Pengine alikuwa ana njaa. Majani akayaona mtini. Uwezo wa kukwea mtini akayale hanao. Ila ipo pikipiki pale. Nijaribu...

Eti 'mbuzi hana akili?' Labda unayemfahamu tu, si wote!
 
 
Shukurani kwa picha: Evans (Dar es Salaam) blogu za GSengo (Mwanza) na Juma Mtanda (Morogoro)
 
 
Rais Kikwete amefika jijini Tanga leo Jumatatu, Aprili 30, 2012 na kulakiwa na mamia ya wakazi wa jiji hilo pamoja na Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyaakzi Tanzania (TUCTA) Bw Nicholaus Mgaya.

Rais yupo jijini humo kwa maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi ambapo atakuwa mgeni rasmi wa Sherehe hizo.

picha: Ikulu
 
 
tungekuwa na dhamira na stamina ii hii katika kila jambo la maana tunalolifanya maishani, badala ya visingizio...!

Picture
licha ya mvua kunyesha wakati fulani, mashabiki hawakukubali kuondoka bila kumuona mwanamuziki "Diamond"
 
 
Wangu Moudy an'tumia ujumbe us'buhi ya leo asema,  

"Leo mvua inakunya sana hapa jijini Tanga, mifereji ya maji inaharisha na kutapika maji huku radi zikijamba na kurindimisha mashuzi ya miale mikali."

Imetosha kunipa taarifa za hali ya hewa ilivyo kwetu Ko'gwe na kuleee Bustanini na mitaa ya Barabara ya ....

Hizi ni picha zinazoonesha hali ya hewa jijini Daresalama asubuhi ya leo.  
Picha zote, shukrani kwa Dkt. V. Mahamba, via PorojoClub aka PiCii.

...linganisha na inavyoonekana Daresalama siku nyingine

Ama kwa hakika mabadiliko ya majira yamewadia... Kipindi: Jiografia! Somo la leo: Vipindi vinne vya majira ya mwaka.
 
 
Jana usiku katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam kulifanyika mpambano wa kuwania ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka (Morogoro) na Mada Maugo (Dar es Salaam).

Pambano hilo lilikuwa la raundi 12 lakini ilipofika raundi ya sita kabla ya kuanza raundi ya saba, Maugo alitangaza kutokuendelea na mchezo kwa kile alichodai kuishiwa na pumzi na kusema, '...sirudi, jmaa ataniua...' huku akivua "gloves" na hivyo kumpa Cheka kwa Technical Knock Out "TKO", uamuzi ambao ulimpa Cheka mkanda wa Ubingwa wa IBF  pamoja na gari (pichani).

Furaha ya ushindi huo imegeuka huzuni leo baada ya Cheka kupata ajali ya gari hilo alilokabidhiwa jana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, akizungumza na "SufianiMafoto" alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea jana usiku majira ya saa nane maeneo ya Manzese na kuwajeruhi dereva na abiria wake waliokuwa katika pikipiki hiyo. Alisema baada ya ajali, dereva wa gari hilo lenye namba za usajili T 321 AAU, aliyefahamika kwa jina la Francis Cheka, alifikishwa kituo cha Polisi cha Oysterbay na kushikiliwa hadi asubuhi ya leo walipofika ndugu zake na kumwekea dhamana. 

Akielezea tukio hilo la ajali, Kenyela alisema kuwa gari la Cheka lilikuwa likitokea maeneo ya Manzese kuelekea Ubungo na pikipiki ilikuwa ikitokea Ubungo kuelekea Manzese na walipofika maeneo ya Tip Top Manzese, dereva wa pikipiki alihamia barabara ya pili ili kuelekea Ubungo na ndipo alipogongana na gari hilo. Aidha alisema kuwa dereva huyo wa pikipiki bado amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala akiendelea na matibabu huku abiria wake akitibiwa usiku wa jana na kuruhusiwa.  

cheka jerry slaa
Cheka akivishwa mkanda wa ushindi wa IBF (picha: superdboxingcoach.blogspot.com)
Picture
Meya wa Manspaa ya Ilala Jery Slaa akimkabidhi funguo ya gari bondia Francis Cheka baada ya kuibuka na ubingwa wa K.O raundi ya 6 jana
Picture
Gari na Mkanda siku chache kabla ya mpambano (picha: superdboxingcoach.blogspot.com)
Picture
Gari baada ya mpambano na ushindi
 
 
Bila shaka ni wengi tumepita humu miongo kadhaa iliyopita, na bado wengi wanapita mumo humo huenda kwa miongo mingine mingi ijayo, ikiwa hatutaishi kwa vitendo maneno yetu yaliyojaa mafikara na ahadi nzuri.

 
 
Wanafunzi wa kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu cha Dodoma, UDOM, wameibuka na ushindi wa vikapu 58 dhidi ya 53 vya Dodoma Spurs (Timu ya Mkoa) katika mchezo wa mpira wa kikapu wa ligi ya mpira wa kikapu inayoendelea kufanyika katika viwanja vya Kitivo Cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha cha chuo hicho.

Picha na maelezo kutoka kwa Josephat Lukaza/ osephatlukaza.blogspot.com 

 
 
Ikiwa ulipitwa kusikiliza taarifa iliyozungumzia hukumu ya kesi ya Tundu Lissu, bofya hapa kurejea toleo lililotangulia.
Picture
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki CHADEMA,Tundu Lissu, akilia muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kanda ya Dodoma, kutupilia mbali mashitaka yaliyotolewa kupinga watokeo yaliyompa ushindi wa Ubunge.
Picture
Mbunge wa Viti maalum Kataru, Manyara, Rose Kamili (karibu na Lissu) alia pia
Picture
Lissu akifutwa machozi na mkewe (picha zote zimepigwa na Nathaniel Limu via: dewjiblog.com)
 
 
Picture
Shuka lenye matangazo ya huduma ya mganga wa kieyeji nje ya nyumba yake katika mji wa Small Sefoda huko Mashariki mwa Sierra Leone, kama lilivyonaswa tarehe 22 Aprili 2012. Kama ilivyo kwa nchi nyingi zinazoendelea, huduma duni za afya zinawanyima wananchi fursa ya kuhudhuria hospitalini na hivyo kulazimika kutafuta tiba mbadala kwa waganga. (picha: Finbarr O'Reilly/Reuters)