Ama kweli penye wajenzi miti hamna'ga 28/01/2010
Nasema hivi baada ya kusoma habari iliyoandikwa katika kazeti la Majira (isome hapo chini) kuhusiana na Wageni kuona tukizembea katika michezo ambayo wao wanaona ingeendelezwa huenda ingewatoa watu kimasomaso. Ninapokubaliana na kauli ya wahenga kuwa penye miti hakuna wajenzi ninamaanisha kuwa, vyote vya thamani vya asili na vya kiutamaduni hatujajua bado kuvitumia kwa faida ya sote hadi aje mgeni atuoneshe umuhimu wake. Nilishangaa zaidi wakati fulani nilipopata safari ya kutembelea miji ya Pwani na Visiwani Zanzibar kuona majengo yakiporomoshwa ati kupisha ujenzi mpya tofauti na nilichokiona wakati fulani mjini Roma nchini Italia ambapo wenzetu hao wanakarabati vyao vya zamani. Katika nchi hiyo watu wengi wamejipatia ajira binafsi baada ya kusoma masuala ha hisroria na miji ya kale katika nchi yao na hivyo kuwa waongozi wa watalii. Sisi badala ya kuiga mazuri wanayoyafanya wao na kusababisha ajira kwa wahitimu wetu, tunabomoa na kukazana kujenga wenyewe twaita, 'kisasa' na bado 'ukisasa' wenyewe si hili wala lile bali kila siku kusikia habari za kuanguka majengo yanayojengwa mapya ama yale ya kale, na hata yakajeruhi ama kuua. "Waingereza waanza kutoa kozi ya mdako, kombolela" - Adolph Bruno, majira.co.tz Walimu wa Shule za Msingi sita za Wilaya ya Temeke, juzi walianza kupata kozi ya siku nne inayotolewa na shirika la michezo la Uingereza la Uk Sports Inter, kwa ajili ya kuwapa ujuzi wa kuwafundisha watoto michezo shuleni ambayo inafanyika katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Shule zinazoshiriki kozi hiyo ni Mgulani, Mtoni, Shalom, Muungano, Kibasila na Yemeni ambapo michezo inayoibulia ni pamoja na kuvuta kamba, mdako, kukimbia na vijiti, kombolela na kukimbia kwa magunia. Akizungumza Dar es Salaam jana Ofisa Habari wa Shirika hilo kanda ya Dar es salaam, Mohamed Mvumbagu alisema kozi hiyo ni miongoni mwa kozi zinazoendeshwa na shirika hilo kwa lengo la kukuza michezo isiyo ya gharama shuleni. "Kama ilivyo kawaida tumeanza jana (juzi), kutoa mafunzo ikiwa hii ni mara ya pili, tangu tulipotoa katika shule ya Chang'ombe na tuliweza kufanya vizuri kwa kufaulisha walimu wengi, ambao sasa wataendeleza mafunzo hayo shuleni," alisema Mvumbagu. Alisema kozi hiyo itamalizika keshokutwa ambayo itafungwa kwa bonanza kubwa litakalofanyika katika Uwanja wa uhuru, Dar es Salaam litakalowezesha kujua jinsi mafunzo yalivyopokelewa na walimu hao. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed