Ni jambo la kusikitisha kuwa katika jamii yetu tunao wazazi na walezi ambao ama wanafanana na kibonzo hiki au wanakaribia kufanana nao, kwa maana kwamba, huikwepa familia yao, watoto wao wenyewe, kwa kuona kadhia, kero, bughudha na usumbufu mwingi. Wengine hata ikiwa hawatamki bayana kusumbuliwa, matendo yao yanatosha kujisemea. Wakikutana katika vijiwe vyao vya starehe kama klabu za pombe, kahawa, bao na gumzo, hadithi za "usumbufu" wa watoto na familia zao ni mojawapo ya ajenda. Ajabu, ni usumbufu wa kuonja tu, hawaujui kwa kina kwa kuwa wanaukimbia na kuwaachia wenza au yaya. Suala la kujiuliza ni, je, familia bora itajengwaje ikiwa unaikwepa? Kwa bahati mbaya, jamii nayo imebadilika, kwani mtoto siku hizi siyo kama "enzi za Mwalimu" kuwa mtoto ni wa kijiji, sasa ni nyakati ya changu ni changu na chako ni chako, usimrudi mwanangu hata ikiwa amekosea. Wazazi mlio na tabia ya kuzikimbia familia zenu jioni na wakati wa wikiendi, kisha mkirudi mnakuwa wageni kwa wanenu au 'wakali kama mbwa mwitu' timizeni ahadi na maamuzi yenu ya kutaka kuwa na familia mlipoamua kuwa na wenza. Usiwe mzazi ambaye akiingia ndani watoto wanatafuta mlango wa kutokea. Usitarajie kwa miujiza kuwa na familia bora, kwani familia bora hujengwa kwa juhudi, maarifa na ushirikiano. Usiache kuwasikiliza watoto kwani nao wanajifunza na wanapenda kusikilizwa na wazazi wao. Nilipokuwa mtoto mdogo nilikuwa ninaamini zaidi maneno ya wazazi, hata kama waliongopa, kuliko nilivyowamini majirani au ndugu baki. Watoto wanaoishi maisha ya kubahatisha na kushindwa kuzilea vyema familia zao wawapo wakubwa mara nyingi hutokana na wasiopata malezi ya wazazi wao wangali wadogo "samaki mkunje angali mbichi". Vunja mnyororo wa familia mbovu kwenye kizazi na ukoo wako utakaofuata, kwa kufanya marekebisho kwenye familia yako. Usipende kutunukiwa sifa usiyoifanyia kazi kwa hamu na gamu. Malezi ya familia ni ya wazazi, siyo mzazi. 1 Comment Mgomo wa Madaktari na Siasa za Tanzania! 26/01/2012
Tatizo la sasa katika sekta ya afya, haliwezi kupatiwa ufumbuzi wa kuduma hata kama watawekwa pale Wizarani, the best Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu kutoka nchi za jumuiya ya madola. Hii ni kwa sababu we always fail to make the right diagnosis, na badala yake kuachia suala hili lijiendesha katika mazingira ya ‘siasa huru’. Nia yangu ni kutoa maoni yangu kuhusu kiini cha tatizo hili, lakini kubwa zaidi, tusaidiane jinsi gani ya kulikabili sasa na kwa siku za usoni. Katika Tanzania, Sekta ya afya inajenga na a 3 Tier System: 1. Basic Clinics, Dispensaries = First Level 2. District Hospitals = Second Level 3. Referral Hospitals and Specialty = Third Level. (e.g. of Referral Hospitals = Muhimbili, KCMC, Bugando, Mbeya) and Speciality (e.g. Specialities = Taasisi ya Moyo, Kansa etc). Moja ya matatizo yaliyopo under this arrangement Pamoja na kwamba 75% ya mahitaji ya wananchi ya afya (health needs) yapo katika first level (i.e. basic clinics and dispensaries), huku asilimia 25% tu ya health needs zikiwa katika higherlevel i.e. referral hospitals and specialty, katika kupanga bajeti za wizara ya afya na ustawi wa jamii kila mwaka, serikali huwa haitengi fedha kwa kufuatana na mahitaji haya. Badala yake, asilimia 75% of Resources (madawa, vifaa, mishahara, posho, education and training etc) huwa zinapelekewa kwenye level ya juu (referral hospitals na Specialties). Jambo hili ni la kushangza kidogo kwa sababu kuu ifuatayo: Katika kila siku ya mwenyezi mungu, outpatient diseases in Tanzania (magonjwa yasiyohitaji mgonjwa kulazwa zaidi ya kuonana tu na daktari kisha kurudi nyumbani), ni yafuatayo: Malaria; Acute Respiratory Infection ; Numonia ; Kuhara; Eye infection; Skin Infection; Anaemia; na UTI = 2%. Magonjwa ya kulala hayapo mengi kama yake ya kutohitaji kulala na haya ni pamoja na complicated malaria (ambayo huwa sio nyingi sana). Complicated malaria accounts for about 70% ya magonjwa yote yanayohitaji mgonjwa kulala. Mengine katika the remaining 30% ni TB, Ukimwi, na kuhara. Hoja ya msingi hapa ni kwamba asilimia 90% ya magonjwa yote Tanzania yanaweza kupatiwa tiba katika vituo vya afya (dispensaries and clinics), iwapo vitapatiwa tu wataalam wa kawaida, vifaa basic tu vya diagnosis, na madawa. Lakini kutokana na serikali kutojali eneo hili in terms of budget and resources allocation, matokeo yake ni wataalam wengi kurundikana kwenye higher levels of the 3 tier health system, na kupelekea uwepo wa hali ya – too much manpower chasing too few resources. Kwanini Serikali inaendekeza jambo hili? Sijui, lakini ningekuwa Waziri wa Afya ningeweza kutetea kwa hoja zifuatazo:
1. Suala la kwanza – pamoja na resources nyingi kwenda to higher level, kwanini magonjwa yote makubwa uhitaji serikai kupeleka wagonjwa India na kwingineko. Fedha zinazotengwa kila mwaka hazitoshi kuzuia hili? 2. Suala la pili ni juu ya mahitaji ya fedha nyingi kwa serikali to train wataalaum wanaohitajika mikoani/wilayani/vijijini. Pamoja na fedha za walipa kodi kutengwa kwa wingi sana kila mwaka kwa ajili ya zoezi hili, kwanini Tanzania bado inabakia kuwa moja ya nchi yenye the highest ratio ya population per doctor. Requirement ya World Health Organization (WHO) ni kwamba, kila daktari anatakiwa ahudumie watu wasiozidi 10,000 (elf kumi). Lakini sasahivi, hali ipo vipi Tanzania? Kwa hali ya Sasa, kwa wastani (national in Tanzania) ni karibia watu 64,000 per doctor. Na kuna mikoa ambayo hali ni mbaya sana, kwa mfano: · Mkoa wa Mara = 167, 000 people per doctor. · Kigoma kwa Mheshimiwa Zitto na Kafulila, 308, 000 people Per Doctor. · Mwanza = 144, 000 per doctor · Rukwa kwa Mh. Pinda = 121, 000 people Per doctor · Tabora kwa Mh. Sitta = 121, 000 people per doctor. Inakuwaje hakuna uwiano wa wingi wa fedha zinazotengwa kila mwaka kwa ajili ya zoezi hili, hazina uwiano na takwimu hizi za afya kitaifa? Ni mikoa michache sana yenye ahueni katika hili, nayo ni: · Arusha = 22,000 people per doctor · Pwani = 32, 000 people per doctor · Morogoro = 56,000 people per doctor · Dar-es-salaam = 24,000 people per doctor · Ruvuma = 57,000 people per doctor. 3. Suala la tatu: Katika Tanzania ya leo, karibia 50% (nusu) ya hospitali zote ni za NGOs, huku nusu iliyobakia ni mchanganyiko wa serikali na sekta binafsi. Na hali hii imekuwa hivi miaka nenda miaka rudi. Kwanini hali hii haibadiliki kulingana na fedha nyingi za walipa kodi kutengwa kwa ajili ya bajeti ya wizara ya afya miaka nenda miaka rudi? 4. Suala la nne: Katika Tanzania ya leo, karibia 25% ya clinics na dispensaries ni za NGOs, huku zilizobakia zikiwa ni za serikali. Nyingi ya hizi zipo vijijini. Lakini kama tulivyokwisha ona, ni asilimia 25% tu ya bajeti ya serikali ndio uelekezwa kwenye mahitaji ya vijijini ambako asilimia 70% ya watanzania ndio wanaishi. Ndio maana, kwa ujumla, Clinics na Dispensaries zote Tanzania zilizo chini ya serikali hazina wataalam wa kutosha, vifaa, wala madawa. Matokeo yake ni kwamba, asilimia 70% ya Watanzania wanategemea huduma za afya zinazotolewa na NGOs, Waganga wa Kienyeji, huku wengine wengi wakiamua kupotezea tu magonjwa mengi na kumwachia mungu awaongoze. 