Naomba kutoa angalizo, usikasirike ikiwa huelewi lugha iliyotumika kwenye toleo hili. Ni sanaa ya lugha imetumika kuweka katika maneno yale yote yanayotukia katika anga la Tanzania. Ikibidi kusoma mara nne, sawa tu na hata ukimaliza mata tano na usipate maana, usijali. Huyu jamaa, kusoma maandiko yake huwa tunamwambia inabidi mtu uwe umekula umeshiba, huna 'stress wala frustrations' na kamusi ya mwaka 1947, Shakespear na ile ya mtaani, zote zikiwa 'standby' ndipo uelewe 25% ya alichoandika. Uandishi wake ni wa ajabu. Nachelea kusema, "a genius is considered a fool until he is understood, then we call him a genius."
Toleo la wikiendi. Wikiendi njema! 1. Excess personnel and too many job classifications and outdated organisational structure (form fails to follow strategy). - Ofisi ya Raisi Mipango na Visivyoonekana
- Ofisi ya Wito, Matamshi, Maadili na Nidhamu
- Idara ya Ukakamavu
- Kitengo cha Sura ya Nchi
- Ofisi ya Imani za Bunge
- Ofisi ya Kulisha Viapo
- Msaidizi wa Kikosi Maalumu cha Wapandisha Bendera
- Ofisi ya Waendesha Vikao na Itifaki
- Wakuu wa Wilaya
- Kurugenzi ya Samani, Udhibiti na Uthibitishaji wa Nyaraka
- Tume ya Uwasilishaji
- Kombania ya Utoaji Mashauri ya Sera, Mipango na Mikakati
- Jumuia ya Idara Ndogondogo za Utendaji na Kushughulikia Ithbati na Sheria za Elimu-uganga mbadala (JINUKISHE)
- Wenyeviti wa Kamati za Usuluishi za WIlaya
- Makamu wa Kwanza (na wa Pili, na wa Tatu, na wa Nne) wa Waziri Mkuu
- Waziri Kiongozi Kivuli
- Mshika fimbo wa Bunge
- Ustawi wa Jamii na Tawala za Mikoa
- Mwenezi wa Takwimu
- Mrajis wa Kumbukumbu na Huduma za Miito
- Msawiji
- Meneja Mfawidhi Huduma Changa
- cheki maneci weeeeengi odn- lkn kazi nehi, cheki wafyekaji MNH, lkn mazingira mchundo, cheki bungeni 239, mawaziri, manaibu, maspika, makamati etc 2. Tolerance of incompetence (failure to dismiss poor performers). - kumbukia EPA, Radar, Loliondo, Jeshi, Meremeta, Kiwira, Songas, IPTL, BriwaRiz, Harbours, Taa-nesko, Helkopta, Wakimbizi, NEC. Takokuu, General Tyre, UFI, TRC, endeleza list.... 3. Cumbersome administrative procedures (too much red tape) with deteriorating downward communication and excessive centralisation.- fika oficin- njoo umwone kesho; piga simu- bosi ana kikao, joo jumatatu; Oohhooo bwana Kijenge, ujue nilisafiri, tukutane baciii - kesho baada ya kazi!!!! 4. Powerful staff who deride line mangers as being too conventional and unsophisticated (paralysed hierarchy of authority). - mnaagizwa mwende kwa wakuu wa wilaya zenu (HESLB) - lakini Maimuna Kihiyo anagoma kusaini 5. Form over substance – strategic planning rules are more important than strategic results.- Prosidya prosidya prosidya. hata kama karatasi ni kuukuu, hata kama haionekani vizuri, utaambiwa kajaze tuu kinachoonekana, ulete. Land valuation, milolongo kibao, TRA, Surveyor, kwa Architect, Kwa wapima, kwa Kurugenzi ya Taka, kwa mthamnishaji, kwa korombwezo.... 6.Unclear goals and criteria for measuring organisational success. Kama haya: MKAKATI, MKUKUTA, MCHAKATISHO, MKUZA, KILIMO KWANZA, MKURABITA, MMEEM, WEZESHA, TWANGANA, MMES, MEMKWA, D by D, HIFA 2015, MDGBONGO 7. Intolerance for conflict (harmony at all costs!).- Hapana, naye ni ndugu yetu, mwenzetu, mmoja wetu, komredi wetu, kijana wetu, tunamfahamu huyu, hatuangushani cc, .... - Jamani, tuitunze amani, hakuna kitu bora kama amani,. - Nayakubali matokeo (wakati umepigwa PR kavu hadi damu zinatoka mdomoni (reversed peristalysis)) 8. Poor service delivered by demoralised employees.Kazi za kulipualipua tuuu, malengo ya ku-copy pahala, na kupaste bila ground realities. Utasikia: - kazi zenyewe hizi bwana zinanichosha tu
- haa, wacha nigange njaa
- ngoja nimalize kazi za wenyewe, au kazi za mhindi hizi
- au utasikia, nipo nazuga zuga tu, au nipo napigapiga kidogo, bora mkono uende kinywani
- Hii hata serikalini: utasikia hadi TANESKO wanalalama: aaa, gharama tunazotoza hatupati faida yoyote, ni hand to mouth tuu
9. Decreased product and service innovations.Kila mahali, kilio ni kuagiza nje. Utasikia vituko: - Bwana, tunasubiri vipuri
- aaah, bwana, mpaka viagizwe bwana, hadi pini za kutolea funza (ebikwasi), chupi, mkasi, njiti za meno, karatasi za kuzibia nyuchi zetu (ashakum!)
- hatupati faida yoyote, tunajiendesha kwa hasara , damn!
Nigaago
g2 G
 Hata tiGo wanaweza kuwavuta kwa kiasi cha mboga tu...  VodaCom wanaweza kuita wa kutosha...  Kwa Kikwete watakwenda wengi...  Kwa Slaa watakwenda wengi... Shida yenyewe ni, Je, watakwenda kupiga kura siku ya Jumapili Oktoba 31?
Na shida kubwa kuliko yote, ni Je, watampigia kura nani?
Hapo tu ndipo shida kuu iliko ng'wanawane!
 photo: Victor Maleko - McKepha blog Hii ni karne ya ishirini na moja, na hawa ni Wananchi, wakazi wa Kayenze, Magu, Mwanza.
Karne ambayo watu huteka maji miferejini (bombani) bila kupoteza muda na nguvu ya kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo kwa kwenda umbali mrefu kuyakinga maji. Karne ambayo dunia inajitahidi kuzuia kabisa magonjwa ya mlipuko yatokanayo na matumizi ya maji yasiyofaa au kutokupatikana kwa maji kabisa.
Lakini kwa Tanzania, bado ziwani ndiyo chanzo kikubwa cha maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na mifugo badala ya uvuvi, kilimo, viwandani na chanzo cha nishati ya nguvu ya umeme.
Ni katika mazingira haya, watu hupatwa na magonjwa ya kichocho, kuhara, kuhara damu na mengineyo. Lakini watu hawa, watazuiliwa vipi kuyatumia maji haya ikiwa haipo sehemu nyingine ya kuyateka. Ni sawa na suala lile la usafiri toka kijijini kwenda mnadadi au gulioni. Mantiki ni ile ile, kwamba hata ikiwa lipo katazo, watu mtu analazimika kufanya kile kinachowezekana, hata ikibidi kuvunja sheria, ili aweze kukidhi mahitaji muhimu kwanza kwa binadamu. Hilo la kuvunja sheria na kuugua ni wakati ujao, inshaallah, Mungu atulinde. Wananchi hawa hatuwezi kuwatwika lawama za moja kwa moja kuwa wavivu au wazembe, bali kutokana na hali halisi, kiongozi wao anapaswa kuketi nao na kujadili kuhusu tatizo la maji na kutafuta njia ya kulitatua. Ikiwa wananchi hawa elimu yao ni duni, itakuwa ni kuota ndoto za Ali Nacha kudhani kuwa kuwapa elimu juu ya afya bora basi wataelewa na kuizingatia. Itakuwa pia ni uonevu kusema wanakaidi amri, kwani uhitaji ndiyo unaowasukuma kufanya wanachofanya. Ikiwa mtaji wao ni kidogo, hawataweza kulipia gharama za ujenzi wa visima na mifereji majumbani mwao. Wananchi hawa kwa hakika wanahitaji ushirikiano wa hali ya juu toka kwa viongozi wao ili kuyatatua matatizo yanayowakabili. Kwa haraka twahesabu gharama ya tatizo hili: (1) Muda mwingi kupotea kutafuta maji (2) Hatari ya magojwa ya mlipuko, hivyo (3) Gharama za tiba na kupoteza muda tena au (4) Kifo na kupotea nguvu kazi! Wito kwa: Wananchi, chagueni viongozi wenye mawazo dhahiri ya kuondosha kero zinazowakabili ninyi jimboni. Viongozi, toeni ahadi zinazotekelezeka, acheni kutoa ahadi hewa na kujificha nyakati mnapohitajika. ... nchi yangu, bado sana!
Kwa wale waliokuwa wakisubiri kwa hamu kusikiliza mahojiano ya Metty Nyang'oro wa Radio Mbao (kambaye pia hublogu katika mettyz-bongoland-reflections blog), kipindi chake cha "Kombolela Show" alipohojiana na Profesa Joseph Mbele tarehe 2 Oktoba 2010, mahojiano hayo yapo tayari na yameongezwa kwenye pleya ya " Radio Mbao - Kombolela Show" na unaweza kuisikiliza katika ukurasa huo au katika audio iliyopachikwa hapa (kadiri ya urahisi wako wa kurejea). Profesa Mbele anagusia mambo kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na:- Kukemea tabia ya Uvivu miongoni mwetu,
- Anasisitiza kuhusu umuhimu wa Elimu sahihi,
- Himizp la kujijengea tabia ya kusomea vitabu; kwa mfano, watu wawapo safarini kuelekea ng'ambo, mathalan ujumbe unaongozana na Raisi kwenda kwenye ziara ya kibiashara au yoyote itakayowakutanisha na watu muhimu katika uwekezaji, je, waliopo kwenye msafara huo huwa wanabeba na kusoma vitabu ili kufahamu tabia, tamaduni na miendendo ya watu watakaokutana nao, ili kufanikisha azma ya mikutano iliyowapeleka?
- Suala la kulalamika kuhusu lugha, hasa pale watu wanaosema "...andika kwa Kiswahili", yeye anatoa changamoto, "...ni kwa nini watu naowasijifunze lugha ya Kiingereza (au nyinginezo?)"
- Umuhimu wa kuwa mfano kwa jamii, na kuacha tabia ya kustarehe, kuliko kugharimia na kuweka msingi wa mambo muhimu maishani, hasa kwa kizazi kijacho.
- Umuhimu wa huduma kwa wateja; kwa mfano, anasema amewahi kuwa katika migahawa na anachokiona huko ni Meneja kumwita mhudumu ambaye pengine anaendelea na shughuli nyingine "...wewe fulani, mbona kuna wateja pale hamshughuliki?..." il hali yeye mwenyewe ameketi kitini, angewezakunyanyuka na kuhudumia kama wanavyofanya wamiliki wa migahawa nchi za ng'ambo, mwishowe wateja wanapolikimbia eneo lake, Meneja huishia kulalama, "...jirani yangu au mpinzani wangu kibiashara 'ameniloga'..."
- Hatimaye, anatoa mtizamo wake kuhusu swali ambalo Metty huwauliza wote wanaohojiwa katika kipindi hicho, "Sababu kuu hasa inayosababisha nchi yetu kuhesabiwa katika nchi masikini ni ipi hasa?"
Kusikiliza kipindi kizima utapata yote hayo kwa undani zaidi.
Nilidhani kitendo cha wanafunzi kuacha masomo kwa muda, wafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara kusitisha kazi zao kwa wasaa fulani zitakuwa zinahusisha tukio muhimu tu kama vile Raisi kutaka kukutana na wananchi husika kwa jambo muhimu sana au dharura fulani. Kumbe sivyo? Ama!
Nimelazimika kuhoji, iweje utoro darasani ambao huadhibiwa, leo uhalalishwe kwa wanafunzi hawa kukatiza masomo ili kulaki msafara wa kampeni za kisiasa mkoani Iringa wilayani Kilolo, asubuhi nyakati za masomo?
Kwa mantiki hii basi, walimu, ambao hapa wanawakilisha kundi la wafanyakazi, hawafundishi humo mashuleni. Hili si kosa? Hii si hasara? Hii siyo kuchangia 'kuchakachua' elimu kwa kupoteza muda wa masomo (hata ikiwa ni kwa saa chache), ni muda uliopotea ambao kuupata tena haitawezekana.
Kwa watu makini hii ni pesa iliyopotea. Kwa wasiojali, hii haidhuru. Hivi kweli tunao mpango wa dhati wa elimu bora? au tumeridhika na bora elimu? Halafu tunajiuliza vipi viwango vya ufaulu wa Wahitimu wetu?  Wanafunzi wa shule za eneo la Kilolo, Iringa majira ya asubuhi wakisubiri msafara wa kisiasa Wanafunzi hawa sidhani kama nusu yao wana umri unaoruhusu kupiga kura. Ikiwa ndivyo, wanakosa masomo kwa mujibu wa mitaala na kujianika barabarani kwa sababu ipi ya msingi? Tafadhali mtu asiniongopee kuwa "shule zote zilizopo Ilula za msingi na Sekondari, na madarasa yote na vidato vyote, somo (syllabus) la leo linaelekeza kujifunza kwa vitendo kuhusu Siasa - Kampeni za Uchaguzi!"
Ingekuwa wanafunzi hawa wanametilia ngumu ili kushiriki mikutano ya siasa kwa vyama vya ushindani, je, ingekubalika na kuonekana ni sawa?
Ingekuwa wanafunzi na walimu hawa wamejiunga ili kuandamana kudai elimu bora na marupurupu kazini ingekubalika nakuonekana ni sawa?
Ni kwa nini nchi moja, Taifa moja na jamii moja tuwe na sheria mbili zinazokinzana katika suala moja?
Ni muda kiasi gani wa masomo umemegwa na kupotelea kwa wanafunzi kulazimishwa kusoma 'somo la uraia - kipengele cha siasa, mada : kampeni za uchaguzi?' Na, ikiwa wanafunzi, wafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara wataruhusiwa kuhudhuria mikutano ya kisiasa hivi, ndani ya kipindi cha mwezi mmoja nchi itakuwa imekula hasara kwa kupoteza nguvu kazi na uzalishaji kiasi gani? Hasara hiyo itafidiwa vipi?
Tafadhali Raisi na watumishi wote wa Serikali mlio makini, kemeeni mambo haya yasiyo na manufaa kwa Taifa. Tuache kufumbia macho mambo haya. Ingekuwa ni nchi zilizoendelea hii ingezaa kesi toka kwa Wanafunzi dhidi ya Uongozi wa Walimu, Shule na Serikali kwa kuruhusu watoto wao walioagizwa kwenda shule kuelimika, badala yake wakaenda barabarani. Labda uwepo uthibitisho wa maandishi unaoonesha kuwa ratiba ya masomo ya shule hizo mbalimbali, madarasa na vidato vyote, 'syllabus' inaonesha kuwa somo la siku ni 'Siasa - kampeni za Uchaguzi' (or something like that), tofauti na hapo, hii ni kashfa na kesi!
Ni vyema wanafunzi, wafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara wakashiriki mikutano ya kampeni za kisiasa lakini hayo yote yafanyike kwa utaratibu unaokubalika, usioiba muda. N ushiriki uwe wenye uwiano na sawa.
Rafiki yangu mmoja ananitumia ujumbe aniambia, 'Subi, kuna waraka mzuri sana umetungwa, huu hapa usome, naona vyema uutundike kwenye wavuti...' nami namjibu, waraka wenyewe chanzo chake nani? Basi aniambia mwandishi ni Big Lady, nami bila hiyana, nakata mistari michache hapa... 3 Kwa hiyo wasikilizeni na kupima chochote watakachowaambieni. Lakini msiwape kura zenu wala msiyaige matendo yao, maana hawatekelezi yale wanayoyawahutubia. 4 Hufunga mizigo mizito na kuwatwika Watanzania mabegani, lakini wao wenyewe hawataki kunyosha hata kidole wapate kuibeba. 5 Wao hufanya matendo yao yote ili watu wawaone. Huvaa nguo nzuri za gharama, kutembea na magari mazuri ya gharama na kuishi katika nyumba nzuri za gharama zenye hati za majina yao, au watoto wao au ndugu zao. 6 Hupenda nafasi za heshima bungeni na katika karamu au hafla mbalimbali hupenda viti vya meza kuu ili waonekane. 7 Hupenda kusalimiwa kwa heshima bungeni, maofisini au hata barabarani, sokoni, kwenye sherehe au misibani na kupendelea kuitwa na watu: Mheshimiwa. 8 Lakini ninyi msikubali kuitwa kamwe Mheshimiwa maana Nchi yenu ni mmoja tu na wala haijawagawa wa kuheshimiwa sana wala kidogo, nanyi nyote ni Watanzania mlio na haki sawa za Kibinadamu. 9 Wala msimwite Fisadi yeyote hapa duniani Mheshimiwa au Mtukufu, maana Mtukufu ni mmoja tu Mungu aliye mbinguni. ...ikiwa umevutiwa ukataka kusoma waraka mzima, basi jongea JamiiForums.com upate kuusoma!
wavuti.com wish to send many "Thank You" notes to neighbor, Proches Tairo of a great upcoming weblog, BongoLine.com, for allowing a republication and sharing of this article. Please read on... If your spouse has an affair with another person, should you be legally able to sue for damages? Should you be able to bring a lawsuit against the affair-partner? Or put it simply, should any injured partner in a relationship be able to sue the pants off someone who snuggled up to their honey? (Well, technically, their pants were already off, but anyhow).
Now, my question here is limited specifically to the situation in which the couple appears to be happy. The spouse tells his/her other sigificant how much s/he loves her/him, they have all kind of fun with their children, family, friends, everything appears to be just great, but one spouse is secretly having an affair, intentionally lying to his/her other significant and the affair-partner agrees to carry on the affair under wraps.
The injured spouse has many choices for dealing with his partner when an infidelity is discovered. S/he can divorce, break up, stay together, throw things at him/her, you know all. Some even go to the extent of having an affair as well as a reprisal. But the point is that, there is some level of accountability for the betrayer. The injured spouse loses his/her spouse; the family, s/he may have to pay spousal support in divorce, bringing up the children, etc. S/he will also likely to bear the wrath of family, friends and, if the matter goes public, the society.
Even if the spouse who cheated begs his/her other significant for forgiveness and gets lucky enough to get a second chance, s/he will have to go through the arduous process of earning back his/her significant other trust, which usually includes a loss of certain freedoms previously enjoyed, etc. Now, what about the affair-partner? There is that age-old argument that well; it is not HIS/HER fault. The spouse who cheated is the one who chose to break his/her marriage vows. The argument goes: Since the affair-partner did not make any vows to the husband/wife, why should be held responsible? However, there is this new age argument that well, why shouldn’t the affair-partner bears some responsibility as well? Why should the affair-partner not be equally at fault? What if the affair-partner did not make any commitments to the husband/wife? Does that make it right for the affair partner to go after someone else’s husband/wife? Does that make it right that the affair-partner to participate in the lie, the deceit, the fraud? Does that make it OK to intentionally harm and cause emotional injury to the innocent wife/husband? Even, if the cheating husband/wife pursued the affair-partner, should the affair-partner still knowingly enter into the affair? We have decided as a society that certain behaviours are not OK. As a result, we have decided that there are certain standards by which people are obligated to act. We expect people to act according to “that degree of care that an ordinarily prudent person can be reasonably expected to exercise under similar circumstance.” If someone acts “unreasonably” in those situations, then they can be sued for the harm caused to a third person as a result. For instance, if you are injured by a driver who failed to exercise reasonable care when driving on the freeway, you can sue them because all drivers have a duty to act reasonably to prevent harm to other road users. Doctors are supposed to perform their duties as any other reasonable doctor would in a similar situation, or else face liability for malpractice. Store owners must put up a sign when a floor is wet, because society considers that to be the reasonable way to act to prevent someone from harm. Likewise, homeowners must warn guests in their home of any sort of danger that may be posed. If someone punches you, you can sue them for injuries for intentionally hurting you! You can even sue someone for intentionally harming you emotionally and psychologically. If someone tells a bunch of lies about you, you can sue them for defamation and damaging your reputation. You can sue the manufacture of a toy for failing to adhere to certain standards to make the toy safe to play with by your children. You can even sue someone for interfering with a potential business relationship- for convincing someone to breach a contract with someone else. However, in many jurisdictions you cannot sue an affair-partner for interfering with the most important relationship of your life, or for helping them to break their commitments or vows to their wives/husbands. Isn’t it reasonable to expect that other people won’t have a secret affair with your spouse? A handful of states in the United States do allow a wife to sue the mistress. These states have what is called “alienation of affection” laws that allow a spouse to sue the person who ‘seduced’ the spouse and ‘alienated’ the spouse away from his/her husband or wife. To win, an alienation of affection claim, you must prove that, love between the married spouses must have existed; the marital love must have been alienated and destroyed; and the third party's conduct has to be proved to be malicious interference with the marriage relationship. Historically, the alienation of affection law was based on the belief that a wife was the property of her husband. Therefore, when a woman was emotionally or sexually involved with another man, she was considered to have been stolen. Most states in the United States have abolished this type of lawsuit as it is considered to be archaic and an unacceptable form of revenge. Those who want the alienation of affection laws to remain believe that alienation of affection claim protect traditional marriage. It is doubtful if alienation of affection is applicable in Tanzania. Some have argued that all we would be doing is holding them accountable, along with the cheating spouse, for failing to act the way we expect anybody else to act, the way we expect any ordinary person, any reasonable person, to act. And, that, if the affair-partner were required to pay damages to the innocent spouse for the injuries she caused, then perhaps that there would be a deterrent effect and less breaking marriage vows would result all around. I know I am simply discussing general legal principles here and applying them to the circumstance of the “other woman” or “other man.” But is it just and right that people should be held accountable for the harm they cause to others, especially harm to the things most of us consider to be the most valuable, fundamental relationships in our lives? If yes or no under what basis? The article is not intended to be a legal advice. Neither does is answer the question posed. Rather, it explores different arguments and invites you for your comments. If you need legal advice you are advised to seek professional legal adviser. credit: Proches Tairo/ BongoLine.com
 BAADHI ya watahiniwa katika shule ya Msingi, Miburani, Temeke, Dar es Salaam wakishangilia baada ya mtihani wa mwisho wa kuhitimu Elimu ya Msingi. (photo: Bashir Nkoromo). Vijana hawa wananikumbusha siku tuliyokuwa tukiisubiri kwa hamu kubwa sana, 'kumaliza shule' tukiamini ati baada ya kuondokana na adha ya kudamka alfajiri, kushikana mashati na 'konda', kuwahi 'namba' na 'mstarini'... yaani ndoto za kila aina alimradi kujiaminisha usumbufu utakuwa umekwisha kabisa.
Tulijiona sisi ndiyo 'top' hakuna mwingine duniani kama sisi. Hisia za 'kumaliza shule' na kubaki nyumbani wakati wengine wanaamka asubuhi wakiwa na heka heka za ama kwenda shuleni au kazini, zilitutawala.
Siku hizi, tofauti na zamani nilipomwona 'madha mnoko', huwa najivuna sana kuwa na Mama asiye na longolongo wala 'kukopesha maneno' kwani, aliponisikia nikijitapa eti 'nimemaliza shule' siku moja aliniambia,
"...wewe, umemaliza shule ipi? Subi, hujamaliza shule. Umehitimu Elimu ya Msingi tu. Umeimalizaje shule wakati hujafika hata Sekondari? Umesahau methali mlizofundishwa, Elimu ni bahari; Elimu haina mwisho? au ulidhani ukishakariri na kuandika kwenye daftari ukafunga na ulichofundishwa kimefungwa kwenye mkoba? Yaani mwalimu akishafuta ubao na kwenye akili yako vinafutika? (kichwani mwangu nawaza, 'kwani si ndiyo kazi ya shule? unaandika, mnakusanya madaftari, mwalimu anatia 'pata' kama hesabu umekosea fanya masahihisho tu, basi').
Umevuka madarasa ya shule ya awali, sababu ya kuitwa 'msingi' ni kwa kuwa umeweka msingi wa elimu na maisha yako. Ni sawa na kujenga nyumba. Ili iweze kusimama imara, lazima msingi uwepo, tena uwe ni msingi ulio imara. Msingi ndiyo kigezo cha uimara wa nyumba. Umeweka msingi, bado kuta, madirisha, paa, na fenicha na vifaa vingine vya ndani. Lakini la muhimu ni msingi. Ikiwa uliweka msingi imara, nyumba yako itakuwa imara, utaweza kujenga nyumba kuuuubwa au hata orofa, inategemea na uimara wa msingi wake."
Ni baada ya kwenda kwa Bibi na kuwatembelea ndugu, ninarejelewa kauli ya Mama, 'hujamaliza shule' nhe he, ndipo nilipotia akilini, kumbe tulichokuwa tukifurahia 'standadi seven kumaliza shule' ilikuwa ni furaha ya muda tu, tena ya kitoto, bado ilikuwepo kazi kubwa mbele yetu; Kuna kusaidia kazi za nyumbani sasa zaidi ya wengine na; Kuna kuchukua fomu za shule za "private" tena kujaza zaidi ya moja, na kwa ambaye matokeo ya maendeleo yake shuleni kila mhula hayakuwa mazuri, hali kwake ilikuwa ni mbaya, yaani atazijaza fomu za 'private school' hata tano ili walao abahatishe moja ikiwa atakataliwa kwingineko. Nakumbuka nilizijaza mbili, Majengo Secondary na Uru Seminary. Kisha kuna kufanya tena mtihani wa kuomba kujiunga na shule hizo na, ni lazima ufaulu, la sivyo uaibike kwa kuzurura mtaani na kufanya kazi nyumbani wakati wenzio wanaongozana kwenda na kutoka shuleni! Shabash! Hakuna kumaliza shule!
Naam, huo ndiyo wakati nilipoanza kufahamu kuwa ninayahama maisha ya utoto na kuingia ujanani.
Hongereni vijana mliohitimu elimu ya msingi, shule bado hamjaimaliza. Elimu haina mwisho!
Cross posting this from Candy1World blog whom I fully agree with here, and share the lamentations. Nimeamua kuongea kuhusu hili baada ya kuangalia CNN MultiChoice African Journalist Awards. I t is absolutely amazing seeing people making great stories, going to the source of the story, getting the untold and etc. Also the person who took the overall award of this year 2010, Sam Rogers, she was getting the story about the albino killings in Tanzania though I didn't get a chance to see the documentaryOur neighbours Kenya did well in the awards ceremony; not only Kenya but also Mozambique, South Africa and all others. When I switch on the radio and "tune", about 95% of all stations just do music. News will be read for about 5 minutes and it is done. Music is not the problem, the problem is Tanzanian radio stations [are] not interested in things happening around the world. Kama mambo yenyewe ndio hivyo, awards zitakuja kweli huku? Au ndio awards za hukuhuku za kumwaga?... Au ndio wanaona hizi redio za nje, namaanisha BBC au Deutsche Welle or VOA, wakileta habari zao ndio inatosha? I am just asking...
Mungu ibadili Afrika, Wabadili viongozi wake Hekima umoja na ukweli, hizi ni ngao zetu Afrika na watu wake Ibadili, Afrika x2 Tubadili, watoto wa Afrika. Mungu ibadili Tanzania, Wabadili viongozi wake Hekima umoja na ukweli, hizi ni ngao zetu Tanzania na watu wake Ibadili, Tanzania x2 Tubadili, watoto wa Tanzania. Credit, Thanks and COPYRIGHT @ Mdimi Ndosi CC - Creative Commons licence applies
|