Naulizaje, hawa (pichani) waliweza wana nini, nasi tunashindwa hatuna nini? Tunapokaa ama kusimama majukwaani na kuanza kubishana sisi ni masikini kwa laana, na Mungu (au Yeye mwenye Ulimwengu huu) ametuonea kutufanya masikini tuwatumikie wengine, tujaribu kufikiri tofauti. Ikiwa kweli tunafanya tunachopaswa kwa faida yetu na ya wengine, visingizio vyatokapi? Kulala na kuamka n imakelelee kelele juu ya IMF hivi, WB vile, mashirika ya jamii ya Kimataifa sijui nini, kwani, wamekukateni mikono? Nchi zilizoendelea za Ulaya na Asia ambazo zilikuwa sawa kiuchumi na Tanzania (au nchi nyingine za Kiafrika) katika nyakati fulani, zenyewe hazikuwa na usumbufu wa IMF, WB na UN vile eh? Ikiwa hatuelewi jambo na tunataka kujifunza, si ajabu kukawepo ubishani. Lakini hiyo si hoja, alimradi letu lengo ni moja, hoja yetu kuu - kufanikiwa! Ni ujinga kabisa mtu anapomzuia mwingine asikamilishe jambo fulani kwa kisa cha wivu tu kwamba sifa hataipata yeye, ataonekana yeye dhaifu. Watu waacha kutilia mkazo mambo ya maana, wabaki kulumbania kasoro ndogo ndogo, kisha utekelezaji mzima unagota! Hiyo akili hiyo? Nasemaje, It can be done. Just play your part. Do Good, but that's not enough, Do it well. Katika picha zifuatazo (hapo chini), utaona kuwa kweli mambo yalitokea, yamekuwa historia. Yaliyotokea jana ni historia ya leo na yatakayotokea leo yatakuwa historia ya kesho. Ya kesho yatatengeneza historia ya mtondo na mtondo utazaa ya mtondogoo. Faida ya haya yote ipo katika kujifunza kutokana na yaliyopita, ili tuache ndwele, tuganye yajayo. Tuige mazuri, tuepuke mabaya. Taabu yetu siye, twabishana mno hata kwa yale mambo ya msingi kabisa yaliyokwisha fanikiwa kwa kiasi kikubwa sehemu nyingine. DO GOOD and DO IT WELL! CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |






















RSS Feed