Nahodha wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars), Sophia Mwasikili ameondoka Tanzania alfairi ya Januari 30, 2011 kwa ndege ya Turkish Airlines kwenda Uturuki kucheza mpira wa kulipwa. Mwasikili ataichezea "Lüleburgaz Gücü Kulübü" inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ya Wanawake nchini humo. Mchezaji huyo kiungo wa kati wa Twiga Stars aliyekuwa akichezea timu ya Sayari Women amejiunga na klabu yake hiyo mpya kwa mkataba wa miaka miwili. Awali Mwasikili alitakiwa kujiunga mapema na timu hiyo lakini alilazimika kusubiri kwanza mechi ya marudiano ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Twiga Stars na Namibia (Brave Gladiators) iliyochezwa Januari 29 mwaka huu. 1 Comment ![]() Clotilde Drogba, Mama yake Didier Wakati mshambuliaji wa Ivory Coast Didier Drogba akiwa uwanjani, mama yake anawapikia chakula mashabiki wa nchi yake katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Clotilde Drogba amefungua mgahawa karibu na uwanja wa mpira katika viunga vya mji mkuu wa Equatorial Guinea, Malabo, limeripoti shirika la habari la AP. Mama huyo anapika kuku na samaki na wali, ndizi na vyakula vingine kwa ajili ya mashabiki, wakati mwanaye akila chakula cha hoteli aliyofikia pamoja na wachezaji wenzake. Mama yake Drogba pia alipika chakula kwa ajili ya mashabki wakati wa Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani. Drogba ni mmoja wa watu maarufu sana nchini Ivory Coast, na mwaka jana alijumuishwa katika Tume ya Ukweli na Maridhiano iliyoundwa ili kupunguza mvutano uliotokana na utata wa matokeo ya uchaguzi na miaka mingi ya mgawanyiko. Kundi la mashabiki wapatao 60 limesafiri kwenda Equatorial Guinea, ambapo Ivory Coast inacheza mechi zake za awali, na kila siku mashabiki hao wanapata chakula chao cha asili kilichopikwa na mama wa mshambuliaji wao mashuhuri. "Kila mtu anafanya anachopenda kukifanya," Amesema mama yake Drogba, huku akiwa amevalia nguo za rangi ya chungwa ambayo huvaliwa na Ivory Coast. "Hii sio kwa sababu ya mwanangu, ni kwa sababu ya kuunga mkono taifa langu." Mama yake Drogba aliiambia AP kuwa alitazama mechi za ufunguzi kupitia televisheni huku akiwa anakata nyanya na vitunguu na kupika kuku. Amesema ana imani ya kutazama mechi ya nusu fainali kwenye uwanja wa Bata - iwapo Drogba na timu yake watafuzu. Amesema anaheshimu sheria, na hiyo ina maana kuwa mwanaye hawezi kula chakula chake wakati huu - anatakiwa kula chakula cha hotelini tu kwa mujibu wa utararibu. Mama yake Drogba ameiambia AP kuwa ana uhakika atamuona mwanaye akilibeba Kombe la Mataifa ya Afrika. (chanzo cha taarifa) Tanzania (Twiga Stars) 5:2 Namibia 29/01/2012
Wanasema kama Jumapili ya leo hukupata fursa ya kutizama mechi kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Namibia, basi umekosa burudani ya aina yake kwani mechi ilikuwa ya kusisimua hasa goli la 3 la Twiga Stars, wanaliita "classic goal". Nilimsikiliza Sued Mwinyi akisimulia mechi hii kupitia redio TBC, nikatamani ningekuwepo kiwanjani. Ukitaka kusikia sehemu ya simulizi, bofya vipande vya audio vilivyopachikwa hapo chini. Ilikuwa ni mechi kati ya timu ya soka ya wanawake Taifa, Twiga Stars dhidi ya wa Namibia katika kuwania kufuzu kushiriki fainali za soka kwa Mataifa ya Afrika. Mechi hiyo ya marudiano ilifanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Hadi kipindi cha kwanza kinaisha, kila timu ilitoka kiwanjani ikiwa na mabao mawili, kisha Taifa Stars wakapata bao la tatu dakika ya mwanzo tu ya kipindi cha pili. Mabao mawili zaidi yalipatikana dakika ya 86 na 90+. Bao la Namibia la dakika ya 29 lilitokana na mlinzi wa Twiga, Etoe Mlenzi, kujifunga mwenyewe. Bao lao la pili lilifungwa dakika ya 73 na Juliana Skrywer. Wafungaji kwa Taifa Stars walikuwa Mwanahamisi Omari dakika ya 21 na 88 na Asha Rashid dakika ya 46, 88 na 90. Kwa hivyo hadi mwisho wa mchezo, Twiga Stars ilifungasha kibindoni mabao 5 na Namibia 2. Katika mechi ya awali Twiga Stars waliwafunga Namibia 2:0 huko kwao. Tunasubiri kujua tutacheza na nani kati ya Misri na Ethiopia wanaocheza baadaye leo. Pongezi za dhati timu inayofanya vyema ikilinganishwa na maandalizi hafifu inayopewa dhidi ya timu nyingine. Twiga - Fatuma Omary, Fatuma Bushiri, Pulkaria Charaji/Mwajuma Abdallah (52), Fatuma Khatib ‘Foe’, Sophia Mwasikili (nahodha), Mwapewa Mtumwa, Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’, Etoe Mlenzi, Fatuma Mustafa, Asha Rashid ‘Mwalala’ na Fadhila Hamad. Namibia - Susanna Eises, Uerikondjera Kasaona, Lovisa Mulunga, Esther Amukwaya, Stacey Naris, Alberta Dakies/Juliana Skrywer (69), Shirley Cloete, Leticia Manga, Thomalina Adams, Elmarie Frederick and Lydia Eixas. Sehemu ya sauti ikisimuliwa na Sued Mwinyi/TBC moja kwa moja toka kiwanjani katika mechi ya Tanzania na Namibia Busara Promotions makes two announcements concerning two artists scheduled to perform at Sauti za Busara 2012. We are confident all other artists as announced on our website www.busaramusic.org will perform as scheduled. Lady Jaydee Cancels Sauti za Busara Show Lady Jaydee will sadly not be able to perform at Sauti za Busara 2012 due to health reasons. Her eagerly anticipated return to Sauti za Busara since 2006 was scheduled for Thursday 9thFebruary. Festival organisers wish Lady Jaydee a very swift recovery and will soon announce who will take to the stage as headline artist. A statement from her manager Gardner G. Habesh was received today: “As much as Lady Jaydee wanted to be a part of this year's Sauti za Busara, I regret to report that she is sick and her doctor advised that she must have a bed rest for not less than three months before she resume her daily activities. Lady Jaydee will not be seen on any show for the said period.” Yusuf Mahmoud, Festival Director, responded: “We wish Lady Jaydee a speedy recovery back to health. Lady Jaydee is one of Tanzania’s best loved artists. We and our audiences will miss her greatly at the opening night. Of course she is irreplaceable, but we hope soon to announce who will headline for this night.” Passing Away of Seven Survivor Band Leader, Juma Mpogo Busara Promotions is deeply shocked and saddened by passing on of Seven Survivor band leader Juma Mpogo a.k.a. General Lupozi. Juma died Sunday 22nd January. He is survived his wife and two children. He was lead composer, vocalist and keyboard player for theband. Seven Survivor is one of Dar es Salaam's leading exponents playing mchiriku, a style of music that has been extremely popular around disadvantaged areas of Dar es Salaam, Coastal and Morogoro regions for more than twenty years. The band has confirmed their participation despite the absence of their deceased band leader and will battle Jagwa Music Saturday 11thFebruary at the festival for the best mchiriku group title popularly known as Nani Zaidi? About Sauti za Busara Sauti za Busara provides a platform for local musicians to experience music from other parts of Africa, whilst introducing East African music to the visitors. In any society this kind of interchange is vital to the health and development of musical styles. Sauti za Busara provides an example of an event designed to develop, for locals and visitors, an appreciation of the uniqueness, wealth and diversity of music from the region. It shows there is beauty in our traditional music, with employment and income to be gained in sustaining it. Artistic and technical workshops and seminars have been a key element of Busara’s activities, aimed for musicians, media professionals, arts managers, technicians and cultural workers from the region. These workshops have helped to build knowledge and skills for the long-term cultural benefit of East Africa. Festival Sponsors Sauti za Busara music festival, 8 - 12 February 2012 is powered by: The Norwegian Embassy, HIVOS, Mimeta, Roskilde Festival Charity Society, Grand Malt, Toyota, Commercial Bank of Africa, Goethe Institut, US Embassy, African Leisure Centre, fly540, Memories, Zanzibar Grand Palace Hotel, Maru Maru Hotel, SMOLE II, Zanlink, Azam Marine, Embassy of France, ZanAir, fROOTS, Times FM, Multi-Color Printers, Ultimate Security, Tabasam Tours, , Emerson Spice, Monsoon Restaurant, Southern Sun Dar es Salaam, Mercury's, Archipelago Restaurant, Stone Town Café, www.zanzibar.net More Information: www.busaramusic.org Contact: press@busara.or.tz Photo Galleries www.busaramusic.org/SzB2011pics; www.busaramusic.org/SzB2010pics (Hi-res photos available for media on request) TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) sasa imenyoosha makucha yake michezoni kwa kuivalia njuga kashfa ya upangaji wa matokeo ya mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya Simba na Yanga. Jaribio hilo la kupanga matokeo lilifanyika siku chache kabla Simba na Yanga hazijakutana katika mechi ya mzunguko wa Kwanza Tanzania Bara iliyofanyika Oktoba 29, 2011 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika mechi hiyo Yanga ilishinda 1-0. Habari za uchunguzi zinaeleza kwamba tayari Takukuru imekwishawahoji watu kadhaa akiwemo kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa Simba (jina linahifadhiwa) na wachezaji wa Yanga, wiki iliyopita. Msemaji wa Takukuru, Doreen Kapwani, alithibitisha kuwa suala hilo lilikuwa mezani kwao ingawa hakutaka kuingia kwa undani kuhusiana na uchunguzi wao. “Suala hilo lipo mikononi mwetu linafanyiwa kazi, upelelezi ukikamilika tutatoa tamko,” alisema. Vyanzo vya habari vinaeleza kwamba upelelezi unamlenga zaidi kiongozi huyo wa Simba anayedaiwa kumpigia simu mshambuliaji wa Yanga, Pius Kisambale, siku chache kabla ya pambano lao wakati Yanga ikiwa kambini kwenye Hoteli Double Tree iliyoko Masaki, jijini Dar es Salaam. Taarifa zinasema, wakati Kisambale anapigiwa simu alikuwa na baadhi ya viongozi wa Yanga na kwamba simu hiyo iliwashtua viongozi hao, hivyo kumfanya mchezaji huyo aongeze sauti ili nao wasikie kilichozungumzwa. Shuhuda wa tukio hilo anaeleza kwamba mshambuliaji huyo alirekodi maneno ya kiongozi huyo mzito wa Simba, kitendo ambacho pia kilifanywa na viongozi waliokuwa wamemzingira. Katika mazungumzo hayo, inaelezwa kwamba kiongozi huyo wa Simba alimtaka Kisambale acheze chini ya kiwango ikiwa atapangwa na kuahidi kumpatia ‘mzigo’ huku akimwomba awaeleze na wenzake juu ya mpango huo. Hali hiyo inaelezwa kuwakasirisha viongozi wa Yanga walioamua kulipeleka suala hilo Takukuru ili mhusika achukuliwe hatua za kisheria. Taarifa zaidi zinasema wiki iliyopita Takukuru ilimhoji Kisambale na wachezaji kadhaa wa Yanga katika ofisi yao iliyoko Upanga jijini dare s Salaam. Mbali ya Kisambale, kiongozi huyo wa Simba pia amehojiwa na Takukuru kuhusu kashfa hiyo inayoonyesha kukubuhu kwa vitendo vya rushwa michezoni kiasi cha kuporomosha kandanda nchini. “Rushwa imetawala michezoni na watu wanalichukulia kama shamba la bibi bila kujali namna kiwango cha michezo kinavyoporomoka. Sasa watu wamechoka,” kilisema chanzo hicho. Kisambale aligoma kuzungumzia suala hilo na kusema hafamu chochote, huku Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa akiruka kimanga na kusema hawezi kulizungumzia. “Siwezi kuzungumzia,nendeni mkamuulize huyo kiongozi wa Simba mwenyewe, mambo haya yako kwenye vyombo vya sheria,” alisema. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa upelelezi umehusisha mawasiliano mbalimbali ya simu kati ya wachezaji wa Yanga na kigogo huyo wa Simba huku taarifa nyingine zikiongeza kwamba hata mawasiliano baina ya kiongozi huyo na baadhi ya waandishi wa habari za michezo nayo yanachunguzwa. Mbali ya suala hilo, Takukuru pia inadaiwa kuchunguza kashfa inayomhusisha mshambuliaji wa Simba Ulimboka Mwakingwe aliyetaka kumhonga kipa wa zamani wa Mtibwa, Shabaan Kado katika msimu wa 2010/2011. Ulimboka alikamatwa na walinzi wa kiwanda cha sukari Mtibwa akiwa na fedha zinazodaiwa zilikuwa rushwa kwenda kwa Kado ili aachie mabao katika mechi yao ya Ligi Kuu. Vyanzo vya habari vinasema tayari Kado anayeidakia Yanga kwa sasa, amekwishahojiwa na Takukuru, ingawa mwenyewe amegoma kuzungumzia kilichoendelea kwenye mahojiano hayo. Matokeo ya uchunguzi huo yanaweza kubadili sura ya soka la Tanzania ambalo kwa miaka kadhaa limekumbwa na kashfa nyingi za rushwa, upangaji wa matokeo na uamuzi mbovu, hasa likizihusisha timu za Simba na Yanga. Yeyote atakayepatikana na hatia anaweza kuadhibiwa kwa... bofya hapa kumalizia habari hii katika tovuti ya Fikra Pevu Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (wa tano mstari wa mbele kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde, Ikulu, Dar es Salaam, iliyotwaa ubingwa wa Chalenji 1994, Nairobi Kenya. Katika picha hii wamo pia wanahabari walioripoti fainali hizo. Kutoka kushoto mstari wa mbele ni; Mpigapicha Richard Mwaikenda (gazeti la Mfanyakazi ambaye kwa sasa ni Mpiga picha Mkuu wa gazeti la JamboLeo na Mmiliki wa BLOGU YA KAMANDA WA MATUKIO), Steven Kuwayawaya, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi, aliyekuwa Waziri wa Elimu na Michezo, Profesa Phillemon Sarungi, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Tanzania (TFF), Muhidin Ndolanga, Marehemu Moses Nnauye wa CCM, aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa Daily News na Muhidin Issa Michuzi (sasa ni Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais). Mstari wa katikati kutoka kushoto ni; John Hokororo (gazeti la Majira), aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Makame Rashid, James Nhende (aliyekuwa Mhariri wa Michezo gazeti la Mfanyakazi),aliyekuwa mwandishi wa habari za michezo gazeti la Uhuru, Godfrey Lutego (hivi sasa ni Mkuu wa Kitengo cha Matangazo gazeti la Jambo Leo), Japhet Sanga (alikuwa mwandishi wa gazeti la Daily News), aliyekuwa Meneja Usambazaji wa gazeti la Mfanyakazi, Richard Ndasa (sasa ni Mbunge wa Sumve, aliyekuwa Katibu Mkuu wa FAT, Ali Mwanakatwe, Aliyekuwa Mpiga picha wa Mfanyakazi, Deus Mhagale (sasa ni mpiga picha wa gazeti la Mtanzania), aliyekuwa Mhariri wa Michezo wa Daily News na Katibu Mkuu wa Kamati hiyo, Stephen Rweikiza na aliyekuwa Mpig apicha wa gazeti la Mfanyakazi, Joseph Senga (sasa ni Mpigapicha Mkuu wa Tanzania Daima). Wengine msitari wa nyuma kutoka kushoto ni; Mwandishi wa habari Msangi na Evarist Mwitumba ambaye ni Mhariri Mkuu wa gazeti la This Day . picha via blogu ya "Kamanda wa Matukio" Richard Mwaikenda Kwa masikitiko makubwa sana, uongozi wa timu ya African Lyon Fc inapenda kuwaeleza watanzania hususani wapenzi wa mpira wa miguu kuwa, katika jitihada zote za timu yetu ya kukuza na kuedeleza soka hapa nchini, Tumekuwa na mahusiani MABAYA SANA na chama cha mpira wa miguu yaani TFF. Napenda kuweka wazi bila kificho chochote kuwa TFF imekua ikitukandamiza na kutuchafua mbele ya jamii kwa makusudi. Tena ni kana kwamba si mtu mmoja ndani ya TFF bali ni kuwa agenda ya TFF nzima. Kuanzia kwa Rais wa shirikisho kamati ya mtendaji, kamati ndogondogo na pia sekretarieti cha kusikitisha kama si kufurahisha mpaka kwa walinzi wa milangoni siku za mechi. Napenda nitoe baadhi ya mifano michache ambayo tunakutana nayo katika jitihada zao za kutuyumbisha pamoja na vilio vyetu vya kila siku. i. RATIBA YA LIGI KUU. Timu zote ambazo zimekua zikienda kucheza mechi kanda ya ziwa zimekuwa zikicheza mechi zote mbili(yaani kucheza na Toto Fc na Kagera sugar). Kitu ambacho African Lyon Fc chini ya uongozi wetu hatujawahi kukutana nacho. Nakama hiyo haitoshi mechi yetu ya mwisho wanatupeleka Manungu Turiani kucheza dhidi ya JKT Ruvu na hali sisi na JKT uwanja wetu ni Chamazi alafu wenyeji wa Turiani (mwenye Uwanja wao) Mtibwa wanapelekwa Morogoro kucheza dhidi ya Moro United. Ni vigezo vipi vilivyowekwa kutupeleka sisi na si Simba wala Yanga. Je hii TFF ni ya Simba na Yanga tu. ii. MBWANA SAMATA Ndugu watanzania, Tumeandika barua zaidi ya 15 kwa sekretarieti,kamati ya haki ya wachezaji, Raisi Tenga. Lakini hakuna yeyote aliyezungumzia jinsi ambavyo Simba imegushi uhamisho wa Mbwana Samatta kutoka African Lyon Fc. Cha kushangaza ndugu Alex Mgongolwa ambaye pamoja na kupelekewa barua yetu TFF ofisini kwake,kaibuka na timu ya Kimbangulila Fc na African Lyon tumeachwa bila hata kusikilizwa. Napenda kumlaumu kwa nguvu zote ndugu Alex Mgongolwa kwa makusudi yake kabisa tena kwa kukusudia ya kugoma kukaa na sisi na kutisikiliza. Na kwa dharau yake ya kushindwa hata kutujibu japo moja ya barua zetu. Na kwa kuonyesha chuki za wazi kwetu ni pale ambapo aligoma kukutana na WAFADHILI wetu aliokuja kutoka Marekani na Uarabuni kutaka kujua maswala haya hususani ya MBWANA SAMATTA. Hawa ni watu waliotumia fedha na mda wao kuja nchini kwetu alafu mtu anagoma. Na si yeye tu aliyegoma hata uongozi wa juu wa TFF uligoma kukutana nao ili hali hawa wote walipata taarifa wiki moja kabla juu ya ujio wa wageni hawa. iii. YUSUFU SOKA TFF kupitia kwa kaimu Katibu mkuu wake bwana Sunday Kayuni na wakala waliamua kumpeleka Sweden mtaja hapo juu na tunasikia kuwa hivi sasa yupo Jela. Tunalaani na tunaomba vyombo vya dola viingilie kati na sheria ichukue mkondo wake vielelezo vya mchezaji alivyoondoka na wahusika wa safari yake tunavyo. iv. TIKETI ZA MILIONI 35 Mwaka 2009 TFF walituomba tuwaletee tiketi toka Marekani zenye thamani ya shilingi milioni 40 na wakaturudishia tiketi za shilingi milioni 5 zilizobakia baada ya kutumia katika mechi kadhaa hivyo kwa sasa tunawadi milioni 35. Tiketi zenyewe zilitumiwa kwa mechi mbalimbali zikiwemo za Kilimanjaro Taifa Cup na Kagame cup. TFF wamekuwa mara kwa mara wanatoa ahadi hewa juu ya malipo yetu. Hii inatufanya tuzidi kuamini kuwa TFF haina nia nzuri na timu yetu African Lyon Fc. Tunaomba tulipwe. v. SWALA LA KASSIM DEWJI TFF nathubutu kusema kuwa haiko makini kwa jambo lolote lile hapa nchini, baada ya sisi kununua timu 2009/2010. Timu yetu ilipata zawadi ya sh.milioni 5 kama timu yenye nidhamu bora cha kushangaza kaimu Katibu mkuu ndugu Sunday Kayuni alimuandikia hundi kwa jina la Kassim Dewji,huku akijuafika kuwa sisi ndio tunaomiliki timu, na hata kama angekuwa yeye ni mmiliki bado jina lingekuwa ni la timu na sio la mtu binafsi. Kuna uwezekano mkubwa sana hela hizo viongozi wa juu kabisa wamegawana na ndio maana wanalikingia kifua. Tunataka hela zetu, hii ni haki ya wachezaji.Ni nidhamu gani aliyoonyesha uwanjani Kassim Dewji mpaka apewe yeye? vi. FEDHA ZA VODACOM 2010 – 2011 Jamani hadi leo hii tumepokea shilingi 3.5 milioni tu. Je wenzetu wote wamepewa hivyo? Vodacom wanajua? Halafu wanataka bado tuvae jezi za Vodacom ambao udhamini wao ni wa hela ya mboga. TFF wanajipaka matope na aibu iwakute kwa wizi wa mchana kweupe. TAMKO LA AFRICAN LYON African Lyon Fc kwa nguvu zetu zote na tunapenda tuelewe kuwa TFF ina mpango madhubuti wa kuishusha timu yetu daraja kama si kuiondoa kwenye ramani ya soka. Hivyo basi tunatoa siku 30 kwa TFF kukutana nasi na kuzungumzia matatizo yetu na kama ikishindikana basi sisi tunajitoa kwenye ligi pasipo kujali chochote. Asante sana. Kwa maelezo zaidi wasiliana: Sherally Abdallah Hammed 0759 302496 --- [via shaffihdauda.com] Madonna and Elton John became embroiled in a war of words at the Golden Globes on Sunday as they competed in the Best Song category. John started the verbal spat by telling reporters on the red carpet that his rival "doesn't have a f------ chance of winning tonight," and when asked if those were "fighting words," he replied, "No, those are accurate words." Madonna hit back when questioned about John's remarks, asking reporters, "Was he wearing a dress?" adding, "May the best man win." Madonna emerged triumphant as her song "Masterpiece" from "W.E." scooped up the award for Best Original Song over John's "Hello, Hello" from "Gnomeo & Juliet." After her win, Madonna offered an olive branch to her rival, telling reporters backstage, "I hope he speaks to me for the next couple of years. He's known to get mad at me. He's brilliant and I adore him, so he will win another award. And I don't feel bad!" But shortly after Madonna's name was called, David Furnish, John's husband, wrote on his Facebook page: "Madonna. Best song???? F--- off!!! ... Madonna winning Best Original Song truly shows how these awards have nothing to do with merit. Her acceptance speech was embarrassing in its narcissism." "And her criticism of Gaga shows how desperate she really is," he added, referring to Madonna's recent comments about the pop star. Bing: Madonna 'Born This Way' controversy Photos: See all the 2012 Golden Globe winners Source: tv.msn.com ![]() Balotelli katika picha na wanafunzi wa shule hiyo (picha: metro.co.uk) Mcheza soka wa klabu ya Manchester City ya Uingereza mwenye vituko vingi akiwa ndani na nje ya kiwanja amefanya jambo ambalo katika jamii nyingine lingeweza kuwa la kawaida ila kwa jamii nyingine limeonekana kituko. Pengine ni kutokana na wingi wa vituko visivyotabirika vya nyota huyo na wasaka habari wanaopenda kufuatilia nyendo zake ili kupata cha kuandika na kuuza, ama yeye mwenyewe na asili ya uchokozi na utani. Hivi karibuni Balotelli aliegesha gari lake karibu na shule kisha kwenda shuleni hapo kuuliza na kuomba ikiwa angeweza kutumia msala wao. Soma zaidi kisa chenyewe kinavyosimuliwa na espn.go.com Mario Balotelli gave students of a college in Manchester a day to remember after turning up unannounced and asking if he could use their toilet. The eccentric Manchester City striker has entertained English football fans and media alike with his unpredictable behaviour, which has previously included driving into a women's prison, throwing darts at youth team players and reportedly giving a homeless person £1000 after a successful night at a casino. For his latest trick, Balotelli parked up his Bentley at Xaverian College in Rusholme and went into the canteen to ask students if there was anywhere he could relieve himself. After using the toilet he spoke with teachers in the staff room and then walked around the college being followed by hordes of excited Manchester City fans before leaving 20 minutes after he had first arrived. "Xaverian was delighted to receive a surprise visit from Mario, who chatted to some of the students at one of Manchester's most successful colleges," a spokesman for the college said. "We weren't able to enrol him on any courses, but he is welcome back anytime." A number of understandably thrilled students were quoted in the Manchester Evening News, including Edward Gasson, who was sitting in the canteen when Balotelli turned up. "Balotelli parked his Bentley outside then came in and was asking where the toilets were, then he went to the teacher's staff room," he said. "After that he was just walking round campus like he owned the place and everyone was following him around. "I'm a City fan so it was amazing to see him but it was a bit ridiculous for him to come here - you would never expect it to happen. Timu ya soka inayopewa maandalizi hafifu lakini inayojitahidi kufa na kuponae, leo chezo wake wa kusaka nafasi ya kushiriki kinyang'anyiro cha mataifa ya Afrika kwa soka la wanawake, Twiga Stars imefanya vyema katika mechi yake dhidi ya Namibia baada ya kupata ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya timu ya Gladiators ya Namibia. Mchezo huo ulifanyika mjini Windhoek, Namibia na marudio yanatarajiwa kufanyika wiki chache zijazo. Wafungaji wa magoli ya Twiga Stars walikuwa ni Asha Rashid na Mwanahamis Omar. --- Gladiators disappoint against Tanzania Namibia’s Brave Gladiators let in two soft goals in a disappointing 2-0 defeat against Tanzania in their Women’s African Champions Cup qualifying match in Windhoek on Saturday afternoon. The first goal was a shocker - a freekick by Tanzanian striker Asha Rashid that floated high over Namibian keeper Susanna Eises into the goals on 64m, while Omary Mwanahamisi broke through the defence to beat Eises from close range in the 87th minute. Namibia now have a mountain to climb as they will have to score at least three goals in the away leg in a fortnight’s time to go through to the next round. Namibia did most of the attacking with especially Thomalina Adams showing a lot of pace down the right wing. On 22m, Juliana Skrywer latched onto an Adams cross but her shot was well saved by the Tanzanian keeper, Fatuma Omaryjawadu. Two minutes later Adams was once again the provider but this time Skrywer could only manage a weak header which was easily saved. At the end of the first half, Tanzania’s keeper did well to keep out a Namibian corner, while at the other end Namibian keeper Eises saved well at the feet of Mwanahamisi. Namibia continued to create chances in the second half but they could not put them away. A freekick by Shirley Cloete was well saved while Stella Williams came close with a header. Tanzania took the lead against the run of play when they won a freekick on the left flank and Rashid sent in a cross that flew over Eises’ head into the back of the net. Iina Katuta, who came on for Lorraine Jossob missed an open goal on 68m when she shot wide at the far post with no defender in sight. With time running out, Tanzania once again caught Namibia on the counterattack as Mwanahamisi broke clear of the defence and beat Eises from close range with a low shot into the right hand corner. source: www.namibiasport.com.na | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |







RSS Feed