Habari kwa mujibu wa tovuti ya BBC Swahili zinasema ifuatavyo kuhusu majirani zetu:
Nchi ya Marekani imesitisha ufadhili wa dola millioni saba za mpango wa Elimu Ya Bure kwa Shule za Msingi nchini Kenya. Balozi wa Marekani nchini Kenya bwana Michael Ranneberger amesema ufadhili huo utasitishwa hadi pale madai ya ufisadi katika Wizara ya Elimu yatakapochunguzwa. Hatua Marekani kusimamisha ufadhili huo imechukuliwa mwezi mmoja baada ya Serikali ya Uingereza kuondoa ufadhili wake kwa sekta hiyo ya Elimu. Balozi Ranneberger amesisitiza kuwa ni lazima mpango mzima wa Elimu ya bure nchini Kenya ufanyiwe uchunguzi. Marekani imekuwa ikishinikiza serikali ya Kenya kutekeleza mabadiliko mbalimbali nchini humo.


RSS Feed