wa MNH umekiri kwamba hali ya upatikanaji wa huduma katika hospitali hiyo imezidi kuzorota. Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Hospitali hiyo, Aminael Aligaesha aliwaambia waandishi wa habari kuwa madaktari walio wengi wamefika na kujiorodhesha kwenye daftari la mahudhurio lakini wakagoma kufanya kazi. Hospitali za Dar Kwa upande wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, madaktari wamegawanyika wengine waliendelea na mgomo na wengine walionekana wakitoa huduma kwa wagonjwa. “Pamoja na kwamba wagonjwa wanahudumiwa lakini, inachukua muda mrefu kuipata huduma jambo linaloonyesha kuwa mgomo upo,” alisema mmoja wa wagonjwa hospitalini hapo. Taarifa hizo ziliongeza kwamba madaktari waliogoma, jana asubuhi walifika hospitalini hapo na kusaini majina yao kisha kuondoka. Habari zilisema maofisa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, walifika hospitalini hapo kuhakiki majina ya madaktari hao lakini walipoondoka na wao wakaondoka. Katika Hospitali ya Amana, Ilala nako baadhi ya madaktari walifika kazini wakasaini mahudhurio na kuondoka bila kufanya kazi yeyote. Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk Shimwela Meshack alisema hali ni mbaya katika hospitali hiyo kutokana na madaktari wote kufika kazini lakini wakagoma kutoa huduma. Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk Sophinias Ngonyani alisema mgomo huo ulifanywa na madaktari ambao hawajaajiriwa tu. “Mgomo huu upo kwa wale wasioajiriwa ila tunachokifanya kwa sasa ni kuhakiki waliokuwepo na wasiokuwepo kujua idadi ilio sahihi,” alisema. Ofisa Afya wa Manispaa ya Kinondoni, Dk Gunini Kamba alisema hospitali hiyo ina wataalamu wa afya 58, kati yao 42 ni madaktari, watano wako katika kitengo cha wafamasia, watano wengine maabara na sita katika kitengo meno. Hospitali mikoani Mkoani Morogoro, madaktari walifika kazini kama kawaida lakini hawakutoa huduma hali iliyofanya wagonjwa wasote kwa muda mrefu bila huduma. Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk Frida Mokiti alisema madaktari wote wameripoti kwenye maeneo yao ya kazi na kwamba taarifa zaidi angezitoa baada ya muda wa kazi. Hali kama hiyo pia iliripotiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru ambako madaktari waliingia kazini lakini baada ya kusaini daftari la mahudhurio waliendelea na mgomo. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo jana asubuhi alifanya ziara ya ghafla katika hospitali hiyo na kuonana na uongozi. Hata hivyo, hakuna taarifa ambayo ilitolewa juu ya nini kilichozungumzwa. Madaktari wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, waliendelea na mgomo huku baadhi yao wakisisitiza kuwa hawawezi kurejea kazini hadi Serikali itakapoamua kutekeleza madai yao. “Sisi tunachokitaka ni kutekelezewa madai yetu, hiyo kauli ya Waziri Mkuu ya kututishia kutufukaza kazi kama hatutarejea kazi kuanzia leo (jana) wala hatuiogopi hata kidogo, tunachotaka ni haki yetu itendeke,” alisema mmoja wa madaktari kwa sharti la kutotajwa jina. Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk Eleuter Samky alisema hadi saa 7:00 mchana jana kulikuwa na madaktari watano tu kati ya 75 waliokuwa wamefika kazini. Katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi, hali pia imekuwa ya kusuasua. Jana kulikuwa na msururu mkubwa wa wagonjwa wa nje waliokuwa mapokezi, wakisubiri huduma kwa zaidi ya saa nane huku wengi wakilalamikia uchache wa madaktari kwani aliyekuwapo zamu alikuwa mmoja tu. Baadhi ya madaktari ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini walisema mgomo wa sasa ni mbaya kuliko ule wa awali kwani kwa sasa wanaandika majina yao kwenye daftari la mahudhurio lakini hawatoi huduma kwa wagonjwa. Wanasiasa waingilia kati Baadhi ya wanasiasa wameingilia kati mgomo huo wakiwataka madaktari hao kurejea kazini kama walivyoagizwa na Pinda ili kuokoa maisha ya Watanzania. “Uhai wa mtu ni kitu kikubwa sana… Mimi naona ni vyema busara ikatumika ili kuokoa maisha ya Watanzania yanayopotea,” alisema Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia. Hata hivyo, alisema madaktari hao wanayo madai ya msingi lakini akawataka watekeleze wajibu wao huku wakifanya mazungumzo na Serikali. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema madaktari wanapaswa kufahamu kwamba kuendelea kugoma ni kuchezea maisha ya wananchi. Alisema kitu cha muhimu ni madaktari hao kurudi kazini kama walivyoagizwa na Waziri Mkuu na wasifikiri kwamba, Serikali itaendelea kuwavumilia huku ikiona maisha ya Watanzania yanapotea. Aliwataka wajifunze kwa kilichotokea mwaka 2004 wakati wa utawala wa Rais Benjamini Mkapa, ambako waligoma na Serikali ikaamua kutumia madaktari kutoka vikosi vya jeshi. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alimtaka Pinda kuacha vitisho na matumizi makubwa ya vyombo vya dola kwa madaktari wanapotumia uhuru wao wa kikatiba wa kukusanyika huku akisema chama hicho kinaunga mkono madai ya msingi ya madaktari. TUCTA yawageuka Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), limesema haliwaungi mkono madaktari hao kutokana na kushindwa kufuata utaratibu wa mgomo. Katibu Mkuu wa chama hicho, Nicholaus Mgaya alisema sababu ya kutounga mkono mgomo huo ni baada ya madaktari hao kukaidi wito wa kukutana na Serikali jambo ambalo alisema ni kinyume na taratibu za kazi. “Kwa hali hii madaktari wamepotea maboya. Kitendo cha kuitwa na Waziri Mkuu ili kufanya mazungumzo na kukataa ni dhahiri kuwa mgomo huo si halali maana walitakiwa kusikiliza Serikali inasemaje baada ya hapo wangeweza kukataa kama wangeona bado madai yao hayajafanyiwa kazi lakini kitendo cha kugoma bila kufanya mazungumzo ni kosa,” alisema Mgaya. Habari hii imeandaliwa na Geofrey Nyang'oro, Gedius Rwiza, Leon Bahati, , Raymond Kaminyoge na Joseph Zablon, Dar; Godfrey Kahango, Mbeya; Mussa Juma, Arusha na Rehema Matowo, Moshi via gazeti Mwananchi Na F. Mghanga, tanzmed.com Ni Jumatatu asubuhi. Hali ya hewa ya joto la kadiri ilikuwa ni kitu cha kawaida kwa maeneo haya ya Dar es Salaam kipindi cha miezi hii ya mwisho wa mwaka. Tupo darasani kwenye presentation ya somo linalohusu magonjwa ya figo. Mada ilihusu kushindwa kufanya kazi ghafla kwa figo au Acute Renal Failure kwa lugha ya wenzetu. Lilikuwa somo refu lililozungumzia kwa undani tatizo hilo. Baada ya mwenzetu mwasilishaji kumaliza kuwasilisha somo lake kikafuata kipindi cha maswali na majibu na masomo zaidi kutoka kwa Profesa aliyekuwa anasimamia ile mada. Mada ilikuwa moto. Maswali yetu pamoja na uzoefu wa yule profesa ulitosha kuibua somo na majibu yaliyotosheleza kiu zetu za kujifunza zaidi. Kisha baada ya somo akauliza swali kwa hali ya utani kidogo, nani kati yenu anapenda kuwa Nephrologist (daktari bingwa wa magonjwa ya figo). Wote tulibaki kimya tukitazamana kisha mwanafunzi muwasilisha mada huku akitabasamu alininyoshea kidole akasema "Fabby huyo." Profesa aliniangalia kisha akainamisha kichwa chini kwa masikitiko akasema “I feel sorry for you my friend (nakuonea huruma rafiki yangu)”. Sikuelewa kwanini alisema vile nikashtukia tu namuuliza “why Professor?” Huku bado akiendelea kunitazama akanijibu “because you will be seeing your patients dying everyday”. Jibu lake ghafla likanirudisha nyuma kama mwaka mmoja hivi nikiwa nafanya kazi hospitali moja ya Mission iliyopo mkoa fulani kusini mwa nchi. Ilikuwa siku ya Jumatano asubuhi. Hali ya kaubaridi baridi iliyokuwepo siku hiyo iliashiria kuanza kwa siku njema. Ninaingia wodini na kusalimiana na wauguzi wa wodi yangu kabla ya kuingia ofisini kujiandaa na round. Nilikuwa na kawaida ya kuanza siku kwa kufanya round kwa wagonjwa waliolazwa kabla ya kuingia ofisini kuwaona wagonjwa wengine wapya na wale wanaokuja kwa ajili ya follow up. Baada ya kuwaona wagonjwa kadhaa, nikakifikia kitanda cha mgonjwa mpya aliyekuwa amelazwa usiku wa kuamkia siku hiyo na kuonwa na Clinical officer aliyekuwa zamu. Ni binti wa miaka takribani 20 (kwa sababu za kimaadili sitataja jina, umri wake halisi, mahali anapoishi wala details zake nyingine). Hali yake ilikuwa mbaya maana alikuwa amenyong’onyea na alikuwa akipumua kwa shida sana. Mpira wa mkojo ulikuwa ukining’inia pembeni ya kitanda lakini hakukuwa na kitu ndani yake. Uso wake ulionekana kuvimba kwa mbali na alikuwa akizungumza kwa shida. Midomo ilikuwa mikavu na hata ngozi yake ilionekana iliyosinyaa na kavu kuliko kawaida. Nilimuita mwangalizi wake na kuanza kuchukua upya historia ya mgonjwa maana yeye mwenyewe alikuwa akizungumza kwa shida sana. Mwangalizi aliniambia kuwa mgonjwa wake, alianza kupata tatizo la kukosa mkojo kwa ghafla kama siku saba zilizopita. Hawakujua sababu hivyo wakadhani ni mambo ya ushirikina wakaamua kumpeleka kwa mganga wa kienyeji ambaye alikaa naye siku tatu huku akimnywesha kila aina ya miti shamba lakini bila mafanikio. Akasema, “tulipoona hali yake bado ipo vile vile tukaamua kumkimbiza hapa ili tujaribu huduma za kizungu. Kwahiyo kwa ujumla ana siku kama kumi tangu tatizo lilipojitokeza. Wakati tupo kwa mganga angalau hali yake ilikuwa siyo mbaya sana lakini jana usiku ndiyo hali ikabadilika tukaamua kumkimbiza huku. Sasa hivi hali chochote maana analalamika kichefuchefu muda wote, na akijaribu kula tu anatapika chote. Wakati mwingine anaongea vitu havieleweki basi baba ndiyo hivyo hivyo tu”. Baada ya kuuliza maswali zaidi kulingana na taratibu zetu, kwa muonekano wa mgonjwa na historia yake harakaharaka niliweza kuhisi ni kitu gani kitakuwa kinamsumbua huyu mgonjwa. Niliamua kumfanyia uchunguzi wa mwili (physical examination) ili kuona vishiria vingine vya ugonjwa. Alikuwa na dalili zote za mtu mwenye matatizo ya figo, na mbaya zaidi alikuwa katika hali ya hatari zaidi ya ugonjwa. Uchunguzi ulionesha, pamoja na dalili nyingine, kuwa alikuwa amevimba miguu (pedal edema) kwa kiasi fulani, tumbo lake lilishaanza kuvimba (ascites) na alikuwa akipumua kwa shida sana (dysponea), alikuwa na dalili za upungufu wa damu (anemia) na ngozi kavu kuliko kawaida kuonesha kuwa alikuwa amepungukiwa maji mwilini (dehydrated). Nikaagiza tufanye vipimo kadhaa kama vile vya kuchunguza utendaji kazi figo, vya kuchunguza uwiano wa madini/chumvi mwilini (electrolytes analysis), ultrasound ya tumbo, vipimo vya moyo na vipimo vingine kadiri nilivyoona inafaa. Ingawa vingi ya vipimo nilivyoagiza vilishindikana kufanyika ama kwa vile hakukuwa na vifaa vya kufanyia vipimo hivyo au hatukuwa na wataalamu wa maabara wenye ujuzi wa kufanya vipimo hivyo pamoja na kuwepo kwa mashine, bado niliweza kupata jawabu la tatizo lililokuwa linamsumbua mgonjwa wangu ingawa nakiri sikuweza kufahamu chanzo hasa cha ugonjwa wake ni nini kwa vile hatukuwa na vipimo vya kufanya hivyo. Alikuwa akisumbuliwa na kushindwa kufanya kazi ghafla kwa figo yaani Acute Renal Failure (ARF) na kwa dalili zake tayari alishafikia hatua ya kuwa na kiasi kikubwa cha madini ya potassium katika damu (hyperkalemia) na kwamba mrundikano wa uchafu mwilini ulikuwa katika kiwango cha hali ya juu kwa sababu figo zilishaacha kufanya kazi zake inavyotakiwa. Pamoja na kumuanzishia matibabu, katika hali aliyokuwa nayo matibabu sahihi ilikuwa kwanza kufahamu chanzo cha tatizo ili kukitibu, kumfanyia dialysis ili kutoa uchafu mwilini na hatimaye kama ikionekana figo zimekufa kabisa basi afanyiwe upandikizaji wa figo mpya. Nilipowaeleza yeye na mwangalizi wake kuhusu matokeo ya vipimo, hatua ya ugonjwa iliyofikiwa na nini cha kufanya ghafla niliona machozi yanamlengalenga mwangalizi. Kwa kweli alistahili kuwa vile. Kwa unyonge akaniuliza, “sasa baba hayo matibabu mnaweza kuyafanya hapa.” Nilimtazama tena na kwa kujitutumua ilibidi nimueleze tu ukweli kuwa hatuna uwezo wa kufanya dialysis pale kwetu, na wala hospitali ya karibu ya mkoa haina uwezo wa kufanya hivyo mjipigepige mumsafirishe mgonjwa Dar es Salaam kwa matibabu zaidi. Kama aliyekuwa anasubiri bomu zaidi nikamtajia na gharama za kufanya hayo matibabu na muda anaotakiwa kufanyiwa. Mama mwangalizi alinyamaza kwa sekunde kadhaa kama mtu anayefikiria kitu kisha kwa unyonge akasema , “baba kwa umaskini wetu huu hali yenyewe hii unaiona nilivyo. Naomba chonde chonde ujitahidi kufanya lolote lile hapa kama Mungu akipenda kumchukua basi mapenzi yake yafanyike maana hatuna uwezo wa kumsafirisha siyo tu kwenda huko Dar es Salaam bali hata hapo mkoani hatuwezi kufika”. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea na matibabu na kufanya kwa kadiri ya uwezo wangu kuokoa maisha ya mgonjwa wangu. Nasikitika kuwa baada ya masaa kadhaa mgonjwa yule alifariki kwa mshtuko wa moyo kama complication ya hypekalemia. Nilihuzunika sana lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kuchapa kazi kuhudumia wagonjwa wengine. Kwanini nimekikumbuka hiki kisa? Hiki ni kisa kimoja tu kati ya visa vingi vingi ambavyo madaktari wanakutana navyo kila siku katika utendaji wao wa kazi. Kushuhudia uhai ukipotea wakati ungeweza kuokoa maisha lakini huna vifaa au wataalamu wa kusaidiana nawe ni jambo linaloumiza sana kwa daktari na watoa huduma ya afya kwa ujumla wake. Nawafahamu madaktari waliowahi kufanya operesheni kwa kutumia mwanga wa tochi za simu baada ya umeme kukatika hospitalini kukiwa hakuna jenereta wala hata taa ya kandili, wapo waliolazimika kubuni mbinu mbadala baada ya kukosekana maji ya drip (iv fluids) kwa ajili ya matibabu. Hapa majuzi tumesikia kuhusu watumishi wa hospitali moja ya misheni huko mkoani Manyara wanaolazimika kutumia vipande vya nguo na mashuka kama gloves wakati wa kuhudumia wagonjwa, ipo mifano mingi mingi inayoonesha uzembe wa watendaji wanaotakiwa kuboresha mazingira ya kazi ili watoa huduma ya afya waweze kutoa huduma katika mazingira salama kwao wenyewe na kwa wagonjwa wao na hivyo kuokoa maisha yao. Kifo cha mgonjwa yule kingeweza kuzuilika au hata kucheleweshwa kwa mfano kama hospitali ya mkoa ingewezeshwa kutoa huduma ya dialysis kiasi cha kuweza kumkimbiza mgonjwa hospitalini hapo haraka. Lakini pia ingewezekana kuwa katika wakati mzuri wa kutambua chanzo cha ugonjwa wake kama hospitali ile ingekuwa na vifaa vya uhakika vya vipimo na pengine kulipatia ufumbuzi bila hata kuhitaji kumpa referral. Ipo mifano mingi yenye kufanana na hiyo. Mgogoro unaondelea hivi sasa nchini kati ya madaktari kwa upande mmoja na serikali kwa upande mwingine ni jambo linalosikitisha kutokana na jinsi suala hili lilivyoshughulikiwa na watendaji wakuu wa wizara pamoja na kuwa madai ya madaktari hawa ni ya msingi sana. Moja ya madai ya madaktari ni kutaka uboreshaji wa hospitali na vituo vyetu vya afya kwa maana ya vitendea kazi na mazingira ya kufanyia kazi. Dai hili siyo tu lina nia njema ya kuwahakikishia madaktari wanafanya kazi katika mazingira bora yenye vitendea kazi vya uhakika bali pia linahusu afya njema kwa ajili ya wananchi wenyewe. Kwa maneno mengine madai ya madaktari yanahusu pia ustawi wa afya za wananchi wengine na siyo maslahi yao tu binafsi. Ni aibu sana kwa hospitali ya Taifa, kwa mfano, kukatikiwa umeme bila kuwa na chanzo kingine mbadala cha umeme huku ukitegemea watoa huduma hawa kuacha kunung’unika. Haiingii akilini hospitali ya Wilaya kukosa hata strips za kupimia sukari mwilini na kisha ukategemea wafanyakazi wawe na furaha na kazi yao. Haingii akilini wauguzi wafurahie kufanya kazi kwenye wodi ambayo wagonjwa wamelala watatu watatu kwenye kitanda kimoja. Ni aibu, ni aibu, ni aibu. Pamoja na nia njema ya madai hayo, bado inasikitisha kuona jinsi ambavyo serikali kupitia kwa Waziri Mkuu walivyoona kuwa hakuna njia ya kuweza kushughulika na madai hayo zaidi ya KUAMURU madaktari kurudi kazini kana kwamba AMRI inaweza kuboresha mazingira ya kazi. Kumlazimisha tabibu pamoja na watoa huduma wengine wa afya kurudi katika mazingira yale yale wanayoyapigia kelele siyo tu hakutatui tatizo bali kunaongeza ukubwa wa tatizo. Hakuna tabibu na muuguzi atakayefanya kazi kwa moyo mmoja huku akiwa na hasira na kinyongo kwanza kwa kuamrishwa bila kusikilizwa anachodai lakini pili kwa kulazimishwa kurudi katika mazingira yaleyale anayodai yarekebishwe. Hatari ninayoina ni kwa wagonjwa kuzidi kupoteza maisha na wengine kuishia kupata vilema kutokana na matibabu butu watakayopewa na wahudumu wasioridhika. Na haya yakitokea wahudumu wa afya kamwe wasilaumiwe! Amri, vitisho, ubabe wala kamata kamata ya madaktari siyo suluhisho la matatizo. Ni matumaini yangu, wale wenye mamlaka wataona uzito wa madai ya madaktari na kuyapatia ufumbuzi wa kweli badala ya kuyapatia majibu ya kisiasa yenye vitisho na nia ya kufunika kombe ili mwanaharamu apite. Kinyume na hapo ni kuahirisha matatizo na kuendelea kuhatarisha afya za wananchi wengi masikini na wengine kufa kama yule binti. Lakini pia ni matumaini yetu, wananchi watatambua nia njema ya madaktari ya kutaka kuboreshewa mazingira yao ya kazi ili wananchi nao waweze kupatiwa huduma bora zaidi na uhakika tofauti na sasa. Ipo haja ya kuomba hoja ya dharura Bungeni ili kulizungumzia suala la mgogoro wa Madaktari na Serikali kwani hili ni suala linalouhusu umma wa Tanzania nzima. Wasipofanya hivyo itakuwa ni usaliti kwani raia wanakufa kwa kukosa huduma za wataalamu, wataalamu ambao wamedharauliwa kusikilizwa na kupewa majibu ya kuridhisha juu ya madai yao, kutoka kwa viongozi wa nchi wenye dhamana. Nimesikitika sana kusoma mahali ati, Waziri Mkuu na baadhi ya viongozi hawakutaka kuwafuata Madaktari kwenye kumbi walimokuwa wamekutania za Don Bosco wala Star Light hotel kwa kuhofia usalama wa maeneo hayo. Ikiwa Serikali ina waajiriwa wa intelijensia, usalama na polisi wanashindwa kuchunguza raia wao kiasi cha Viongzi kutishika, mwananchi wa kawaida anapaswa kuwa mashakari kiasi gani? Huu si udhaifu wa waziwazi? Hao walinda usalama kazi yao ni kuchunguza mitandao jamii na meseji za simu zinazohusu watu na mahawara zao tu? Ikiwa viongozi walihofia kwenda kwenye kumbi kuonana na madaktari, ni kwa nini madaktari wasihofie kwenda kuwaona viongozi hao? Kwa nini iwe sawa kwao na si sawa kwa wengine? Dhana ya uongozi kuwa kauli itatoka kwa kiongozi tu na mwananchi shuruti yake ni kupokea maelekezo daima dumu ni ya nchi gani? Sitaraji iwe Tanzania inayohubiri kuwa viongozi wake ni wasikivu kwa wananchi. Raia ndiye anayepaswa kutoa kauli kwa kuwa yote yanayofanyiwa kazi yanamhusu yeye, kawapa tu dhamana viongozi kusimamia. Hii nchi ya kuongozwa kwa kutisha watu haipo. Si sasa. Ile kasumba ya kutisha watu kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu si wakati wake huu. Nayo imekwenda na aliyeileta, tusilazimishane. Huu ni upuuzi mkubwa kabisa kuwatisha watu kana kwamba ni wajinga na hawajui wanachokitaka. Hawa viongozi hawajajifunza yaliyotokea kwenye nchi nyingine? Uongozi wa mabavu huku mnajitapa mbele ya uso wa dunia kuwa ni nchi ya kidemokrasia ni upuuzi na ujinga wa hali ya juu. Kuwazuia watu kukutana katika kusanyiko la amani, ndani ya nyumba na si mtaani, ni kuua nguvu ya demokrasia ya uhuru wa kukusanyika na kuzungumza. Hawa Madaktari hawajaenda mtaani kuandamana, lakini kuwazuia kukutana ambako wamekuwa wakikufanya kwa amani hadi saa, ni dhahiri kuwa hatatakuwa na jinsi na hivyo wanalazimishwa kwenda mitaani. Nachelea kuamini kuwalazmisha kufanya hivi ni kwa lengo la kuonesha mabavu na ubabe. Ujinga ulioje! Kuwa Madaktari hawa baada ya kulazimishwa kutokukutana katika kumbi huru, basi watalazimika kwenda mtaani na huko ndiko nguvu ya mabavu itakapojidhihirisha kwa kuwapiga virungu, mabomu ya machozi na maji yanayowasha. Inasikitisha na kuhuzunisha kuwa ati hiyo ndiyo njia viongozi wanaojiita wenye upeo na demokrasia, wanaiona i sahihi, na ya kufuatwa. Madaktari si watu wajinga hadi wadai isiyo stahili kwa kazi zao. Ninaudhika sana kumwona daktari anataraji huruma ya mgonjwa ya kupewa chochote, “chakula cha daktari aka CCD” ili aifanye kazi yake bila kuwaza atakavyotimiza mahitaji ya nyumba yake. Ipo dhana nyingine, kwamba daktari wanapaswa kujiajiri. Hii ni dhana hafifu kwani maneno wanayosema watu wanaoshinikiza dhana hiyo hayaendani kabisa na 1. Kipato cha wananchi wanaopaswa ‘kukamuliwa’ malipo hayo. Ilivyo tu sasa wananchi hawawezi kujinunulia dawa au kulipia baadhi ya vipimo katika hospitali na zahanati za Serikali, wachilia mbali za binafsi. Watumiaji wakubwa wa huduma hizo ni matajiri na viongozi wa Kisiasa na Kiserikali, hao ni asilimia ngapi ya raia wote wa Tanzania? Raia wanaobaki watajipeleka wapi? Mtu unaposema waanzishe ‘private hospitals’ pia uangalie na jamii inayozungukwa. 2. Kipato cha daktari anayetakiwa kuanzisha hostpiali binafsi. Mshahara wa dakatri wa kati ya laki sita hadi nane, ni kiasi cha kuweza kutosha kudunduliza kuianzisha hospitali yenyewe? Ingekuwa ni cha kutosha, wangekuwa na haja gani ya kusumbuana na Serikali wakati huu? Unaposema wakakope, umenayafahamu masharti na ukiritimba uliopo katika kupata mikopo hiyo? Wapo waliofanikiwa kufanya hivyo, waulize ni kwa mbinu gani na "connections" gani walizozitumia. Isitoshe, mshahara gani huo utakuwa "guarantee" kumwezesha kupata mkopo Benki wa kutosha kujiunga na wengine kuanzisha hospitali binafsi? Matokeo yake si ndiyo kuwa na hostpiali zisizokidhi viwango? Kamati za Bunge si zimekutana nazo huko mitaani wakati wa ukaguzi na kuzifungia? Ninaudhika kweli ninapomwona daktari anahangaika kufanya kazi hospitali tatu (wenyewe huita viosk) ili aimudu familia. Si sahihi kumtwisha daktari, mwalimu, askari na kada nyingine mzigo wa kuombaomba na kutegemea huruma za wananchi ili kuendesha maisha. Si sahihi kumsababisha mwajiriwa yeyote aishi kwa kutegemea rushwa kutokana na mshahara usiokidhi mahitaji ya msingi. Ni dhambi na kufuru kumnyanyasa daktari, muuguzi, mwalimu n.k, kuwa kazi zao ni za wito kwa hivyo wanastahili kuwa na uvumilivu kana kwamba walijaaliwa roho ya ziada kuliko binadamu wengine, kwani ukweli ni kuwa walijaaliwa roho ya ziada ya kujali watu na si roho ya ziada ya kuonewa na kukubali uonevu. Hii dhana ya "kazi za wito" ndiyo inayohubiriwa na viongozi kwa nia ya kuwaziba midomo na kuwakandamiza. Kwani, kazi halali isiyo ya wito ni ipi? Si sahihi kulinganisha kada nyingine kusema mbona walimu, viongozi wa dini n.k. hawadai madai ya ziadana kuacha kumlinganisha na wafanyakazi wa sekta nyingine na viongozi wa Kiserikali/Siasa. Tukilinganisha kwa ‘kizio cha chini’ tukumbuke kulinganisha na kwa ‘kizio cha juu’ vile vile. Isitoshe, kwa kada na sekta nyingine kutokudai stahiki zao, hakumzuii daktari au muuguzi kudai yaliyo yake na yanayompasa. Kuwa mjinga na kuongozana kwenye kundi la wajinga ni kosa, ila mmoja katika kundi la wajinga anapoerevuka akajua anaonewa, anapodai haki yake, si mjinga huyo tena asilani. Na mjinga akierevuka, mwerevu yu mashakani. Madkatari msitetereke, vitisho havina budi kuja, hakuna popote ambapo imewahi kutokea 'smooth transition' hakuna, ni lazima kukubali kuingia hasara na gharama, pole ikiwa wewe ndiwe itakayekukuta, kumbuka hufanyi hivi kwa faida binafsi bali kwa ajili ya heshima yako ya sasa, kizazi kijacho na heshima ya “the noble profession”. | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed