Hizi ni video zilizowekwa youtube na Shaffih Dauda, endelea kufuatilia habari mpya kwenye chaneli yake youtube.com/shaffihdauda na tovuti yake:  shaffihdauda.com

Hadi sasa sijafanikiwa kupata linki yenye kuonesha mechi hiyo moja kwa moja mtandaoni, ikipatikana nitaiweka hapa. Kwa mechi nyingine za spoti zinazooneshwa moja kwa moja, tembelea ukurasa wa "wavuti.com -Linki" au bofya hapa.


 
 
Kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini Uingereza kimeripoti kuwa hali ya Patrice Muamba, mchezaji wa timu ya soka ya Bolton Wanderers ya nchini humo, ipo katika "stable condition" katika chumba cha wagonjwa walio chini ya uangalizi wa karibu (Intensive Care Unit - ICU) kwenye hospitali ya London Chest Hospital alipowahishwa kwa matibabu baada ya kuanguka kiwanjani na kudhaniwa amepatwa na ama mshituko wa moyo "heart attack" ama kifafa "epilepsy".

Alianguka mnano dakika ya 41 ya mechi kati ya timu yake na ile ya Tottenham Hotspurs kwenye kinyang'anyiro cha kombe la FA, siku ya Jumamosi, Machi 17, 2012. Timu hizo zilikuwa zimeshafungana 1-1.

Refarii wa mechi hiyo, Howard Webb aliahirisha mechi hiyo baada ya kushauriana na jopo la wahusika.

Fabrice alizaliwa mwaka 1988 huko mjini Kinshasa, nchini Kongo (Kongo DRC wakati huo ikitambulika kama Zaire). Mwaka 1994, baba yake alitoroka Zaire na kuomba hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza ambapo alikubaliwa na ndipo Patrice alipojiunga na shule na kuanza kufanya vyema katika masomo na mchezo wa mpira wa miguu. Alipatiwa hati ya uraia wa Uingereza na ndipo alipoamua kujiunga na kikosi cha timu ya soka ya Taifa hilo na kuiwakilisha nchi hiyo katika mashindano ya U-19 na U-21, hata kushika cheo cha ukapteni. Amewahi kuzichezea timu za Arsenal na Birmigham City kabla ya kujiunga na Bolton Wanderers. Bofya hapa kusoma historia fupi ya Patrice Muamba.
 
 
Katika kombe la Nedbank 2012, timu ya soka ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imejishangaza yenyewe baada ya kuvunja rekodi ya ushindi pale ilipoifunga timu ya Powerlines ya nchini humo humo magoli 24 kwa nunge!

Kipindi cha kwanza kilitimu kwa magoli 10 na kipindi cha pili kikashuhudia magoli 14 yakichomekwa wavuni.

Magoli yalifungwa na wafuatao (namba zinazotangulia majina yao ni dakika za mchezo ambapo mwenye jina alipachika bao wavuni) : 8'Kekana 12'Henyekane 15'Kekana 20'Henyekane 25'Mushekwi 31'Kekana 41'Mushekwi 43'Mushekwi 45+1'Mushekwi 45+2'Mushekwi 50'Kekana 52'Mushekwi 54'Julies 56'Henyekane 61'Kekana 67'Pelembe 70'Pelembe 71'Mokoena 72'Henyekane 74'Henyekane 76'Julies 78'Kekana 80'Kekana 90+1'Mokoena 
 
 
Picture

Nizar Khalfan's tenure with the Philadelphia Union was cut short, as the midfielder was waived by the team.

The Tanzanian international was called up to his national team this week, but the opportunity to play in an Africa Cup of Nations Qualifying match did not prevent the Union from placing Khalfan on MLS waivers. Khalfan was originally acquired by Philadelphia in November of last year through MLS's Waiver Draft.

Khalfan, 23, was competing for playing time in a crowded midfield, and may have lost his chance of making the Union due to the return of left midfielder Keon Daniel. The Union are currently carrying four other players - Daniel, Gabriel Farfan, Michael Farfan and Jimmy McLaughlin - that naturally play on the outside, leaving Khalfan as unneeded.

The former Vancouver Whitecaps player will seek a place on the sixth team of his career (if both iterations of the Whitecaps are included as a single entity).

The Union now have seven international roster spots open out of nine, but one of those spots will be filled by signing Home Grown Player Christian Hernandez, a source informed the Brotherly Game on Tuesday.

via brotherlygame.com 

 
 
Picture
Football star Aaron Ramsey was being bizarrely linked to Whitney Houston's death by fans last night after a series of odd coincidences.

Every time the Arsenal midfielder scores, a famous figure dies. Whitney was the fourth in under a year.

Her body was found hours after Ramsey, 21, netted during the Premier League game against Sunderland on Saturday.

The coincidences began last May when Ramsey scored against Manchester United. Next day al-Qaeda terror leader Osama Bin Laden was killed.

In October he scored against Spurs, three days before Apple boss Steve Jobs died. 

Later that month he scored against Marseille in the Champions League. Next day Libyan tyrant Colonel Gaddafi was shot.

One fan wrote on a forum: "I'm worried things will get out of control when he scores more."

via TheSun

 
 
Nahodha wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars), Sophia Mwasikili ameondoka Tanzania alfairi ya Januari 30, 2011 kwa ndege ya Turkish Airlines kwenda Uturuki kucheza mpira wa kulipwa.

Mwasikili ataichezea "Lüleburgaz Gücü Kulübü" inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ya Wanawake nchini humo.

Mchezaji huyo kiungo wa kati wa Twiga Stars aliyekuwa akichezea timu ya Sayari Women amejiunga na klabu yake hiyo mpya kwa mkataba wa miaka miwili.

Awali Mwasikili alitakiwa kujiunga mapema na timu hiyo lakini alilazimika kusubiri kwanza mechi ya marudiano ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Twiga Stars na Namibia (Brave Gladiators) iliyochezwa Januari 29 mwaka huu.
 
 
Picture
Clotilde Drogba, Mama yake Didier
Wakati mshambuliaji wa Ivory Coast Didier Drogba akiwa uwanjani, mama yake anawapikia chakula mashabiki wa nchi yake katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. 

Clotilde Drogba amefungua mgahawa karibu na uwanja wa mpira katika viunga vya mji mkuu wa Equatorial Guinea, Malabo, limeripoti shirika la habari la AP. 

Mama huyo anapika kuku na samaki na wali, ndizi na vyakula vingine kwa ajili ya mashabiki, wakati mwanaye akila chakula cha hoteli aliyofikia pamoja na wachezaji wenzake.

Mama yake Drogba pia alipika chakula kwa ajili ya mashabki wakati wa Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani.

Drogba ni mmoja wa watu maarufu sana nchini Ivory Coast, na mwaka jana alijumuishwa katika Tume ya Ukweli na Maridhiano iliyoundwa ili kupunguza mvutano uliotokana na utata wa matokeo ya uchaguzi na miaka mingi ya mgawanyiko.

Kundi la mashabiki wapatao 60 limesafiri kwenda Equatorial Guinea, ambapo Ivory Coast inacheza mechi zake za awali, na kila siku mashabiki hao wanapata chakula chao cha asili kilichopikwa na mama wa mshambuliaji wao mashuhuri.

"Kila mtu anafanya anachopenda kukifanya," Amesema mama yake Drogba, huku akiwa amevalia nguo za rangi ya chungwa ambayo huvaliwa na Ivory Coast.

"Hii sio kwa sababu ya mwanangu, ni kwa sababu ya kuunga mkono taifa langu."

Mama yake Drogba aliiambia AP kuwa alitazama mechi za ufunguzi kupitia televisheni huku akiwa anakata nyanya na vitunguu na kupika kuku.

Amesema ana imani ya kutazama mechi ya nusu fainali kwenye uwanja wa Bata - iwapo Drogba na timu yake watafuzu.

Amesema anaheshimu sheria, na hiyo ina maana kuwa mwanaye hawezi kula chakula chake wakati huu - anatakiwa kula chakula cha hotelini tu kwa mujibu wa utararibu.

Mama yake Drogba ameiambia AP kuwa ana uhakika atamuona mwanaye akilibeba Kombe la Mataifa ya Afrika.

(chanzo cha taarifa)

 
 
Wanasema kama Jumapili ya leo hukupata fursa ya kutizama mechi kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Namibia, basi umekosa burudani ya aina yake kwani mechi ilikuwa ya kusisimua hasa goli la 3 la Twiga Stars, wanaliita "classic goal". 

Nilimsikiliza Sued Mwinyi akisimulia mechi hii kupitia redio TBC, nikatamani ningekuwepo kiwanjani. Ukitaka kusikia sehemu ya simulizi, bofya vipande vya audio vilivyopachikwa hapo chini.

Ilikuwa ni mechi kati ya timu ya soka ya wanawake Taifa, Twiga Stars dhidi ya wa Namibia katika kuwania kufuzu kushiriki fainali za soka kwa Mataifa ya Afrika. Mechi hiyo ya marudiano ilifanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Hadi kipindi cha kwanza kinaisha, kila timu ilitoka kiwanjani ikiwa na mabao mawili, kisha Taifa Stars wakapata bao la tatu dakika ya mwanzo tu ya kipindi cha pili. Mabao mawili zaidi yalipatikana dakika ya 86 na 90+.

Bao la Namibia la dakika ya 29 lilitokana na mlinzi wa Twiga, Etoe Mlenzi, kujifunga mwenyewe. Bao lao la pili lilifungwa dakika ya 73 na Juliana Skrywer.

Wafungaji kwa Taifa Stars walikuwa Mwanahamisi Omari dakika ya 21 na 88 na Asha Rashid dakika ya 46, 88 na 90.

Kwa hivyo hadi mwisho wa mchezo, Twiga Stars ilifungasha kibindoni mabao 5 na Namibia 2.

Katika mechi ya awali Twiga Stars waliwafunga Namibia 2:0 huko kwao. 

Tunasubiri kujua tutacheza na nani kati ya Misri na Ethiopia wanaocheza baadaye leo.

Pongezi za dhati timu inayofanya vyema ikilinganishwa na maandalizi hafifu inayopewa dhidi ya timu nyingine.

Twiga - Fatuma Omary, Fatuma Bushiri, Pulkaria Charaji/Mwajuma Abdallah (52), Fatuma Khatib ‘Foe’, Sophia Mwasikili (nahodha), Mwapewa Mtumwa, Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’, Etoe Mlenzi, Fatuma Mustafa, Asha Rashid ‘Mwalala’ na Fadhila Hamad.

Namibia - Susanna Eises, Uerikondjera Kasaona, Lovisa Mulunga, Esther Amukwaya, Stacey Naris, Alberta Dakies/Juliana Skrywer (69), Shirley Cloete, Leticia Manga, Thomalina Adams, Elmarie Frederick and Lydia Eixas.

Sehemu ya sauti ikisimuliwa na Sued Mwinyi/TBC moja kwa moja toka kiwanjani katika mechi ya Tanzania na Namibia
 
 
Busara Promotions makes two announcements concerning two artists scheduled to perform at Sauti za Busara 2012. We are confident all other artists as announced on our website www.busaramusic.org will perform as scheduled.

Lady Jaydee Cancels Sauti za Busara Show

Lady Jaydee will sadly not be able to perform at Sauti za Busara 2012 due to health reasons. Her eagerly anticipated return to Sauti za Busara since 2006 was scheduled for Thursday 9thFebruary. Festival organisers wish Lady Jaydee a very swift recovery and will soon announce who will take to the stage as headline artist.

A statement from her manager Gardner G. Habesh was received today: “As much as Lady Jaydee wanted to be a part of this year's Sauti za Busara, I regret to report that she is sick and her doctor advised that she must have a bed rest for not less than three months before she resume her daily activities. Lady Jaydee will not be seen on any show for the said 
period.”

Yusuf Mahmoud, Festival Director, responded: “We wish Lady Jaydee a speedy recovery back to health. Lady Jaydee is one of Tanzania’s best loved artists. We and our audiences will miss her greatly at the opening night. Of course she is irreplaceable, but we hope soon to announce who will headline for this night.”

Passing Away of Seven Survivor Band Leader, Juma Mpogo 

Busara Promotions is deeply shocked and saddened by passing on of Seven Survivor band leader Juma Mpogo a.k.a. General Lupozi. Juma died Sunday 22nd January. He is survived his wife and two children. He was lead composer, vocalist and keyboard player for theband. Seven Survivor is one of Dar es Salaam's leading exponents playing mchiriku, a style of music that has been extremely popular around disadvantaged areas of Dar es Salaam, Coastal and Morogoro regions for more than twenty years. The band has confirmed their participation despite the absence of their deceased band leader and will battle Jagwa Music Saturday 11thFebruary at the festival for the best mchiriku group title popularly known as Nani Zaidi?   

About Sauti za Busara

Sauti za Busara provides a platform for local musicians to experience music from other parts of Africa, whilst introducing East African music to the visitors. In any society this kind of interchange is vital to the health and development of musical styles. Sauti za Busara provides an example of an event designed to develop, for locals and visitors, an appreciation of the uniqueness, wealth and diversity of music from the region. It shows there is beauty in our traditional music, with employment and income to be gained in sustaining it.

Artistic and technical workshops and seminars have been a key element of Busara’s activities, aimed for musicians, media professionals, arts managers, technicians and cultural workers from the region. These workshops have helped to build knowledge and skills for the long-term cultural benefit of East Africa.

Festival Sponsors
Sauti za Busara music festival, 8 - 12 February 2012 is powered by: The Norwegian Embassy, HIVOS, Mimeta, Roskilde Festival Charity Society, Grand Malt, Toyota, Commercial Bank of Africa, Goethe Institut, US Embassy, African Leisure Centre, fly540, Memories, Zanzibar Grand Palace Hotel, Maru Maru Hotel, SMOLE II, Zanlink, Azam Marine, Embassy of France, ZanAir, fROOTS, Times FM, Multi-Color Printers, Ultimate Security, Tabasam Tours, , Emerson Spice, Monsoon Restaurant, Southern Sun Dar es Salaam, Mercury's, Archipelago Restaurant, Stone Town Café, www.zanzibar.net

More Information: www.busaramusic.org
Contact: press@busara.or.tz

Photo Galleries
www.busaramusic.org/SzB2011picswww.busaramusic.org/SzB2010pics (Hi-res photos available for media on request)
 
 
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) sasa imenyoosha makucha yake michezoni kwa kuivalia njuga kashfa ya upangaji wa matokeo ya mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya Simba na Yanga.

Jaribio hilo la kupanga matokeo lilifanyika siku chache kabla Simba na Yanga hazijakutana katika mechi ya mzunguko wa Kwanza Tanzania Bara iliyofanyika Oktoba 29, 2011 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika mechi hiyo Yanga ilishinda 1-0.

Habari za uchunguzi zinaeleza kwamba tayari Takukuru imekwishawahoji watu kadhaa akiwemo kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa Simba (jina linahifadhiwa) na wachezaji wa Yanga, wiki iliyopita.

Msemaji wa Takukuru, Doreen Kapwani, alithibitisha kuwa suala hilo lilikuwa mezani kwao ingawa hakutaka kuingia kwa undani kuhusiana na uchunguzi wao.
“Suala hilo lipo mikononi mwetu linafanyiwa kazi, upelelezi ukikamilika tutatoa tamko,” alisema.

Vyanzo vya habari vinaeleza kwamba upelelezi unamlenga zaidi kiongozi huyo wa Simba anayedaiwa kumpigia simu mshambuliaji wa Yanga, Pius Kisambale, siku chache kabla ya pambano lao wakati Yanga ikiwa kambini kwenye Hoteli Double Tree iliyoko Masaki, jijini Dar es Salaam.

Taarifa zinasema, wakati Kisambale anapigiwa simu alikuwa na baadhi ya viongozi wa Yanga na kwamba simu hiyo iliwashtua viongozi hao, hivyo kumfanya mchezaji huyo aongeze sauti ili nao wasikie kilichozungumzwa.

Shuhuda wa tukio hilo anaeleza kwamba mshambuliaji huyo alirekodi maneno ya kiongozi huyo mzito wa Simba, kitendo ambacho pia kilifanywa na viongozi waliokuwa wamemzingira.

Katika mazungumzo hayo, inaelezwa kwamba kiongozi huyo wa Simba alimtaka Kisambale acheze chini ya kiwango ikiwa atapangwa na kuahidi kumpatia ‘mzigo’ huku akimwomba awaeleze na wenzake juu ya mpango huo.

Hali hiyo inaelezwa kuwakasirisha viongozi wa Yanga walioamua kulipeleka suala hilo Takukuru ili mhusika achukuliwe hatua za kisheria.

Taarifa zaidi zinasema wiki iliyopita Takukuru ilimhoji Kisambale na wachezaji kadhaa wa Yanga katika ofisi yao iliyoko Upanga jijini dare s Salaam.

Mbali ya Kisambale, kiongozi huyo wa Simba pia amehojiwa na Takukuru kuhusu kashfa hiyo inayoonyesha kukubuhu kwa vitendo vya rushwa michezoni kiasi cha kuporomosha kandanda nchini.

“Rushwa imetawala michezoni na watu wanalichukulia kama shamba la bibi bila kujali namna kiwango cha michezo kinavyoporomoka. Sasa watu wamechoka,” kilisema chanzo hicho.

Kisambale aligoma kuzungumzia suala hilo na kusema hafamu chochote, huku Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa akiruka kimanga na kusema hawezi kulizungumzia.

“Siwezi kuzungumzia,nendeni mkamuulize huyo kiongozi wa Simba mwenyewe, mambo haya yako kwenye vyombo vya sheria,” alisema.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa upelelezi umehusisha mawasiliano mbalimbali ya simu kati ya wachezaji wa Yanga na kigogo huyo wa Simba huku taarifa nyingine zikiongeza kwamba hata mawasiliano baina ya kiongozi huyo na baadhi ya waandishi wa habari za michezo nayo yanachunguzwa.

Mbali ya suala hilo, Takukuru pia inadaiwa kuchunguza kashfa inayomhusisha mshambuliaji wa Simba Ulimboka Mwakingwe aliyetaka kumhonga kipa wa zamani wa Mtibwa, Shabaan Kado katika msimu wa 2010/2011.

Ulimboka alikamatwa na walinzi wa kiwanda cha sukari Mtibwa akiwa na fedha zinazodaiwa zilikuwa rushwa kwenda kwa Kado ili aachie mabao katika mechi yao ya Ligi Kuu.

Vyanzo vya habari vinasema tayari Kado anayeidakia Yanga kwa sasa, amekwishahojiwa na Takukuru, ingawa mwenyewe amegoma kuzungumzia kilichoendelea kwenye mahojiano hayo.

Matokeo ya uchunguzi huo yanaweza kubadili sura ya soka la Tanzania ambalo kwa miaka kadhaa limekumbwa na kashfa nyingi za rushwa, upangaji wa matokeo na uamuzi mbovu, hasa likizihusisha timu za Simba na Yanga.

Yeyote atakayepatikana na hatia anaweza kuadhibiwa kwa... bofya hapa kumalizia habari hii katika tovuti ya Fikra Pevu