5. Na suala la mwisho: Madaktari wengi wanaosomeshwa na fedha za walipa kodi hutumia muda mwingi sana kutoa huduma za afya katika hospitali binafsi, kuliko kule walipoajiriwa na serikali. Je, ni nini kinawasukuma kufanya hivi? Ni mishahara midogo au kuna sababu nyingine? Makala imeandikwa na Mchambuzi (JF Member) via FikraPevu.com Mtoto mdogo wa kike anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka tisa,amelazwa wadi namba saba katika Hosiptal ya Mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi akiuguza majeraha aliyoyapata yanayodaiwa kutokana na kipigo ambacho amekuwa akikipata kutoka kwa shangazi yake ambaye ni Mwalimu wa shule ya Msingi Narumu iliyopo wilaya ya Hai. mtoto huyo ambaye kwa sasa ameathirika kisaikolojia kutokana na tukio hilo,inadaiwa na wasamalia wema kuwa,mwanamke huyo amekuwa akimpa vipigo mara kwa mara kwa kutumia waya. Taarifa ya jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro iliyotolewa kwa vyombo bya habari imedhibitisha ukatili dhidi ya mtoto huyo na kwamba mtuhumiwa aliyetajwa kwa jina la Anna John(28)mkazi wa mtaa wa Kiusa katika Manispaa ya Moshi, bado anashikiliwa kwa mahojiano zaidi. Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni matokeo ya wanawake wanaojihusisha na uuzaji wa mboga mboga na matunda wa mtaa wa Kiusa mjini Moshi kuamua kufuatilia nyerndo za mtoto huyo baada ya kutumwa sokoni na mtuhumiwa na kisha kurejea tena sokoni akiwa analia na kuwapa hofu kina mama waliokuwa sokoni na kuhoji kulikoni. Kamanda wapolsisi mka wa Kilimanjaro Absalom Mwakyoma katika taarifa yake kwa vyombo vya habari juzi amedai kwua,baada ya kina mama hao kuhoji kulikoni mtoto huyo alidai shangazi yake asiyek uwa na chembe ya utu hata kidogo alimpiga kwa madai kuwa vitu alivymtuma sokoni si vile alivyonunua. Kwamba mtoto huyo alipewa sh,2,000 ili akanunue ndizi mbichi,nyanya na nyama robo lakini mtoto huyo alinunua ndizi mbivu pamoja na nyanya na kupeleka nyumbani akiamini kwamba ametimiza kile alichotumwa. Wasamalia wema ambao ni kina mama wauzaji wa mbogamboga pale Kiusa moshi wlailazimiak kumwongeza mtoto yule pesa ili anunue nyama robo pamoja na ndizi mbichi na kumpa ili apelike nyumbani kuepuka vipigo tena. Mtoto huyo alirejea sokoni kwa mara ya pili akilia tena hali ambayo lishtua kina mama hao na kuamua kuhoji kulikoni?,hapo wakaanza kumchunguza mwilini na kubaini unyama uliofanywa na shangazi yake na hapo wakaamua kwenda polisi wakiwa na mtoto huyo na hapo polisi wakaingia kazini na kumtia mbaroni mtuhumiwa. baada ya kuchunguzwa zaidi mtoto huyo amebainikak uwa ma makovy ya zamani na makovu mapya tumboni,ubavuni pamoja na mgogoni na baadhi ya makovu mapya hadi jana yalikuwa yakitoa damu kuonyesha ni jinsi gani alivyoteswa. Mtalamu mmoja wa masuala ya kitabibu katika Hospital ya mawenzi (jina limehifadhiwa) amesema mtoto huyo kisaikolojia ameumia, atakuwa mwoga na hata shule hawezi kufanya vizuri kwa maana nyingine ni kwamba anakabiliwa na msongo wa mawazo ambao unaumiza kuliko hata ungonjwa wenyewe. Katika Hospital ya Mawenzi alikolazwa mtoto huyo,umati mkubwa wa watu uijaza hapo ukiongozwa na mbuge wa Viti maalumu (CHADEMA), Lucy Owenya na waliokuwapo hapo wamelaani unyama huo na kutaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya mtuhumiwa. Hata hivyo wengi wamehoji kama unyama huo unatendwa na mtu aliyeenda shule mwenye taaluma ya mwalimu ambaye siku zote jamii inaamini mwalimu ni mlezi wa watoto,huko kwingine hali ikoje? Kama mwalimu anamtenda hivi mtoto ambaye ni damu yake kwa maana ya mtoto wa kaka yake,itakuwaje kwa watoto wa wengine hasa anaowafundisha darasani ? (picha na habari "credit" Charles Ndagulla via Kalulunga blog) ![]() Dkt. Lucy Nkya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Lucy Nkya ametoa maelezo kuhusiana na suala la madaktari walio katika mazoezi ya uboreshaji wa taaluma kwa vitendo (Internship) katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa kusema kitendo cha wataalamu wa Muhimbili kutoendelea na mazoezi kwa vitendo kilisababisha uongozi wa hospitali hiyo kuwaandikia barua ya kuwarudisha wizarani ambako ndiko ombi la kuitaka hospitali hiyo iwape utaalamu madaktari hao lilitolewa. Akasema kuwa hadi sasa, tayari Wizara imeshawalipa Madaktari wote husika, stahiki ya kiasi cha fedha walichokuwa wanadai. Kwa mantiki hiyo, Serikali imepuuza madai yote mawili ya yaliyotolewa na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), kutaka kurejeshwa kwa madaktari wote waliokuwa wakifanya mazoezi ya vitendo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na kupitiwa upya uamuzi wa kuhamisha madaktari bingwa 61, kutoka hospitali hiyo ya taifa. Madaktari 194 waliokuwa wakifanya kazi Muhimbili waliondolewa na kupelekwa katika vituo mbalimbali baada ya kuibuka mgomo huku madaktari hao bingwa nao wakipelekwa kwenye vituo mbalimbali. Naibu Waziri pia alitetea uamuzi wa kuwahamisha na kuwapangia vituo vipya vya kazi. Katika tamko hilo, Dk Nkya alisema tathmini iliyofanywa na wizara ilibaini kuwa idadi ya madaktari waliokuwa katika mafunzo kwenye hospitali ya Muhimbili ni kubwa kuliko uwezo wake akisema wingi wao ungeathiri mafunzo ya taaluma yao. Alisema madaktari hao hawakufukuzwa kazi, bali walirejeshwa wizarani ili kupangiwa vituo vingine vya kazi kumalizia muda wao wa mazoezi kwa vitendo, baada ya kuvunja mkataba na uongozi wa hospitali hiyo. “Kitendo cha madaktari hao kugoma licha ya Serikali kuwaeleza bayana kuwa ilikuwa inaendelea na hatua ya kushughulikia madai yao, si cha kiungwana na kilikiuka mkataba walioingia na uongozi wa hospitali unaokataza kugoma,” alisema na kuongeza kwamba kitendo hicho pia kilikiuka kiapo chao kinachowataka kutetea uhai wa watu muda wote. “Kwa kuzingatia hatua zilichokuliwa na wizara na jinsi wahusika walivyotekeleza maagizo ya Serikali, hadi sasa ni dhahiri kuwa tamko la MAT kuhusu kunyanyaswa kwa madaktari walioko mazoezini halina msingi wowote,” alisema. Baada ya mgomo Nkya alisema baada ya madaktari hao kugoma, wizara ilichukua hatua za haraka za kuziba pengo kwa kuwaingiza madaktari 51 kwenda kufanya mazoezi ya vitendo Muhimbili huku akisema hadi kufikia juzi, Jumatatu madaktari hao 194 waliogoma walikuwa wamepokea barua za kuripoti katika vituo hivyo vipya vya kazi. Alisema madaktari hao walipangwa katika vituo vingine na waliorejeshwa Muhimbili ni 86 huku wengine wakihamishiwa katika vituo vya Temeke, Amana, Mwananyamala, Mgulani na Aga Khan. MAT kiliitaka Serikali kuwarejesha wataalamu hao Muhimbili ili wamalize mafunzo yao na kwamba kitendo cha Serikali kuwahamisha madaktari bingwa 61 mwaka jana hakikufuata taratibu hali inayosababisha wengi kushindwa kuendelea na kazi. Hadi taarifa hii inachapishwa hapa wavuti.com leo Januari 18, 2012, saa tano adhuhuru Chama cha Madaktari Tanzania, MAT, kinaendele na mkutano na wanachama wake ili kuamua hatua za kuchukua. Uchunguzi wa kuaminika uliofanyika katika maduka mengi Dar, Moro na miji kadhaa mingine umegundua kuwa wauza nyama wamekuwa wakifanya mchezo hatari wa kupulizia nyama sumu za kuua wadudu ili kuzuia inzi. Sumu zinazotumika sana sana ambazo watu wengi hutumia kuua mbu ni rungu, Hatari, expel, Baygon, Hit, doom na nyinginezo. Katika maduka mengi siku hizi ukienda utaona nyama imetundikwa sehemu ya wazi lakini hakuna inzi. Wafanyabiashara wa nyama wameona kuwa hiyo ndiyo mbinu ya kuvutia wateja ambao wengi hawapendi kununua nyama ambayo imekaliwa na inzi. Uchunguzi huo ulifanyika kwa kuwauliza wauza nyama ambao baadhi walikiri kufanya hivyo ili kuvutia biashara. Uchunguzi pia umebaini kuwa pamoja na kufanya zoezi hilo kwa usiri mkubwa, baadhi ya wanunuzi wamekuwa makini kwa kuinusa nyama wanayonunua, kwani kwa kufanya hivyo harufu ya 'sumu' huwa dhahiri. Napenda kuwatahadharisha tunapoenda kununua nyama tuwe makini, maana madawa haya japokuwa yanasemwa kuwa hayana madhara makubwa kwa binadamu, lakini mojawapo ya ingredient yake (piperonyl butoxide) iliyomo kwenye hizi sumu, inafahamika kuwa ina madhara makubwa kwenye kukua na kukomaa kwa ubongo hasa kwa watoto. (via JamiiForums) "Tears cannot explain it. This kid will be walking a total of 22miles with a heavy load on her head. 4 gallons of water, and that's all she can offer her family in exchange for missing her classes. God Save us, please recommend the page to your friends." - The John Mashaka Foundation. "I am trying to build a water pumping station. It will cost roughly $475,000. That's expensive but will be worth it. Still putting together the necessary resources. If you go to the website www.mashakafoundation.org you will see the picture of the tower." - The John Mashaka Foundation Kikongwe aitwaye Asagwile Kihaka (78) mkazi wa Kata ya Ghana jijini Mbeya, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kubaka mwanafunzi wa darasa la saba (12) (jina lina limehifadhiwa), katika shule ya msingi Mbata jijini hapa. Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Desemba 14, mwaka uliopita nyumbani kwake baada ya kumrubuni mtoto huyo kwa kumtuma aende kununua kuni za shilingi 1,000 na kuagiza ampelekee nyumbani kwake, ndipo alipochukua jukumu la kumbaka mtoto huyo hadi kuzirai. Binti huyo ambaye mpaka sasa hajaweza kusema kwa kinywa hadi jumapili ya Januari 8, mwaka huu ambapo alifanyiwa maombi katika kanisa la PHM lililopo jijini hapa, ambapo aliweza kuzungumzia tatizo hilo kwa maandishi na kudai kuwa mzee Kihaka ndiye aliyemtendea unyama huo. Uchunguzi uliofanywa na Hospitali ya wazazi Meta umebaini kuwa binti huyo mara kadhaa amefikishwa hospitalini na kupatiwa matibabu ya homa, lakini hakuzungumza kilicho msibu hadi pale aliupokuja kuandika kuwa kabakwa na mzee huyo na kugundulika sehemu za siri zikiwa na michubuko na vidonda hali ambayo ilithibitishwa kuwa kaingiliwa na mwanaume. Hata hivyo wananchi waliitisha mkutano wa hadhara kutokana na kuchoshwa na vitendo vya Mzee Kihaka ambapo imetajwa kuwa ni tukio la tatu la mzee huyo kutenda na viongozi wa Kata ya Ghana kumfumbia macho. Mzee Kihaka alikamatwa Januari 2, mwaka huu na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Kati cha Mkoa, ambapo Mtendaji wa Kata hiyo aliwasilisha barua ya kumwekea dhamana hali iliyopingwa na wakazi na kuamua kuitisha mkutano wa hadhara Januari 13 kwa hofu alikamatwa na kurudishwa mahabusu siku moja kabla ya mkutano huo wa hadhara Januari 12. Siku ya mkutano wa hadhara Diwani wa Kata hiyo Bwana Anjelo Chavaligino hakuhudhuria mkutano huo hali iliyopelekea kuleta hasira kwa wananchi hao na kisha kumtafuta hadi kumpata na kumleta kwenye mkutano huku akizomewa na wananchi wengine walienda kupiga mawe vioo vya nyumba ya Mzee Kihaka. Mtandao huu umeshuhudia familia ya mzee huyo ikiangua kilio baada ya kunusurika na mawe hayo. Jeshi la polisi mkoani Mbeya lilifika eneo la tukio na kuzuia ghasia hizo na Diwani wa kata hiyo Bwana Chavaligino ameahidi kuitisha mkutano ili kujadili mstakabali wa Mzee Kihaka, huku kwa upande wao wananchi wamemtaka Mzee huyo na familia yake kuhama eneo hilo. --- via habari na picha via logu ya Mbeya Yetu Picha unazoziona hapo ni za wakazi wa Japan wanaotaka kuwa tofauti na wanadamu wengine kwa kujitafutia maumbo ya ajabu ajabu, almaaruf "bagelheads". Niliwahi kuhadithiwa na Mwitaliano mmoja kuwa nyakati fulani wanaume katika jamii yao walipenda kufanya operesheni ya kukuza taya za chini ili kufanya sura zao kuwa pana kidogo, umbo lililofananishwa na uzuri wa kuwavutia wanawake. Hivi majuzi katika ripoti ya uchunguzi iliyofanywa nchini Marekani, wanaume wengi zaidi ya ilivyorekodiwa miaka iliyotangulia, walikiri kuhudhuria kliniki mbalimbali kwa ajili ya kufanya "bro-tox" (kinyume cha botox) ili kuondoa mikunjo na "kasoro" walizohisi wanazo katika sura zao. Uchunguzi huo uligundua kuwa wanaume laki tatu walifanya brotox. Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 29 tu alipoulizwa sababu ya kufanya bro-tox, alisema inatokana na kukerwa na mikunjo inayotokea usoni anapocheka au kuzungumza. Jibu la kijana huyu lilinishangaza kwani ni jambo la kawaida kabisa kwa mwanadamu asiye na kasoro. Misuli huchora mikunjo mwilini kufuatia vichocheo vya hisia vinavyozaliwa kulingana na aina ya maongezi, shughuli au jambo fulani. Tunapozungumza na watu ana kwa ana, mikunjo hii husaidia kurahisisha maelewano kwa kuongeza maana kwenye maneno yanayotamkwa. Wakati mwingine mikunjo ya uso tu, kama vile kukonyeza, kutikisa nyusi, kupinda mdomo nk, bila hata ya kuzungumza neno moja, hutosha kabisa kutuma ujumbe kwa anayekutizama. Leo hii mikunjo hiyo ikiondoka, mathalani inavyotokea kwa wagonjwa waliopooza sehemu fulani za miili yao kutokana na kuzaliwa hivyo au kwa hali ya ugonjwa, huwa inahitaji usikivu wa ziada ili kuweza kumwelewa vilivyo mtu huyo. Mimi nadhani, ikiwa mikunjo mwilini haina madhara makubwa kwenye afya kuadhiri mahusiano na watu wengine katika maisha ya kila siku, basi ni sahihi kabisa kujikubali na kuacha asili iwe ilivyo, kwa mfano tujifunze kwa Seal. Penis Tattoo Blamed for Permanent Erection A 21-year-old Iranian man now suffers from a permanent erection after getting a tattoo on his penis, according to a report of his case. The man had the Persian phrase "borow be salaamat," meaning "good luck with your journeys," tattooed on his penis. He also had the letter M, the first letter of his girlfriend's first name, tattooed on it, according to the report. His condition is medically known as priapism, which is said to occur when an erection is not caused by sexual stimulation and lasts longer than four hours. The condition most commonly happens in boys ages 5 to 10, and men ages 20 to 50. The case report, published Jan. 3 in the Journal of Sexual Medicine, notes that this is the first case of tattooing causing the condition. Tattoo troubles A tattoo artist created the design with a handheld needle, according to the report. After the tattooing, the man bled from tissue deep within the penis, and experienced pain for eight days. His penis then became semi-erect, 24 hours per day. When he visited the doctors, his erection had been ongoing for almost three months. The doctors conducted numerous tests to rule out other possible causes, such as a urinary tract infection, leukemia or syphilis. They determined that the tattooing was probably to blame, and suggested the needle may have been inserted too deeply. The doctors determined that blood was still flowing in and out of the man's penis, so they diagnosed him with a nonischemic priapism. This occurs when blood enters the penis faster than it can go out, leaving the penis permanently erect, due to the increased pressure. An ischemic priapism, in which blood is no longer flowing, is a much more serious condition, and can cause severe damage if not treated. Treatments Doctors recommended that the man undergo a shunt procedure to drain excess blood. But the shunt did not work. According to the report, the man did not wish to undergo additional surgery because he can still have sexual intercourse and he is not in pain. He also does not regret the tattoo, the report said. The doctors do not recommend penile tattooing, according to the study. Pass it on: Penile tattooing left one man with permanent semi-erection. This story was provided by MyHealthNewsDaily, a sister site to LiveScience. Follow MyHealthNewsDaily on Twitter @MyHealth_MHND. Find us on Facebook. Pakua kipande kilichopachikwa hapo au bofya hapa kwenda RaiaMwema.co.tz kujisomea makala hiyo.
Jeshi la polisi Mkoani Ruvuma linamshikilia Frank Jota (26) mkazi wa kijiji cha Litisha Wilayani Songea kwa tuhuma za kumbaka mama yake mzazi mwenye umri miaka 54 ambaye jina lake limehifadhiwa wakati amelala nyumbani kwake majira ya saa za usiku. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea Januari Mosi mwaka huu huko katika kijiji cha Litisha kilichopo nje ya mji mdogo wa Peramiho. Amesema kuwa usiku wa siku hiyo, Jota alikwenda nyumbani kwao ambako alimkuta mama yake mzazi akiwa amelala na baadaye alianza kutafuta namna ya kuingia kwenye nyumba hiyo ambayo mlango wake ulifungwa na komeo kwa ndani. Jota baada ya kuona hivyo akaamua kuuvunja mlango wa nyumba hiyo kuingia ndani na kwenda moja kwa moja kwenye chumba alicholala mama yake mzazi (jina limehifadhiwa). Imeelezwa kuwa, baada ya kufika chumbani, Jota alianza kumtisha mama yake kwa kisu alichokuwa ameshika mkononi na baadaye alimkaba shingo na kufanikiwa kumvua ngo ya ndani aliyokuwa amevaa kisha kumbaka. Wakati Jota akiendelea kubaka, watu waliokuwa jirani na tukio walisikia kelele za mtu akipiga mayowe na walipofika kwenye eneo hilo la tukio waliingia ndani ya nyumba hiyo na kumkuta Jota akitoka kwenye chumba alicholala mama yake. Jota alipowaona watu alijalibu kukimbia lakini majirani hao walifanikiwa kumkamata na kumpeleka kituo kidogo cha polisi cha peramiho. Kamanda Kamuhanda ameeleza kuwa polisi walimhoji mtuhumiwa ambaye alikiri kulitenda kosa hilo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara tu upelelezi utakapokamilika. --- habari imeandikwa na mwandishi wa blogu ya Stephano Mango | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 | ||||||














RSS Feed