Kichwa cha habari hapo ni tafsiri niliyoikokotoa kwenye nukuu ya comment inayosomeka hapo chini. Tafadhali usiache kusoma sehemu ya 'comments' (maoni BOFYA HAPA) zipo hoja moto sana zimeibuka kutokana na hii comment ya huyu mtu aliyesema IQ za Waafrika zimelala doro. Ukishasoma hiyo comment sasa, usikasirike wala kunikasirikia mimi. Hebu ujiulize, 'utafanya nini kwa vitendo vizuri kupinga kauli hiyo'? Hii kusema ooh, sisi tuna akili, historia inajieleza, kuna weusi walifanya maajabu, sijui nini na nini, saaawa yote hiyo, lakiniii kiasi cha mboga tu hicho, kwa wakati huu je? What can you show? Mkono mtupu haulambwi bwana, what do you have to show (not say) pliz? Kazi unayoifanya unaweza kujismama na kujipiga kifua na kusema 'mweupe' asingeweza kufanya hii? Ninawapongeza wale wote ambao hata kama hawawezi kusimama kusema nimefanya zaidi, bado wanao ujasiri wa kusema, nimefanya kwa levo ile ile ya kwao, tena bila mawaa. Sawa. Najua fika kuwa hata wao 'weupe' si wote wametengeneza kitu cha ku-show, lakini, ukweli unabakia kuwa wemetengeneza vya ku-show na wametuzidi. Utadai waliturubuni na kutuibia. Kweli? Sisi mbona tusiwarubuni sasa na kuwaibia? Wametuzidi kete? au waache tu Mungu anawaona eeh? teh teh teh usitake 'ncheke. Utadai tena kuwa wao wengi zaidi yetu, hivyo yatarajiwa kuwa yao mengi kuliko yetu . Hivyo ni sawa kabisa? hivi eeh... hebu statistician afafanue hapo katika uwiano wa wao wengi, vyao viwe vingi na sisi wachache, vyetu viwe vichache, halafu itabalansi? Ufafanuzi pliz. Na kama umekasirika, pole! halafu, what can you show? hasira haisaidii kufuta hii deep rooted mentality ya some 'white' folks. What can you show? Jitetee. Ukishindwa kusoma hapo, ifuate nilikoitoa kweye linki ambapo utakuta comment ya kwanza kisha ya pili: allafrica.com/comments/list/aans/post/post/id/200912280212.html CommentsDk. Kiva 30/12/2009 12:42am
Kuna ukweli,
Reply
.mpiga kura (Dk. Lelo) 30/12/2009 12:45am
Mengi sana ya kuandika muda hauruhusu, nadhani hapa unaweza kuandika makala kabisa ila sijui nianzie wapi. Kwa kifupi ni kwamba IQ sidhani kama tuna low IQ ila kipimo ndio kina bias kama kipo. kuhusu sisi kuwa inventers bado itakua ngumu sana kwani tunasoma historia ya science na hatusomi science. Jaribu ujiulize ni watoto wangapi wanaofika University wakiwa hawajui hata litmus paper ni nini? ni wangapi wanaofika Form Six wakiwa hawajui hata baadae wanategemea wawe akina nani? Ni nani aliyeanzisha mitihani ya alternative to practical alikua na nia gani? kama sisi ambao tunaaminiwa ni wanasayansi hatujui kitu unategemea tunaweza kutoa support kwa wale wasiosoma wakainvent? Kwa kuwa tunasoma Historia ya sayansi ni wazi kila siku tutakua nyuma ya muda na tutaendelea kutoweza kuvumbua vitu mpaka turudi kupumzika kwa Mungu baba ambapo wote tutakua sawa. Wakati hujaweza kutengeneza toothpick mwenzako anatengeneza meli, utamfikia lini? Hapa dawa ni bara letu liwekewe vikwazo vya kiuchumi tuanze moja angalau tutakwenda mbele otherwise ni hapa hapa hakuna kusogea.
Reply
.mpiga paka (Dk. Kiva) 30/12/2009 12:49am
TO ADD salt in the wound, can you imagine people like Mugabe being in power for over 25 years, yet the citizen can not make the ends meet, no bread, no medical services, no electricity, no running water, yet when they come for next election they are put into power? Someone going to 80 years yet we let him ruleor to lead us? You may say people are frightened or intimidated whatsoevr or there is stealing of vote but who dopes the stuff -we- and not others. Can you imagine that from indepemdence up to now we can't even make our Mama deliver in a comforatable way but we use mountains of dollars to buy Radar and Presidential jets, send 100 delegates to the enviromental forum while trees are falling like hell? Tanganyika, Nyasa, Victoria, Malagarasi, bahari tele sijui Manyara na hata nyumba ya Mungu yet hatuna runnning water - ndo IQ HIYO???
Reply
Dr. Fabi 30/12/2009 12:55am
........naendelea ulipoishia.....
Reply
Dr. Bruno aka LeBron 30/12/2009 12:57am
Ukumbuke kuwa viongozi ni product ya uraiani, wana mentality tulionayo wengi, kwao hawaoni taabu watu wakipata taabu, kwani nao walikua humo humo, may be hawaoni tofauti, au wameshakuwa fatigued na usugu wa matatizo,..hebu niambie unaongozaje taifa la wavivu kama Tz,..si-justify uzembe wa viongozi, ila najaribu pia kukaa sehemu yao na kuangalia chini,..deep kwenye roots kuanzia kwa katibu kata mpaka kwa katibu mkuu kiongozi,..woote siasa tu, hakuna anayefanya kazi, hakuna aliye responsible,..hakuna anayethubutu kumwajibisha mwingine,..imagine,..na hapo ndio utapata jibu..kuwa mabadiliko yatakuja kama ka-kizazi kakiwa nullified kakaja kengine-msemo wa Kundy "Mungu atuchukue alete wengine."
Reply
Dr. Isaac 30/12/2009 12:58am
Au inawezekana kuwa tumezungukwa na umaskini wa kutupwa kiasi kwamba tunatumia muda wetu mwingi kuangalia namna ya ku-survive na mwishowe tunakosa muda wa ku-invent?? hii mwisho wa siku ina negative feedback kwa kusababisha uzazi wa watoto wasio na nia wala wazo la ku-invent na kuishia kuhangaika ili mkono uende kinywani tu baasi kwishnehi?? kipi ni kipi hapo...
Reply
Dr. Lelo 30/12/2009 12:59am
jamani naombeni nisaidiwe hicho kipimo cha IQ kinatumia vigezo gani maana nakiona kama usanii hivi.
Reply
Dr. Tonny aka Supika 30/12/2009 1:00am
Nimewasoma wote, The bottom line is kuwa na akili jamani sio kufaulu masomo, ni kuwa na mabadiliko yatakayosaidia vizazi na vizazi.
Reply
Subi 30/12/2009 1:01am
.mpiga kura,
Reply
DHK 30/12/2009 1:02am
Rafiki yangu nilikuwa nampa hii story ananiambia hapa LET THEM BE EXPERTS IN INNOVATION and LET US BE EXPERTS IN APPLICATION'.
Reply
Dr. Barnabas 30/12/2009 1:03am
Wazungu wanasema tu, wapi waligundua matumizi ya chuma??
Reply
Evans Wenger 30/12/2009 1:05am
Sina mengi ya kuongeza. Mengi mumeongea,Kiva,Fabian balaa tupu.. mmenena yote.
Reply
Subi 30/12/2009 1:23am
kujibu swali la .mpiga kura soma haya maelezo niliyotoa kwenye website moja:
Reply
Evan Wenger 30/12/2009 1:25am
@ Barnabas umezungumza pointi, Kwa wale wasomaji wa historia wanajua kitu gani kilikuwa kikiendelea kule Afrika Magharibi viwanda kibao,Nini kilikuwa Uganda na ile teknolojia ya nguo 'embugo' so much more. Ukarimu wetu wa kuwasaidia wageni ulitupeleka kubaya... na mpaka leo ndo inatuandama. Umasikini umeleta ulafi..
Reply
Dr. Fabi 30/12/2009 1:26am
Mzee Supika umenena.
Reply
.mpiga paka (Dr. Kiva) 30/12/2009 1:28am
sasa Wenger what do you mean wao kutudhulumu sisi ni kosa kwao au kwetu wenyewe? Does it means hatukuamka baada ya kuanguka? Hatujajifuta vumbi kisa tuliuwawa babu zetu kina Mkwawa na Kinjekitile?
Reply
Keku (Dr. GT) 30/12/2009 1:32am
nimewasoma halafu mkaniongezea hasira!!!!!!, kwanza sikubali kwamba IQ yetu ni ndogo kulinganisha na hao wengine, sema tu tumezi-direct kuwaza mambo mengine. Ukimchukua mtoto wa miaka 5 pale kijijini anaweza kuhakikisha yeye na wadogo zake wanas-urvive na kutumia akili zake kuwaza how, ukichukua the same kwa hao unaofikiri wana IQ kubwa sidhani kama wanaweza hilo zaidi ya kupiga simu Polisi nakuomba msaada na kuchukuliwa na watu wa social well fare,ambazo kwa wenzetu zipo supa. Ishu niionayo,t unaongongozwa na wabinafsi, wasioangalia maslahi ya wengine na waoga ku-act, na wasomi walishajikatia tamaa na kujifanyia mambo kutokujali. Hivi unaweza jenga nyumba ya billion wakati unaowaongoza wanakaa kwenye nyumba ya nyasi? hata ungejengewa kwa nini usikatae? The same for..., utapangishiwaje nyumba za dola 8000 kwa mwezi kweli, acha wale waliokataa kukaa yile nyumba walizojengewa wanakaa Kempiski, hivi kweli? Mnaagiza MaVOGO ya 2009 spots ili iweje? Labda tuache kusingizia IQ zetu na tuache woga wa kuingia risk na tu act ndo tutajua kama tuna IQ ndogo au vipi.
Reply
.mpiga paka (Dr. Kiva) 30/12/2009 1:35am
way foward nafikiri na ambayo ipo feasible kwa sasa ni personal mission au hata joint lakini with achievable mission. Fighting will not solve kwani kwa vile IQ ndogo hata (nanihii) wakilipwa laki moja na bia za bure na sigara tu atakuua kwa ajili ya mwanasiasa.
Reply
Supika (Dr. Tonny) 30/12/2009 1:38am
Hayo unayoyasema GT ndio nayosemaa hatuna akili.
Reply
Mose B 30/12/2009 1:39am
Kuna ukweli ndani yake kuwa sisi waafrika uwezo wetu wa kugundua mambo ni mdogo achilia mbali uwezo wa kufaulu katika masomo tunapokuwa katika taasisi za elimu. Wakati mwingine kinachoturudisha nyuma katika ugunduzi ni fursa (opportunities) ya kutumia uwezo wetu katika ugunduzi. Kuna mmoja wetu amecomment kuwa sisi tunasoma historia ya sayansi, hilo nadhani halina ubishi kwani mitaara yetu ndo ilivyo na haiendi na wakati. Ukiangalia watafiti wetu wengi lengo kuu si ugunduzi na kuchangia kukua kwa knowledge katika sayansi bali utafiti umekuwa kama MKUKUTA. Researchers wetu wanaandika proposals ili ziwatoe, sina kumbukukumbu ya profesor mtanzania kuandika kitabu chochote but nakumbuka tu kulikuwa na VIHEREHERE vya kutosha.
Reply
Tripple M (The Pioneer) 30/12/2009 1:43am
Wakuu, nimewasoma vizuri tu n hakika ni mantiki tupu. Fabiani, ukitoa single hapo mistari imepangika ni kutafuta vina tu....(analeta soga huyu kwenye mambo serious).
Reply
Dr. Sung 30/12/2009 1:44am
Great thread!
Reply
Dr. Bruno aka LeBron 30/12/2009 1:45am
Reading and re-reading this thread makes me even more angry,..simply because i have come to one conclussion,..
Reply
Subi 30/12/2009 1:46am
Mucho, sidhani kama IQ inaweza kubaki constant kwani yenyewe ni kipimo cha uwezo wa mtu ku-learn na retain information kwa kiwango fulani na has kulingana na mazingira kisha uwezo wa ku-recall na retrieve informations mbalimbali inapotakikana na time atakayotumia mtu kutoa hiyo correct information, ndiyo maana maswali yote ya IQ ni timed isije ikatokea mtu anatoa majibu sahihi within 1minute akawekwa kundi sawa na aliyetoa jibu sahihi after 30minutes achilia mbali yule asiyejua kabisa.
Reply
Subi 30/12/2009 1:48am
GT,
Reply
Dr. Mor 30/12/2009 1:50am
occupations typical of various IQ levels:
Reply
Subi 30/12/2009 1:51am
teh teh, Dr. Mor, acha kutilia focus kwenye issue ndogo ambayo yenyewe ni utata mtupu, hata Bill Gates (Microsoft and the Bill & Melinda Gates Foundations zinazolea Malaria, TB & HIV and improving Education standards across the world) hakumaliza chuo na kwenye msururu wake wamo Michael Dell (Dell Computers), Steve Jobs (Apple Computers), Simon Cowell (POP and American Idol), Walt Disney, Henry Ford, Milton Hershey (chocolate za Hershey), Frank Lloyd Wright sasa ukijumlisha na ambao si Professors lakini ndiyo wanaongoza huu ulimwengu kwa humanitarian aids utasema IQ zao ni ndogo? Oprah Winfrey, Mother Theresa (RIP), Founders of Kiva.org, wapiganaji wa kundi la Nelson Mandela? na waliokufa je? Steve Biki, Julius K. Nyerere, Anwar Sadat, Kwame Nkrumah, Patrice Lumumba, Samora Machel yaani wote hao utalinganisha IQ zao na za maprofesa wa leo?
Reply
Dr. Mor 30/12/2009 1:53am
(chocolate za Hershey),
Reply
Subi 30/12/2009 1:54am
Yaa, nakukumbusha kuhusu chololate za Hershey ili hapo Kijijini ambako mna Kahawa na mawezi kuitengenezea heleri hadi Starbucks ainunue kwa kilo dola 5 halafu yeye anauza kikombe kimoja tu dola 5 uniambie mwenye IQ hapo ni wewe na wanakijiji wenzio walima kahawa au ni mwenye Starbucks? na nimesikia ndugu zako wale wa Nyanda za juu kusini wanafufua kilimo cha kakao, soma gazeti tando la AllAfrica.com utaikuta hii habari, sasa IQ yenu kulima, wao ndo wanakupangieni bei ya kuinunua na kisha wanakuuzieni ikiwa imefungwa tuduuuchu kwenye tukaratasi, ninyi mnabaki na majani na miti yenu, na bado mnaambiwa mnaharibu mazingira na hiyo miti mnayo wakati wao wanapuliza moshi wa kutengeneza hiyo chokoleti... IQ hoyeeeeeeee!
Reply
Keku (Dr. GT) 30/12/2009 1:59am
Hebu jamani lets assumme ndo tunaiongoza nnji, na priority yetu ikawa
Reply
30/12/2009 9:58am
Naona mjadala huu umetawaliwa na wasomi (ma-dkt) mpaka wengine tunaogopa kuchangia sasa. Mada nzuri.
Reply
Jamani nawaomba mnijibu swali langu, je kunayo mashine ya kupima IQ?
Reply
wavuti 30/12/2009 4:58pm
Shukrani Prof. Matondo kwa machango wako, hata na hivyo walioachangia hapa wasikusababishe ushindwe kuchangia kwani katika nchi yetu kila mmoja anayo nafasi ya kuchangia na haki ya kusema wazo lake na ni kwa vipi angependa kuiona nchi inaendelea. Nakushukuru kwa kubaki katika LENGO KUU la mada.
Reply
Mutta 30/12/2009 5:56pm
kwa maoni yangu ni kwamba sijui walitumia nini kulinganisha waafrika na wengineo. niliposoma hapa nikaamua kuifanya ili nione IQ yangu. nikakuta maswali ambayo kwa kweli yanahitaji ufahamu zaidi wa kizungu na au mahesabu. maneno kama "octagon" sisi tuliokimbia hesabu siyo rahisi kuyajua n.k. nadhani hapo kuna kaupungufu kidogo kwani haijali mazingira.
Reply
Ndokoo Namwa 30/12/2009 8:42pm
Ndugu zangu nawasisitizieni mu "Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka, wewe pamoja na jamaa yako". Huu ndio msingi wa maisha,sio mambo ya IQ.
Reply
30/12/2009 9:44pm
Da Subi. Asante.
Reply
Alledros 30/12/2009 9:52pm
Subi umewasha moto! Ila kuokoka si maneno! umepewa vipaji uvitumie na utaokoa nchi na roho yako!
Reply
Kamanzi 30/12/2009 9:54pm
Ndokoo Namwa. Unachekesha!
Reply
Benjamin 31/12/2009 3:04am
Mie nipo Ujerumani, ninasoma hapa na ninamshukuru sana Mungu ambaye amenipa kibali cha kuja kusoma huku na kuona mambo mengi ya wazungu. Ninachoweza kusema hakuna ukweli wowote kuwa waafrika wana IQ ndogo kuliko wazungu, Wazungu ni watu wa kawaida kabisha, tofauti yetu kubwa sisi tunakosa fulsa ambazo mtoto wa kizungu anazipata. Mtoto wa kiafrika ambaye anazaliwa huku na kusoma huku na anapata fulsa sawa wanakuwa na uwezo mkubwa sana na wakati mwingine zaidi ya watoto wakizungu. Kwa nchi kama Tanzania ambayo ninaifahamu vizuri, Hakuna sayansi wa Technologia. Ninaweza kusema sayansi tanzania imekufa kabisa. Siku za nyuma angalau tulikuwa na afadhali sasa hali imekuwa mbaya. sekondari za ufundi zimekufa, sekondari hazina vifaa vya maabara na zingine hata jengo la maabara halipo. Itachukuwa muda mrefu sana kutatua tatizo hili kwana hata walimu wa sayansi katika shule zetu walisoma katika mazingira ya mabovu. Kama Mwalimu hakuelewa atafundisha nini watoto waelewe? wewe fuatilia vyuo vikuu vingapi vina kozi za sayansi au technologia. vyuo vingi vinafundisha kozi za uongozi na maendeleo. HAKUNA MAENDELEO KAMA HAKUNA SAYANSI NA TECKNOLOJIA. hapa ujeruma ukiangalia vyuo vya technology na science huwezi kuamini mambo ambayo yanafanyika kuwapa ujuzi vijana wao. Mfumo wetu wa Elimu ni kikwazo cha maendeleo yetu. Kimsingi hatuwezi fikia maendeleo waliyo fikia wazungu kwa sasa. Kinachonisikitisha hata kile kidogo tulichokuwa nacho kinakufa na hakuna mtu anashituka. Uchumi bila uzalisha katika viwanda na kilimo tutabaki kumtafuta mchawi. mchawi wa maendeleo yetu sio IQ ni mfumo wetu wa elimu na vipaombele vyetu ya maendeleo. Mwisho namaliza kwa kusema Historia ya bara la afrika, biashara ya watumwa ina mchango mkubwa sana katika umasikini wa Afrika na Waafrika wenyewe.
Reply
wavuti 01/01/2010 9:51am
Nimefaidi mawazo na mtizamo wenu @Mutta, Matondo, Alledros, Kamanzi na Benjamin.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed