Hesabu gharama kwanza... 07/22/2010
Fomu yalipiwa shilingi Milioni Moja na ushee hivyo... Kuna 'shoki-shoki' na 'masheli-sheli' 07/22/2010
Siku moja kule kijiweni Facebook naandika, 'hii ni misheli sheli', rafiki yangu pale Hassan anirekebisha asema picha ul'oweka ya 'shoki shoki', yaani kidogo nimpoteze dogo Arnold. Sasa leo napata picha ya 'mishoki shoki' hivyo nimeamua kuziweka zote hapa na kuzitambulisha rasmi, tupate kufayamu yepi masheli sheli na ipi shoki-shoki. Shukrani kwa Othman Maulid Othman kwa picha zote zilizomo kwenye posti hii. Kuelekea kilele cha mlima Kilimanjaro 07/21/2010
Huu ni muonekano wa mojawapo ya maeneo yanayokaribia mwinuko wa mlima Kilimanjaro. Kuona picha zaidi za maeneo yanayouzunguka mlima kwa karibu, tembelea TembeaTz.blogspot.com "Update": Kwa mujibu ya taarifa ya Habari iliyosomwa saa mbili usiku na TBC1, ni watu 18 walionusurika kifo katika ajali ya Coaster iliyotokea majira ya saa nane mchana. Kamanda wa Polisi wa mkoa Maalumu wa Kipolisi Temeke, David Missime amesema hakuna yeyote aliyoepoteza uhai katika ajali hiyo. Dk. Asha Mahita wa hospitali ya Temeke amesema kuwa watu 13 waliojeruhiwa wamepatiwa matibabu katika hospitali ya Temeke na wengine 3 waliojeruhiwa vibaya wamepelewa katika Hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi. Basi aina ya Coaster lenye namba za usajili T 323 BEB linalofanya safari zake kati ya Mbagala na Buguruni limepata ajali mbaya baada ya kuanguka katika Mto Kizinga uliopo Mtoni Mtongani Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya abiria waliokuwa katika basi hilo wamejeruhiwa na inaripotiwa kuwa abiria watano wamefariki dunia katika ajali hiyo. Kwa habari na picha zaidi, tembelea GPL (credit) Mtizamaji, shuhudia jinsi gari hilo, ambalo hakuna uhakika kama ni maalumu kwa uzoaji taka au la, lilivyojazwa taka kiasi cha kuziba vioo vyote anavyotakiwa kuvitumia dereva wakati akiendeshagari awapo barabarani. Tizama nafasi ya upana iliyochukuliwa na taka hizo ulinganishe na ukubwa wa bodi ya gari ufikiri dereva aliyeko nyuma na anayepishana naye pembeni anatakiwa kukadiria vipi ukubwa halisi wa gari hilo. Kwa mwendo huu kweli ajali za barabarani tunapambana nazo vilivyo au ni nadharia tu? Vikosi vya kusimamia na kuhakikisha uwepo wa usalama barabarani wangekuwa wanafanya kazi yao ipasavyo, huenda wazoa taka hawa wasingethubutu kujaza uchafu kwa kipimo hiki. Lau, wananchi tungekuwa tunajali afya zetu na kutii sheria, tusingekuwa tunafanya au kukubali mambo hatarishi hivi. Picha kama hizi pia za uvunjaji sheria kwa magari yanayozoa taka jijini Dar Es Salam, amekuwa akizipiga na kuziposti katika blogu yake bwana Othman Michuzi / Mtaa kwa Mtaa blog Wakati mbunge wa jimbo la Iringa mjini Monica Mbega akiwa katika majonzi makubwa ya kufiwa Baba yake mzee Ngezi, baadhi ya wagombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo wameamua kutumia msiba huo kwa kufanya kampeni za Ubunge, baadhi yao wakionyesha fomu zao za kuwania Ubunge makaburini hapo. Wagombea hao waliwashangaza watu wengi waliohudhuria shughuli za maziko hayo yaliofanyika katika makaburi ya Kitwiru mjini Iringa, kwa kitendo cha kila mmoja wao kuonekana akiwa katika jitihada za kujipitisha kwa wana CCM ambao baadhi yao ni wafiwa na kuomba kura. Jambo hili halijapata kutokea. Aidha, wagombe wengine waliamua "kujionesha" kwa kushika spedi kwa la kufukia mchanga katika kaburi hilo ili kuonekana kwa wapiga kura jinsi wanavyoshiriki bega kwa bega katika matatizo ya wananchi. Nina usemi niupendao sana, kuwa 'Siasa si hasa, bali visa na mikasa'! Mwananchi wa kawaida nchini Tanzania 07/19/2010
Baadhi ya watu huuliza, 'unaposema mwananchi wa kawaida, unamaanisha nini hasa? Basi wanaoonekana katika picha hii ni baadhi ya Wanawake ambao wanawakisha sehemu tu ya dhana ya 'wananchi wa kawaida" katika nchi yao ya Tanzania. Hongera kwao kwa kuchapa kazi, ingawaje katika mazingira magumu na vifaa duni ikilinganishwa na wanavyofanya nchi zenye maendeleo ya viwanda. Picha zaidi katika blogu ya Mroki Mroki Pichani ni Profesa Joseph Mbele ni Mhadhiri katika Idara ya lugha ya Kiingereza katika Chuo Kikuu cha St. Olaf kilichopo jimboni la Minnesota nchini Marekani ambaye alipata fursa ya kuhudhuria darasa la Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ambapo wanafunzi wa Shahada ya Juu ya Kiswahili walikuwa wakijadili wakijadili "utendi wa Hamziya", zaidi juu ya hudhurio hilo, bofya hapa kusoma posti fupi katika blogu yake. Profesa Mbele Amekuwa akialikwa kuzungumza katika vyuo, makongamano na warsha mbalimbali ndani na nje ya Marekani. Amekuwa akichagiza Wananchi kujenga tabia ya kupenda kujisomea vitabu na kujifunza mambo ili kuongeza ufahamu na kuweza kupata mbinu za kumudu na kukabiliana na maisha. Profesa pia amekuwa mstari wa mbele kabisa kupinga uvivu na kuendekeza starehe zisizo na tija maishani. wavuti.com inayo furaha ya pekee ya kufahamiana na kuendelea kushirikiana na Profesa Joseph Mbele. ChaiMaharage na Markiti - Zanzibar 07/17/2010
Safari ya Othman Michuzi akitembea Mtaa kwa Mtaa huko Zenji... 'Chaimaharage' ni jina lililozoeleka miaka ya 90 na linalotumika kumaanisha vyombo vya usafiri kwa umma ama 'daladala' kwa Dar Es Salaam au 'matatu' kwa Nairobi na 'chapa' (hutamkwa 'shapa') huko Maputo. Samaki wa kubanika, utamaduni asilia. 07/16/2010
|