TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 


Hivi karibuni chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilielezea kile ilichoeleza kuwa ni kutishwa na wimbi la mauaji yanayotishia amani ya nchi kikidai kuwa jumla ya wanachama wake 15 wameuawa katika wilaya ya Igunga peke yake.

Madai hayo ya CHADEMA, pamoja na wanachama wengine na mashabiki wao, yalitolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, ambaye alidai kuwa mauaji hayo yana mkono wa serikali ya CCM, ambayo kwa madai yao imeona wazi kuwa upepo wa kisiasa umekiendea vibaya na sasa kinataka kujiimarisha katika utawala kwa kuua watu wanaoipinga.

Akifungua kikao cha Baraza Kuu la chama hicho jijini Dar es Salaam Aprili 29 mwaku huu mwenyekiti huyo alifafanua kuwa mbali na kuuawa kwa watu wanne kwa pamoja na juzi kifo cha mwenyekiti wao wa tawi huko Arumeru mkoani Arusha, jumla ya wanachama wake 15 wameuawa katika wilaya ya Igunga peke yake tangu kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo mwaka jana.

Mbowe katika maelezo yake alijaribu katika maeneo kadhaa kuihusisha CCM na au serikali yake katika matukio kadhaa yaliyowakabili baadhi ya wanachama na viongozi wa Chadema katika maeneo mbalimbali nchini likiwemo lile la Mbunge Highness Kiwia ambaye Suala lake bado Lipo mikononi mwa vyombo Vya dola likishughulikiwa.

Katika sehemu kubwa ya maelezo ya Ndg. Mbowe amejitahidi kuonesha kuwa mauaji yote yaliyoikabili na yatakayokuwa yakiikabili Chadema kupitia wafuasi wake yanafanyika kisiasa, Jambo ambalo ni la uzushi, kwani Halina ushahidi wa kisheria hata kimazingira, wa Moja kwa Moja unaoondosha ujinai au makosa hayo, na kuwa ni makosa yanayolenga muktadha wa kisiasa.

Huku akitaka kuuaminisha umma kuwa huo ndio ukweli, Ndg. Mbowe amesisitiza kuwa hilo lime kuwa likitekelezwa na CCM kwa lengo la kuwatisha wananchi kujiunga na chama hicho hoja ambayo haina msingi wowote wa kiutafiti.

Hivyo CCM kwa kutambua kuwa Suala la mauaji linabeba Kosa la jinai, na kwa kuwa Ndg. Mbowe ameshutumu Moja kwa Moja CCM na serikali yake kuihusisha na mauaji hayo, ni vema sasa nasi tukatoa msimamo wetu dhidi ya tuhuma, hiyo.

Kwanza, si busara hata kidogo kuihusisha CCM katika matukio hayo, kwani uchunguzi unaofanywa na vyombo vya dola umeshindwa mpaka sasa kuhusisha matukio hayo na siasa, badala ya kuyahusisha na makosa ya jinai ambayo hufanywa na watu kwa malengo tofauti na yale ambayo Ndg. Mbowe anataka kuwaaminisha watu.

Pili, CCM haijawai, haiwezi, na haitakuja fanya jambo lolote lenye lengo la kuvuruga Amani na Usalama wenye utulivu ndani ya taifa letu, hivyo uzushi na usingiziaji uliofanywa na Mtu Kama Ndg. Mbowe, si vema kuuacha kimya, badala yake nimetumia wasaa Huu muhimu Kujibu, na kutoa ufafanuzi ili Kuupa umma wa watanzania habari sahihi.

Ni aibu kwa Chama kama Chadema kujitahidi kwa nguvu zote kujaribu kuficha ukweli wa mauaji yanayotoa roho za watanzania wenzetu kwa kuyapa sura ya kisiasa. Hizi ni juhudi za makusudi za kutaka kuficha ukweli wa kinachotokea.

Ni aibu kwa chama kama Chadema kujaribu kutumia mauaji mabaya kama haya kutafuta mtaji wa kisiasa. Huku ni kuonyesha jinsi gani wamefilisika kisiasa mpaka wanafikia mahali pa kuamini kuwa wanaweza kutumia chochote kama mtaji wa kisiasa, vikiwemo vifo vya watanzania wenzetu. Huku si kufilisika tu ila kwakweli ni unyama unaotakiwa kulaaniwa na kila muungwana.

Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Ideology and Publicity Secretary

--
via  blogu ya CCMChama
 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua BIBI MWANAHAMISI OMARI KITOGO kuwa MSAIDIZI WA RAIS, HUDUMA ZA JAMII.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue leo, Jumanne, Mei 8, 2012, mjini Dar es Salaam inasema kuwa uteuzi huo umeanza Mei Mosi, mwaka huu, 2012.

Kabla ya uteuzi wake, Bibi Mwanahamisi Omari Kitogo alikuwa Mkadiriaji Ujenzi Msaidizi (Assistant Quantity Surveyor) katika Kampuni ya COWI, Tanzania.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

8 Mei, 2012


 
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Gazeti la kila wiki la Dira ya Mtanzania toleo la leo, Jumatatu, Mei 7, mwaka huu, 2012,  limechapisha habari yenye kichwa cha habari, “Familia ya JK yachafuliwa”.

Katika habari hiyo, Gazeti hili linadai kuwa familia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete inafanya biashara na kampuni ya Home Shopping Centre (HSC) ya Dar es Salaam.

Aidha, Gazeti hili linadai kuwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Bwana Said Saad ndiye msimamizi wa biashara za familia hiyo ya Mheshimiwa Rais.

Tunapenda kuujulisha umma habari hizo si za kweli. Ni uongo unaolenga kuupotosha umma na kuchafua jina la Mheshimiwa Rais Kikwete na familia yake. Na, au vinginevyo unalenga kuchafua jina la Kampuni ya Home Shopping Centre. Kama nia ni kufanya hivyo tafadhali msilitumie jina la familia ya Rais. Mheshimiwa Rais Kikwete haendeshi, hajawahi kuendesha, na wala hana mpango wa kuendesha biashara iwe ni yeye binafsi au na familia yake. Shughuli azipendazo na ambazo anajishughulisha nazo ni kilimo na ufugaji. Kwa ajili hiyo ana mashamba Sanzale, Kiwanga na Msoga. Hata shughuli hizo hazijafikia kiwango cha kibiashara kwani hutumia pesa yake ya mfukoni kugharamia shughuli hizo.

Badala ya kutoa tuhuma za jumla jumla zisizokuwa na ushahidi wowote ni vema muwe wawazi. Ni vema gazeti likaeleza namna gani au likamtaja ni nani ndani ya familia ya Mhe. Rais Kikwete anaendesha biashara kwa kushirikiana na Kampuni ya Home Shopping Centre.

Kwa kufanya hivyo , Gazeti la Dira ya Mtanzania litawathibitishia Watanzania kuhusu ukweli wa habari hizo. Aidha, litaondoa doa baya na chafu linalotaka kuelekezwa kwa Rais na Familia yake. Kitendo hicho hakimtendei haki Rais na Familia yake.

Ni imani yetu kuwa Gazeti hili litatoa majibu ya masuala haya muhimu katika toleo lake lijalo, vinginevyo Familia ya Mheshimiwa Rais itakuwa na haki ya kuchukua hatua stahiki za kisheria. 

Imetolewa na

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, 
Ikulu
Dar es Salaam

7 Mei, 2012
 
 
Mercedes Benz, M-class (ML 350)

Engine type and volume: petrol , 3750 cc

Year of manufacture : 2003

Odometer reading: 63822 (zinaongezeka as the car is not in the warehouse)

Tyres changes a week ago

Serious buyers call 0779484351 (no middle parties!)

 
 
BUSINESS NETWORK INTERNATIONAL (BNI)

BNI is a Business and Professional network Association, with a mission of helping members increase their business through a structured, positive, and professional 'word of mouth' program that enables them to develop longterm, meaningful relationship with quality business professionals.

You are invited to attend the breakfast-networking meeting on Wednesday 16 MAY 2012, 06:30am to 08:30am @ MBEZI GARDEN HOTEL.

This is opportunity for serious entrepreneurs who wants to increase the volume of their businesses thru business referral, to meet and exchange information and contacts.

Meeting fee is only Tsh 10,000.

To comfirm your participation call Dr. Eva on 0783-535202, Dellilah N. Mgaya 0784-706891, Hellen 0713-551391 or Haika 0714-750404
 
 
Nimefurahi kuwa taarifa ya Mwanasheria Mkuu inatoa ufafanuzi wa maswali yale mawili ya jana yaliyokuwa hapa (bofya kuona). Pia sikiliza taarifa ya habari ya TBC ya leo (hapa) iliyosomwa saa mbili usiku kumsia Jaji Werema akitamka kuhusu masuala haya.

Ni jambo jema kuwa Serikali inasikia pia tunaozungumza mitandaoni kwa kuwa wameijumuisha mitandao katika moja ya sehemu ambapo taarifa hizi za mkanganyiko zimekuwa zikisambaa.

Jambo jema sana hili!

---- 

TAARIFA KWA UMMA
___________


Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, tarehe 4 Mei, 2012 alitangaza mabadiliko katika safu ya Baraza la Mawaziri.  Katika uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri, Mheshimiwa Rais aliwateua Mawaziri wapya kutoka miongoni mwa Wabunge aliokuwa amewateua na kuwatangaza.  Baada ya uteuzi huo, kumetolewa maoni kwamba hatua ya Mheshimiwa Rais kuwateua Wabunge Wapya ambao hawajaapishwa Bungeni kuwa Mawaziri ni kitendo cha uvunjaji wa Katiba.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayachukulia maoni haya kama ni jambo lenye maslahi ya jamii na linalohitaji kufafanuliwa; kwa upande mmoja lakini pia, kutolewa kwa elimu ya Umma; kuhusu Mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge. 

Msingi wa Katiba tunaoanza nao ni maelekezo ya masharti yaliyomo kwenye Ibara ya 55(4) kwamba:

“Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka     miongoni mwa Wabunge”

Pili, ni mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge aliyopewa na masharti ya Ibara ya 66(1)(e) yenye aina ya Wabunge wasiozidi kumi watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizotajwa katika aya za (a) na (c) za ibara ya 67 na angalau Wabunge watano kati yao wakiwa Wanawake.  Wabunge aliowateuwa Mheshimiwa Rais wanatokana na Ibara hii.

Tatu, baada ya hatua zote hizi ikumbukwe kwamba aliyeteuliwa au kuchaguliwa kuwa Mbunge anakuwa Mbunge ama baada ya kutangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi; au baada ya kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa wale Wabunge wa viti maalum au anapochaguliwa na Baraza la Wawakilishi au anapoteuliwa na Rais akitumia Mamlaka yake ya uteuzi yanayotokana na Ibara ya 66(1)(e). Hivyo Wabunge wanaohusika hawahitaji kuapishwa kwanza Bungeni ili wawe Wabunge.  Kiapo cha Mbunge Bungeni kinamwezesha tu kushiriki katika shughuli za Bunge. 

Katiba ya nchi haiweki kwa Rais masharti kwamba kabla ya kumteua Mbunge wa aina hiyo kuwa Waziri au Naibu Waziri Mbunge huyo awe ameapishwa Bungeni kwanza.  Masharti mawili muhimu na ya kuzingatia ni kwamba mteule wa nafasi ya uwaziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka kwa mujibu wa Ibara ya 56 ya Katiba, awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.  Sharti la pili, litahusu kiapo cha Uaminifu katika Bunge kabla Mbunge hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge kwa masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba.  Viapo hivyo havitegemeani na vinaweza kufanyika kwa nyakati tofauti.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inasisitiza kwamba Wabunge ambao hawajaapishwa ndani ya Bunge ni Wabunge na wanapoteuliwa kushika nafasi ya Uwaziri au Naibu Waziri ni halali kwa kuwa uteuzi huo haukiuki masharti yoyote ya Kikatiba au Sheria.  Aidha, katika kutekeleza madaraka ya kazi ya Uwaziri au Naibu Waziri Mbunge atahitaji kiapo mbele ya Rais hata kama hajaapishwa Bungeni.  Busara ya uandishi wa Katiba na Sheria imetambua kwamba kunaweza kukatokea uteuzi wa aina hiyo wakati Bunge limeahirishwa kama ilivyo sasa.  Masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba yatazingatiwa katika kikao cha Bunge kijacho.

Bila shaka ufafanuzi huu utaleta uelewa katika jambo hili na kuepusha mikangayiko isiyokuwa ya lazima.

Imetolewa na Jaji Frederick M. Werema (Mb)


MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

06 Mei, 2012
_______________________

 
 
Do you want to study, visit friends, family, attend the Olympic games or be reunified with your family or spouse in the United Kingdom?

T UK Visa consultancy is a company based in Dar-es-Salaam Tanzania that currently provides the following service.
  • Assess the merits of your UK Visa application and advise you on the best course of action
  • Completing the relevant UK visa application form on your behalf
  • Advise on the supporting evidence that you should provide to support your application.
               We cannot guarantee you a visa to the United Kingdom

                 We can guarantee professional service at an affordable rate
               

You can contact us at :  Plot 31, 8th Floor, Social Security House
                                   Azikiwe/ Samora Street
                                   Dar-es-Salaam, Tanzania


                                   Email: info@tukvisaconsultancy.co.tz


                                   Telephone landline: +255222139502

                                   Mobile:+255785317659


                                   Skype: t.ukvisaconsultancy (Please note we can provide advise through Skype upon prior arrangement) 
 
 
Ujumbe ufuatao umetumwa na Richard M.,
---

Wanablog,

Nawataharisha wizi wa kupitia mtandao wa kusafirisha pesa kwa simu za mkononi unaoendelea Dar es Salaam kwa kasi ya ajabu. Watu wengi wamelizwa. Na ukifika huko makao makuu mnajikuta mko wengi mnaolalamika.

 
 
Mbunge wa Ubungo, John Mnykka (CHADEMA) anatupasha katika blogu yake  haya yafuatayo:

Tumemaliza majumuisho ya kesi dhidi yetu. Hukumu imepangwa kutolewa tarehe 24 Mei 2012. Mawakili wote wawili wa upande wa utetezi wametimiza wajibu wao. 

Pamoja na kuwa mawakili kwa ujumla walizungumza kwa zaidi ya saa saba, namnukuu kiduchu Wakili wetu Mbogoro: “Mshindi wa uchaguzi anatokana na maamuzi ya watu wengi, haki ambayo huipata kwa nadra kila baada ya miaka mitano na ni mchakato unaotumia fedha nyingi za walipa kodi. Hivyo kiwango cha uthibitisho wa madai yoyote lazima kiwe bila ya shaka yoyote... mlalamikaji Hawa Ng’umbi amesema mwenyewe mahakamani kuwa hana tatizo na matokeo ya toka vituoni, malalamiko yake sio juu ya nani mshindi. Kwa kawaida kesi za uchaguzi hufunguliwa na wenye kupinga ushindi wanaodai kuwa wangeshinda wao iwapo sheria zisingekiukwa; kama hapingi matokeo ya vituoni ambayo majumuisho yake ndio yamempa Mnyika ushindi; tunaweza kujiuliza tuko hapa kwa ajili gani?” 

Tuungane pamoja katika sala na swala kumwombea kwa Mwenyezi Mungu Jaji Upendo Msuya afanye maamuzi ya haki.
 
 
Anahitajika Mwekezaji wa kujenga jengo la ofisi au hoteli katika mkoa mpya wa Geita.

Kiwanja kipo kandokando ya barabara kuu iendayo Mwanza.

Ardhi ina uwezo wa kujenga jengo la orofa hadi saba.

Ni eneo zuri la kibiashara katika mkoa mpya na linafaa kwa shughuli za kibenki na ofisi nyinginezo.

Kiwanja kipo plot #97
Kitalu C
Kalangala
Geita Mjini

Yeyote mwenye nia ya kuwekeza anakaribishwa.

Wasiliana kupitia simu namba 00 255 78 429 6751