Tamko toka Ikulu kukanusha taarifa za Mwananchi/The Citizen kuhusu Rais kubariki posho za Wabunge 31/01/2012
Gazeti la Mwananchi la leo, Jumanne, Januari 31, 2012 limeandika habari zenye kichwa cha habari – JK abariki posho mpya za Wabunge: Kila mmoja kulipwa sh 330,000 kwa siku. Habari hizi siyo za kweli na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inataka kutoa ufafanuzi ufuatao: Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi. Maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo: Kwanza, Mheshimiwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hili. Pili, Mheshimiwa Rais Kikwete amewataka Wabunge kutumia Kikao cha sasa cha Bunge kulizungumza upya suala hilo. Mwisho. Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu. Dar es Salaam. 31 Januari, 2012 (source) 10 Comments Nimeanzisha tovuti hii ya Elimu na Habari za Utafiti wa Afya ili kuwapa mwanga watanzania nini kinachoendelea duniani. Katika tovuti hii pia Mwananchi anaweza kutuma Maswali yakajibiwa na wataalamu wa afya (nikiwemo mimi mwenyewe) kwa ufasaha. Jina: Marafiki wa Afya Site Admin: Kahabi G Isangula Link: www.friendsoflifetz.org Kwa kutuma maswali: friendsoflifetz.org/ushauri-wa-afya Facebook inapatikana kama: Marafiki wa Afya STATEMENT FROM SAVE LAMU ORGANISATION Today the Minister of Lands, Orengo and yesterday the PS of Transport, Dr. Cyrus Njiru downplayed the plight of the people of Lamu over the Lamu Port-Southern Sudan-Ethiopia Transport (LAPSSET) Corridor. They keep ignoring that Lamu people are not only demanding land rights and are not against the lamu port but asking for transparency, information, consultation, and mitigation for the whole LAPSSET project. And still keep using the old constitution to violate the land rights of the people of Lamu. Yesterdays comments by Mr. Orengo that the Lamu people are squatters on GOK land so the port must go on since they are squatters on GOK land were therefore very arrogant.... http://youtu.be/SrIwY3eLKkg. The new constitution clearly states that there is no government land but only Public land. In article 62(2) it says: "Public land shall vest in and be held by a county government in trust for the people resident in the county, and shall be administered on their behalf by the National Land Commission..." Since we have no County government yet and their is no National Land commission, they think the land is theirs automatically yet the constitution is very clear that the County government is holding it in trust for US not the GOK. Why can't they wait till we have our county government is in place to start the project? Why an't they rush to create the National Land Comission Bill before tehy carry out the port?? Because they want to steal while they still can just like Kilindini... WAKE UP TO THE REALITY PEOPLE!! So people of Pwani, people of Kenya, I ask you to wake up to their clear arrogance. They want to marginalize the people of Lamu the same way the people of Mombasa were with the Kilindini port. The same way they took Masaai land and converted it into national parks without benefit-sharing. Today, the Kilindini port is closed and run down after all of them pocketed their own money. And the people of Mombasa... not even a house or title to show for it. The Masaai the same. When will the people of Pwani and Kenya as a whole join forces against this clear oppression? Tumechoka! Nimechoka! The new constitution is very clear. It must be followed!! No excuses. No ifs. No buts! February 8th, 2012 is the court date for the port case in Malindi... www.savelamu.org... I say my dear friends, we should show them that while the people of Lamu may be weak, the people of Pwani are a force to reckon with and the people of Kenya are a BIGGER force to reckon with!! No more corruption, no more oppression... a port but with information, consultation, and mitigation!! Prof. Mbele anasema, Mwaka 2002 nilisajili kampuni katika jimbo la Minnesota ambayo niliita Africonexion. Nilichagua aina ya usajili iitwayo "sole proprietorship" yaani mmiliki na mhusika mkuu ni mimi. Nilianzisha Africonexion kama chombo cha kushughulikia elimu kuhusu tamaduni duniani, kwa kuandika, kuchapisha, na kuuza vitabu, na kutoa mihadhara na ushauri kwa watu binafsi, mashirika, taasisi, makampuni, na kadhalika, kama ninavyoripoti katika blogu zangu. Africonexion ni kampuni ndogo sana kwa wakati huu, kwa maana kwamba sina timu ya wafanyakazi au washiriki. Lakini nimeitumia vizuri kama fursa ya kujielimisha, kwa kuzingatia kuwa elimu ni mtaji bora kuliko hata fedha. Shughuli zote ninazofanya, iwe ni kuandika au kutoa mihadhara au ushauri kwa watu binafsi, ni kama shule kwangu. Nimejifunza mengi sana, na bado najifunza. Maelezo na picha vimenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Profesa Mbele. Unaweza kupata maelezo zaidi ya kampuni hii kwenye tovuti ya africonexion.com au kwenye blogu yake ya hapakwetu.blogspot.com au wasiliana naye kupitia barua pepe: info@africonexion.com Serikali ya Sudan imesema iko tayari kuleta madaktari ili wasaidie kutoa mafunzo kwa madaktari wa Tanzania hasa kwenye fani ya upasuaji wa moyo (Open Heart Surgery). Hayo yamesemwa leo mchana (Ijumaa, Januari 27, 2012) na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dk. Yassir Mohamed Ali wakati alipofika kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam. Balozi huyo alimweleza Waziri Mkuu kwamba wamekwishaanza mazungumzo na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kuona utekelezaji wa suala hilo. Alisema pia wanaangalia uwezekano wa kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Kitanzania kwenye eneo la uzalishaji nishati na umeme. Kwa upande wake, Waziri Mkuu alimshukuru Balozi huyo na kumuahidi kufuatilia suala la uanzishwaji wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission -JPC) ili maamuzi yanayofikiwa yaweze kuwa na mfumo maalum wa ufuatiliaji. Aliiomba nchi hiyo iisaidie Tanzania kufundisha pia wataalamu wa kilimo cha umwagiliaji maji kama njia ya kuinua uzalishaji wa mazao nchini. Alimweleza Balozi huyo kwamba akiwa Arusha wiki iliyopita, alibaini kuwa Chuo cha Ufundi Arushs (ATC) kinakabiliwa na wakufunzi na wataalamu na akaiomba nchi hiyo isaidie kufundisha mafundi sanifu wa umwagiliaji (irrigation technicians) kwa vile imebobea kwenye kilimo cha umwagiliaji kwa muda mrefu sana. Mapema leo, Waziri Mkuu alikutana na Balozi mpya wa Japan, Bw. Masaki Okada na kujadiliana naye masuala mbalimbali yakiwemo ya uendelezaji kilimo, miundombinu na miradi ya maji. Aliishukuru Serikali ya Japan kwa kuwatuma wakufunzi wawili kwenye Chuo cha Ufundi cha Arusha lakini akatumia fursa hiyo kuomba wataalamu zaidi ili wasaidie kuongeza idadi ya kada ya chini ya wataalamu wa miundimbinu ya umwagiliaji. “Tunataka kuongeza idadi ya watalaamu wa kilimo cha umwagiliaji maji hasa mafundi sanifu kwa sababu ndiyo wanaohitajika kujenga miundombinu ya umwagiliaji… tumedhamiria kuinua kilimo chetu na hatuna budi kuandaa wataalamu wa kutosha,” alisema. Aliishukuru Serikali ya Japan kwa misaada ambayo imeipatia Tanzania kwa kipindi chote cha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU, S. L. P. 3021, DAR ES SALAAM. IJUMAA, JANUARI 27, 2012 Swahili interpreter needed, If possible would actually need one for today. Call Maria Mayer Trippett of Compass Languages Production (410)451-4298 www.compasslanguages.com Source: diasporamessenger.com/i MAELEZO YA WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII, MHE. DKT. HADJI HUSSEIN MPONDA (B) KUHUSU HOJA ZA MADAKTARI TAREHE 26/01/2012 Utangulizi: Uongozi wa Wizara umekuwa ukifanya vikao mbalimbali na Viongozi wahusika wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) katika kutatua suala la Madaktari wanaofanya mazoezi kwa vitendo (internship) na hatimaye suala hili kumalizika. Baadaye MAT waliwasilisha Hoja nane za ziada Tarehe 21/01/2012. Wizara ilifanya mkutano na Uongozi wa Chama cha Madaktari kujadili hoja zilizowasilishwa. Wizara ilitoa maelezo kama ifuatavyo:- Madaktari kupewa nyumba za kuishi karibu na Hospitali
Wizara imefanyia kazi, maboresho ya pohso hiyo ya kuitwa kazini baada ya saa za kazi (On call allowance), na imewasilisha kwa mamlaka husika, kwa ajli ya kupata kibali. Mapendekezo hayo, yanatofautisha posho hiyo kulingana na ngazi za Madaktari na watumishi wengine. Rufaa za wagonjwa (hasa viongozi) wanaopelekwa kutibiwa nje ya nchi Malalamiko ya Madktari ni kwamba baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na wa Serikali hushinikiza Daktari anayewahudumia awape rufaa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi hata kwa magonjwa yanayoweza kutibiwa hapa nchini. Maelezo ya Wizara ni kwamba Wizara hugharamia matibabu nje ya nchi kwa Watanzania wote bila kujali hali zao za kijamii au kisiasa ili mradi vigezo vimetimizwa. Wizara hupokea rufaa za wagonjwa hao, ambazo zimetokana na ushauri wa Jopo la Madaktari bingwa wa fani husika wasiopungua watatu. Madaktari hao baada ya kuwachunguza wagonjwa na kuamua kuwa wanahitaji rufaa huandika majina yao na fani zao katika fomu za rufaa husika. Madaktari hao wana uhuru wa kuandika katika fomu ya rufaa kama mgonjwa anastahili kupelekwa nje ya nchi au anaweza kutibiwa hapa nchini na kwa hiyo hamna ulazima wa kumpelekea nje ya nchi. Hata hivyo katika kipindi cha miezi mitatu (Oktoba hadi Desemba 2011) jumla ya Wagonjwa 223 walienda nje kwa ajli ya matibabu, kati ya hao ni awgonjwa 19 (8.5%) tu walikuwa viongozi wa Serikali na Siasa (Waheshimiwa Wabunge na Viongozi waandamizi Serikalini). Majina kwa ajili ya udhamini wa madaktari wanaochukua mafunzo ya Uzamili Malalamiko ya Madaktari ni kwamba baadhi ya Madaktari waliopata nafasi ya kuchukuwa mafunzo ya Uzamili katika Vyuo mbalimbali kukosa udhamini wa Wizara. Hapo awali ni Madaktari 50 tu kwa mwaka ndiyo walipata udhamini kwa mafunzo ya Uzamili. Baada ya kuanza uktekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM), hapo 2007, idadi hiyo iliongezeka na kufikia Madaktari 300 kwa mwaka. Hii iliwezekana kutokana na Serikali kuwa na fedha za kutosha kutokana na ufadhli wa Benki ya Dunia. Mwaka jana ufadhili huu haukuwepo na hali ya fedha haikuwa nzuri, kiasi kwamba, ilielekezwa kupunguza bajeti. Fedha iliyobaki ilitosha kudhamini Madaktari 50 tu. Wizara inafanya jitihada za kutafuta fedha zkwa ajili ya udhamini wa Madaktari waliokosa udhamini. Tayari baadhi ya Wadau wa Maendeleo wako tayari kwa hili. Kuhamisha Madaktari Bingwa wenye mikataba ya Ajira na Hospitali ya Taifa Muhimbili. Wizara kuwahamisha Madaktari Bingwa iliyoingia nao mkataba wa udhamini wa masomo ya uzamili na wakati huo huo wakiwa na mikataba ya ajira na Hospitali ya Taifa Muhimbili. Wizara imekwisha rekebisha kasoro ya mikataba hiyo. Hospitali ya Taifa Muhimbili tayari inatumia mikataba mipya inayoonesha kuwa daktari akipata ufadhili wa Wizara atapangiwa kutuo kulingana na mahitaji ya taifa. Baada ya Serikali kupandisha hadhi ya hospitali za Mikoa kuwa Hospitali za Rufaa na Mikoa, ni muhimu sana kwa Madaktari Bingwa kwenda kufanya kazi katika hospitali hizo. Daktari Bingwa ndiye anayepaswa kuwa kichocheo cha kuifanya Hospitali husika ipate rasilimali zinazotakiwa (vifaa, watumishi, majengo na fedha). Aidha ataifanya hospitali hiyo itoe huduma zinazotakiwa. Hii ni kulingana na Sera ya Afya na Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM). Mpango Mkakati wa Afya Na. 3 aunaozipandisha hadi Hospitali za Mikoa kuwa Rufaa, ili kuongoza huduma za uningwa karibu na wananchi. Posho ya mazingira hatarishi (Risk Allowance) Hapo awali, Seirkali ilijumuisha posho mbalimbali kwenye mishahara ya watumishi, posho ya mazigira hatarishi ikiwa ni mojawapo ya posho hizo. Hata hivyo, Serikali imetambua umuhimu wa kuzitenganisha posho hizo na mishahara kwa watumishi wa kada za afya wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi. Wizara kwa kushirikiana na mamlaka husika wanalifanyia kazi suala hili. Ajira za Madaktari Wizara imewaajiri Madaktari wote walioomba kuajiriwa. Tatizo kubwa ni kwamba wengi wa Madaktari hao hawaendi kule wanakopangiwa kwa kuwa wanapenda kbaki Dar es Salaam, ambapo hata hivyo nafasi ni chache. Ilikubalika kuwa MAT na vyama vingine vya kitaaluma viwe ni wadau katika kutoa taarifa kwa Madaktari na Wataalamu wengine kuhusu kuwepo kwa nafasi za ajira za Madaktari. Aidha Serikali imekuwa ikiongeza nafasi za ajira za watumishi wa kada za Afya kutoka nafasi 1,677 mwaka 2005/2008 hadi kufikia nafasi 9.391 kwa mwaka wa fedha 2011/2012. Kutaka Mshahara wa Shilingi Milioni 3.5 kwa mwezi: Mishahara ya watumishi wa Serikali, hufuata Miundo ya Utumishi (Scheme of Service) iliyopo. Aisha, serikali imeboresha muundo wa watumishi wa sekta ya afya. Baada ya kuboreshwa kwa muundo huo, kwa hivi sasa, Watumishi wa afya wanapata mishahara mikubwa kuliko watumishi wengine serikalini. Wito kwa Madkatari walio katika mgomo
Samahani ikiwa kuna herufi/maneno yaliyokosewa kwani nimelinukuu tamko kwa maandishi kutoka kwenye picha, unaweza kuzibofya kuzikuza. Ukitaka nakala tafadhali ipakue kwa kubofya hapa au hapa. Wale samaki waliopotea kama vile mboju, nshonzi, mpala, ningu, nkuyu n.k, sasa waweza kuwapata toka kwa ndugu KAZAURA kwa simu namba +255787315665. Kilo moja ni Shilingi 6500/= Pia vinapatikana yakula vya asili kama viazi vikuu, kashuli n.k. Duka lake lipo Sinza, Mori, Dar es Salaam. Wasiliana naye kwa maelezo zaidi. Mtu ni afya. Tupende vya asili! Gazeti la Tanzania Daima la leo, Jumatano, Januari 25, 2012, kwenye ukurasa wake wa kwanza limechapisha habari yenye kichwa cha habari, “Ndege ya JK utata: Iko nje kwa miezi miwili. Serikali yakwama kuilipia.” Miongoni mwa yaliyoandikwa kwenye habari hiyo ni pamoja na “Ukata unaiokabili Serikali umesababisha kukwama kuilipia ndege hiyo maalum ya Rais…Ndege ya Rais mahususi kwa ajili ya safari za namna hiyo imezuiliwa nje baada ya Serikali kukwama kulipia gharama za matengenezo yake…Kutokuwepo kwa ndege hiyo, kumesababisha Rais Kikwete na ujumbe wake wa watu 14, ulioondoka nchini jana kwenda Davous, nchini Sweden kuhudhuria mkutano wa dunia wa uchumi, kuondoka na ndege ya Shirika la Ndege la Qatal”. Limeendelea Gazeti hili la Tanzania Daima kudai kuwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa ndege hiyo ya Rais gharama za safari hiyo ya Rais zimeongezeka na ziara hiyo ya Rais ya siku nne kuhudhuria mkutano huo itagharimu kiasi cha shilingi milioni 300. Aidha, Gazeti hili linadai kuwa mkutano huo hauna tija kwa taifa, kwamba Rais Kikwete amehudhuria mikutano hiyo mara nyingi lakini hakuna faida iliyopatikana kwa taifa. Kwa hakika, maandishi na kauli hizi za ovyo na zisizokuwa za kweli za Gazeti la Tanzania Daima zinalenga kuupotosha umma wa Tanzania bila sababu za msingi na hivyo kuusababishia umma chuki isiyokuwa na msingi kwa Rais. Katika kuuelezea umma ukweli wa safari hiyo ya Mheshimiwa Rais Kikwete tunapenda kutoka ufafanuzi ufuatao: Kwanza, kama tulivyoeleza, kwa usahihi, katika taarifa yetu kwa vyombo vya habari jana jioni, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekwenda katika mji/kijiji cha Davos, nchini Uswisi kuhudhuria Mkutano wa World Economic Forum (WEF) unaoanza leo. Rais Kikwete hakuwenda katika mji wa Davous, nchini Sweden kama linavyosema Gazeti hili. Aidha, Rais Kikwete na ujumbe wake umesafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Qatar na siyo Qatal kama linavyoripoti Tanzania Daima. Pili, Serikali haijakwama, kwa sababu zozote zile, kulipia matengenezo ya kawaida (routine maintenance) ya Ndege ya Rais. Hili limefafanuliwa vizuri na ipasavyo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali, Rubani Kennan Paul Mhaiki jana. Isipokuwa ni vyema kuongeza kuwa matengenezo ya ndege hiyo yalimalizika juzi tu, Jumatatu, Januari 23, mwaka huu, wakati ndege hiyo ilipofanyiwa safari ya majaribio (test flight) kule Savannah, Georgia, Marekani na wala siyo miezi miwili iliyopita kama linavyodai Tanzania Daima. Hivyo, madai kuwa ndege hiyo imezuiliwa nje kwa miezi miwili sasa kwa sababu ya Serikali kushindwa kulipia gharama za matengenezo ni porojo tu zisizokuwa na msingi. Tatu, ni vigumu kujua Gazeti la Tanzania Daima limepata wapi habari kuwa safari hiyo ya siku nne inagharimu kiasi cha sh. milioni 300. Ukweli ni safari ya Mheshimiwa Rais Kikwete na ujumbe wake ni ya siku nane, kama tulivyoeleza jana, ambako atahudhuria mikutano ya WEF na ule wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia atakapowasili Jumamosi, Januari 28, 2021. Hivyo, si kweli kwa Gazeti hili kudai kuwa nauli tu na matumizi ya safari ya Mheshimiwa Rais ni shilingi milioni 300 kwa siku nne tu. Nne, Tanzania Daima linadai kuwa safari za Mheshimiwa Rais mjini Davos hazina tija na wala faida yoyote. Huu pia ni uongo mwingine wa dhahiri wa Gazeti hili. Tunapenda kukumbusha faida chache tu zilizotokana moja kwa moja na Mheshimiwa Rais Kikwete kushiriki mikutano ya WEF kama ifuatavyo: (a) Moja, ni kubuniwa na kupitishwa kwa Mpango Kabambe wa Uendelezaji Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania wa Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT) uliozinduliwa wakati wa WEF mwaka jana. Mpango huu utakaotekelezwa kwa pamoja na sekta binafsi na sekta za umma kwa kushirikisha Serikali ya Tanzania, Mashirika ya Kimataifa, Makampuni ya Kimataifa unalenga kuleta faida zifuatazo: (i) Uwekezaji wa kiasi cha dola za Marekani bilioni 3.4 katika kilimo cha Tanzania na kuongeza uzalishaji wa kilimo hicho mara tatu katika miaka 20 ijayo. (ii) Kuchochea uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara kwenye eneo ya hekta 350,000. (iii) Kutengeneza kiasi cha ajira 420,000 za kudumu. (iv) Kuwatoa kwa namna ya kudumu kiasi cha watu milioni mbili katika umasikini. (v) Kuleta usalama wa kudumu wa chakula kwa kuhakikisha kinapatikana chakula cha kutosha kwa Tanzania na nchi za jirani. (vi) Kuboresha miundombinu ya umwagiliaji, barabara, reli, nishati na bandari katika eneo lote la Mradi wa SAGCOT. (vii) Kuwahakikishia wakulima masoko ya mazao yao, kuwawezesha kupata dhana za kisasa, na kuwaanzishia mifumo ya kisasa ya umwagiliaji. (viii) Kuingizia wakulima mapato ya kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.2 kila mwaka. (Kiasi cha dola za Marekani milioni 50 zinaendelea kuingizwa katika mfuko wa uanzishwaji wa Mpango wa SAGCOT utakaotelekezwa kwa kuanzia katika maeneo ya Sumbawanga (Rukwa), Ihemi na Ludewa (Iringa), Kilombero (Morogoro), Mbarali (Mbeya), na Rufiji (Pwani) (b) Pili, ni uwekezaji kabambe wa kiasi cha dola za Marekani milioni 20 katika mfumo wa upakuaji wa mbolea kwenye Bandari ya Dar es Salaam unaofanywa na Kampuni ya Yara International, moja ya makampuni makubwa zaida ya uzalishaji wa mbolea duniani. Yara International ni mmoja wa washirika wakubwa katika SAGCOT na uwekezaji wake unalenga kuhakikisha kuwa Tanzania na hata majirani wanapata mbolea ya kutosha kwa ajili ya kuimarisha kilimo. (c) Tatu, mikutano ya WEF ni shughuli moja inayomwezesha Kiongozi wa Nchi kukutana na kufanya mazungumzo na wakubwa wote duniani – wawe wa siasa, wa biashara, wa uchumi, wa uwekezaji, wa kijamii – katika jitihada zake za kuitangaza Tanzania kama kituo muhimu cha uwekezaji. Katika siku tatu zijazo, kwa mfano, Mheshimiwa Kikwete miongoni mwa watu wengine atakutana na Bwana Bill Gates wa Bill&Bellinda Foundation, Naibu Waziri wa Uchumi, Nishati na Kilimo wa Marekani Bwana Robert Hormats, Rais wa Benki ya Dunia Bwana Bob Zoellick, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Australia Bwana Kevin Ruud, Mkuu wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani Bwana Raj Shah, Mtendaji Mkuu wa Benki ya ABSA Bi. Maria Ramos, na Waziri Mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra. Tunapenda kumalizia kwa kusisitiza, kwa mara nyingine tena, kuwa ni vyema Gazeti la Tanzania Daima lijiridhishe na usahihi na habari zake kabla ya kuzichapisha kama inavyoelekeza misingi mikuu ya uandishi wa habari na weledi wa kazi hiyo. Uandishi wa habari za uongo unaleta hofu na kuanzisha uzushi usiokuwa na sababu zozote miongoni mwa wananchi na hiyo siyo kazi ya uandishi wa habari. Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM. 25 Januari, 2012 --- (taarifa via blogu ya Lukwangule) MWALIKO WA WADAU KUTOA MAONI KATIKA MUSWADA WA SHERIA MBALIMBALI ZA BIASHARA "THE BUSINESS LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS) ACT, 2011" (PUBLIC HEARING) Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara inawaalika wadau wote kwenye mdahalo wa kupokea maoni kuhusu Muswada wa Sheria Mbalimbali za Biashara "THE BUSINESS LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS) ACT, 2011". Kikao hicho kitafanyika kesho tarehe 26/01/2012 katika Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam kuanzia saa 4.00 asubuhi. Lengo la Muswada huu ni kufanya marekebisho katika Sheria mbalimbali kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania. Sheria zinazopendekezwa kurekebishwa ni:
Nakala za Muswada husika zinapatikana Ofisi ya Bunge iliyopo Mtaa wa Shaaban Robert, Jijini Dar es Salaam, na wahusika wamuone Ndg. Kaboneka (Simu 0755-362852). Karibuni nyote ili tuweze kuboresha Muswada huu. Imetolewa na Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimatifa. DAR ES SALAAM | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |








RSS Feed