Kuna masuala ya kijamii, ni magumu kuliko maelezo. Ndio kwenye familia, ndoa, n.k.

Mmesikia hii ya kupunguza masharti ya dini?

Eti, Kanisa Katoliki (KK) limeruhusu ndoa mseto, yaani ndoa kati ya Mkatoliki na Muisilam. 

Zamani ilikuwa dhambi hata Mkatoliki kuoana na Mkristo mwenziye ila wa dhehebu tofauti. Sasa kimekuja kizazi chetu kisichotanguliza dini kwenye mambo yake hasa ya ndoa, jamaa wameona badala ya kupoteza waruhusu jamaa waone.

Je! Kweli ndoa kati ya dini tofauti ni dhambi?

Mimi nadhani bila shaka, ni hapana. Leo hii kwenda na wakati imeruhusiwa. Je, waweza kumuacha umpendaye kisa kiongozi wako wa dini hataki muoane? Huo utakuwa chizi fulani au pengine humpendi kweli.

Wakatoliki sasa mko huru kuoa Waislamu.

Hongera!

imeandikwa na, Kamala Lutatinisibwa
 
 
Ni kawaida maishani kwamba watu waliowahi kutusaidia na kufanya historia zetu kuwa zilivyo au nzuri zaidi huwa tunajihisi kutoa fadhila angalau kwa kudumisha urafiki / ukaribu nao kwa njia za kutembeleana, kusamilimiana, kuwasiliana na hata kuheshimiana.

Lakini, hufika hatua watu waliowahi kukusaidia unalazimika hata kuwakwepa hata kutokungea nao. 

Kuna ambao wanataka kila mtu atambue kuwa aliwahi kukusaidia.

Kuna waliokusaidia ukapiga hatua mbele lakini unaona kama hawataki usonge mbele. 

Maswali huzuka juu ya msaada waliowahi kukupatia wewe, walilazimika? walitafuta jina? au walikwepa aibu ya jamii? 

Mbona wanakuwa hivi?

Basi wakati mwingine wajikuta ulazimika kuwa mbali na hata ikibidi kuwakwepa kabisa.
---

Kamala L Lutatinisibwa "Kijiweni Nyegerage"
KamalaLuta blog
 
 
Ni kweli nimezaliwa katika familia ya kikristo iliyonifanya kuwa mmoja wa wanaosheherekea siku kuu iamanikayo kuwa ni ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, kiongozi mkuu wa ukristo na labda chimbuko halisi la ukristo duniani na hivyo kujikuta nikiwa mmoja wa wapendao sana kusheherekea siku kuu ya Noel, Christmas au X-Mass kwa kikwetu tuliita "Nwelyi" badala ya Noel.

Katika kukua kwangu nilipenda sana na kutamani siku hii inafika. Lakini kila ilipofika na kupita, sikukuimbilia tu luisubilia Nwelyi Nyingine kwa hamu, bali nilichukua muda na kipindi kirefu kutafakari si kuu hiyo. Kwa kweli nilibakia na maswali bila majibu juu ya siku kuu hii, kama vile; mbona hamna tofauti na siku nyingine? Mbona ni yakawaida tu? Mbona hamana jipya? Mboona ni wakati wa viumbe wengine kuteswa na kuuwa ili wawe kitoweo waliwe na binadamu wakati wote wameumbwa na Muumbaji mmoja? Mh!

Nikaja kugundua ya kuwa kumbe "Nwelyi" ni siku kama siku nyingine tu na kumbe siku zote zinalingana na kila siku ni kubwa au ni siku kuu tu kama siku nyingine kwani siku uliyokwisha iona na uliyonayo ndiyo kuu kuliko ijayo na ile iliyopita. Kumbe "Nwelyi" ni siku ya kuomboleza wale wanyama wafao ili binadamu afurahia na kkumtukuza Mungu wake.

Kumbe hata maandiko ya biblia ambayo wakristo wengi hadai kuyafuata, hamnaga habari za kusheherekea siku kuu ya kuzaliwa kwa Yesu bali angalau imetajwa ile ya kufa (fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu). Kumbe hata siku aliyozaliwa yesu ina utata kuliko uhalisia kama kweli ni 25 Disemba n.k., n.k.

Ndiyo maana basi niaachana na biashara ya kusheherekea sikukuu kwani nasheherekea kila siku kwa kuwa kila siku ni kubwa tu hamna inayozidi nyingine ukuu na labda zile ziitwazo sikukuu ni wakati mwafaka wa kuomboleza vifo vya wanyama kwa ajili ya sherehe ya binadamu.

Kamala J Lutatinisibwa
 
 
Kuna wanaodai juu ya tofauti kati ya dini na Mungu, Mungu na vitabu vyake na tofauti kati ya vitabu vya dini (vitakatifu?) na dini yenyewe.

Katika Ukristo, watu wameamua kutumia Biblia na kumuabudu Mungu wa kwenye Biblia. Mungu huyu ni Baba na sifa zake zinaendana kwa kiasi kikubwa na baba zetu wa duniani. Anachukia haraka, anaadhibu, anapiga viboko, anaharibu vibaya, hasira yake ni kali, lakini pia ana upendo.

Mabaya mengi yatokeayo kwa mtizamo wa Mungu wa Biblia, ni adhabu, ni onyo na fundisho. Katika ibada, huwa tunaambiwa zaidi juu ya shetani na ghadhabu ya Mungu na kwamba siku za Mwisho kuna adhabu kali itokanayo na hukumu ya Mungu na kuchomwa moto na kuteketea.

Mungu wa Kiisalamu, haitwi Mungu bali Allah. Huyu ni Mungu, hana jinsia kwa hiyo sio baba (kama wa Biblia) wala Mama kama yule wa dini za Asia na nyinginezo. Lakini ana masharti makali pia.

Kuna Mungu wa dini za Asia, baadhi ya dini hizi humrejea Mungu kama Mama. Mungu huyu ana maelekezo mengi ya kimama, yaani yenye upendo, kulea, kurekebisha, kuvumilia n.k., kwa ujumla kama vile mama amleavyo mtoto au ampendavyo mtoto. Masharti ya Mungu huyu yana nafuu.

Lakini sasa kuna changamoto juu ya Mungu aliyeandikwa vitabuni na kile tukiabuducho. Watu wameachana na Mungu aliyeandikwa vitabuni na kuanza kuabudu vitu vinginevyo. Kuna wanaoabudu Sanamu za Mungu asiye na sura, wengine huabudi mitume wake kama vile Yesu Kristo.

Kwa Wakristo wengi wanachukua muda mwingi kumsifia Yesu aliyekataa sifa yoyote akiwa duniani. Tafsri ya maneno ya misahafu zimeshindikana kwa akili ya binadamu na hiyvo waumini kuaminishwa kichangamoto zaidi ya uhalisia. Na waumini wengi wamekaa kimya kusubiri kutafsiriwa.

Dini nyingi zimegeuka kuwa asasi za kijamii kuliko kuwa pahala pa kukuzia watu kiroho kutokana na ukweli kwamba zinaongozwa na wasomi wa kidunia ambao pia hawajakua kiroho na hivyo kujikuta wakiwa mhanga wa wale wayahubiriayo wengine.

‘ego’ nayo imeteka dini, kila dini ni "superior" mbele ya nyingine, kila dhehebu pia ni "superior", hata ndani ya dhebu kuna ubaguzi wa waliozaliwa mara ya pili na ambao bado, "charismatic" na wasio "charismatic" n.k., n.k, na hii ni kwa kila dini.

Mahubiri ya siku hizi yamekaa kisiasa na kijasiriamali zaidi. Mafanikio ya nyumba za ibada na viongozi wake hayamo tena kwenye kukuza waumini kiroho bali makusanyo ya fedha. 

Ni kweli kuna tofauti juu ya Mungu na kile tukiabuducho siku hizi.

Na, Kamala J Lutatinisibwa
 
 
Nilipokuwa mdogo nilikuwa namaswali magumu juu ya dini yangu. 

Nimezaliwa katika familia ya Kilutheri iaminiyo imeokoka na hivyo kwenda kanisani ilikuwa kwa lazima tu usipofanya hivyo ni kiboko ni misonyo kibao, nikajiuliza juu ya ulazima mpaka kiboko juu ya Mungu asemakanaye ni wa UPENDO mwingi.
 
Ilitokea majambazi wakawa wenge vijijini, tukaamua kwenda Kanisani kumuomba Mungu atuepushe na majambazi, Jumapili iliyofuata tukaenda ibadani na kukuta Kanisa (a.k.a nyumba ya Mungu) tulimokaa kuomba tukiamini majambazi watatoka, limeibiwa vioo vyote vya madirisha, nikahoji juu ya uwezo wa Mungu huyu kutulinda sisi kama hawezi jilinda yeye na mali zake yaani kanisa! Nikapata kipigo.

Mchungaji wetu aliyekuwa akiombea watu wasiugue, akaugua na kushindwa kutibika pale karibu akakimbizwa KCMC Moshi. Nikahoji juu ya Yule aombeaye wagonjwa na wazima wasiugue, anaugua na kushindikana, sasa kutuombea kule si geresha? Nikapata kipigo kutoka kwa bibi kwa swali hilo.

Nikahoji juu ya kisemekanacho kuwa Yesu alinifia maelfu ya miaka kibao iliyopita, je uhalali ukowapi? Vipi kama sikutaka wala kutamani kufiwa na huyu Yesu a.k.a Mwana wa Mungu? Jibu langu lilikuwa ni kipigo na mifinyo kutoka kwa bibi yangu aliyekuwa mashuhuli katika hilo.

Dini huwa zina vibwagizo ambavyo lazima ujibu vile inavyotazamiwa, ukienda kinyume basi umekufuru.

Siku moji nikiwa katika mkutano wa dini,akasimama jamaa mmoja na kusema; bwana Yesu asifiweeeeeeeeeeee! Nikiwa najiandaa kujibu AMEEENN, jamaa mmoja pembeni akajibu kwa sauti badala ya kujibu Ameen akasema KWA LIPI!!! Nilishtuka, nikajawa na kicheko, then nikajiuliza kumbe sio lazima kujibu ulivyofunzwa bali vile utakavyo au vile inavyokidhi haja yako?

Sio kufuru bali ni kutaka kujua zaidi kwamba kwa lipi? 

Kwa nini kumsifu yesu na sio Mungu au mchungaji au jirani au mwalimu au mwingineyo?

Na Kamala J Lutatinisibwa
 
 
Kilimanjaro
picha: kiliair.com
Sikuupigia kura mlima Kilimanjaro na wala sikuwa na mpango wa kuupigia kura na nisingeweza kuupigia kura. 

Ni kweli ungekuwa maajabu ya dunia tungepata pesa nyingi. Lakini kwa nini kushiriki kuupigia kura mlima Kilimanjaro?

Tanzania hupata pesa nyingi kutokana na utalii, ufadhili na vyanzo vingine. Lakini pesa hizo huishia wapi?

Tunazidi kukamuliwa kodi na kumasikinishwa. Wakulima kama mimi tumekosa mitaji, huku Rais wetu akionekana kila siku anawakaribisa matajiri kutoka nje ili wajekuchukua vijishamba vyetu kuwekeza eti.

Mapato yoote hayo pamoja na utalii huishia wapi? Hhamna huduma za msingi za jamii, shule alizozijenga Nyerere ndo bado zipo zinakaribia kuwaangukia wanafunzi.

Pesa za kufisidi huwa hazikosi na mafisadi wako huru kuiba watakacho, anasa za watawala nazo hazikosagi pesa. Wananunua magari ya kifahari, Pinda eti anakataa gari la kitajiri kwa kuwa anaendesha gari la kitajiri hivyo gari alilolikataa linapelekwa kwenye idara nyingine...!

Kwa nini kuupigia kura mlima huu?

Kamala J Lutatinisibwa