Eti we mwoga wa mende kama huyu? 03/03/2010
Humu duniani watu tunatofautiana kiwango cha ujasiri. Lakini wapo watu wengine japo wawe jasiri kiasi gani, ikiwa wana ugonjwa wa kuogopa, baadhi ya vitu (phobia) ujasiri wake ni kazi bure katika nyakati fulani. ![]() bofya pichani utizame video hii fupi Ninakumbuka nilpokiuwa Sekondari dada mmoja alikuwa mwoga sana wa wadudu kama vile sisimizi, nyenyele, maji ya moto nk. Mwanzoni nilidhani ni utani kwa kuwa umbo lake lilikuwa kubwa kuliko wanafunzi wengi, na hivyo tulitarajia mtu mkubwa asiweze kuogopa kidudu kidogo hata siku moja. Tena, nilipokuwa chuoni, nilisoma na dada mwingine ambaye ni rafiki yangu pia, naye alikuwa mwoga wa wadudu hasa aliyekuwa akimtikisa maini alikuwa mdudu mende. Halafu hivi vidudu bwana hata sijui vinakuwa vimetumwa na nani kwani hisia zao huwa ni kali na mara moja huwapeleka kwa yule mtu mwoga. Hii nadhani ni kutokana na msisimko (stimulation) zinazosababisha kemikali fulani kuzalishwa mwilini na mtu huyu baada ya kumwona mdudu au kiumbe anayemwogopa. Siku moja hivi tupo koridoni, nje ya milango ya vyumba vyetu ambavyo vilikuwa vinatenganishwa na uwazi wa kuelekea bafuni, alikuwa akijipita mende katika harakati zake za pengine kutafuta chakula. Ghafla, rafiki yangu ambaye kwa wakati huo alikuwa amesimama kati ya mlango wa chumba chao na kile cha kwetu huku akiukabili mlango wa bafuni, ghafla alipiga ukelele wa nguvu mara moja. Ndipo tulipostuka na kumwuliza, 'nini?' huku akinyoosha mkono akawa anasema, 'yule, yule', siye kumtizama ni mende, mimi mawazo yangu nilidhani kamwona nyoka ama ng'e ama pengine sijui kidudu gani cha kutisha. Loh, kumbe alikuwa akimwogopa mende. Alitetemeka, akamkamata mmoja wetu bila ya kumwachia akisema, 'mwue, mwue' nasi kwa kuwa tuliona kichekesho, hatukumwua, ndipo yule mende ghafla aligeuza akashika njia kuelekea upande alikokuwa amesimama yule dada muda wote akimshikilia mwenzie. Kuona vile, yule rafiki yetu huyu akaanza kujisogeza nyuma zaidi kadiri mende alivyomkaribia. Mende alipomkaribia kabisa yule dada aliyekuwa ameng'ang'aniwa, ndipo rafiki yetu alipiga hatua moja kuelekea nguzo iliyokuwa imeshikilia dari, la haula, mende anaye. Mende kama katumwa, akamfuata katika ile nguzo, ndipo rafiki yetu akapiga tena ukelele wa nguvu, 'nakufaaa...' Utaniuliza, 'kwa nini hakukimbilia chumbani kwake?'. Ni hivi, alishindwa kuwahi kuufungua mlango wake; vile vile, alitaka kuhakikisha kuwa mende anauawa ili apate amani kuwa hatamfuata chumbani kwake usiku. Ilibidi mmoja wetu amwue (sikumbuki alikuwa nani kati yetu) ili kuepusha watu kujaa na kutaka kujua kulikoni mtu 'anakufa' vile vile kutaka kuondoa ile aibu yakuwa dada fulani ni mwoga wa mende. Muda wote huo tulikuwa tunashikilia mbavu kwa kicheko (adabu zetu ndogo wakati huo, tunacheka msiba). Ilikuwa ni 'full' kuelewa somo la saikolojia ilipofika siku ya kufundishwa kipengele cha 'phobia' kwa maana kila mmoja aliikumbuka ile songombingo ya mende koridoni. Ndipo tulipong'amua kuwa alaa, kumbe ni ugonjwa. Na hapo ndipo nilipomkumbuka dada yuleee, wa Sekondari. Ama kwa hakika, usilolifahamu ni kama usiku wa kiza. Bofya hapa umtizame mtangazaji mmoja wa hali ya hewa akiteswa na mende studioni. By Dr.Mallaba Tanzania changes will depends on the most creative and talented young people,rather than rely on politicians or who will be a president. As president has his