Mambo mengi yametokea katika miaka ishirini iliyopita. Mabati yenye kutu Kariakoo yametoweka na uingiapo Dar kwa juu mji unapendeza. Vikwangua anga vimezagaa hadi Kijitonyama (with all due respect), shule za kupendeza zimejengwa mijini na za zamani zinaendelea kusota. Kwa waliosoma Origins of the Species ya Darwin wanajua kuwa hii ndiyo survival of the fittest na hatima yake inajulikana. Niliwahi kwenda bwenini kwangu miaka ya nyuma na sikushangazwa na niliyoyaona. Niingiapo mjini kwetu hupita shule niliyosoma nikiwa mdogo - toka vidudu, kukiwa na madirisha ya vioo, madawati na hata msafisha vyoo - leo ni magofu kama ya Bagamoyo. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema: Inawezekana timiza wajibu wako - ni maneno machache lakini yanahimiza mambo mengi ndani ya jamii ikiwa ni pamoja na kuepuka rushwa na kuwajibika. Uwajibikaji mkubwa hata hivyo ni wa Taasisi husika ambazo ni sisi wenyewe - kwani ni sisi tunaojenga majumba ya mamilioni Tegeta na ni sisi tunaowajibika kuendesha miundo mbinu ya afya, elimu, uchumi na huduma zote za jamii. Pengine mwalimu alisahau kuongeza "...ila itangulize nafsi yako". Rafiki yangu mmoja ambaye haamini Mungu anaamini kuwa wanaodhulumu haki za watu iko namna watawajibika - namna gani, hajui - anachukia sana rushwa..." Kassim S. Mwitondi - 23 Januari 2010 CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed