Simba yawafunza mpira Toto Afrika; nayo Misri yatwaa ubingwa Afrika; wakati ManU wainyoa Arsenal 31/01/2010
![]() Timu ya Simba Sports Club leo imefanikiwa kuendeleza dozi zake kwa kuifunga Toto Afrika katika uwanja wao wa nyumbani goli 2 kwa nunge. Hadi kipindi cha kwanza kinakwisha, timu zote zilikwenda mapumziko kwa suluhu ya kutokufungana. Kipindi cha pili dakika ya tano, Mussa Hassan 'Mgosi' alifungua darasa la magoli akifuatiwa na Ramadhani Chombo 'Redondo' aliyefunga kitabu cha magoli dakika nne baadaye. Hadi mwisho wa mtanange huo, Simba 2 Toto Afrika 0. Hongera Simba kwa kuondoa aibu ya mwaka jana kwa kufanya malipizi ya aina yake kwa mwaka huu! Na katika mechi zilizochezwa kwingineko duniani, Mshindi wa kombe la mpira wa miguu kwa Mataifa ya Afrika amekuwa Misri baada ya kuitandika Ghana bao moja ambalo lilifungwa dakika ya 85. Hivyo hadi mwisho wa mechi, Misri 1 Ghana 0. Nchi ya Misri inaweka rekodi ya kuwa nchi iliyonyakua kombe hilo mara nyingi zaidi kuliko nchi nyingine yoyote. Na kisha huko Uingereza matokeo ni Manchester United 3 Arsenal 1. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed