Kiswahili kinachanja mbuga na kukua na kukubalika katika ulimwengu wa lugha kwa sasa. Katika kukua huko, watu wamekuwa wakidaka maneno na kuyatumia kadiri watakavyo. Wengine wamekuwa wakitafuta maana halisi toka kwa wazungumzaji asili wa lugha hiyo, il hali wengine wamekuwa wakichukua neno na kulitumia kutokana na urahisi wa kulitamka au usikivu masikioni. Hili kundi la pili hili ndilo limenigusa posti ya leo baada ya kukutana na habari inayozungumzia kuhusu 'ulanguzi.com'. Kama kawaida ya udadisi, huwa tunataka kujua hiyo ulanguzi.com inajishughulisha na nini hasa ukizingatia maana halisi ya neno, 'ulanguzi' ni kuuza bidhaa kwa gharama isiyo halali, udokozi, kutumia ujanja -hasa katika biashara- ili kujipatia fedha kubwa nk. (in English ULANGUZI is the Swahili word literally meaning to take advantage of, black-marketing, speculation, profiteering, conjecture etc) Matarajio yalikuwa iwe ni tovuti inayojishughulisha na maana halisi ya neno lenyewe, hasa ukizingatia kuwa wahusika wametoa maana ya neno 'ulanguzi' kuwa linatokana na neno la Kiswahili. Maana ya neno lile si sahihi kwa walivyoitamka wao. Tizama picha iliyoambatanishwa hapo ujionee walichoandika. Naam, Kiswahili kinachanja mbuga, lakini lazima tafsiri ya maneno yake iendane na tafsiri halisi tunayoifahamu sisi Waswahili na si watu wakurupuke tu kubandika tafsiri wanazozijua wao ili mbeleni huko waje wakaipotoshe jamii kuhusu maana halisi ya neno lenyewe. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed