Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA Dk Willibrod Slaa, amesema kuwa  vigogo wa CCM hawana ubavu wa kumnyooshea kidole kuhusu maisha yake  binafsi.
Akihutubia wananchi katika mji wa Babati, mkoani Manyara, Dk.  Slaa alisema iwapo wataendelea kuacha masuala ya kitaifa na kujihusisha  na maisha yake binafsi, naye atawavaa na kuwavua nguo mmoja baada ya  mwingine, kwani anawajua.
Willibrod Slaa akihutubia Babati, Manyara
Na kwa kuanzia, alimtaka Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, awaeleze Watanzania kwa nini alifukuzwa ualimu wa shule ya msingi. Dk. Slaa alisema yeye hakufukuzwa Upadri, kama Makamba anavyodai; bali aliamua kuacha kwa kufuata sheria za kanisa, na akapewa kibali kutoka Vatican kinachomruhusu kuwa mlei na kuoa.
Alisema iwapo Makamba atadanganya Wananchi kuhusu kilichosababisha afukuswe ualimu, Dk. Slaa atamuumbua.
Wajuzi wa mambo wanajua kuwa Makamba alifukuzwa Ualimu (Mkuu) wa shule kwa kosa la kumbaka na kumpa mimba mtoto wa shule.
Naye Mkuu wa msafara wa Dk. Slaa, Suzan Kiwanga, alimtolea uvivu mke wa rais, Salma Kikwete, akisema anatumia pesa za umma kuzunguka nchi nzima anafanya kampeni huku akijua kuwa hatambuliki katika ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kauli ya Kiwanga iliongezewa uzito na Dk. Slaa aliyesema: "Nchi hii ina rais mmoja, ni Kikwete. Mke wa rais si rais. Anatembea kwa msafara wa magari 21 huku akilindwa na kupewa heshima zote na viongozi wa serikali; kama nani? Na raisi mwenyewe atatumia magari mangapi? Lakini hii yote ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi, na huu ni ufisadi," alisema huku akishangiliwa na umati uliokusanyika katika uwanja wa Kwaraha mjini Babati.
Ilisemekana kwamba, asubuhi ya leo, kabla ya mkutano wa Dk. Slaa, Salma alitaka kuuteka uwanja huo na kuutumia kwa mikutano yake ya hadhara, lakini wananchi wa Babati wafuasi wa CHADEMAwalimtolea macho na kumfukuza uwanjani hapo. Hali hii ndiyo ilisababisha kauli ya Kiwanga, ambaye alisema: "Laiti ningemkuta hapa, sementi hii (sakafu) ingegeuka vumbi." Akasisitiza kwamba kama Salma angekuwa anataka kufanya siasa, angechukua fomu agombee urais kama mumewe ili apate fursa ya kuzurura na kufanya mikutano.
Lakini si vema kutumia pesa za Ikulu au za asasi yake ya WAMA kufanya siasa.
credit & copyright of this cross post goes to Ansbert Ngurumo "Utakapojua hujui ndipo utakapojua" blog
Kuhusu Mgombea Ubunge kupitia NCCR Magezuzi James Mbatia,  Marando alisema ndiye aliyesababisha yeye kukihama chama hicho.
“Mimi ni mkazi wa jimbo hilo, maendeleo ya jimbo hili yananihusu,  nilimwambia Mbatia kama atagombea Ubunge katika jimbo nitakihama chama  hicho kwa kuwa yeye hana uwezo wa kuongoza na amekiua chama hicho,”  alisema Marando.
Huku  akishangiliwa na umati wa watu Marando alisema; “ Nilipozunguzia hili  wakati wa kufungua kampeni TBC (Shirika la Utangazaji la Tanzania )  walikata mitambo yao, sasa leo narudia tena na hapa hukuna mitambo sijui  watakata nini,”alisema Marandu na kucheka.
“Niliwaambia kumfunga  Liyumba, kumshitaki Maranda na wengine ambao kesi zao ziko mahakamani  kwa sasa siyo suluhisho la ufisadi hapa nchini, nasema hivyo sababu wale  waliofikishwa mahakamani ni matawi tu na mafisadi ni mti mkubwa ambao  unatakiwa kung’olewa.
Mafisadi halali ni wale waliotajwa na  Dk.S laa waziwazi katika Viwanja vya Mwembe Yanga, alitaja majina yote na  kuonyesha Watanzania wote kuwa kumbe wizi uko hata (BOT) mahali ambapo  Watanznaia hata siku moja hamukuamini kama kuna wizi unafanyika,”  alisema Marando.
Akifafanua maana ya ufisadi alisema; “Mafisadi  maana yake ni viongozi wanaotumia nafasi zao kuchota fedha za umma  zilizotengewa kwa ajili ya ujenzi wa huduma za kijamii kama shule,  zahanati, barabara n.k na kuzitumia wao binafsi na marafiki zao.”
credit: Na Elvan Stambuli/GPL
Lake Victoria Environment Management Project (LVEMP) hivi karibuni waliandaa mashindano ya muandishi bora wa habari za mazingira katika ukanda wa Ziwa Victoria. Pichani ni waandishi wa habari waliofanya vizuri katika zoezi hilo. Kutoka kushoto ni Bw. Deus Bugaywa kutoka gazeti la The Guardian, Katikati ni Bw. Vedastus Msungu kutoka ITV/Radio One na Kulia ni Bi. Diana Nachilonga kutoka Gazeti la Mwananchi.
credit: McKepha "Lifetime" blog
Matokeo ya utafiti yamethibitisha  kuwa dawa za kutibu ugonjwa wa Malaria, zinazotolewa kwa nchi kadhaa  barani Afrika, huibwa na kisha kuuzwa katika mahospitali na maduka binafsi ya madawa.
kwenye ripoti iliyochapishwa na jarida moja la  matibabu, watafiti kutoka Marekani na Uingereza walinunua dawa kutoka  miji kumi na moja barani Afrika na kugundua kuwa dawa moja kati ya ishirini  ilikuwa ni mali ya zahati na hospitali za Serikali. Wataalamu wengine wamethibitisha kuwa matokeo ya  utafiti huo ni ya kweli.
Takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya watu milioni moja hufa kila mwaka barani Afrika kwa ugonjwa  wa malaria.
credit: BBC Swahili
YATOKANAYO
Nami ingawaje sijafanya utafiti wa aina yoyote, ninaafiki matokeo ya utafiti huu kutokana na tetesi na vitendo vya kutilia mashaka ambavyo vimekuwa vikitendwa na baadhi ya watumishi wasio waadilifu katika hospitali, zahanati, bohari za madawa na vitengo kadhaa katika Wizara husika.
Ni jambo la kusikitisha kuona kuwa Serikali inahujumiwa il hali dawa hizo zimetengwa kwa ajili ya kumsaidia mwananchi ambaye, mtumishi wa Afya na Serikali atamtegemea awe na afya njema ili aweze kuzalisha na kumwezesha yeye kupata ujira wake, kwa kufanya kazi ya kuelimisha na kuboresha afya za wananchi.
Inasikitisha zaidi kuona kuwa akili zetu zinatutuma kujiibia sisi binafsi, kwani kuiba toka Serikalini ni sawa na kujikata vidole vya mikono, hatimaye viwiko vitakuwa kigutu na kuishia kuwa mzigo tegemezi.
Tunapohimiza Serikali na viongozi kutimiza wajibu wao, nasi tukumbuke kuwa tunalo jukumu la kutenda kazi zetu kwa uaminifu. Pale tunapokosa ujira na malipo yanayoendana na nguvu kazi tunayotoa, basi tuidai panakostahili kwa taratibu zake badala ya kuhujumu Serikali kuendeleza rushwa katika Taifa.
Tutajatolea hesabu matendo yetu. Natumai faili lako litakuwa safi siku litakaposomwa. Tubadilike!
Kocha wa timu ya mpira wa pete (netball) kwa wanawake Tanzania Bara, Simone McKinnis na kocha wa timu ya soka ya wanaume Zanzibar, Stewart Hall wamewasili nchini tayari kutumikia vibarua vyao.
Kocha wa timu ya netiboli ambaye ni raia wa Australia ataifundisha timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili, wakati kocha wa timu ya soka na raia wa Uingereza atatumikia mkataba wake wa kipindi cha miaka mitano.
credit: Jane John
Jitihada za Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi na mbunge anayemaliza muda wake katika Jimbo la Nyamagana, Lawrence Masha, za kupita bila kupingwa katika kinyang’anyiro cha ubunge katika jimbo hilo zimegonga mwamba baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutengua uamuzi wa awali wa msimamizi wa uchaguzi kumzuia mgombea wa CHADEMA.
Taarifa zinadai kuwa NEC imeamua kumrejesha mgombea wa CHADEMA, Ezekiah Wenje ambaye alikuwa wakifanya kazi NMG hapa Harbour View jijini Dar es Salaam, baada ya kuridhishwa na vielelezo vya uraia wake.
Kurejeshwa kwa Wenje katika kinyang’anyiro hicho kitazidisha chachu ya uchaguzi wa ubunge, ambayo tayari ilionekana kutokuwa na msisimko baada ya Masha kuwa mgombea pekee.
NEC leo itatangaza uamuzi huo ambao umepokewa kwa hisia mbalimbali na baadhi ya wakazi wa Jimbo la Nyamagana na wafuatiliaji wa masuala ya siasa.
Waziri Masha aliwasilisha pingamizi dhidi ya Wenje kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Wilson Kabwe, ambaye aliridhika na nyaraka zilizowasilishwa na waziri huyo, hivyo kuamua kumuengua mgombea huyo.
Baada ya uamuzi huo, Wenje aliamua kukata rufaa NEC kwa kuambatanisha vielelezo vyake kuthibitisha kuwa ni raia wa Tanzania na si raia wa Kenya kama Waziri Masha alivyodai.
Mmoja wa viongozi wa juu wa CHADEMA alithibitisha kuona barua ya NEC, ikiwaarifu kulitupa pingamizi lililowekwa na Waziri Masha, hivyo kumruhusu Wenje kuanza pilikapilika za kampeni.
kiongozi huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe kwa misingi kuwa si msemaji wa chama hicho, alisema tayari wameshaanza maandalizi ya kampeni na wana uhakika wa kumbwaga tena Waziri Masha katika kinyang’anyiro hicho.
“Ni kweli NEC imemrejesha mgombea wetu baada ya kuona vielelezo vilivyotolewa na mgombea wa CCM vina upungufu na vya mgombea wetu kuwa ni sahihi… tunaamini kwamba haki imetendeka na kinachofuata ni mapambano sasa,” alisema kiongozi huyo.
credit: Mpoki Bukuku "Mzee wa Sumo" blog
Watu watatu akiwamo Rubani wa ndege na Mkuu wa wilaya wa zamani wa  wilaya ya Kyela mkoani Mbeya Hussein Mashimba  wamenusurika kifo baada  ya kuanguka mita chache wakati ikiwa imeruka katika uwanja wa ndege wa  Sumbawanga mkoani Rukwa.
Ajali hiyo imetokea leo katika eneo la SIDO majira ya saa 10:00 alasiri  ikiwa ni umbali wa mita 15 kutoka ukingo wa uwanja wa ndege wa mjini  Sumbawanga na kuhusisha ndege aina ya CESSINA 206 NO. 5H-TCC mali ya  kampuni ya Flight Link ya mkoani Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa jeshi la polisi mkoani  Rukwa Bw. Isuto Mantage ndege hiyo ilikuwa ikitokea mjini Sumbawanga na  kuelekea JIJINI Dar es salaam ambako ilikuwa ikimsafirisha Mkuu huyo wa  wilaya wa zamamni wa wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.
Kamanda Mantage amesema kuwa ndege hiyo ilianguka ikiwa pia na Mganga  mmoja wa hospitali ya mkoa wa Rukwa Dkt. Laswai na Rubani aliyefahamika  kwa jina moaja la Navele.
Kwa mujibu wa Mganga wa hospitali ya mkoa wa Rukwa Dkt. Gasper Nduasinde  hali za majeruhi inaendelea vizuri na hadi sasa ni Mashimba pekee ambaye  bado yuko hospitalini hapo kutokana na kuumia mguu wake wiki iliyopita  alipokuwa mjini Sumbawanga na kulazimika kuletewa ndege hiyo kwaaajili  ya kupelekwa Dar es salaam kwa matibabu zaidi.
Dkt. Nduasinde amesema katika ajali hiyo ya ndege Mashimba aliumia  kidogo katika sehemu ya mgongo wake lakini sio jeraha kubwa na hali yake  inaendelea vizuri.
Mashimba anadaiwa kuvunjika mguu mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya  kuanguka bafuni katika nyumba mmoja ya kulala wageni mjini hapa alikuwa  katika msafara wa kampeni wa CCM akimnadi Rais Kikwete.
credit: Sammy Kisika, Sumbawanga via DulloNet
Mwenyekiti  wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ametakiwa kuomba radhi kufuatia  kauli yake kuwa Rais mstaafu wa Zanzibar, marehemu Idris Abdul Wakil,  alishika nafasi hiyo akiwa na elimu ya darasa la saba.
Idris Abdul Wakil - R.I.P
Kauli hiyo ilitolewa na CCM Zanzibar jana kupitia Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Vuai Ali Vuai.
Vuai alisema kauli ya Mbowe ni upotoshaji  kwa Watanzania kwani Rais  huyo mstaafu alikuwa ni miongoni mwa wasomi  wazuri aliyepata Shahada ya  kwanza Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda.
Alisema CCM  imeshitushwa na kauli hiyo na  kumtaka Mbowe awaombe radhi Watanzania na  wanafamilia kwa vile kiongozi  huyo alikuwa ni wa kitaifa.
Hata  hivyo, alisema CCM haifikirii  kuchukua hatua zozote za kisheria,  lakini kiungwana lazima wahusika  wakubali wamefanya makosa kutangaza  jambo kinyume na ukweli wake.
Akizungumza katika uzinduzi wa  kampeni za  uchaguzi za CHADEMA wiki iliyopita katika viwanja vya  Jangwani,  Mbowe alisema marehemu Abdulwakil alikuwa na elimu ya darasa  la saba  lakini aliweza kumudu vyema uongozi kwa vile ni hekima na  busara. Aliyasema hayo baada ya wanachama  wa CCM kudai kwamba mgombea  mwenza wa urais wa Muungano kupitia Chadema  ana elimu ya darasa la  saba.
Hatahivyo, Mbowe akizungumzia suala hilo  alisema  anatafakari hatua hiyo ya CCM na kama itathibitika marehemu  Abdulwakil  alikuwa na elimu ya chuo kikuu sio makosa kwa yeye kuomba  radhi.
“Hilo nalitafakari na kama kweli ikithibitika kiungwana sio makosa kuomba radhi”, alisema.
credit: Nipashe/IPP Media