Kampuni ya Haki za Wasafiri 31/01/2010
Nimefurahishwa na hatua hii ambayo kwa namna fulani, pengine itatia msukumo na kuchangia katika kuhimiza uangalifu kwa wamiliki wa vyombo vya safari na waendeshaji vyombo kuwa makini na kujali uhai wa binadamu. Mwandishi Richard Konga kutoka Arusha anairipotia Majira.co.tz kuwa Kampuni ya kutetea wasafiri yaanzishwa. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Haki za Wasafiri na ajali Bw. Godson Kirita amesema ameanzisha kampuni hiyo ili kutetea haki ya wasafiri wa ndani na nje ya nchi mara wapatapo ajali na wakati huo kukosa chombo cha kuwatetea. Akizungumza na Majira Bw. Kirita alisema ajali zinazotokea mara kwa mara husababisha familia nyingi kuwa yatima na wajane na wengi wao kuwa na vilema vya maisha hivyo kuwa mzigo kwa jamii, pia husababisha ongezeko la watoto wa mitaani. Akitoa mifano ya ajali zilizotokea hivi karibuni katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Bw. Kirita alisema ajali hizo zimepoteza maisha ya watu wengi wasio na hatia ambao, ndio nguvu kazi ya Taifa, wakati huo huo hakuna chombo kinachojishughulisha kuwatetea watu hao ili kupata haki zao. Alisema amekuwa akifarijika na jitihada za serikali katika kushughulikia masuala ya usafirishaji wa abiria lakini amesikitishwa na madereva wazembe wasiotekeleza, maagizo ya serikali hususani juu ya mwendo kasi wa magari yao na kuiomba serikali kurekebisha sheria ya usalama barabarani. Wananchi wakiwemo wafanyabiashara wameonesha kufurahishwa na chombo hicho walichokiita mkombozi wa usafiri wakati wa majanga ya ajali na kwamba kitawasaidia kutetea haki zao. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed