Habari iliyoripotiwa na mtandao wa AFP inasema kuwa, Tanzania itatumia kiasi cha dola za Kimarekani $750,000 kuwaleta vifaru wapatao 32 kutoka nchini Afrika Kusini hadi kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Akiongea kwa njia ya simu na AFP, Mkurugenzi wa Mipango wa Mbunga za Wanyama TANAPA bwana Allan Kijazi amesema kuwa inatarajiwa kuwa hadi ifikapo mwezi Aprili mwakani, vifaru 32 watakuwa wameshahamishiwa katika mbuga hiyo iliyopo mkoani Arusha. Inakadiriwa kuwa, idadi ya vifaru walimo katika mbuga ya Serengeti ni kati ya 30 -35, idadi yake inaweza kufikia 67. Ameongeza kusema kuwa, aina hii ya vifaru, yaani vifaru weusi (Diceros bicornis) awali walichukuliwa kutoka Tanzania na kupelekwa Afrika kusini na sasa wanarejeshwa katika makazi yao ya kawaida. Habari kwa lugha ya kiingereza inapatikana katika linki ifuatayo: google.com/hostednews/afp CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed