Add Comment Picha: Ikulu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wa Asasi Zisizokuwa za Kiserikali (AZISE) wamekutana leo, Ijumaa, Februari 3, 2012, Ikulu, Dar Es Salaam, kuzungumzia mapendekezo ya Asasi hizo kuhusu jinsi ya kuboresha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Nambari 8 ya Mwaka 2011. Ujumbe huo wa watu 17 na ulioongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la AZISE, Bwana Humphrey Polepole umefanya mazungumzo ya kiasi cha saa tatu na Mheshimiwa Rais Kikwete na kutoa mapendekezo yake juu ya kuboresha Sheria hiyo na mchakato nzima wa kutungwa kwa Katiba Mpya. Mbali na Bwana Polepole, ujumbe huo ulishirikisha pia wajumbe wengine saba wa Baraza hilo, na wajumbe kutoka taasisi za Tanzania Youth Coalition (TYC), mjumbe kutoka The Leadership Forum/Jukwaa la Katiba, SHIVYAWATA, FEM ACT, mjumbe kutoka Legal and Human Rights Centre/Jukwaa la Katiba, SAHRINGON, na Youth of United Nations (YUNA). Mazungumzo kati ya Rais Kikwete na ujumbe huo yamefanyika katika mazingira ya maelewano na miongoni mwa mambo mengine pande hizo mbili zimekubaliana kama ifuatavyo: Ujumbe wa wataalam wa ASIZE kukutana mara moja na ujumbe wa watalaam wa Serikali kuona namna gani ya kushirikisha mawazo ya Asazi hizo katika mchakato unaoendelea wa Marekebisho ya Sheria na ule mpana zaidi wa Katiba yenyewe Kwamba Katiba inayotafutwa ni Katiba ya Watanzania wote na ya nchi ya Tanzania, na wala siyo ya chama kimoja cha siasa, ama ya kabila moja ama ya kikundi kimoja cha dini. Hivyo, Katiba hiyo itafutwe kwa kujali na kutilia maanani kulinda Umoja na mustakabali wa Taifa. Kwamba kila mwananchi awe na uhuru kamili kushiriki katika Mchakato wa Kutunga Katiba Mpya lakini uhuru huo utumike kusaidia kufanikisha mchakato na wala siyo kuvuruga nchi. Ujumbe huo pia umempongeza Mheshimiwa Rais Kikwete kwa ujasiri wake wa kuanzisha mchakato wa Kutafuta Katiba Mpya kwa namna ambayo haijapata kufanyika tokea kupatikana kwa Uhuru miaka 50 iliyopita na kufanikiwa kwa Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964. Rais Kikwete mwenyewe amewashukuru wajumbe hao kwa kukubali kukutana naye kujadili suala muhimu kwa maslahi ya nchi na kusema kuwa utashi wake ni kuona Tanzania inapata Katiba nzuri na inayotelekezeka na kwa wakati uliokubaliwa. Hili ni kundi la nne kukutana na Mheshimiwa Rais Kikwete kuhusiana na mchakato huo. Kabla ya hapo, Rais Kikwete amekutana na kufanya majadiliano na uongozi wa vyama vya siasa vya CHADEMA, CUF na NCCR. Mwisho. Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Raia, Ikulu. Dar es Salaam. 03 Februari, 2012 Watoto wenye hemophilia walitembelea Bagamoyo hivi karibuni. Ziara iliandaliwa na Hemophilia Society of Tanzania. taarifa na picha via Richard Minja, Rais wa HST. ---- Ufunguo: Hemophilia ni tatizo la damu kutoganda kutokana na hitilafu anayorithi mtu wakati wa kuzaliwa. Dalili zake zinazoonekana kwa macho ni pamoja na kutokwa damu mfululizo kwa muda mrefu unapotokea mchubuko, kukatwa/kujikata, kutoneshwa/jitonesha kidonda n.k. Vipimo vya maabara huthibitisha ikiwa dalili hizo ni za ugonjwa wa hemophilia ama la. FNB Tanzania officially launched 02/02/2012
Since commencing its operations in July 2011, FNB's operations have performed well in Tanzania and are in line with expectations illustrating the sound investment and business opportunity provided in the country, the bank says. To date, the bank has successfully opened three branches in Dar es Salaam, with a fourth branch expected to open before the end of the year. Further expansion into areas such as Arusha, Mwanza and Mbeya will follow and the expansion is set to continue over the coming years until true national representation is achieved. A round of applause rings after President Jakaya Mrisho Kikwete has officially launched the First National Bank Tanzania (FNB-Tanzania) yesterday at the Kilimanjaro Grand Hyatt hotel in Dar es salaam. Others from left are the High Commissioner of South Africa to Tanzania, Mr Thanduyise Henry Chiliza, the CEO of FirstRand, Mr Sizwe Nxasana and the Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Finance Ms Elizabeth Nyambibo. (Photo by State House) “For First National Bank, this is a significant development for our expansion strategy and growth in East Africa, West Africa and Southern Africa as we see this presence core to our Africa footprint. We have identified Tanzania as a key growth market for the banking group and see a bright future for investment and expansion in the country,” said Sizwe Nxasana, CEO of FirstRand Bank. “FNB has launched a range of products into the Southern African and African markets over the last few years, and we intend to do the same in Tanzania,” added Richard Hudson, CEO of FNB Tanzania. “We consider ourselves to be a market leader in introducing new and innovative products and will be tapping into the systems and expertise of the group to ensure the smooth roll-out of these products in Tanzania. These products are all aimed at making the banking experience more efficient and more rewarding for our customers, and even more so for the unbanked market.” Hudson explained that the investment in Tanzania was aligned to the group's strategy of being a significant player in the banking industry in Africa. He added that there were many compelling reasons for investing in Tanzania in its own right and these included, but were not limited to, the country's large population, strong economic growth, a sizeable GDP, a well regulated banking industry and a stable political environment. “We remain committed to our brand promise and we intend to continue to deliver on that promise. We look forward to partnering with the people of Tanzania by making a positive contribution to the economy and hope that the FNB experience will be a rewarding one, where customers truly experience the spirit of “helpfulness.” concluded Hudson. A pickup truck for sale 01/02/2012
For serious buyers, please CALL: +255777000214 Waliyosema wahenga kuwa "shida huleta maarifa" "shida huleta akili" hawakukosea kwani, kwani mfano huu wa picha inayoonekana hapa ambapo watoto wanavuka barabara kwa kushikana mikono na na kuvuka kwa pamoja, ni njia nzuri ya kuepukana na shida za waendesha vyombo vya usafiri barabarani ambao baadhi yao si makini katika kuwaruhusu waenda kwa mguu kuvuka barabara. Wengine hawajali kabisa watoto wadogo ambao ndiyo wanajifunza matumizi ya barabara. Kila leo wanafunzi wanagogwa na kuachwa na vilema huku wengine wakipoteza uhai wao. Mbinu hii ya kuvuka barabara nadhani ni sahihi zaidi hasa maeneo yasiyo na alama za pundamilia za kuvukia barabara. Taarifa Habari TBC na BBC Swahili - Dkt. Mponda na Dkt. Ulimboka kuhusu mgogoro wa Madaktari 31/01/2012
Audio ya BBC Swahili kipindi cha Dira anasikika Dkt. Ulimboka na Waziri, Dkt. Mponda wakizungumza kuhusu mgogoro wa Madaktari na Serikali Taarifa ya Habari TBC leo ikizungumzia suala la mgogoro wa Madaktari na suala la posho ya Wabunge. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hadji Mponda (kushoto), akizungumza na baadhi ya madaktari toka vikosi vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Dar es Salaam jana, walipofika kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ili kutoa huduma kwa wagonjwa kufuatia mgomo wa madaktari unaoendelea nchini. (Picha: Rajabu Mhamila) Madaktari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiangalia maiti iliyoletwa ili kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es salaam jana, Serikali imeagiza madaktari wa vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama kuhudumia wagonjwa ili kuziba pengo la madaktari waliogoma. (Picha: Rajabu Mhamila) picha via blogu ya MbeyaYetu Ajali iliyotokea Mafinga yaua wanne 29/01/2012
Barabara eneo la Nyololo kilometa chache kufika Makambako, Iringa ni baya, hasa wakati wa mvua kuna utelezi sana. Jana siku ya Jumamosi basi New Force one lilokuwa likitokea Dar es Salaam lilipinduka, na kusababisha ajali. Madereva wanapaswa kuwa waangalifu wakati wa 'overtaking lorries' wakati wa mvua na kwenye miteremko. (RPS) Gari, Toyota Caldina linauzwa 28/01/2012
Limeingia karibuni kutoka Japan. Lmetembea km 57000 tu. Liko kwenye hali nzuri sana. Limeshafanyiwa registration. Kupata bei na maelezo mengine, tuwasiliane, Emmanuel, email ni: matechi@gmail.com au simu 0713 764488 | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |















RSS Feed