part however he will never make a big difference if the given society were sleeping, I say the society is sleeping because even when they see some garbage instead of taking and put in a proper place they complain of government, we see somebody is destroying the road instead of taking an action and report to the specific department we complain of the government... government ? I believe a lot of things they are source of our laziness and wait to be done by government leaders.Let us play our part and the government will do its best. The most surprising is that those who complain on everything without even taking an action some are graduates, business workers who are in big cities, so what about those illiterate and villagers? what will they say? Let us stop complains and concentrate on solving those problems. I say Tanzania depends on young and most talented people because our development will neither depends on foreigner investors nor depends on foreigner donors. I do not mean that we don't need them, no, we need them in a strategic manner. Foreigner investors are key to any development economy but such nation shall never rely on, this is due to the fact that despite of their massive investment they can leave the country at any time and the good example we saw during the economic downturn(crisis) the way a lot of foreigner investors withdrew their money and flew back to their country,this tell us that the domestic investors are better than those even though always never get good treatment policy from the government. On my thinking if a talented and young Tanzanian will realise their roles many changes will be done. As they are the holder of everything in the society I am very confident and very enthusiastic that we are able to make a big different in Tanzania. For me as among of them I'll do whatever I can to make it done. I call upon all young Tanzanian wherever they are to rise up and realize that this is our time, we can no longer leave fisadis to continue to lead us while we can do it. I know may young creative and talented Tanzanians are already disappointed on many government policy and some just saying "we are observers". Remember If we can not rise and cooperate our selves nothing will be done, but if we join together will move forward and be like other emerging countries such as China, India and Brazil. If consider China for example, about 80 percent of its Scientist they have been abroad(returnees)and are the one driving the development and success of China in almost each aspect like High -tech,engineer, computer,high way,medical sciences etc. Remember our heroes such as Nkwame Nkrumah, JK Nyerere, Martin LK, Nelson Mandela etc who struggled and sacrificed their life to African people while dreaming to have the so called United States of Africa, however their dreams didn’t yield (succumb) more fruits as they expected maybe due to social, politics, economics and cultural differences between those leaders. I do remember JK Nyerere spoke after declaring an Independence in 1961 he said Tanzanian have 3 enemies which are poverty, illiteracy and diseases. It's about 50 yrs now since that time Africa is still facing the same problem and even worsen than before, where are we going? are we backsliding or have we slept? Its very shame seeing very little progress in terms of economy in African countries in-spite of having plenty of minerals and other resources. This is the 5th year in china I’ve learned a lot, how Chinese are serious and very patriotic that they are ready even to refuse to buy anything made abroad.Their hardship and patriotism have taught me that “impossible is just something you can not do” “and nothing is what you can not think”. We have to keep in mind that it's not just about the numbers of people who died; it's also the manner which many of these victims met their deaths. For some reason, I seem to be bothered whenever I see acts of injustice and assaults on people's civil liberties. I imagine what I write in the future will follow in that vein. Whether it's fiction or non-fiction I believe that a better Tanzania is yet to come but very near than we started. God bless Tanzania. Dr. Mallaba (drmallaba@yahoo.com) ![]() Hivi kwanini sisi wabongo tunapenda sana kufanyiana roho mbaya, ntimanyongo, ubangaizaji na short cuts? Wengi wetu hatupo honest... ukimpelekea fundi kitu atakulipulia ili mradi urudi tena... mwingine anaweza kukubadilishia kifaa akakupachikia kibovu akaondoa chako kizima... Ukienda kununua kitu unauziwa kwa kuangaliwa sura kwanza mimi nitaambiwa buku mbili, Supika kwa sababu kakaakaa kama Mzulu atapigwa kilo nzima... kitu kimoja bei tofauti kulingana na mtu... Ukijenga Uswahilini na nyumba yako ndo pekee ikawa na bomba la maji basi uwe mvumilivu kwa majirani... wengine wanaweza kukuamsha saa sita eti anataka kuchota maji... Ukipanga uswahili ukawa na ka-home thieta kako weka grill manake vibaka lazima waje kukutembelea... Una saa nzuri mkononi huna amani ukikatiza Magomeni mateja wanaweza kukufanyia kitu mbaya... Kwa walio ughaibuni unatuma pesa nyumbani ujengewe sahau hakuna cha tofali wala vumbi la kokoto litakalonunuliwa... Ukiharibikiwa na gari unaomba msaada wa kusukumwa kidogo lazima uwe na senti senti za kutoa... Ukipotea njia ili uelekezwe unaulizwa una hela? Nina barua ndogo ninahitaji bosi anisainie tu, utazungushwa wee na Sekretari wake mpaka utakata tamaa, kisa anajua ikisainiwa utapata mshiko, ukitaka umuone kwa chai kidogo... Unadai pesa za malimbikizo bosi anakuzungusha tu makusudi ili usiipate pesa yako au ukate tamaa kufuatilia wakati pesa haitoki mfukoni mwake. Hizi roho mbaya sijui zinatoka wapi? Kwa nini tupo hivi sisi? Mpaka tutwangane bakora? Yaani watu hawawezi kuwa honest japo kidogo? Yaani tabu tabu tabu... ah bubu husema... Monsignor, China Nukuu ya leo toka kwa Mtanzania 02/24/2010
![]() We are the victims of our own selves! We have never been exposed to situations which seriously need a change of mindset throughout our growing up period! Sure it won't be easy to change when all but our own pride seems to fall apart as we continue to age and be caught up with life. Throughout our lives we have lived inside a cage, a cage which had rules, rules of which if followed gave us results we desired TO PASS! Now we are thrown out in the world unfair and unequal ground. Sure it is a difficult battle and we evidently seems to be loosing the battle so we go back and find a place and space where we can impose boundary and establish a platform that we can simply win! Only to realize it's ourselves we are hurting! To me it is simply an act of cowardliness... if you really want to be superior go out there in the world and do that! Then and only then you will become my role model! Dr. Isaac Maro, Tanzania Shaffi Ramadhan Kondo ameishi gerezani kwa miaka kumi. Hapa anamwelezea mwandishi wa BBC, Josephat Mwanzi, hali halisi ya magereza ya Tanzania. Bofya kifute cha play upate kusikiliza mahojiano hayo mafupi. Tutatuma wagonjwa nje ya nchi hadi lini? 02/15/2010
TIME LIMIT FOR SENDING PATIENTS ABROAD FOR TREATMENT (TUTATUMA WAGONJWA NJE YA NCHI HADI LINI) By Raphael Mallaba Jr Ni miaka mingi sana wakati nikiwa kijana mdogo nilikuwa nikisikia tu kuwa wagonjwa fulani wenye magonjwa mbalimbali wanapelekwa nje ya nchi kwa ajiri ya matibabu, aidha katika kipindi hicho katika mawazo yangu mafinyu nilijua kuwa Tanzania haina madaktari wakutibu magonjwa hayo au hakuna vipimo husika. Kweli sana tuko karne ya 21 na taifa letu likiwa linasherehekea uhuru wake wa karibu miaka 50 lakini kila mwaka ninaendelea kusukia kuwa wagonjwa wanapelekwa nje ya nchi kutibiwa kama India na nchi zingine. Maswali yangu ni mengi sana ila siwezi kuyaandika yote katika hii makala moja ila yananipa wasiwasi sana wa hii nchi yangu Tanzania kwani ni aibu sana kwa taifa kutuma wagonjwa nje ya nchi kila mwaka utafikiri taifa halina madaktari . Moja, je tatizo hakuna madaktari wa magonjwa hayo husika? Au je tatizo ni la hao madaktari kutojiamini na wanalofanya? Nasema hivyo nikimaanisha kuwa kama ni madaktari nauhakika kabisa wapo na wanaweza kabisa kutibu au kufanya upasuaji wa wagonjwa husika. Nakubaliana kipindi cha nyuma kulikuwa na upungufu sana wa madaktari wa upasuaji wa magonjwa yamoyo (cardio surgeon) lakini kuna madaktari zaidi ya 100 walimaliza masomo yao miaka miwili iliyopita nchini India na sasa wapo hapo hospitali ya Taifa ambao walikuwa wameandaliwa maalumu ili kuanzishwa kwa huduma za upasuaji wa moyo Muhimbili. Sasa bado kuna haja gani ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi? Pili, Inawezekana wakasema tatizo ni vyombo vya huduma vya magonjwa husika labda havipo nchini mfano MRI, CT,L aparascopy, Endoscopy, and other Radiological Imaging. Kweli vyombo vingi vya kisasa ni gharama sana na hiyo ndo inayosababisha gaharama kubwa za matibu sababu kabla ya kupata diagnosis lazima kwanza upitie vipimo husika.Hivi vifaa na uhakika kabisa kwa mahospitali makubwa kama Muhimbili, Bugando, KCMC n.k vyote vipo labda kwa new generation vinaweza kukosa. Hata kama havipo je serikari na wizara husika inamalengo gani? Je Tanzania itaendelea kuwa nchi ya kutuma wagonjwa kila mwaka nje ya nchi? Je mnatambua kuwa gharama za mamilioni manazotumia kila mwaka kutuma wagonjwa nje ya nchi si zaidi ya miaka miwili vifaa vyote mhimu vingeweza kununuliwa? na watu hao kuendelea kutibiwa nyumbani kwa gharama nafuu kabisa? Tatu, Kwa nini tuwe wategemezi kila siku au ni kutojiamini kwetu ndo kunakosababisha haya yote ? Kama hakuna mda maalum wa kusitishwa kutuma wagonjwa nje, basi hili litakuwa ni dili la watu wakubwa maana kila wanapotuma wagonjwa kunakuwa na percentage yao wanayopata kwa hiyo kazi hii itakuwa ni ya kudumu, hata kama kuna madaktari na vifaa vya kutosha bado wagonjwa watapelekwa nje ya nchi. Hii ni aibu sana kwa nchi na madaktari nchini kwani inaonyesha kuwa tatifa zima halina madaktari bingwa wakuweza kutibu wagonjwa wao. Inanikumbusha siku moja rafiki yangu alikuwa akipata matibabu nchini China na madaktari wakamuuliza je nchini kwenu hakuna madaktari wa kumfanyia hii operation au hamna vifaa? Lilikuwa ni swali gumu sana kwangu ukizingatia gharama nchini China ni ghari sana ukilinganisha na nyumbani. Naomba waziri wa afya na wizara husika ilifikirie kwa undani hili swala, kwani nilazima ifikie mahali mabo ya kuzoeleka tuyaache kabisa na tufanye vitu vyenye tija kwa taifa letu. Au mnataka hili nalo mpaka aje mwekezaji kutoka nje awaambie ndo mkumbuke kuwa uwezo mnao?? God bless Tanzania Raphael Mallaba Jr. drmallaba@yahoo.com P.R.CHINA. Kuna mjadala mzito unaoendelea huko nyumbani kwenye vijiwe na mablogu kuhusu huyu jamaa aliyeandika hicho kijitabu kinachowabomoa mafisadi wa elimu. Lakini swali ninalojiuliza je huyu jamaa anapowasema hawa ni mafisadi wa elimu aliegemea kwenye kigezo gani hasa (maana bahati mbaya sijafanikiwa kupata nakala ya hako kakitabu nikamsoma). Je ni kwa sababu wana vyeti feki au kwa sababu wamesoma vyuo visivyotambulika duniani (non-accredited colleges and Universities) au kwa sababu wamesoma substandard elimu? Kama ni kufoji vyeti sawa hili ni jambo lililo wazi na linaeleweka na wala halihitaji mjadala kabisa lakini kama ni kutotambulika kwa chuo nadhani hili suala ni pana na linahitaji uchambuzi wa kina. Hivi leo Tanzania tuna baadhi ya vyuo ambavyo ni non-accredited kwa viwango vya TCU na NACTE lakini bado tuna watu wengi waliosoma na wanaoendelea kusoma hapo na kila mwaka registration ya wanafunzi wapya inafanywa lakini sijasikia hizi bodi zikipiga kelele. Nakumbuka miaka fulani huko nyuma kulikuwa na ile issue ya IMTU TCU waliwakomalia mpaka jamaa wakarekebisha mambo fulani walau leo wanatambulika lakini vipi kuhusu chuo fulani hapo Dar ambacho inasemekana hakipo accredited mbona hawapigi kelele zozote. Hii ina maana kama tutabase katika kigezo cha kusoma katika non-accredited vyuos basi mafisadi wa elimu Tanzania watakuwa wengi sana. Kuna suala la kuwa na standards katika elimu. Unaposema standards hapa inabidi tujiulize je tunazungumzia standards za wapi? Tanzania, Japan, Britain, Korea au USA? Maana kila nchi ina standards zake zinazotofautiana ama kidogo au sana na nyingine. Utakuta kozi fulani, kwa mfano, Tanzania inasomwa miaka miwili lakini Australia kozi hiyohiyo mtu ataisoma kwa mwaka mmoja, je huyu akirudi Tanzania utamwambia ni fisadi wa elimu au elimu yake ni substandard kwa vile amesoma kwa mwaka mmoja? Na je yule aliyeisoma kozi hiyo hiyo UK kwa miezi tisa utamuitaje? Kuna baadhi ya nchi kwa mfano hapa China, unaweza kuanza kusoma Masters ya miaka mitatu na ikitokea kwa mfano katika mwaka wa kwanza (unakuwa umesoma basics subjects) ukafaulu vizuri sana unaruhusiwa kuunganisha PhD ambayo utatakiwa kuifanya kwa miaka mitano, kwa maana ya mitatu ya Masters yako na miwili ya PhD na hivi unapograduate mwishoni mwa hiyo miaka yako mitano unapewa vyote viwili, masters na PhD (kwa maana ya MMed/ PhD). Sasa je mtu wa namna hii tutasema ana substandard education kwa vile tu system ya elimu aliyosomea ni tofauti na ya kwetu? Hebu chukulia mtu aliyesomea udaktari Germany, system yao ni tofauti kabisa na Tanzania. Wakati sisi kwetu mtu anasomea MMed kwa miaka mitatu au minne, Germany wao hawana hiyo system ya MMed. So huyu aliyesomea Germany utasema ni substandard kwa vile tu haendani na standards za Tanzania? Kuna mifano mingi mingi ya jinsi standards na systems za elimu zinavyotofautinan kati ya nchi na nchi. Lakini pia suala la standards linaweza kupimwa na mtaala na njia inayotumika katika kufundishia. Sitegemei hata siku moja mwanafunzi wa MD asomee kozi yake online kwa maana katika mtaala wake unamtaka awe darasani kwa masaa kadhaa kwa semester na sehemu nyingine awe wodini ama thietre akishughulika na wagonjwa na kujifunza baadhi ya procedures. Hivyo mtu atakayesema yeye ni daktari aliyesomea kozi yake online huyo moja kwa moja atakuwa feki kwa maana ya elimu yake kuwa substandard. Lakini kuna baadhi ya kozi ambazo nadhani mtu bado anaweza kusomea online na bado akatoka akiwa amewiva kabisa. Kozi kama DS, International Relations, MBA, MPH, MSc. Epidemiology na nyinginezo naamini bado mtu anaweza akazisomea kwa njia ya distance learning na akawiva kabisa. Lakini pamoja na hayo maswali ya kujiuliza hapa ni je hivi vyuo vinatambulika katika kutoa elimu ya njia hii? Je kuna kipindi mwanafunzi anatakiwa kuwa na contact na mwalimu wake? Je muda wa kozi ni sufficient enough kuwezesha topics zote kuwa covered? Je mwanafunzi anapimwaje kuweza kujua kuwa amewiva na anastahili kupewa cheti? Na hapa ndipo issue ilipo. Utakuta chuo kinajitangaza kuwa kinatoa online PhD ya kitu fulani. Ukiuliza muda wa hiyo PhD ni miezi 9!!! Jamani PhD ya miezi tisa kweli?? Hapa ndipo nilipo na tatizo. Ingawa PhD haikuhitaji sana kuwepo darasani lakini bado kule kuandika thesis na kuifanyia kazi ni shughuli tosha ya kukufanya uwe bize kiasi kwamba siamini hata siku moja kama kweli unaweza kuifanya PhD online tena kwa miezi tisa au hata mwaka kama baadhi ya wanasiasa wetu walivyotudanganya na kujipachika mavyeti ya uongo. Lakini je kuna muda uli standard wa kuifanya PhD duniani? Sidhani. Ninavyojua kila nchi ina muda wake minimum ambao walau mtu anatakiwa awe ameutumia kufanya PhD. Kwa mfano nikichukulia China the minimum time ni three years (hii ni nje ya ile system niliyoisema hapo awali). Na hii inatofautiana kati ya nchi na nchi. Poland kwa mfano minimum ni three years lakini kama unaunganisha (wenyewe wanaita fast track PhD kama hiyo ya China) inakuchukua only two years. Sasa leo ukiniambia mtu amefanya PhD online tena kwa miezi tisa hapo kwakweli nitashangaa na kuanza kudoubt. Kwahivi simtetei yeyote aliyesemwa kwenye hicho kijitabu kwa sababu wengi wao sizijui elimu zao lakini najaribu tu kuthink na kuview rationally. Nimeraise hii issue ili siku moja na sisi tusijeambiwa kuwa na elimu za kudesa kwa vile tu tulisomaga fasttrack PhD, MPH au International Health za online. Monsignor, China. Nukuu ya leo toka kwa Watanzania 02/11/2010
![]() ...kuna wanabidii, wanakijiji, wapiganaji, wanamapinduzi etc. Usisahau, hawa wote ni Watanzania wanapaza sauti, wanataka maisha bora! Oh Lord, hear us! - BaMbo, Botswana. Graciously hear Us! - Monsignor, China. ![]() Nyie msijali, mkufuruni Mungu tu kwa kumchagua kaka Chenji, Mlamba Rombo, Low-A-Sir Manduli na kule Bookoba msimuache Kaa-la-Maji pia na huku na huko wachagueni tu. Mnayajua mabaya yao yote ila wachagueni tu hata kwa kanga na tisheti tu. Wala msijali Mungu atawasikia tu; japo kawapa akili na hamtaki kuzitumia sasa mnalia tu. Chagueni mafisadi kisha msubiri uokovu wa Mungu tu. Wala msijali. - Mpiga Paka, Tanzania. ![]() Mpiga Paka, hilo nalo neno...Watanzania wanalalamika maisha magumu, na kweli wamechapika, wanatia huruma, wamejikondea, mama zao wanakufa wakati wa uzazi, watoto wana unyafuzi, wenyewe wanakufa kwa njaa, watoto wakifaulu wakaenda kwenye shule za kata wanapata div sufuri, mahospitalini hamna dawa, barabara hazipitiki, hata ile reli ya mkoloni ilishaharibika, kila kitu kiko hoi, na mchawi wao wanamjua, amekuwepo nao miaka nenda rudi, wanamjua ila hawataki kumuondoa, wanafikiri malaika atatoka Mbinguni kuwabadilishia hali yao, wanaamini hamna mwingine awezae kubadili hali yao isipokua aliyepo... ndo hao ndugu zao wa Bahariadi, Manduli, Bookoba, Rambo, na kwingineko... unafikiri hawaoni? ...wanaona sana, na ndo maana watawarudisha mjengoni kwa vema nyingi (daftari litajaa pata, vema)... kisha wataanza tena kulalamika... watapaza sauti kuilalamikia Serekale, ambayo wameiweka madarakani kihalali...we subiri, si utaona?! - LeBron, Japan. Habari za kusikitisha toka kijijini Ibaraizibu wilayani Bukoba katika mkoa wa Kagera zinasema kuwa Evance Rwelamira (miaka 25) amefariki baada ya kujinyonga kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni baada ya kufeli mtihani kwa mara tatu mfululizo. Taarifa za sababu ya kifo hicho zimetolewa na ndugu wa marehemu, bwana Device Rwelamira ingawaje marehemu hakuacha ujumbe wowote kuhusu sababu ya kuondoa uhai wake. Kamanda wa polisi mkoani Kagera Bw. Henry Salewi alithibitisha kifo hicho alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kwamba mwili wa marehemu huyo ulikutwa ukining'inia juu ya mti. WAZO PEVU ni... Ni kweli kuwa msongo wa mawazo, kukata tamaa na kukosa msaada wa kisaikolojia huweza kkuchangia kwa kiasi kikubwa kupata hisia za kujiua ili kujitahidi kuepukana na kadhia hiyo. Baadhi ya shule huwa na Walimu Washauri ambao mbali na kazi yao ya kufundisha, pia huchukua nafasi ya ulezi na kuwa watu wa karibu, washauri na waelekezi kwa wanafunzi, hasa wanafunzi wanaoonekana kusumbuliwa zaidi na masuala ya masomo au masuala binafsi ambayo ni vigumu kupata utatuzi katika familia. Baadhi ya wanafunzi pia huhitaji msaada zaidi hivyo huonwa na wahudumu wa afya wanaofanya kazi ya ushauri nasaha na saikolojia ambao husaidia kukabiliana na hali ngumu na msongo wa kiakili na kimawazo. Kwa kweli tunahitaji walimu wenye kuweza kutoa ushauri elekezi kwa wanafunzi. Ili kuwapata walimu hawa, tunahitaji Wizara husika kujali maslahi ya Walimu ili nao waweze kuwajali Wanafunzi. Posti iliyotangulia nimeandika namna ya kupata matokeo ya kidato cha nne. BOFYA HAPA kusoma. Nimeshindwa kuvumilia, acheni tu leo niseme, nimeshikwa na hasira ni vile nimekosa viwembe na chupa za kutosha za kujimaliza. Nitatafuta sumu ya panya baadaye nikishamaliza kumwaga hasira zangu leo. Nasema wizara ya Elimu na vitengo husika hasa cha IT na mambo ya tovuti mnatia aibu, mnakera na kuchefua. Nasema hivi kutokana na usumbufu ambao wahitimu wa kidato cha nne na sita wamekuwa wakiupata kila msimu wa matokeo unapowadia. Leo najivisha cheo cha kuwasemea wadogo zangu hawa. Iko hivi: Kila matokeo yanapotangazwa kuwa yametoka rasmi, vijana wamekuwa wakijituma kwenda Wizarani; punde wanapofika huko hutakiwa kupunguza msongamano na kuelekezwa kwenda mashuleni ambako nakala za vitabu vyenye matokeo hayo vimewekwa. Huko kwenye mashule nako ni usumbufu ule ule. Mara mwalimu husika na vilipo vitabu hivyo haonekani. Mara ofisi yenye vitabu haijafunguliwa. Mara mwalimu ana shughuli maalumu subirini. Alimradi tu watapewa vijisababu mia kidogo wakitakiwa kusubiri pasina kujua wasubiri hadi muda gani. Hivi lengo lenu kuwafanyia hivyo ni kuwakatisha tamaa au mnadhani kwa kufanya hivyo mnakwepa usumbufu? Kwa taarifa yenu tamaa hawakati wala usumbufu hauondoki msipowaonesha matokeo; zaidi sana mnawatia hasira tu za bure, bure kabisa! Mtu mwenye akili timamu lazima ajifunze kuona mbele kuwa mtu uwapo katika hali ya uhitaji iliyo na simile ndogo (desperation) ni rahisi kupandwa jazba (to be provoked) kutokana na kunyimwa iliyo haki yako. Hili likitokea bila shaka tutasikia katika vyombo vya habari wahusika wakisema wanafunzi si wastaarabu na wavumilivu. Nashindwa kuelewa wahusika hao wanashindwa vipi kukumbuka saikolojia ya vijana? Lau hawana elimu ya saikolojia hiyo, japo wakumbuke wao wakiwa katika umri huo walikuwa wakijisikia vipi wanapohangaishwa na majibu yao? ule mchecheto walikuwa wanauzima vipi? wao wanadani vijana wa sasa hawana mchecheto? Historia ya tatizo: Kwa mara ya kwanza kusoma vilio hivi ni wakati wahitimu wakitafuta matokeo ya mtihani wa mwaka 2007. Tukajipa moyo kuwa kwa bahati mbaya huenda maji yamezidi unga, si neno, tusubiri mwakani. Mwaka ulofuatia kelele ilikuwa ni ile ile na pengine kuzidi. Tena mwaka huu 2009! Jamani eeh, imezidi hii. Miaka mitatu (2007, 2008, 209) mfululizo tatizo ni lile lile, ina maana kuwa hamsikii au hamtilii maanani kadhia hii mnayosababishia vijana wetu? Yaani ni kweli kuwa Wizara imeshindwa kutenga fungu la kununua bandwidth kubwa kwa wizara hii nyeti ya Elimu ili kukidhi mahitaji ya muda huu mfupi? Isisingiziwe gharama au hasara hapa jama. Sioni hasara yoyote kwani bandwidth itakayotumika ni maalumu kwa kipindi kifupi tu lakini muhimu sana hivyo inaweza kulipiwa kwa kipindi fulani tu. Naomba mtu asiniongopee kuwa haliwezekani kwani ninafahamu, tena si kufahamu tu, ninajua kuwa inawezekana. Tatizo lililopo ni la wahusika kutokutaka kuuliza na kupata maoni ya kipi cha kufanya. Wahenga walisema kuuliza si ujinga, na asiyeuliza hanalo ajifunzalo. Enyi wahusika wa kigengo hiki, kila leo mambo hubadilika; ulilojifunza jana leo laweza kuwa halifai, elimu ya usiku yaweza kuwa kiporo cha asubuhi, tena katika ulimwengu huu wa teknolojia ambapo kila leo zinazaliwa scripts na codes mpya. Tafadhali muache 'kujiona' na mkubali kupatiwa ushauri na kuufanyia kazi ule unaofaa. Suluhisho ama pendekezo langu? Mi nadhani suluhisho mojawapo ni kwenu ninyi wahusika wa IT kuwa elekezeni maswali yenu kwenye kundi la eThinkTankTz (eTTTz) kwani ninayo imani kubwa kuwa mtapatiwa ufumbuzi kutoka kwa wataalamu wengi wanachama wa kundi hili. Nafahamu mnaifahamu eTTz, ila ni 'ego' yenu imekuwa kubwa kuliko masilahi yetu tulio wengi. Linki yake ni www.ethinktanktz.org. Humo wapo watu ambao wamejitolea kabisa ku-host tovuti hii bila malipo yoyote ili tu kuondoa kadhia hii. Ninajua Wizara itajitetea kuwa ni chombo cha Serikali hivyo mtu binafsi au shirika lisio la kiserikali haliwezi kupewa ruhusa ya kufanya hivyo; ikiwa huo ndiyo utetezi na taratibu za kiserikali, basi tupatieni tovuti inayofanya kazi hasa katika kipindi inachohitajika kuliko wakati mwingine wowote. Nimekasirika? Ndiyo! Tena sana tu! Ni aibu na inakera! Ninyi watu kweli mfikage mahali muondoe 'ego' zenu zilizojaa maringo mbuzi na mvae utu na maslahi ya wote mbele. Yaani mi nachukiaga! Sasa nimesema sana, naweza kwenda kutafuta ile sumu ya panya ninywe.... Loh! Thubutu yake. Hanywi mtu sumu wala nini hapa. Ttutapambana na kero hizi hadi liamba walahi. Ala! |