Vijimambo hivi vlitokea pale Mbuge wa Moshi Mjini bwana Ndesamburo (CHADEMA) alipotua kwa Helikopta yake wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere. Ilikuwa majira ya saa tano asubuhi wanafunzi wa vyuo mbalimbali walipokuwa wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM bwana Amos Makala katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika na Stadi za Biashara (MUCCOBs) wakati helikopta ya mzee Ndesa ilipotua huku akishangiliwa na nderemo za, 'babu babu babu'... ilibidi Makala asitishe kuongea kama dakika tano hivi halafu akaachia kali ya mwaka, ati: "Hata mimi ningepewa helkopta na Chama cha Mapinduzi ningekuja nayo, nami nishuke nayo hapa lakini nimekuja na gari sio kwamba sisi hatuna …tunazo nyingi lakini sisi ni wastarabu zaidi" Mzee Ndesa akasema: "Ikiwa kweli nchi inataka kumuenzi Mwalimu basi ifanye aliyoyataka yeye kwa kukemea rushwa ,ukabila, udini na kuwaondoa madarakani viongozi wasio waadilifu. Watu waache kumuenzi kwa maandamano na kuvaa sare. Viiongozi ambao Mwalimu alisema hawafai kuwa viongozi wamepewa uongozi na kufanya mambo maovu kwa serikali yetu na tunaendelea kuwafunika kwa blanketi la Chama, badala ya kuwachukulia sheria. Tunamuenzi vipi mwalimu? Tuache kumuenzi kwa maneno wananchi wamechoshwa na maneno" alisema Mzee Ndesa aka Babu ndiye Mzee Ndesamburo! Hivyo ndivyo vijimambo vya Siasa toka Moshi. CommentsEvans 01/11/2009 11:40pm
Hivyo kweli vijimambo? Mzee Ndesa alitaka tu kuvuta umati wa watu kupitia helikopita.Uzuri ni kwamba Wazee wa Moshi wanamkubali.Yaani yule atakuwa mbunge wao na mwaka ujao.
Reply
Wavuti 02/11/2009 7:34pm
Teh, teh, Evans, siasa za Moshi zinaweza kubadilika ghafla bin vu, wale wazee wanaangalia 'heleri' tu teh teh hayo mengine yanafuata b'dae.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed