sijui anafanyaje kazi ya kutunza familia na kuwashughulikia hawa wale zake
Reply
GRACE
05/01/2010 03:18
Naumia sana kuona jinsi Waafrika ambavyo wanaendekeza mila sisizofaa wake wote wa nini ni unyanyasaji mkubwa wa wanawake je ana muda wa kumtumikia Mungu wake>>>>>>>>>> Taifa Je<<<<<<<<<
Reply
Sabato Tarimo
06/01/2010 02:16
Sasa huyu Jacob Zuma ni mkristo au mpagani? Huyu baba anaaibisha ukristo na Waafrka wote kwa kuendekeza mila la ajabu ajabu
Navyofikiri mimi, binadamu anatawaliwa kifikra kwa aidha IMANI ya dini rasmi zilizokubalika kimataifa au IMANI ya mila aliyokulia, aidha ikubalike au isikubalike kimataifa. Baadhi ya watu, mila ndiyo msingi wa dini na imani yao, yaani mila kwanza kisha masuala ya dini rasmi yatafuata baadaye, wakati wengine ni kinyume cha hivyo, yaani dini rasmi iliyokubaliwa kwanza kisha mila na desturi zitakubalika ikiwa hazipishani na dini.
Sasa hapo ndipo pagumu kwa pande mbili hizi kukubaliana hata katika mambo ya msingi kabisa ambayo upande mmoja wanaona ni sawa kabisa na wanashangaa ni kwa vipi upande unaowapinga hauelewi, nao upande unaopinga unashindwa kujua ni kwa jinsi gani wenzao hawaoni kuwa wanachokifanya hakifai kabisa katika jamii.