Bloga Bernard Rwebangira ametoa rai katika blogu yake, bongopicha.blogspot.com, akitahadharisha wananchi kukaa chonjo na aina hii ya utapeli.
Ninafahamu kuwa wengi wetu tueshaelewa muundo wa aina hii ya utapeli na hatukubali kudanganywa tena, ila, wapo bado wageni katika ulimwengu wa email na walafi wachache ambao hutumbukia kwenye mtego huu. Tafadhali muwatahadharishe na kuwaonya kutokupenda fedha za chap chap. Hakuna bwerere duniani.
Yeyote anayetaka kutoa misaada kwa ajili ya watu wa Haiti basi afanye hivyo kupitia vyombo rasmi vilivyoorodheshwa katika linki hii: bagtheweb.com/b/9UiJNI2Sup7d yenye kichwa cha habari "20+ Ways to Help Haiti".
Dear Friend,
I am Major Bruce Roberts of the United Nations Armed Forces here in Haiti, I am a very close friend and personal adviser to the Haiti President Mr. Rene Garcia Preval.
( hapa kuna blah blah blah ndeeefu za kujitetea na sababu mia kidogo.....)
I and my fellow military personnel immediately went to the president palace and we recovered 4 big trunk boxes each containing $13.6Million (thirteen million six hundred dollars) each. Please keep this information highly confidential between us and respond back to me with your telephone number via my personal e-mail; bru******@hotmail.co.uk so we can discuss better on how I will be transporting this box out of here to you. Thank you and bye for now.
Major Bru R.


RSS Feed