Mkulima amejiwa na Mwaandishi wa magazeti kumuhoji kuhusu maisha ya shambani. Mkulima huyu hawapendi Waandishi wa habari akaona vyema amchoshe katika kujibu maswali, na mambo yakawa hivi: MWANDISHI: Wewe unawalisha ng'ombe chakula gani? MKULIMA: Ng'ombe yupi? Mweupe au Mwekundu? MWANDISHI: Ng'ombe mweupe. MKULIMA: Ninamlisha nyasi na viguta vya mahindi. MWANDISHI: Na mwekundu? MKULIMA: Vilevile nyasi na viguta vya mahindi. MWANDISHI: ahaa sawa, na sehemu ya kulala ni wapi? MKULIMA: Ng'ombe yupi? mweupe au mwekundu? MWANDISHI: Mweupeee!!!!XXCCCZZZZHH!!!! MKULIMA: Mweupe ninamlaza bomani kulee... MWANDISHI: na mwekundu? MKULIMA: Vile vile namlaza na mwenzie. MWANDISHI: Hii sehemu yote majumba mengi, wakati wa kulisha unafanyaje? MKULIMA: Yupi mweupe au mwekundu? MWANDISHI: Woooteeee!!!! [akifuka kwa hasira] MKULIMA: Mweupe ninamfunga kamba na kumzungusha malishoni na kumrudisha. MWANDISHI: na mwekundu vilevile? MKULIMA: Mwekundu? Mwekundu yeye ninamfunga kamba na kuzunguka nae kama mwenziwe tu. MWANDISHI: Kwanini kila mara nikikuuliza huduma za ng'ombe wako unaniuliza mweupe au mwekundu halafu inatokea kuwa kazi zao wote ni sawa????? MKULIMA: Kwa sababu ng'ombe mweupe ni wangu. MWANDISHI: Na mwekundu? MKULIMA: Na mwekundu ni wangu vilevile. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed