Picha zote ni kwa hisani ya blogu ya Jube Tranquilino 2 Comments Mwana habari mkuu katika habari za jamii kwa njia ya blogu Bw. Muhidin Issa Michuzi anaondoka leo kuelekea London, Uingereza, kuhudhuria kongamano la pili la Watanzania wanaoishi nchi za nje (Diaspora 2 conference) kwa mwaliko maalumu akiwa kama bloga. Bw. Michuzi, ambaye ametoa mchango mkubwa katika kutangazai habari za jamii mtandaoni kupitia blogu yake maarufu ndani na nje ya nchi ya issamichuzi.blogspot.com, amealikwa huko mkutanoni na ubalozi wetu Uingereza ili kutoa mada inayohusu "umuhimu wa habari za jamii mtandaoni" katika kujenga daraja kwa walio ndani na nje ya nchi. ![]() Muhidin Issa Michuzi Taarifa tulizozipata kwa njia ya barua pepe kabla ya kukwaa pipa la shirika la ndege la Emirates, Bw. Michuzi ambaye pia ni maarufu kwa majina kama Mzee wa Libeneke, Mdau na Ankal, amesema amefarijika sana kuona kumbe kuna wanaotambua mchango mkubwa unaoletwa na vyombo vya habari za jamii mtandano, hasa blogu. Aesema anajisikia mwenye furaha sana kuona azma yake ya kuifanya tasnia hii ya kupashana habari kwa njia ya intaneti kwa waandishi wa hapa nyumbani unatambulika na kukubalika na kupewa heshima stahili kama ilivyo kwa vyombo vya kawaida kama vile magazeti, redio na luninga. Bw. Michuzi, anayeweka rekodi ya kuwa bloga wa kwanza nchini kualikwa kama bloga kwenye mkutano muhimu kama huo, anaushukuru ubalozi wetu Uingereza chini ya Balozi Mh. Mwanaidi Maajar ambaye naye anakuwa miongoni mwa wazalendo wa kwanza kuutambua hadharani mchango wa wanahabari za jamii mtandaoni kwa kutoa mwaliko huo. "Nilijua iko siku wanahabari za jamii mtandaoni tutatambulika na mwaliko huu hakika umekuja wakati muafaka kwani msisimkmo na mwitikio wa jamii kuikubali njia hii ya mawasiliano hapa nyumbani umekuwa mkubwa kuliko ilivyotarajiwa". siku hizi habari za jamii mtandaoni zinachukua kiti cha mbele katika kusomwa na wenye kuwa na intaneti kutokana sio tu na habari kuwa za uhakika, zisizochujwa na za haraka bali pia kwa kule wasomaji kupata fursa ya kuchangia habari waionayo tofauti na ilivyo kwa magazeti, redio na luninga. "...dunia imezidi kuwa kijiji kimoja kidogo kwa teknohama hii ambayo hata Rais Jakaya kikwete yuko mstari wa mbele kutaka iendelezwe mijini na vijijini ili kuwezesha wananchi wawe na habari za uhakika, za haraka na zenye kutoa fursa ya wasomaji kuchangia maoni" alisema Bw. Michuzi. Blog ya issamichuzi.blogspot.com ilianza rasmi Septembe 8, mwaka 2005 katika jiji la Helsinki, Finland, ambako alikwenda kuhudhuria mkutano wa Helsinki Conference akiwa kama mwandishi na mpiga picha wa gazeti la Daily News. Alikuwa ni bloga wa siku nyingi aliyekuwa anaishi Marekani wakati huo, Bw. Ndesanjo Macha, aliyemshawishi Bw. Michuzi kufungua blog yake na kuwa bloga wa kwanza wa Tanzania kuupasha ulimwengu ya kila linalojiri nchini, kazi ambayo ameifanya kwa ustadi mkubwa kiasi ni hivi majuzi tu ameweza kufikisha wasomaji milioni 8, kati ya hao asilimia 30 wakiwa ni wasomaji wa Tanzania. Bw. Michuzi ameweka wazi kwamba amefurahi na kusisismkwa sio kwa sababu anakwenda Ulaya, kwani ameshatembelea karibu miji mikubwa yote duniani, ukiondoa Australia na New Zealand, ila amefarijika kwa sababu hatimaye blogu zimeanza kutambuliwa rasmi. Anatoa masikitiko yake kwamba pamoja na fanaka hiyo, lakini bado hapa nyumbani jamii, hasa ya mahafidhina (conservatives) wasiotaka mabadiliko wamekuwa wazito kukubali kwamba vyombo vya habari za jamii mtandaoni vimeshapata nguvu sawa na vyombo vya kawaida kutokana na wingi wa wasomaji na hata kupelekea kujitokeza kwa wadhamini wanaotangaza biashara zao humo. Pamoja na mambo mengine, Bw. Michuzi amesema anatamani sana kuanzisha umoja wa wanahabari za jamii mtandaoni ili kutetea na kulinda maslahi yao pamoja na kuindeleza tasnia hii ambayo inakua kwa kasi za ajabu. Kwa mahesbu ya haraka haraka hivi sasa kuna blogu zinazotumia lugha ya Kiswahili zipatazo 200 ambapo pia blogu takriban 10 zinaanzishwa kila siku, na kuifanya Tanzania kuwa nchi inayoendelea katika tasnia ya habari kwa njia ya mtandao. Tangu kuibamba tovuti ya TBC mtandaoni wakati fulani na kufurahia sana ujio wake, furaha yetu haikudumu saa chache kwani ilizidiwa na wingi wa watembeleaji na 'kufulia bandwidth' na hivyo kutokuwepo hewani. Wiki hii, tovuti hiyo inaonekana kuwa hewani muda wote, tunadhani sasa imerudi ikiwa imejitosheleza kamilifu tayari kwa zoezi zima la upashanaji habari. Tovuti ya TBC inapatikana kupitia anwani ifuatayo: www.tbc.go.tz Mganga mkuu wa wilaya ya Hai, Paul Chaote (aliyevaa miwani) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai, Deodatus Nyoni wakiwa nje ya moja ya bucha wilayani humo walipokuwa wakikagua maduka ya kuuza nyama jana katika mji wa Bomang'ombe baada ya Serikali kuamuru yote kufungwa baada ya kuibuka kwa ugonjwa wa Kimeta Wilayani humo ambao tayari umeua watu wawili. Photo credit: Daniel Mjema/Mwananchi.co.tz Ndiyo majibu toka kwa waliotarajiwa kutoa ufafanuzi kama inavyosomeka hapa kutoka kwa Mohammed Mhina wa Jeshi la Polisi Jeshi la Polisi nchini limesema halina taarifa za wizi wa shilingi Bilioni 300 zinazodaiwa kuibwa kwa njia ya mtandao wa kompyuta kutoka katika mabenki mbalimbali yaliyounganishwa na mtandao huo hapa nchini. Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika, amesema leo kuwa taarifa zilizoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusiana na wizi huo hazijafikishwa Polisi. Kamanda Mssika amesema kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kamishna Robert Manumba, aliyedaiwa kukaririwa na chombo hicho cha habari, amesema kuwa hana taarifa ya tukio la wizi wa shilingi Bilioni 300. Kamishna Manumba amesema kuwa mawasiliano kati yake yeye na Mwandishi wa taarifa hiyo kwa upande wake binafsi yalihusu tukio la wizi wa fedha katika benki ya NMB Tawi la Bank House Jijini Dar es Salaam ambapo mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu, Jeshi la Polisi lilibaini kuibwa kwa shilingi milioni 360 kwa njia ya mtandao wa kompyuta fedha ambazo zilihamishiwa katika tawi moja wapo la benki hiyo lililopo mkoani Shinyanga. Kamanda Mssika amefafanua kuwa, mara baada ya fedha hizo kufika Mkoani Shinyanga, zilitawanywa kutoka katika tawi hilo na kupelekwa kwa njia ya mtandao wa kompyuta kwenda katika akaunti mbalimbali za watu binafsi kwenye matawi mengine ya benki hiyo katika baadhi ya mikoa hapa nchini. Kutokana na wizi huo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Benki ya NMB limeshafanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 319 kati ya shilingi milioni 360 zilizoibwa na kwamba tayari baadhi ya watuhumiwa waliohusika katika wizi huo wakiwemo watumishi watano wa benki wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu shitaka lao. Hata hivyo Kamanda Mssika amesema kutokana na taarifa za kuibwa kwa shilingi bilioni 300, kama ilivyoandikwa, ametoa wito kwa Makampuni ama Taasisi za Kifedha zinazoweza kuwa zimefanyiwa hujuma hiyo ya wizi na iwapo rasimu zao za ndani kiuchunguzi zimekamilika, basi wawasiliane na Mkurugenzi wa makosa ya Jinai nchini Kamishna Robert Manumba, ili hatua za uchunguzi ipasavyo kwa kuvishirikisha vyombo vya dola ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo. Tanzania shuts down its UK diamond office Tanzania has closed down the London offices of its diamond sorting firm and transferred its operations to Dar es Salaam... (click here to continue reading). Uniform park fees for EA residents Residents of the East African Community will now pay the same fees as Tanzanians to enter the country’s national parks... (click here to continue reading). Bilioni 300 zaibiwa kimafia Dar WATU wasiofahamika wameghushi nyaraka za malipo na kuiba zaidi ya Sh300 bilioni katika benki tatu kubwa nchini na kusababisha mtikisiko mkubwa katika sekta ya fedha... (bofya hapa kusoma habari nzima). Nyinginezo: The government has asked for the new guidelines on treatment of malaria from the World Health Organisation (WHO). The guidelines will enable Tanzania make necessary changes in the local policy. Speaking to this paper yesterday, Ministry of Health and Social Welfare's head of communication unit Mr Nsachris Mwamaja said the document would be used by a team of experts to examine the guidelines before making any decision. However, Mr Mwamaja said, according to the abridged copy of the document, Tanzania has already started implementing some of the recommendations issued by WHO. He said for instance that the country’s malaria treatment policy is discouraging the use of oral artemisinin-based monotherappy as the new WHO malaria guidelines advocates. The global health watchdog has released a new Malaria treatment guidelines as well as the first guideline on procurement of safe and effective medicines, in a move to intensify the campaign against the leading killer disease. The new guidelines also endorse the use of the artemisinin-based combination therapies (ACTs), as the major treatment regime for malaria while discouraging the use of artemisinin-based monotherapy since its use will hasten the development of parasite resistance. The WHO also cautions in its new guidelines on the need for proper application of the recommended treatments. “In recent years, a new type of treatment called artemisinin-based combination therapy (ACTs) has transformed the treatment of malaria, but if not used properly, the medicine could become ineffective,” says the WHO statement. Written by By Frank Kimboy, thecitizen.co.tz ![]() John Mnyika Ni wakati wa mabadiliko ya kweli; tuwajibike
Natangaza rasmi dhamira ya kugombea ubunge 2010 Utangulizi Wapendwa wananchi wezangu na marafiki zangu ndani na nje ya jimbo la Ubungo. Ninayofuraha kuwatangazia rasmi dhamira yangu ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Nimefikia uamuzi huu baada ya kusikia maoni ya wengi wenu na kuisikiliza pia nafsi yangu katika kipindi cha kuanzia mwishoni mwa mwaka 2009 mpaka mwanzoni mwa mwaka 2010. Wakati wa kampeni bado, hivyo sitazungumzia kwa sasa ahadi zangu kwenu wala ilani ya chama; lakini inatosha kuwaambia tu kwamba: ni wakati wa mabadiliko; tuwajibike. Naamini katika kuwa na uongozi bora wenye dira na uadilifu wa kuwezesha uwajibikaji katika kusimamia rasilimali za umma ikiwemo kodi zetu na mali asili za nchi yetu kwa ajili ya kujenga taifa lenye kutoa fursa kwa wote. Nautambua wajibu; tushirikiane Naamini kwamba mbunge (ambaye pia kwa nafasi yake ni diwani katika halmashauri) ana wajibu katika maeneo makuu manne (kwa kadiri ya umuhimu). Mosi; Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi bwana Joseph Mbatia akihutubia wakazi wa Kawe Dar es Salaam leo wakati akitangaza rasmi nia yake ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kawe kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi huku wakati wa vitongoji vya Kawe wakimsikiliza. Jimbo hilo kwa sasa linaongozwa na Ritha Mlaki wa CCM. Shughuli hiyo ilifanyika katika viwanja vya Tanganyika Perckers, Kawe jioni ya Machi 20. Picha kwa hisani ya Mroki Mroki aka Fadher Kidevu ![]() Mubelwa Bandio Juzi kaka mdogo Mubelwa Bandio aliandika habari ya kumshukuru Dk. A. Kinasha na wengine wote katika hospitali ya Muhimbili na kwingineko ambao walishughulikia suala la afya yake iliyokuwa halijojo hadi kupata ahueni. Ni mara ya tatu sasa ninasoma mrejesho wa waliopatiwa huduma katika sekta ya afya kwa njia ya blogu. Kwanza nilisoma kutoka kwa Prof. Matondona pili ikawa ile ya dada Yasinta akisimulia na kushukuru kuhusu mdogowe Asifiwe. Napenda kuamini kuwa wapo watu wengine wengi tu waliofanya hivi kwa njia mbalimbali ikiwemo ya barua, maneno ya mdomo, kupiga simu, kwenye redio, televisheni na hata kuandika magazetini na kwenye vijarida kadha wa kadha. ![]() Yasinta Ngonyani Ninaafiki kuwa si watu wote wanaweza kuwa wamezisoma (kama ilivyo habari za kwenye blogu na tovuti, si wote wanaozipata). Lakini faida ya kuandika mrejesho kwa huduma alizopewa mtu zina umuhimu wa hali ya juu kwa wale wote wanaojali na kuzingatia maana na dhana ya neno 'huduma' na katika hilo nikimulikia sekta ya Afya ambayo imekuwa mojawapo ya sekta zinazolalamikwa sana, niliziandika katika posti iliyopita (unaweza kubofya hapa kuirejea). Kilichonigusa katika posti ya Mubelwa, si tu maandishi yake ambayo niliyapeleka kunako jiko, bali pia maoni yaliyotolewa na wadau, mosi kutoka kwa Kaka Simon Kitururu na pili toka kwa Kaka Prof. Matondo. ![]() Simon Kitururu Kwa mfano, katika sehemu ya maoni yake, Simon anaandika, "...Huwa unanifanya nifikirie ni WANGAPI maishani mwangu ambao sijawashukuru na WASTAILIO shukurani za DHATI ." Maneno haya ni kama vile Simon aliyasema kwa niaba yangu (na pengine wengi) kwamba katika kusoma habari za watu wengine, je, tunapata kujifunza kutokana na maneno yao? Kama kuna jambo la pekee sana kutoka kwa Mubelwa ambalo mtu aweza kujifunza, basi ni utamaduni wa KUSHUKURU na kusema ASANTE. Kwa hili Mubelwa ameendelea kunikumbusha tena na tena. Nami kwa sina budi kusema Asante Mubelwa kwa kunikumbusha kushukuru. ![]() Prof. Masangu M. N. Mfano mwingine ni maoni ya kaka Matondo, ambapo sehemu katika maoni yake kwenye posti hii anauliza, 'Hivi madaktari bingwa kama hawa wakistaafu wanakwenda wapi?..." na kisha anamalizia, '...Ningekuwa "serikali", ningewapa kila kitu wanachohitaji na kuwaomba wabakie kazini mpaka umri utakapowaamuru kuacha." na hapa ndipo aliponikumbusha juu ya maisha ya wasomi na wastaafu wetu. Ananikumbusha habari niliyowahi kuisoma katika jarida pepe la IRINnews.org (TANZANIA: Pensioners step in to plug medical gaps) kuhusu baadhi ya wastaafu hawa katika sekta ya Afya nchini Tanzania. Kisha, upo mjadala uliowahi kujadiliwa na redio ya BBC katika kipindi chake cha Africa Have Your Say (bofya hapa kusikiliza) ambako nako walisikika wastaafu na wasio wastaafu wakizungumza kuhusu faida ama/na hasara ya kuendelea kuwa na watu wa umri ambao unadhaniwa kuwa ni wa kustaafu, wakiendelea kushika nafasi zao za kazi kadiri ya uhitaji si wao binafsi tu, bali kwa taifa lao pia. Kuna jambo ambalo umewahi kufanyiwa na kuridhika hata ukatamani urejeshe shukrani? Fanya hivyo. Je, lipo jambo ambalo umewahi kufanyiwa likakuudhi na ukakereka sana hata ukatamani utoe dukuduku ambayo itaonya na kusababisha wahusika wajirekebishe? Liseme. Hii ni karne ya TEKNOHAMA, wakati muafaka kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano kusema ili usikike. Elimu, Maarifa, Wajibu, Shukrani... katika maisha ya Mwanadamu. Tuambizane. Tusemezane. |


















RSS Feed