Indiketa hatari kwenye mahusiano 22/01/2010
Inaaminika kuwa, unapokuwa katika mahusiano ya urafiki wa karibu au mapenzi kisha kuanza kuona majibu ya aina hii, basi ng'amua kuna kiti si sawa hapo. Ila, wapo ambao majibu yao yapo hivi tangu siku ya kwanza kabisa ya mahusiano. Wanaozungumziwa hapa ni wale wanaoanza kwa mahaba moto moto kisha inafuata: Sms: “Sweet, nimekukumbuka sana leo, natamani tungekuwa sote mida hii. Upo wapi mpenzi?” Jibu: “Nipo” Sms: “Yaani nimekutafuta kweli mpenzi, mbona ulikuwa hupatikani? Mwenzio sijalala nakufikiria wewe my love. Umenimiss?” Jibu: “Simu iliisha charge” Sms: “Baby leo nakula chakula kitamu kweli. Sijui wewe unakula nini. Natamani tungekuwa wote. Karibu mpenzi” Jibu: “Poa” Sms: “Honey, yaani ile perfume uliniletea inanukia vizuri ajabu. Yaani hapa nipo nasikia harufu yake na kukuwaza wewe, tena nakumbuka leo umetoka fresh na ile tshirt nilikununulia. Ukisoma hii sms wewe unapata hisia gani?” Jibu: “Tshirt inanibana” CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed