Kumbukumbu za Martin Luther King Jr 22/01/2012
Juu ni gari lililohifadhiwa katika jumba la makumbusho ya Mchungaji mpigania haki, usawa na uhuru nchini Marekani, Martin Luther King Jr. Gari hilo la kukokotwa na farasi ndilo lililoubeba mwili wa marehemu Martin Luther King Jr. kwa ajili ya maziko kufuatia kupigwa risasi na kuuawa. Picha ya chini ilipigwa siku ya maziko ya Mch. Martin Luther King Jr. Picha zote zimepigwa na "Dewo" alipozuru jumba hilo lililopo Atlanta, Georgia, Marekani (Januari 2012). Kwa mengi zaidi kuhusu Martin Luther King Jr, fungua tovuti iliyotengenezwa mahsusi kwa ajili yake: thekingcenter.org Add Comment Jioni yaleo, Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbrod Slaa pamoja na viongozi na wajumbe wengine wa CHADEMA wamekutana Ikulu kwa mwendelezo wa mazungumzo ya mchakato wa muundo wa kupatikana kwa Katiba Mpya ya Tanzania. Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Freeman Mbowe, Tundu Lissu, John Mnyika, Said Arfi, John Mrema, Profesa Mwesiga Baregu na Profesa Abdallah Safari. Katika mkutano wa awali ambapo Rais alikutana na baadhi ya viongozi wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa hakuhudhuria. Zifuatazo ni picha za Ikulu za mkutano wa leo. (Picha za mkutano uliotanguli aunaweza kuziona kwa kubofya hapa). Mkutano huo ulihitimishwa saa tano na robo usiku! Huko Ikulu leo, Rais Jakaya Kikwete amekutana na uongozi wa chama cha NCCR-Mageuzi kufuatia ombi la kutaka kuonana naye ili kuwasilisha mapendekezo ya chama hicho kuhusu mchakato wa jinsi ya kuipata Katiba Mpya ya Tanzania. Zifuatazo ni picha toka Ikulu za mkutano huo. Rais Kiwete leo Jumamosi, Januari 21, 2012 ameongoza mamia ya viongozi na wakazi wa Dar es Salaam waliofika katika viwanja vya Karimjee kwenye hafla ya kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru, marehemu Jeremiah Sumari. Zifuatazo ni chache ya picha za zilizopichwa na Mpiga picha wa Ikulu (na nyingine toka blogu ya Richard Mwaikenda.) Tangazo la taarifa ya kusudio la kuandamana ilitangazwa kwenye vyombo vya habari ikiwemo hapa. Maandamano yamefanyika katika maeneo kadhaa nchini. Ifuatayo ni taarifa toka Morogoro na picha za Dar es Salaam na Morogoro. --- Mamia ya Waislamu wa Morogoro wakiwemo Wanafunzi na Vijana wa Kiislamu wameandamana hadi Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwasilisha madai yao mbalimbali yakiwemo ya kupinga mfumo Kristo ndani ya Serikali. Maandamano hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi na Vijana wa Kiislamu Mkoa wa Morogoro, yalianza mara baada ya swala Ijumaa kutoka Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro eneo la Msamvu , kupitia katikati ya mitaa ya Manispaa ya Morogoro hadi nje ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa . Hivyo pamoja na kufikisha risala hiyo, wameipa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa siku 21 kuanzia Januari 20, mwaka huu kuyashughulikia madai ya Waislamu wa Mkoa wa Morogoro na kupatia uvumbuzi wa kudumu, vinginevyo watayashughulikia wao wenyewe. Wakati maaandamano hayo kijumuisha baadhi ya wasilamu wengine njiani , Polisi Mkoa wa Morogoro chini ya Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Joseph Rugira, waliwahi kuziba njia karibu na Ikulu ndogo yakiwemo na Makazi ya Mkuu wa Mkoa sambamba na lango la kuingilia Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Hata hivyo wakati maandamano hayo wakisika kasi kwa waislamu hao kubeba mabango yaliyoanzidikwa ‘Kupinga mazira mfumo kristo Tanzania’ ‘No Peace without justice ‘pia walibeba mabango yaliyoandikwa kwa vitambaa yakiwa na ujumbe ‘Majengo ya Serikali Ardhi ya Kanisa . JK Thibitisha …lazima kieleweke’ na ‘ Pasipo haki hakuna usawa’. Azma ya kufanyika kwa maandamano hayo ni kushinikiza Serikali kuuondoa mfumo kristo , kudhulumiwa , kunyanyaswa na ukandamizaji wa wanafunzi wa Kiislamu mashuleni, Vyuoni na kubakizwa nyuma kwa makusudi katika elimu , ajira na maeneo mengine mbalimbali na kupewa majina mabaya kama magaidi ili kuhalalisha dhuluma dhidi ya Waaislamu. Pamoja na kurupushani hizo, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Rugira, aliwataka Waandamanaji hao kuteua wawakilishi watano wataowasilisha risala yao kwa Mkuu wa Mkoa na wao wabakie wakisubiri kupatwa majawabu. Hatua hiyo iiliafikiwa na Waaislamu hao, na waliwateua wawakilishi watano kupeleka ujumbe katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa , ambapo pamoja na kufika Ofisi hiyo, Mkuu wa Mkoa alikuwa safarini na wao wakimtaka Ofisa Elimu wa Mkoa ili asikilize madai yao. Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mgeni Baruani, aliazimika kutoka nje ya lango kuu walipokuwa wameketi waandamanaji hao ili kusikiliza risala yao iliyosomwa na Shehe Mohammed Mohammed , ambaye pia alikuwa ni Mratibu na Msemaji wa Maandanano hayo. Katika risala yao, walidai kuwa Serikali ya Tanzania haiwathamini Waislamu wala kujali shida zao , pamoja na sauti za vilio na hivyo kutoa tamko la kuitaka Serikali kuu na Mkoa iwachukulie hatua za kisheria wanafunzi, walimu, watendaji wanaongoza kuleta migogoro ya Kidini Shuleni na sehemu za kazi. Hata hivyo katika mambo yao sita ni kuwa watapambana wenyewe watakapoona wanadhulumiwa katika kutetea haki kwa vile ni wajibu wa waislamu kufanya hivyo na kwamba huo ndiyo msimamo wao wa kuueneza nchini kote hadi pake Serikali itakapoonesha kujali na kudhamini waislamu. Akizungumza baada ya kupokea risala ya madai yao, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Baruani, aliwataka Waislamu hao kuwa watulivu na kwamba Mkuu wa Mkoa mara atakaporejea atakabidhiwa ili kuyapitia na yenye kuhitaji kuchukua hatua zaidi ya kuwasilisha kwa Rais Jakaya Kikwete. Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Rugira, ambaye pamoja na safu yake walijitahidi kuzungunza na baadhi ya viongozi wa Maandamani hayo kuwataka watulize jazba na baada ya kuwasilisha kilio chao aliwataka watawanyike kwa amani na utulivu. Hata hivyo kabla ya kutawanyika walimtaka Kaimu Kamanda huyo wa Polisi, kuwaachia wenzao watatu waliokamatwa kwa madai ya vinara wa maandamano hayo na dai lao lilikubaliwa na kuwawachia Siamini Said, Athuman Seba na mwanamke mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja. Lakini Waislamu hao walitaka Jeshi la Polisi limlipe fidia mmoja wao aliyetambuliwa kwa jina la Mgeni Athumani aliyepasukiwa na bomu sehemu ya kichwani na kusababisha majeraha. Hata hiviyo Waislamu hao mara baada ya kuwasilisha madai yao walitii agizo la kuwataka kutawanyika eneo la Ofisi za Mkuu wa Mkoa na waliodoka kwa amani majira ya saa kumi jioni kurejea kuendelea na shughuli zao nyingine. --- taarifa via blogu ya Lukwangule; picha via blogu za Michuzi (za Dar es Salaam) na JumaMtanda (za Morogoro) Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (wa tano mstari wa mbele kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde, Ikulu, Dar es Salaam, iliyotwaa ubingwa wa Chalenji 1994, Nairobi Kenya. Katika picha hii wamo pia wanahabari walioripoti fainali hizo. Kutoka kushoto mstari wa mbele ni; Mpigapicha Richard Mwaikenda (gazeti la Mfanyakazi ambaye kwa sasa ni Mpiga picha Mkuu wa gazeti la JamboLeo na Mmiliki wa BLOGU YA KAMANDA WA MATUKIO), Steven Kuwayawaya, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi, aliyekuwa Waziri wa Elimu na Michezo, Profesa Phillemon Sarungi, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Tanzania (TFF), Muhidin Ndolanga, Marehemu Moses Nnauye wa CCM, aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa Daily News na Muhidin Issa Michuzi (sasa ni Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais). Mstari wa katikati kutoka kushoto ni; John Hokororo (gazeti la Majira), aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Makame Rashid, James Nhende (aliyekuwa Mhariri wa Michezo gazeti la Mfanyakazi),aliyekuwa mwandishi wa habari za michezo gazeti la Uhuru, Godfrey Lutego (hivi sasa ni Mkuu wa Kitengo cha Matangazo gazeti la Jambo Leo), Japhet Sanga (alikuwa mwandishi wa gazeti la Daily News), aliyekuwa Meneja Usambazaji wa gazeti la Mfanyakazi, Richard Ndasa (sasa ni Mbunge wa Sumve, aliyekuwa Katibu Mkuu wa FAT, Ali Mwanakatwe, Aliyekuwa Mpiga picha wa Mfanyakazi, Deus Mhagale (sasa ni mpiga picha wa gazeti la Mtanzania), aliyekuwa Mhariri wa Michezo wa Daily News na Katibu Mkuu wa Kamati hiyo, Stephen Rweikiza na aliyekuwa Mpig apicha wa gazeti la Mfanyakazi, Joseph Senga (sasa ni Mpigapicha Mkuu wa Tanzania Daima). Wengine msitari wa nyuma kutoka kushoto ni; Mwandishi wa habari Msangi na Evarist Mwitumba ambaye ni Mhariri Mkuu wa gazeti la This Day . picha via blogu ya "Kamanda wa Matukio" Richard Mwaikenda Mpiga picha amepiga picha hii akiwa amesimama eneo la Hippo Camp, Mloka nje kidogo ya pori la akiba la Selous kipindi hicho hali ya kina cha maji kwenye mto Rufiji ilikuwa sio ya kuridhisha kabisa. Sehemu kubwa ya mto ilikuwa imekauka na kuacha visiwa vya mchanga. Kwa picha zaidi za maeneo ya utalii, mbuga za wanyama zuru blogu ya TembeaTz
Tafadhali bofya namba katika kisanduku cha picha ili kuona picha mbalimbali zinazotamatia na Rais akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Regia Mtema huko Ifakara leo, Januari 18, 2012.--- * Makundi yakaribia kupigana, * Makani aanguka, * Kafulila ashangiliwa, * Mbowe aisema Serikali Makundi mawili ya wanachama wa CHADEMA yanayopingana, jana nusura yazichape kavukavu yalipokuwa katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya chama hicho, Regia Mtema huko Ifakara, kutokana na chuki na makovu ya uchaguzi wa wa ndani wa chama hicho wa mwaka 2010. Wakati hayo yakitokea huko Ifakara, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alitumia fursa aliyopewa wakati wa kuaga mwili wa mbunge huyo kuipiga vijembe Serikali huku Mwenyekiti Mstaafu wa chama hicho, Bob Makani akianguka ghafla. Marehemu Regia ambaye alifariki dunia Jumamosi iliyopita kwa ajali ya gari iliyotokea Ruvu, Pwani, unatarajiwa kuzikwa leo Ifakara. Katika tukio la Ifakara, mgogoro baina ya kambi mbili zilizotokana na makovu ya uchaguzi huo wa ndani kati ya wafuasi wa marehemu na ya Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Kiwanga ulisababisha kutimuliwa msibani hapo kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kilombero, Salum Ngozi. Ilielezwa kwamba baada ya Ngozi kufika msibani hapo juzi majira ya saa moja usiku na kusalimiana na viongozi wa Serikali, alifuatwa na baadhi ya makada wa chama hicho wakimtaka aondoke eneo hilo jambo ambalo aliligomea. Wafuasi hao wa CHADEMA waliamua kutumia nguvu kumwondoa hali iliyowalazimu polisi waliokuwa eneo hilo kuingilia kati. Askari walimtoa mwenyekiti huyo na kumpeleka katika Kituo cha Polisi Wilaya. Hiyo ilikuwa mara ya pili kwa Ngozi kutimuliwa katika msiba huo. Mara ya kwanza ilikuwa juzi na kumlazimu Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Francis Miti kuingilia kati. Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Ngozi alikiri kutokea vurugu hizo msibani na kudai kwamba, alifanyiwa fujo na kikundi cha watu aliowaita wahuni na kwamba amefungua kesi ya kufanyiwa vurugu katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kilombero na kwamba baada ya kumalizika kwa mazishi atasimamia suala hilo ili haki itendeke. Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe mbali na kukiri kuufahamu mgogoro huo, alisema asingependa kuzungumzia suala hilo sasa wakati watu bado wanaendelea na msiba. Mzee Makani aanguka Hata hivyo hafla hiyo iliingia dosari baada ya Makani kuanguka muda mfupi baada ya kuuaga mwili wa marehemu. Baada ya tukio hilo, alibebwa na kupelekwa pembeni ambako alipepewa kwa takriban dakika tano kisha kurejea katika hali yake ya kawaida na kurudi kwenye kiti chake. Baadaye Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia ambaye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakimpatia Mzee Makani huduma ya kwanza aliwaambia waandishi wa habari kuwa alianguka baada ya kuishiwa nguvu ghafla, “Sasa anaendelea vizuri na amerudi kushiriki kumuaga mpendwa wetu katika safari yake hii ya mwisho,” alisema Mbatia. Mbowe aipiga vijembe Serikali Jijini Dar es Salaam, tukio la kuaga mwili wa marehemu Regia liligeuka jukwaa la siasa baada ya Mbowe na Makinda kupiga siasa. Mbowe alitumia msiba huo kutoa dukuduku lake juu ya shughuli za chama chake kisiasa na kiutendaji wakati akitoa salaam za rambirambi kwa marehemu.Mbowe aliirushia kombora Serikali na vyama vingine vya upinzani kuhusu mwenendo wa CHADEMA kuendesha siasa katika vyuo vya elimu ya juu akisema ni mpango maalumu kuwanoa wanasiasa mahiri. Aliishauri Serikali na vyama vingine vya siasa kuiga utaratibu huo wa CHADEMA akisema unasaidia kukuza vipaji na kuwaandaa viongozi makini kwa kuwapa nafasi vijana kushiriki katika uongozi, “Kuna jambo moja ambalo ningependa Serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vingine walitafakari na wasilibeze hili. Viongozi huandaliwa na viongozi makini hawazuki tu,” alisema na kuongeza; “Naeleza hivyo maana mara nyingi tumekuwa hatueleweki na tumekuwa tukibezwa. Sisi tunatambua viongozi wa baadaye kisha tunakuza vipaji na kutoa fursa za nafasi za uongozi kwa vijana.” “Vijana lazima waandaliwe kimaadili na ndiyo maana tuliingia vyuo vikuu lakini tukatafsiriwa kuwa ni wakorofi na wachochezi wa vurugu. Lakini leo tumepata viongozi wazuri vijana kwa njia hiyo kutoka vyuoni kama vile Mheshimiwa Zitto (Zuberi Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini), Mnyika (John Mbunge wa Ubungo, Mdee (Halima-Mbunge wa Kawe), Silinde (David Mbunge wa Mbozi) na Mtema (Regia Marehemu). “Hawa tuliwaandaa, hawakuzuka. Rai yangu kwa Serikali na kwa wazazi ni kwamba vijana hawa wakifanya siasa tusiwakwaze na kuwafukuza, bali tuwalee.” Spika Makinda katika kile kilichoonekana kama ni kumjibu Mbowe, alitumia fursa hiyo kufafanua uendeshaji wa shughuli za Bunge akisisitiza kwamba linaendeshwa kwa kanuni na wala si kufurahisha watu. Alimsifia marehemu Mtema kwamba alikuwa akizijua vyema kanuni za Bunge: “Bunge huendeshwa kwa kanuni na si kwa matakwa tu ya kufurahisha watu. Yeye marehemu alizijua kanuni ndiyo maana hata wakati alipokuwa akikosea alikuwa tayari kuomba radhi.” Kafulila ashangiliwa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila jana alishangiliwa kwa makofi baada ya kutangazwa kuwa mmoja wa wabunge walioteuliwa na Ofisi ya Bunge kuwamo katika msafara kusindikiza msiba huo akiwakilisha chama chake. Baada ya kiongozi wa shughuli hiyo, Ofisa Mwandamizi wa Ofisi ya Bunge, Saidi Yakub kumtaja Kafulila baadhi ya waombolezaji walishangilia kwa makofi, vicheko vya chini kwa chini na minong’ono ya hapa na pale. Hatua hiyo ya waombolezaji inatokana na hali ya kisiasa ilivyo kati ya Kafulila na chama chake hicho ambacho mwishoni mwa mwaka jana kilitangaza kumvua uanachama hatua ambayo ameipinga mahakamani. Kama ikitekelezwa, itamvua ubunge. --- Habari via gazeti Mwananchi, picha via MjengwaBlog, Richard Mwaikenda blog, MoDewji blog na Nyakasagani blog. Picha nyingine unaweza kuziona katika Michuzi-Matukio blog Nadhani kazi anayoifanya Isaac Kireti kama inavyoonekana kwenye picha hizo hapo, ni nzuri na sahihi kwa kutia changamoto na kuhamasisha umma kuyatunza mazingira ya maeneo wanamoishi na kufanyia shughuli zao za kila siku. Inaonekana kama vile anaifanya kazi bila usaidizi hali watu wameketi wengine wakiwa wameshika tama, wengine kuikunja mikono katikati ya miguu na kusimama mbali kabisa kana kwamba kinachofanyika ni kituko. Pengine wana sababu, sijui. Ninachodhani ni kuwa, mambo mengine hufanywa na watu wenye akili za tofauti na ingawaje huwa vigumu kueleweka wakati huo, matunda ya kazi hiyo yakiwa mema, hukubalina na kuonekana yenye manufaa baadaye sana ama pengine na kizazi kingine kabisa. Shughuli nyingine ili zifanikiwe, inahitaji mtu mmoja mwenye nia na azma kwanza, ili kulishawishi kundi kubwa. Pongezi kwa juhudi hii ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira! Kwa hili nakuunga mkono! "Tears cannot explain it. This kid will be walking a total of 22miles with a heavy load on her head. 4 gallons of water, and that's all she can offer her family in exchange for missing her classes. God Save us, please recommend the page to your friends." - The John Mashaka Foundation. "I am trying to build a water pumping station. It will cost roughly $475,000. That's expensive but will be worth it. Still putting together the necessary resources. If you go to the website www.mashakafoundation.org you will see the picture of the tower." - The John Mashaka Foundation | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |









RSS Feed