Juzi ile, nanihii alisema stima itakuwa kwishnei kwenye vijumba sita hivi vya hapa kijiweni.

Ujue jamaa mi n'lishindwa nimshangaeje, maana ndo nlikuwa nasubiria tu lini atasema hivyo, mwaka ndo unakaribia kukatika huu. Sijui cha juu safari hii anapata nani. Si unajua siye kijiweni kazi yetu kupokea tu taarifa, utauliza vipi? na hata ukiuliza unadhani utakosa jibu? ah, tena unapewa majibu mwenyewe unakubali na kuchangia kwenye jibu, ama vipi unapewa mengi unaambiwa uchague la kukubaliana nalo kisha jivute.

Stori za mwaka elfu mbili na nne umezisahau? enzi hizo wamelipua kisemo kigeni 'la nina'? Basi keleleee kelele wakati huo ni ukamee, ukame, ukamee, ukame, yaani kero tupu! si umeme hamna shauri ya ukame mabwawa hayana maji?!

Kulaleki walahi, si mwaka elfu mbili na tano ikatokea 'el nino'? mvua hiyo babake kuku hatoki bandani lakini umeme hakuna! Usichekelee, umeme ulikatika. sababu? si mabwawa yalijaa matope! Ebo, 'asa we unategemea matope yale yakiingia kwenye mashine itafanya vipi kazi? unakuwa na akili ka za ukutiukuti bwana? Mashine ya kunyonyea tope haijagunduliwa bado we dogo, usijifanye mjuaji.

Eti?
...!
Rudia tena?
...ndi!
tuna mafundi? mafundi gani? waliosoma injiniaring au? we bwana usitake kuleta msala hapa
Skiza, mvua iwepo isiwepo umeme kukatika Tanzania ni ada, sawa dogo? Kuna sababu chungu mbovu za kwa nini umeme ukatike na kama akili zako nyingi za kushauri eti tufanye hivi na vile ndo umeme usikatike, dogo, hizo dili kama hazina namna ya kuchomeka ten pasenti hapo utakuwa umefulia.

Ebu tufanye dili la maana.
We si unaenda kusoma USAgara? alaaa, samahani, kumbe ulimepata mchongo wa UKerewe kwa Bi Mkora? okei, sasa halijaharibika jambo, fanya hivi, utafute wawekezaji wa kitasha huko..., alimradi si kwenye suala la umeme, pengine nishati nyingine, tuna maji, gesi asilia, jua miezi sita, na nini na nini...
Wao waje kuwekeza na kwingine tu, kuna vitega uchumi kibao! Kwanza we si umesoma jografia? na historia? si unaijua nchi? sasa wasomeshe hao watasha, 'afu wao wakija hapa miradi yao hiyo ya kiwekezaji inabidi wanunue jenereta! Sasa hapo ndo kwenye dili yenyewe, wananunua majenereta ya hapa hapa dukani kijijini kwetu kwa mshikaji Sefu yale yake kayanunua Dubaiii...

Dili hilo mwanangu, 10% ya kutesea ughaibuni na mabinti wa kitasha hukosi, au vp?

Hapo shwari mkubwa.


Chakarika dogo...

Poa!
 


Comments

RP
26/10/2009 11:31

Ebwan nimeikubali hii post..full mzuka mwana..yaani hapo umenipeleka kijiweni kabisaaa.

Yup yup

Reply



Leave a Reply